CHADEMA, Vipi Tuuboreshe Muungano?

Ewe mwenye shingo ngumu hujawahi kusikia baba wa Taifa akisema nje ya muungano ni wachaga na wangoni? sasa unaposema muungano uvunjike kwanza una maana gani? ushindwe
 
Mie naafiki kimsingi hakuna muungano kuna muungano wa kisiasa na maneno meeeengi!
 
Ikiwa huo ndio msimamo wa chadema niko pamoja nao kwa hilo, au mleta mada anatafuta sympathy tu?
 
sijawahi kuona faida ya muungano ni nini....hata ukivunjika leo sioni hasara, bali faida tu. tutawabeba wana mdebwedo hadi lini? tuachane nao na uamusho wao.
 
Sio kweli hata kidogo, hapo baba wa taifa alikuwa ameudhika tuu na hata siku moja hajaikataa TANGANYIKA.
Ewe mwenye shingo ngumu hujawahi kusikia baba wa Taifa akisema nje ya muungano ni wachaga na wangoni? sasa unaposema muungano uvunjike kwanza una maana gani? ushindwe
Jiulize kama Zanzibar ingekuwa haipo hapo ingekuwaje. Dhana yako ni ya WOGA tuu na sijui ni kwa nini!
 
wao wana nchi yao ,wana bendera yao , wana bunge lao ,wanavikosi vyao vya ulinzi , je Tanganyika yetu ipo wapi , babu zetu waliochangia hela zao kutoka kwnye mashamba ya mkonge,chai ,kahawa walichangia kwa ajili ya TANGANYIKA na wala Tanzania maana kabla ya 1964 hakukuwa na nchi kama hyo lakini TANGANYIKA ilisurvive, na kingne kinachotuudhi hawa wenzetu kuhisi tunawanyonya , bora huu muungano utupiliwe mbali na wala kuc we na muungano mkataba , maana wenzetu ni wasumbufu, kila mtu achukue chake na ajue lwake kama EAC mwaka 1977.
 
GHIBUU

kwanini usiandike japo summary ya hiyo You Tube video ili na sisi tunaotumia simu zenye uwezo mdogo kuingia jf tuweze kusoma na kuelewa?.
 
Last edited by a moderator:
Ewe mwenye shingo ngumu hujawahi kusikia baba wa Taifa akisema nje ya muungano ni wachaga na wangoni? sasa unaposema muungano uvunjike kwanza una maana gani? ushindwe

hiv ww kwani nyerere ni Mungu kwamba kauli yake sikuzote iko sawa?
hivi kwa mawazo yako unajua kuwa muungano utadumu milele?
nibora tukaishi maisha ya amani na utulivu kuliko kuishi ndani ya muungano tukiwa na hofu tele. kwanii wewe hapo ulipo unafaidika na nini kutoka kwa muungano bila shaka ni indirect way ila madhara yake yakitokea yatakugusa moja kwa moja
 
kwanini watu watanzania bara wanalichukia neno tanganyika hali yakua wazanzibar wao wanafurahia jina leo?muungano unatuunganisha ama unatuumiza kichwa?zanzibar wananchi yao,wimbo wataifa lao,bendera yao na rais wao kama.kwanini tanganyika hawana bunge lao,rais wao,nyimbo ya taifa lao,bendera yao ama muungano ndo tanyanyika?jee?hapa nyerere amekosea ama kuna ajenda ya siri?kwakweli muundo wamuungano hatuulewi.bora uvunjike.
 
Kutakuwa na Vyama vitatu serikalini.
CCM, CHADEMA NA CUF.

Nini itakuwa hatima ya Muungano huu?
 
Mods, napenda isomeke CHADEMA ikiingia madarakani
badala ya ikichukua nchi, nimeshindwa kubadili heading
 
Ukweli ni kwamba muungano utafanyiwa marekebisho ili uwe muungano wa watanganyika na wazanzibar na sio huu wa Nyerere na Karume

Lakini mbona inaonekana Watanganyika wanafagilia muundo Huu wa muungano!.

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
 
Hata majibu ya jambo kama hili huna??????????????
  1. Raisi Mstaafu Karume amekwambia ni vema Muungano wa watu wawili ukajadiliwa upya na ukaundwa upya....na hapa ndipo walipoanzia kumuita Uhamsho.
  2. Kila upande hususani Zanzibar wananchi wa kawaida wanaona Muungano hauna faida kwao bora uvunjwe au ujadiliwe upya.
  3. Muungano maana yake ni vingi kuwa kimoja.....Kuna Zanzibar na Tanzania hakuna Tanganyika, na hapa ndio kuna tatizo kubwa.
  4. Angalia Marekani ni Muungano wa Nchi nyingi sana na leo inaitwa USA....yaani United States of America.
  5. Usawa wa umilikaji rasilimali unaonekana kuwa ni tatizo.
  6. Uwakilishi katika bunge pia ni tatizo, wabunge wa visiwani wanaingia bunge la Jamuhuri (Dodoma) wakati wabunge wa bara awaingii bunge la visiwani.

Je hata haya machache hukuyajua?? Huoni kuwa yanatosha kujadili upya Muungano????

Pia tambua Muungano CUF na CCM ni makubaliano ya vyama viwili tu hakuna chama kingine kilishoshirikishwa??? wewe unaamanini kuwa ccm na cuf ndio watakaoendelea kuchaguliwa na wazanzibar? nani aliamini kuwa uchaguzi wa juzi cuf walizidiwa kura na cdm???? :majani7:
 
Wanaofagilia ni viongozi wachache sana na baadhi ya wana ccm ambao chochote cha baba mwalimu kwao hakina sehemu ya kujadiliwa wala kubadilishwa:majani7:
 
Ukweli ni kwamba muungano utafanyiwa marekebisho ili uwe muungano wa watanganyika na wazanzibar na sio huu wa Nyerere na Karume

Kama wakichukua hatua ya kuufanyia mabadiliko muungano, litakuwa jambo zuri sana!
 
Back
Top Bottom