CHADEMA, umati wa Jangwani si nguvu ya chama! Ni kuchoka kwa vijana

Leteni data CDM imefanya nini katika kuinua uchumi wa Tanzania au wabunge wa CDM wamefanya nini kwenye Majimbo yao,,,
 
Kama ulikuwa mbele ya runinga na hukuelewa basi tukuombee tu. Hoja ya muda umechemsha. Mrema alisema atampunguzia dk 5 wala si kumpa dk5! Kadhalika kwa mazingira yale ni ngumu kama utakavyo. Hoja ya wahudhuriaji ni dhaifu sana. Nilikuwa frontline kabisa. Watu wanakwenda pale kwa mapenzi na si nyie mnaosuburia kwenye runinga. Umeme ungekatika ungepata muda wa kusema hayo? Suala la kufungua matawi mkiti alitoa maelezo na namba za simu kwa ajili ya maelekezo zaidi. Akazirudia tena na tena. We Profesa wa wapi?

Si kila kitu ni cha kukosolewa kiholela tu maana yote uliyokosoa, mkuu majibu yake yalikuwa ndani yako kama ungeamua kuwa makini.

Ukiangalia CHADEMA ukiwa bado unaye pepo mchafu wa Magamba lazima utatoa judgement zenye harufu ya kubeza kama Profake. Unatakiwa uwe delivered kutoka Mipepo ya ki-CCM nd o unaweza kutoa unbiased comments. Kwa hiyo jueni bado profake yuko possessed na nguvu za giza za CCM na atakuwa mzima pale atakapofunguliwa na hatimaye kuvua gamba.
 
kama vijana wamchoka kwa nn wasikusanyike CDM SQUARE bila viongozi wa chama au chama chenyewe? ni kweli tumechoka lakn CDM ina rahisisha mikusanyiko hiyo.
 
Nimefurahishwa na michango mingi mizuri kuhusu mada hii. Nimesikitishwa na baadhi ambao sina uhakika sana na elimu au rika lao kwa kuandika maneno dhaifu yasio na mantiki. Ninaogopeshwa sana na ushabiki wao, maana hawafiti CDM wala kwenye chama chochote. Kwa hali ya sasa ushabiki ndio unaoongoza siasa, na kama tunavyojua ushabiki unategemea na mchozo unavyokwenda.

Kwa msisitizo, wote tunakumbukia siku Mh JK anateuliwa kuwa mgombea wa Uraisi kwa tiketi ya CCM, nderemo na vifijo na shangwe kemkem. Nilikuwa na watu kama kumi, nliwaambia hivi jinsi wanavyomshabikia kwa wingi huu anavyoingia, ndio hivyohivyo watakavyomshabikia atoke. Binafsi sikuwa nimeona kitu cha kipekee cha kiuongozi cha kumpa yeye madaraka, zaidi ya kampeni zilizompa umaarufu hasa kupitia vyombo vya habari. Kwa siasa za siku hizi ujanja kupata na si kuwahi. na wengi walikuwa vijana waliomshabikia, na hii ni kutokana na matarajio makubwa walionayo. Ukiachilia mbali matatizo aliyokutana na yo katika mbinu zake za kisiasa, umaarufu wake umeyumba sana kwa takribani kipindi cha kuelekea uchaguzi wa pili an hata baada ya uchaguzi, sababu ni moja tu, kujenga matarajio yasiofikika hata kukaribia tu.

Nimefurahishwa sana na mtoa hoja aliyesema ni vema kuwaambia watu ukweli kuliko kuwajengea matarajio hewa. Na ni vema kuwahamasisha watu kuchukua jukumu wao wenyewe la maendeleo kuliko kuwaahidi kuwafanyia ili tu wakupe dhamana. Iko siku watapima na watajua nani anayeleta matarajio ya kweli.

Tujifunze kutoka Zambia na Malawi, hakuna lingine zaidi ya wananchi kuwa so "desparate" na kuwa na matarajio makubwa ambayo yuasipo wekwa sawa mapema huweza kukisambaratisha chama, kwa kuwa huwa juu kuliko uhalisia na uwezo wa chama kuyatatua. Matokeo yake hata wale waliopewa dhamana hawakuwa na uhakika na kuwepo kwao madarakani, wakatumia vibaya madaraka yao, na "the cricle goes on".

CCM tumefanya makosa ya wazi. Kuingia madarakani kwa CDm si kitu cha ajabu, ila nisingependa kuona ninachokiona kwenye nchi nyingine, mabadiliko yanakuwa ya gafla mno yasio na maandalizi yanayoishia kuiweka nchi pabaya.

UWE CDM au CCM au chama chochote, at the end of the day wewe ni Mtanzania, na hilo ni muhimu kuliko yooote.
 
Washabiki wa CDM mnaotoa matusi na kejeli badala ya hoja mnakiaibisha chama. Onyesheni upevu wenu wa mawazo kama wana CDM.
 
Umati uliojitokeza jana pale jangwani ulichangiwa na matangazo kupitia vyombo vya habari hilo halina ubishi na sidhani kama ule umati ulikuja kusikiliza sera mbadala

bila matangazo watu habari wangepata wapi? Na nini mbna ya matangazo?
 
Back
Top Bottom