Chadema tv

MFUKUZI

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
933
699
Jamani wadau kwa utafiti nilioufanya, tangu CHADEMA wafanye maandamo ya nguvu huku kanda ya ziwa na kulalamikiwa na viongozi wa serikali na baadhi ya wanasiasa uchwaraa, sijaona hata kituo kimoja cha TV hapa nchi kuwafanyia mahojiano maalum viongozi wa CHADEMA kufafanua juu ya tuhuma hizo. Ninachoona ni vipindi kibao na mahojioni mengi kwa mawaziri na wapambe wao wanapewa airtime ya kutosha kuponda haki ya wananchi kuandamana.

WITO!!! Nawaomba CHADEMA wafanye haraka kuanzisha TV station yao, au WanaJF na wadau wengine wanaopenda mabadiliko makubwa ya kisiasa ya nchi yetu waanzishe TV stations zisizokuwa na uoga wala upendeleo kwa kunarusha habari na makongamano ya wasomi na makundi mbalimbali ya wanaharakati yanayodai uhuru na haki za wananchi na kupata mustakabali wa nchi yetu

TANZANIA BILA CCM INAWEZEKA, TIMIZA WAJIBU WAKO.

NAOMBA KUWASILISHA!!
 
nani atawapa kibali, unafikiri kuwa this tv gonna survive for long time bila kufungiwa au kutishiwa? Unamjua vizuri mkwere anavyopenda madaraka huku uchapakazi ukiwa ni " F"?
 
Kamuulize Tido alipotoa fursa sawa kwa vyama vyote yuko wapi!!, ila nakuunga mkono kwani inawezekana kabisa cdm kumiliki tv station + radio station! Nashauri wamiliki wa magazeti mwanahalisi na raiamwema pia kuchukua hili na kulifanyia kazi!
 
Msikose kumangalia wassira akizungumzia maandamo ya CDM ITV kesho saa 3:00usiku
 
Kwani lazima iyo TV station isajiliwe TZ? wanaweza kuisajili hata Rwanda na tukapata matangazo yote kama kawa... tena ikaunganishwa na DSTV, Star Times and kwenye dish and etc. Hakuna kisichowezekana!!
 
waanze na radio tu ya kusikika tz nzima then tv ambayo itaonekana miji mikubwa kwa kuanzia.inawezekana.
 
Mchangiaji uliyesema hiyo tv itakayoanzishwa angalau ipatikane miji mikuu, inaelekea wewe umekulia mjini pekee. Siku hizi vijijini wananchi wanazo satelite dishes na tv program zote wanazipata, wengine wana hata dish za Dstv. Na kama lengo ni kutoa elimu kwa umma, maeneo ya vijijini elimu hiyo ndiyo inahitajika zaidi. Amka tafadhali.
 
Kwani lazima iyo TV station isajiliwe TZ? wanaweza kuisajili hata Rwanda na tukapata matangazo yote kama kawa... tena ikaunganishwa na DSTV, Star Times and kwenye dish and etc. Hakuna kisichowezekana!!
Mashushushu wetu wataliacha hilo litokee?
 
hapa sio kuishia kujadiri tu tuna taka wale wenye nafasi ya kuonana na viongozi wa juu wafanye hivyo halaka, kisha watupe matokeo
 
in connection to this, mimi kwa sasa nipo mbali kidogo na our beloved bongo.nikiwa hapo magazeti yangu huwa ni mwanahalisi, tanzania daima, mwananchi then nipashe majira. sasa kwenye mtandao nikiangalia gazeti la mwanahalisi silioni kabisa,ukilipata ni baada ya siku kadhaa kupita,wana tatizo gani?nakosa sana investigative taarifa zao! nifanyagaje? afadhali mwananchi,t.daima wanaonekanaonekana
 
Kwani lazima iyo TV station isajiliwe TZ? wanaweza kuisajili hata Rwanda na tukapata matangazo yote kama kawa... tena ikaunganishwa na DSTV, Star Times and kwenye dish and etc. Hakuna kisichowezekana!!

Kaka hujaelewa ni kwanini sasa ni sheria kwamba matangazo yarushwe kwa mfumo wa digitali? Unajua role ya Tume ya Mawasialiano (TCRA)? Ni kudhibiti mawasiliano nchini. Hata kama ungesajili wapi, wakiamua wanaweza kuzuia matangazo yasirushwe kwenye anga la TZ. Hivyo la muhimu ni kufuata taratibu zinazotakiwa kisheria na siamini kama itashindikana mbona Radion Uhuru na magazeti ya Mzalendo na Uhuru ni vyombo vya propaganda vya chama cha siasa? Lazima iwezekane.
 
WITO!!! Nawaomba CHADEMA wafanye haraka kuanzisha TV station yao, au WanaJF na wadau wengine wanaopenda mabadiliko makubwa ya kisiasa ya nchi yetu waanzishe TV stations zisizokuwa na uoga wala upendeleo kwa kunarusha habari na makongamano ya wasomi na makundi mbalimbali ya wanaharakati yanayodai uhuru na haki za wananchi na kupata mustakabali wa nchi yetu

TANZANIA BILA CCM INAWEZEKA, TIMIZA WAJIBU WAKO.

NAOMBA KUWASILISHA!!

Hapo kwenye RED, wana-JF na a.k.a. zao usiwategemee wakuunge mkono kuanzisha luninga, ushujaa wao ni hukuhuku mafichoni!
 
Hapo kwenye RED, wana-JF na a.k.a. zao usiwategemee wakuunge mkono kuanzisha luninga, ushujaa wao ni hukuhuku mafichoni!

Siamini kama wanaJF wote wanaogopa. Wapo wenye uwezo wa kujitokeza na kushiriki waziwazi katika kuanzisha Kituo cha kuhamasishs wananchi kushiriki ipasavyo katika kudai haki zao.
 
hoja sahihi-naunga mkono na viongozi CDM wafanyie kazi mapema ili kuwq na direct response kila serikali na ccm wanapopotosha umma juu ya dhana fulani.
 
Kila kitu kinaanzia idea,najua inawezekana,ila nasikitika kuona cdm hawataki hata kumiliki gazeti wala redio mpaka sasa,nasema wanakataa maana sijapata ujumbe wowote wa jitihada izi ili japo zigonge mwamba. Kwa tv inataka maandalizi ila redio hata wakitaka kule mbeya kuna redio zaidi ya 10 kutwa wanapiga miziki kwa nini wasiwaombe mbinu,elewa kati ya matamko ya cdm,tunapata si zaidi ya 40% kwenye media,kama wanataka kusikika plz wafanye jitihada za dhati mapema!
 
Back
Top Bottom