Chadema: Tutatoa elimu ya kisasa, kuruhusu siasa vyuoni

UNAONAJE HUU MKAKATI WA CHADEMA KWENYE ELIMU?

  • MBONA UNAFANANA NA WA CCM?

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    4

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Monday, 20 September 2010
Imeandikwa na Vick Kombe na Geodfrey Nyang'oro

"Chadema inaamini kuwa kuwekeza katika elimu ndio nyenzo kuu ya kukabiliana na matatizo yote yanayoikabili nchi yetu, ikiwemo umasikini.

Tukifanikiwa kuwa na elimu bora tutakuwa tumejipatia silaha muhimu ya kukabiliana na maadui ujinga na maradhi na nyenzo muhimu ya kukuza uchumi imara na shirikishi. Hivyo basi, serikali ya CHADEMA itatilia mkazo sana ubora wa elimu badala ya bora elimu" Hivi ndivyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinavyoanza kueleza katika ilani yake ya uchaguzi kuhusu sekta ya elimu.

Chama kinasema kitaweka mkazo katika kuhakikisha kuwa shule na taasisi zote za elimu zinatoa elimu inayochochea fikra, udadisi, maarifa, uchunguzi uibuaji wa vipaji kwa lengo la kuhakikisha kuwa kila hatua ya kielimu inamuwezesha mhitimu kujitegemea na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya nchi na jamii aliyomo.


Elimu ya msingi na sekondari

Lengo la serikali ya Chadema ni kubadili mfumo wa elimu ya msingi ili iweze kujitosheleza kwa kuhakikisha kuwa wahitimu wanapata maarifa na stadi za maisha zitakazo wawezesha kujitengemea kimaisha. Ili kufikia dhima hii, serikali pamoja na mambo mengine itaongeza muda wa elimu ya msingi kutoka miaka saba hadi kumi na kupanua mtalaa wa elimu ya msingi kwa kuingiza muhtasari wa kidato cha kwanza na cha pili wa sasa katika elimu ya msingi.


Elimu ya sekondari itabadilishwa kutoka miaka sita hadi minne kwa kuunganisha mihutasari ya kidato cha tatu, nne, tano na sita, kuimarisha shule za umma ili zitoe elimu bora, kuimarisha ufundishaji wa lugha zaKiswahili na Kiingereza, kuimarisha ufundishaji wa sayansi na hisabati kwa kuandaa walimu wa masomo hayo kwa uhakika, kujenga maabara za masomo hayo zenye vifaa vyote vya msingi pamoja na kemikali vinavyohitajika.


Mambo mengine ni kuinua ujira wa walimu kwa kuangalia upya viwango vyao vya mshahara na kuimarisha mazingira ya kazi na makazi, kurudisha posho ya mazingira magumu kwa walimu wanaofundisha maeneo magumu ya vijijini hasa katika mkoa inayotambulika ni ya pembezoni, kupitia upya mfumo na mtalaa wa elimu ili kuhakikisha kuwa pamoja na taaluma, wahitimu wanapata utaalamu na stadi sahihi za kujitegemea.


Kuhimiza ufundishaji wa stadi za maisha na Teknohama,kuingiza elimu ya uzazi katika mitalaa, kugharamia elimu ya msingi na sekondari, kurudisha utaratibu wa kutoa chakula cha mchana na kuzihuisha na kuanzisha shule mpya za kitaifa za bweni za sekondari.


Elimu ya Juu na Vyuo Vikuu


Chama kinakusudia kuifanya elimu ya juu kuwa ya kisasa zaidi na inayoweza kumwandaa msomi wa Tanzania kushiriki katika kutumia elimu yake kuiletea maendeleo Tanzania na vile vile kumpa nyenzo za kisasa za kielimu kuweza kumuandaa na maisha ya ulimwengu wa kisasa.

Katika kupanua wigo wa kuboresha elimu ya juu, serikali itachukua hatua mbalimbali ikiwemo kuanzisha mfuko wa elimu kwa ajili ya kugharamia masomo katika vyuo vikuu vya umma kwa wanafunzi wanaofaulu katika kiwango cha daraja la kwanza na pili , kuvunja Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na kuunda chombo kipya cha utoaji na usimamizi wa mikopo ya elimu ya juu.


Vyuo vikuu vitapewa fursa ya kujiendesha kuanzia utawala hadi kitaaluma bila kuingiliwa na serikali, Vyuo hivyo vitakuwa na fursa kamili ya kuchagua viongozi wao bila kuingiliwa na serikali, itarejesha na kuruhusu uwepo wa siasa katika vyuo vikuu vyote nchini kama shughuli ambazo ni nje ya masomo.


Ili kuchochea ubunifu na kuviweka vyuo vikuu katika nyanja za kimataifa, serikali itaanzisha Baraza la Taifa la Utafiti ambalo pamoja na jukumu lake la kuratibu na kusimamia tafiti mbalimbali za kisayansi na teknolojia, kazi yake mojawapo itakuwa ni kutoa fedha kwa vyuo vikuu kwa njia ya kuvipatia uwezo vyuo hivyo kufanya tafiti mbalimbali ambazo matokeo yake yatakoleza matumzi ya sayansi na teknolojia nchini.


Ili kuchochea kasi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia, serikali ya Chadema itabadilisha vyuo viwili vya sasa ili viwe vyuo vikuu vya teknolojia,kuanzisha utaratibu wa kuwa na vyuo vya kati vya jumuiya ambavyo vitatoa elimu sawa na itayotolewa katika miaka miwili ya kwanza ya chuo kikuu kwa lengo la kutengeneza kundi la wasomi wa elimu ya kati ambao kutokakana na sababu mbali mbali wasingeweza kupata elimu kamili ya chuo kikuu.


Serikali ya itafufua huduma ya maktaba kwa kuhakikisha kuwa kila Halmashauri ya Mji inakuwa na mfumo wa huduma ya maktaba. Ili kurudisha moyo wa utumishi miongoni mwa wahadhiri wa vyuo vikuu, Chadema itahakikisha kuwa katika bajeti yake ya kwanza, madeni yote ya wanataaluma ya posho na pango kwa wanaostahili yanalipwa na mpango wa kuboresha mafao ya uzeeni utatekelezwa kikamilifu.


Ili kuendelea kutumia utaalamu na uzoefu wa maprofesa hapa nchini katika kuwanoa vijana wetu vyuo vikuu, serikali ya Chadema itajadiliana na wanataaluma pamoja na mabaraza ya chuo kuona uwezekano wa kuongeza umri wa kustaafu kwa maprofesa kamili kutoka miaka 60 hadi 70 alimradi chuo husika kitakuwa kimejiridhisha kuwa maprofesa husika bado ni wanataaluma kikamilifu.
 
Back
Top Bottom