CHADEMA tuokoeni wana Kigamboni

CHADEMA piga kazi hapo kwa magamba,nyinyi sasa ndio viongozi halali wa hii nchi;CCM wamebaki watawala tu!
 
Hivi kwanini watu wafikirie kuwa uchaguzi hauna matokeo? Sera na itikadi za CCM zinaeleweka; mipango yake inaeleweka na uwezo wa viongozi wake unaeleweka. Lengo la kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano ni kuwapa nafasi wananchi kubadilisha chama na uongozi usiowafaa; sasa Kigamboni walipewa nafasi ya kuchagua wakachagua sasa iweje waanze kukataa matokeo yake? Magufuli ni Mbunge wa CCM na Mbunge wao ni Mbunge wa CCM; sasa iweje walilie CDM chama ambacho hakina serikali au Mbunge? Sijui hata kama kuna diwani wa CDM huko Kigamboni.

Nawashauri walilie CCM
 
Vuneni mlichopanda sasa. Wakati wa uchaguzi simnaweka akili uvunguni,na mnatumia masaburi kupiga kura?:lol::lol: now ndio mnawakumbuka CDM? kwani mbunge na madiwani mliowachagua wako likizo?Nyasi Mtakula na Kama vp pigeni mbizi, hii ndio CCM

Ni kwa nini mnatuhukumu wana Kigamboni? Ni kwa nini mnadhani kuwa sote na ujumla wetu kwamba tulichagua Ccm? Baada ya kutusaidia hapa jamvini sasa imekuwa kuwa sisi tulichagua Ccm ni lazima tu fill the peanch? It does bring the sense, Hapa hoja ni Chadema ije na plan B, na kuwa ninajua bei itashushwa. Sisi sote tunakumbuka bei ya sukari, mafuta, Chadema walipolisemea tu, serikali ilikuja haraka haraka na kulitolea kauli. Hebu tuache unazi wetu ndg zangu na tujadili logic
 
Mzee Mwanakijiji, haya siyo mawazo yako kamwe, mkuu nakujua tangu 2006, wewe mtu unaweza kupembua mambo, kauli hii hapa unataka utuaminishe kwamba, sisi wana kigamboni tunastahili adhabu hii ya magamba? Be careful my brother, nadhani hapa umeteleza. JE UNAFAHAMU MBUNGE WA Ccm alimzidi mama Komu kura ngapi? Si busara kutudharau sisi wapiga kura tuliokigia chadema. Mzee mwanakijiji ni swali dogo tu..., je wewe unaungana na mawazo ya hawa wanaodhani kuwa upandishwaji wa nauli ni sawa?
 
Vuneni mlichopanda sasa. Wakati wa uchaguzi simnaweka akili uvunguni,na mnatumia masaburi kupiga kura?:lol::lol: now ndio mnawakumbuka CDM? kwani mbunge na madiwani mliowachagua wako likizo?Nyasi Mtakula na Kama vp pigeni mbizi, hii ndio CCM

Ni kwa nini mnatuhukumu wana Kigamboni? Ni kwa nini mnadhani kuwa sote na ujumla wetu kwamba tulichagua Ccm? Baada ya kutusaidia hapa jamvini sasa imekuwa kuwa sisi tulichagua Ccm ni lazima tu fill the peanch? It does bring the sense, Hapa hoja ni Chadema ije na plan B, na kuwa ninajua bei itashushwa. Sisi sote tunakumbuka bei ya sukari, mafuta, Chadema walipolisemea tu, serikali ilikuja haraka haraka na kulitolea kauli. Hebu tuache unazi wetu ndg zangu na tujadili logic
 
Ni siku tano sasa tangu lile ongezeko la nauli limeanza kutelezeka, hakika mambo yanakwenda ndivyo sivyo. kwa kawaida mtu anaweza kudhani sisi ni walalamishi tusiyopenda kuchangia pato la taifa ( cost shareling) shida inakuja pale hata pale bei ya mizigo ilipopanda,

Mfano mwenye guta ( baiskeli ya miguu mitatu sh ni 3500, sasa kiuchumi zile cost anazibeba mlaji wa bidhaa hizo, bei hizi zimepanda mara dufu.

Kwa wale wanafunzi wa vyuo(IFM, MAGOGONI , DIT, CBE Pamoja na Mwalimu nyerere memorial academy) wamepndishiwa nauli sasa ni sh 200

Nadhani sasa Chadema huu ndiyo wakati wenu wa kulisimamia Taifa kutoka kwenye uonevu wa watanzania wanyonge, semeni kitu ndugu zangu najua serikali hii itawasikia

Tumebaki mayatima hatuna hata mtetezi.

kuwa mwerevu wewe........ongezeko la sh 100 tu since 1997?? afu Chadema itakusaidia nn....iitishe maandamano..ninavyowajua mm chadema are more concerned na mambo muhim ya Taifa hili...sio wabahili wachache...unajua Tanzania nzima, ni kivuko cha kigamboni pekee chenye nauli ndogo?? fanya uchunguzi wako....yakiwa mabov yale nyie ndo wakwanza kutukana...yale yanahitaji service, mafuta, wahudumu walipwe, na baadhi ya mapato yaende serikalini wabunge wakalipwe laki 3........
 
Swala la msingi hapa si kupanda kwa bei. Kila kitu kinapanda bei na ikumbukwe kuwa nchi inajengwa na wananchi. Tatizo hapa ni hizo hela zinazokusanywa zinakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa??? CDM wanatakiwa kuibana CCM ili hizo hela zisiende kwa mafisadi. nadhani hilo ni lamsingi.
 
Wana wa kigamboni Mliona CCM ndio ya kutatua Matatio sasa Maji yamemwagika CHADEMA itafanya nini sasa?
 
kuwa mwerevu wewe........ongezeko la sh 100 tu since 1997?? afu Chadema itakusaidia nn....iitishe maandamano..ninavyowajua mm chadema are more concerned na mambo muhim ya Taifa hili...sio wabahili wachache...unajua Tanzania nzima, ni kivuko cha kigamboni pekee chenye nauli ndogo?? fanya uchunguzi wako....yakiwa mabov yale nyie ndo wakwanza kutukana...yale yanahitaji service, mafuta, wahudumu walipwe, na baadhi ya mapato yaende serikalini wabunge wakalipwe laki 3........

wewe mambo muhimu ni yapi? Ok..nadhani upeo wako na mtizamo wako ktk swala hili, nadhani pia uwelewa wa mambo kimataifa kwa bado shida kwako, sijui kama umebahatika kufika hapo Mombasa - Kenya, Nchi ya kibepari, lakini pale Likoni kivuko ni bure, eti Chadema hawana muda kulizungumzia hili, je wewe ndg yangu ndiye msemaji wa Chadema? haujui hata pato linalopatikana pale kwa siku ni sh ngapi wewe unawaunga mkono Magamba waendelee kutuumiza, ama ndg yangu unafaidika na mfumo huu?
 
Ni kwa nini mnatuhukumu wana Kigamboni? Ni kwa nini mnadhani kuwa sote na ujumla wetu kwamba tulichagua Ccm? Baada ya kutusaidia hapa jamvini sasa imekuwa kuwa sisi tulichagua Ccm ni lazima tu fill the peanch? It does bring the sense, Hapa hoja ni Chadema ije na plan B, na kuwa ninajua bei itashushwa. Sisi sote tunakumbuka bei ya sukari, mafuta, Chadema walipolisemea tu, serikali ilikuja haraka haraka na kulitolea kauli. Hebu tuache unazi wetu ndg zangu na tujadili logic

"Sisi sote
tunakumbuka bei ya sukari,
mafuta, Chadema
walipolisemea tu, serikali
ilikuja haraka haraka na
kulitolea kauli."

UMENIKUMBUSHA yule mama aliegusa upindo wa nguo ya BWANA NA MWOKOZI WANGU Yesu Kristo akapokea muujiza wake! Na nyie guseni upindo wa GWANDA mwaka 2015.
 
Ha ha ha, wamesema yametosha, ni kweli ni uchungu sisi wote tumeangalia huu mchezo wa kuigiza kwenye TV hatukuamini utakua kweli, kichefuchefu zaidi ni kumsikia magufuli eti akisema yeye amefuata sheria ya vivuko na hajali chochote, hivi kachaguliwa na sheria ama na watu? halafu anathubutu kuwaamuru wabunge wa Dar kama watoto wa shule na wao wamefyata mkia, sasa chadema wanaingiaje wakati kweli nambari one ni CCM? kuleni matunda ya utamu huo japo tunajua kuna wengi kama hawakuchagua CCM lakini wanaponzwa na kushindwa kuonyesha kutoridhika kwao, ni sawa na sisi wote 67% ya wapiga kura tuliomchagua Slaa na kumkataa kabisa huyu mwingine lakini leo hii wametunyanganya kura zetu na kutuweka chini ya utawala wa ki imla. Lakini sio haki kutegemea chadema ndio kila siku waingilie mambo ya magomvi wakati kwenye amani hamuwakumbuki. Nyie mliohamasika muanze kutoa hiyo elimu ya uraia
 
Mtavuna mlichopanda.
Umepanda bangi unataka kuvuna karafuu??
Mkome kuwachagua magamba.
 
Haaa!? yaani nyie mlikaa kwenye foleni siku nzima kuchagua viongozi wenu, leo mnaona haya kuwaeleza matatizo yenu! Mnaanza kututupia lawama sisi wa CDM, tuwasaidieje sasa!
 
Ha ha ha, wamesema yametosha, ni kweli ni uchungu sisi wote tumeangalia huu mchezo wa kuigiza kwenye TV hatukuamini utakua kweli, kichefuchefu zaidi ni kumsikia magufuli eti akisema yeye amefuata sheria ya vivuko na hajali chochote, hivi kachaguliwa na sheria ama na watu? halafu anathubutu kuwaamuru wabunge wa Dar kama watoto wa shule na wao wamefyata mkia, sasa chadema wanaingiaje wakati kweli nambari one ni CCM? kuleni matunda ya utamu huo japo tunajua kuna wengi kama hawakuchagua CCM lakini wanaponzwa na kushindwa kuonyesha kutoridhika kwao, ni sawa na sisi wote 67% ya wapiga kura tuliomchagua Slaa na kumkataa kabisa huyu mwingine lakini leo hii wametunyanganya kura zetu na kutuweka chini ya utawala wa ki imla. Lakini sio haki kutegemea chadema ndio kila siku waingilie mambo ya magomvi wakati kwenye amani hamuwakumbuki. Nyie mliohamasika muanze kutoa hiyo elimu ya uraia

mdondo, ni ngumu sisi kulianzisha, pale kivukoni wamewajaza Suma JkT na FFU unaanzaje bila Chadema? Halafu tukiandamana kuja posta, hawa ninavyowajua watatusubili tuvuke kisha utasikia huduma ya pantoon imesitishwa..., sasa tutarudije makwetu? Nakwambia ni mtihani, ndg zangu tuko tunduni, tukiandamana tu, huduma ya pantoon itakatwa sasa itakuaje jamani? Sisi hatukuichagua Ccm ndg zangu na ndiyo maana jimbo letu lilichelewa kutangazwa.
 
sh 200 mnataka chadema wawaokoe, je ikifika 500 si mtaomba msaada kutoka NATO kabisa??? kigamboni acheni ubahili, mbona sie huku tunatozwa nauli mia nne na mtu unapanda basi mbili kwenda kazini na hatujaomba kuokolewa kwa hilo?
 
mchotile, Hakika uko sawa kabisa kwani wewe umeshindwa kuelewa kuwa population ya kigamboni na hali za watu hawa wanaoishi huku ni chini kabisa, sasa wewe mchotile unaposema kuwa kivuko kijiendeshe chenyewe, unajua pato la kila siku hapa fell? ama ndugu yangu mchotile umekurupuka!! tafakari hapa ....

Umeweza kujiuliza kwa yule kibarua aliyeajiria kwa muhindi, mshahara wake ni sh 120, 000 na anakwenda kwa siku 6 kwa wiki kazini (go and return ) kwa mwezi mzima atakuwa ametumia sh 15000 kwenye kivuko tu. na hapo asiwe anaishi kibada, Geza ulole ,Vijibweni au Kisiwani. sasa mchotile ongeza 28, 000 za daladala toka hapo fell mpaka mtu huyo anapoishi. Kama atakuwa anafanyia kazi mwenge ama ubungo atakuwa na ongezeko la sh 24, 000, Jumla itakuwa sh 67, 000. ukitoa sh 120000 ambao ndiyo mshahara unamkuta mtu yule anabaki na ......... jaza mwenyewe.

Na ndiyo maana mchotile ninasema Chadema waingilie kati ili watunusuru na gharama zisizokuwa za lazima.please try to analyse the figure na usikurupuke mchotile.

mchotile vipato vyetu viko chini sana ndugu yangu.

Ndugu yangu na wana JF wote swala la kupanda kwa nauli kwa kivuko cha Kigamboni inabidi liangaliwe katika mapana. Kwanza kuna hoja ya sheria-Tanzania Ferry Act ambayo muimba ngonjera Magufuri amesikika akiimba utafikiri ni sheria 10 za Mwenyezi Mungu ambazo hazitenguliwi lakini na zenyewe ili uzielewe hazihitaji akili ya kibinadamu bali ni unyeyekevu, hofu ya Mungu, lugha iliyotumika na wakati. Nje ya hapo ni brabra. Tatizo la watawala nani kukariri vifungu vya sheria na kuwaimbia wananchi mithili ya kasuku bila tafsiri ya maana na kimantiki. CDM sio watunga sheria hiyo maana na wao ni wachache bungeni. Ili sheria ifanywe marekebisho inahitaji uungwaji mkono wa theluthi mbili za wabunge wote. Sasa katikati ya udikteita wa sheria hii CDM watawaokoaje?

Pili tattizo hili liangaliwe katika muktatadha wa CCM inayoangalia maswala katika upeo mdogo. Kwao wanafikiri kila Mtanzania anapata marupurupu kama waheshimiwa mawaziri na viongozi wa chama wanavyopata tena vikiwa ni jasho la wananchi walipa kodi. Mtu mwenye upeo hawezi akatekeleza swala kama hili ghafla bila kuwaelimisha wananchi, kuweka makundi ya kulipa kiasi tajwa kuliko wote kuwaweka kapu moja kana kwamba wana mapato sawa. Uvivu wa kufikiri, kupanga na kuchagua ni sifa ya CCM ya sasa.

Tatu tunaishi katika zama ambazo CCM haina hofu ya Mungu maana laiti ingekuwa na chembe ya hofu isingefanya inayoyafanya. Wakati viongozi wa CCM-Rais na mawaziri wanajilipa vizuri na kupata marupurupu kwa njia ya safari na vikao wananchi wanatabika. Kumbuka wahanga wa mabomu ya Mbagala na G'MBOTO, kumbuka wazee wa iliyokuwa Jumuia ya Afria Mashariki, kumbuka wastaafu wanavyoshinda hazina wakifatilia malipo yao, kumbuka walimu wanayoteseka kwa kudai malipo yao, kumbuka manesi na madaktari, hospitali wagonjwa wanne juu ya kitanda kimoja na waliokosa vitanda wanalala sakafuni. Litani ni ndefu ndugu zangu. Serikali hiyohiyo inayodai haina fedha za kuwalipa makundi haya pamoja na mengine nisiyosema inaweza kufanya sherehe ya kumbukumbu ya uhuru kwa billioni 60. Rais wake anaweza kutembelea nchi za nje kiasi cha kuitwa Vasco da Gama, anaweza kuwa na msafara wa magari 20 na kuendelea akiwa anakwenda mapumziko ya wwekend kwakwe Bagamoyo na Msata. Wabunge wanadai posho tena wanasema hazitoshi. Hii ni ukosefu wa hofu ya Mwenyezi Mungu.

Cha msingi ndugu yangu Watanzania ni kubadilika na kuhakikisha come 2015 tunachagua chama chenye kusaidai kuondoa kero hizi. CDM inaonekana ni ina mwelekeo mzuri lakini inahitaji uungwaji mkono katikati ya unyangau wa CCM. CCM inatumia vyombo ya dora JESHI, MAHAKAMA, POLISI, USALAMA WA TAIFA, TUME YA UCHAGUZI NA HAZINA kuhakikisha inashinda hata pale inapooekana dhahiri kushindwa. Tunahitaji kuunganisha nguvu, kuwashawishi wananchi waikatae CCM na siku ya kupiga kura tuchague chama makini na tufanye kama majimbo mengine tusikae mbali na vituo vya kupigia kura ili CCM wasiibe. Na kwa kuwa kuna ujanja wa kutangza kwanza kura za wabunge ili wananchi watawanyike na kuachia CCM wabadilishe kura za rais tusikubali kuwa tunatoka katika vituo vya kupigia kura mpaka pale mastokeo ya rais ayatakopjulikana na kuridhiwa katika vituo husika
 
Funzo la mjinga ni taabu na shida, kwa ujinga wenu wa kupokea kofia, pilau, khanga na tisheti mlijiona wajanja, kutaabika na shida mnazozipata ndilo funzo lenu leo, hapa chadema haina msaada wowote kwenu, endeleeni kupigika huku mkijipanga ili 2015 mfanye kweli ili msaidiwe
 
Bigaraone, inatia uchungu sana, unamkuta mtu hapa jamvini anachangia hoja hii anavyotaka, badala ya kuonesha strategies na jinsi ya kuichallenge government, badala yake anaendelea kukitetea chama cha Magamba na kusema ni sawa kupandisha nauli bila hata hoja.

Bigaraone nakushukuru kwa uchambuzi wa kina nadhani kidogo umeipunguza hasira yangu
 
Back
Top Bottom