CHADEMA: Tumeshinda

Molemo
Lini tunafanya sherehe za ushindi?

Chama
Gongo la mboto DSM....

Mkuu utafanyika mkutano mkubwa kuwahi kushuhudiwa kusgerehekea kumnyanganya adui kata 3 na kuendelea kushikilia tulizokuwa nazo.
 
CDM kimsingi imeitikisa NYINYIEM...CDM imecheza OFFENSIVE GAME while CCM imecheza DEFENSIVE GAME...so
 
Huku si kuishiwa kweli? Hivi hakuna mwana-CDM mwingine anayeweza kukisemea hiki chama?.....[/QUOTE]

Kama huelewi si vibaya kuuliza. Au hata kuuliza nako hadi ufundishwe?
 
Kwani hizo tano uchaguzi ukiopita zilikuwa za nani ritz???
Kweli wewe na nape ni vimeo,yaani ulikuwa na ng'ombe 29 katika zizi lako mwenyewe.asubuhi ukakuta wamepungua hadi 22 then unajusifu umeimarisha ulinzi kwenye zizi lako,hata ainbu hamna kabisa kujisifu wakati mnaona hali inabadilika.
Waswahili husema "bandu bandu...............?"
 
Na hata sio taratibu kama inavyodhaniwa. Iko namna hii: hata pale CCM waliponyakua kiti, bado idadi ya kura walizopata CHADEMA zimeongezeka idadi ukilinganisha na uchaguzi uliopita. Kwa hiyo grafu ya kura inapanda huku ile ya CCM ikishuka.

Igunga CCM walikumbana na moto kama huu wakajifanya hawaelewi. Kama umetoka 72% mpk 50% ni dhahiri kuwa unashuka na aliyetoka 0 hadi 46% ni dhahiri amepanda sana.

Kama unatumia akili za Zimbabwe + Zanzibar + Tanganyika = Tanzania huwezi kuyaona haya. Mwache Nape aendelee kushangilia ujinga, mdomo wake utapata breki baada ya maboresho ya daftari la wapiga kura. Kwa sasa acha wawe bize na View attachment 69759
 
Heche tuambie wapenzi wa CDM , Peza zote zilizotumika kwenye M4C na kwenye kampeni ndo matokeo ambayo tulikuwa tukiyatarajia kweli? au ndo unataka kutufunika tusione kama mnatumia fedha za walipakodi kwa manufaa ya wachache na siyo kwa manufaa ya chama?

CDM na pesa za walipa kodi wapi na wapi? Ebu fafanua; CDM inatoza kodi kwa nani? Au umekaririshwa na mabwana zako wa CCM?
 
Nimeipenda hii una watoto 29 halafu unafiwa watoto 7 ghafla. Then unafanya sherehe ya kujipongeza kwa kubakiwa na watoto 22! Akili ya Magamba.
 
Chadema kweli wanashangilia ushindi kwa kupata kata 5 kata 2 kutoka Kaskazini kwenye kambi ya Chadema. kata ya Nanjara Reheha, Rombo, na kata ya Daraja Mbili Arusha...

Chadema ngome yao ni Kaskazini, CUF, ngome ya Pemba.. Wakishinda huko huwezi kusema ni ushindi..

Chadema wametumia nguvu nyingi kuzunguka Tanzania nzima kwa miaka mitatu na operesheni za kila aina na saizi wana M4C na hatimaye wamepata kata 3 kwao ni ushindi mkubwa. Wakati kila siku wanatuaminisha humu JF kuwa CCM haipo tena sasa hizo kata 22 wamezipataje.

Chadema hongereni kwa ushindi wa kishindo Chadema ni nguvu ya umma.
 
Tatizo Daftari la wapiga kura,

kabla ya uchaguzi ccm alikuwa akitetea kata 27 Chadema 2, baada ya uchaguzi ccm kata 22 na Chadema kata 5, anagalia na uelewe nani anashuka na nani anapanda ingawa ni kwa mwendo wa taratibu lakini unaweza kuona mwelekeo.

pia hata kule amabapo ccm ameshinda angalia idadi ya kura wamepishana kwa uwiano upi, trust me mabadiliko yanakuja though ni kwa taratibu kutokana na uelewa finyu wa walio wengi.

Mkuu hizo kata Chadema walizoshinda wametumia daftari gani?
 
Nilishasema hili na nalirudia tena;bila kuweka base vijijin cdm tutakesha na hawa magamba, watu wanahitaj mwamko kaskazin tumefanikiwa ila bado kuna maeneo ya nchi bado sana, kuna maeneo mtu unakwenda watu wanakushangaa kama umetoka sayari ya mars, kazi bado sana, kijua ndo hiki tusipouanika sasa tutautwanga mbichi!

Nataka kukubaliana na hoja yako ya kuweka base vijijini lakini nataka na wewe uniambie unaposema vijijini unakusudia maeneo gani? Kigoma kaskazini, Mpanda vijijini, Biharamulo magharibi, mbozi magharibi, Bukombe, Maswa mashariki, maswa magharibi na Meatu ni mijini kwa tafsiri yako?

Kuna vitu vya msingi sana ambavyo watu hawataki kuviangalia isipokuwa wanaangalia matokeo tu ya harakaharaka. Tuachane na siasa za kwenye keyboards twende kwenye fields, sisi wengine tulishaamua kufanya siasa kwenye field kwahiyo tunafahamu uzito wa kazi tuliyonayo. Watanzania hawa ambao wamekulia chini ya mfumo wa kifisadi wa ccm sio jambo rahis kuwabadilisha "overnight" hii ni process ambayo inahitaji muda na rasilimali za kutosha kufikia malengo.

Hata mimi sijaridhika na idadi ya viti vya udiwani tulivyopata lakini nikiangalia katika "angle" nyingine naona wingi wa kura za wagombea wetu walizopata pamoja na kugubikwa na mazingira ya rushwa, vitisho, majeruhi na hila yaliyotapakaa katika chaguzi hizi.

Kama kweli wote tunasononeshwa na hali ya maisha ya mtanzania na tunataka kupata mabadiliko na tunaamini kwamba Chadema ndiyo inaweza kutukwamua hapa tulipo basi tuachane na siasa za mitandaoni twende tukafanye kazi, tujitokeze twende tukagombee nafasi mbalimbali za chama na zaidi tujitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za kitaifa.
 
Molemo,ndiyo tumeshinda,lakini ushindi ni mdogo sana kulingana na kasi ya mabadiliko,tatizo liko wapi??
Mkuu, kwani hii kasi ya mabadiliko wewe umeipima kwa kutumia nini?
Kumbuka kwamba unapokuwa na wapiga kura wale wale wa mwaka 2010, kisha ukaweza kupata kura za kuwatishia CCM, na kuwafanya CCM washinde kwa margin ya kawaida sana, huo ndio ushindi wenyewe, wanaoikubali CHADEMA wanaongezeka.

Lazima tukubali kwamba, mabadiliko hayawezi kutokea overnight, lakini pia tuache tabia ya kutaka kusheherekea ushindi tu. M4C ina muda mfupi sana tangu iasisiwe, inafanya kazi nzuri so far. Lazima kufahamu pia kwamba chaguzi hizi sio kipimo cha uimara wa vyama or CHADEMA in that case.

jambo la mwisho ni kwamba, siasa za level ya Kata ni siasa za tofauti kidogo hasa vijijini, ukilinganisha na siasa za level ya jimbo na taifa.

Hebu CCM waache Igunga na Arusha waone habari yake, Sumbawanga tayari kazi imekwisha...!!
 
Mkuu hizo kata Chadema walizoshinda wametumia daftari gani?
attachment.php
attachment.php
 
Heche tuambie wapenzi wa CDM , Peza zote zilizotumika kwenye M4C na kwenye kampeni ndo matokeo ambayo tulikuwa tukiyatarajia kweli? au ndo unataka kutufunika tusione kama mnatumia fedha za walipakodi kwa manufaa ya wachache na siyo kwa manufaa ya chama?
Mkuu operation zimefanyika na wote ni mashahidi,sasa sijui ulitaka wapiga kura wapelekewe hizo fedha kama rushwa?
 
Chadema kweli wanashangilia ushindi kwa kupata kata 5 kata 2 kutoka Kaskazini kwenye kambi ya Chadema. kata ya Nanjara Reheha, Rombo, na kata ya Daraja Mbili Arusha...

Chadema ngome yao ni Kaskazini, CUF, ngome ya Pemba.. Wakishinda huko huwezi kusema ni ushindi..

Chadema wametumia nguvu nyingi kuzunguka Tanzania nzima kwa miaka mitatu na operesheni za kila aina na saizi wana M4C na hatimaye wamepata kata 3 kwao ni ushindi mkubwa. Wakati kila siku wanatuaminisha humu JF kuwa CCM haipo tena sasa hizo kata 22 wamezipataje.

Chadema hongereni kwa ushindi wa kishindo Chadema ni nguvu ya umma.

Kama ulijaribu kujifunza hesabu japo ya kidato cha pili utakuwa unafahamu kwamba katika chaguzi hizi zilizomalizika ukichora graph kwa vyama vyote, ccm, chadema, cuf, tlp, nccr mageuzi na tadea vilivyoshiriki uchaguzi utaona upande wa Chadema imeongezeka/imepanda wakati kwenu ccm imeshuka.

Haya si mafanikio makubwa sana lakini huwezi kuyabeza kwakuwa mafanikio yameanza kuonekana. Pamoja na ukweli kwamba mmepata kata 22 kwa gharama kubwa sana ya fedha lakini kati kati ya fedha bado wananchi wameonyesha imani kubwa nasi. Jambo la muhimu ni kwamba M4C itaendelea na wananchi wataendelea kupatiwa elimu ya uraia hadi watakapoamua kwa kauli moja kwamba ccm basi, iwe ni kwa rushwa, vyombo vya dola, nec ama vitisho na vifo lakini tutawang'oa tu madarakani , na siku jizo si nyingi kwani 2015 is just around the corner!
 
Nataka kukubaliana na hoja yako ya kuweka base vijijini lakini nataka na wewe uniambie unaposema vijijini unakusudia maeneo gani? Kigoma kaskazini, Mpanda vijijini, Biharamulo magharibi, mbozi magharibi, Bukombe, Maswa mashariki, maswa magharibi na Meatu ni mijini kwa tafsiri yako?

Kuna vitu vya msingi sana ambavyo watu hawataki kuviangalia isipokuwa wanaangalia matokeo tu ya harakaharaka. Tuachane na siasa za kwenye keyboards twende kwenye fields, sisi wengine tulishaamua kufanya siasa kwenye field kwahiyo tunafahamu uzito wa kazi tuliyonayo. Watanzania hawa ambao wamekulia chini ya mfumo wa kifisadi wa ccm sio jambo rahis kuwabadilisha "overnight" hii ni process ambayo inahitaji muda na rasilimali za kutosha kufikia malengo.

Hata mimi sijaridhika na idadi ya viti vya udiwani tulivyopata lakini nikiangalia katika "angle" nyingine naona wingi wa kura za wagombea wetu walizopata pamoja na kugubikwa na mazingira ya rushwa, vitisho, majeruhi na hila yaliyotapakaa katika chaguzi hizi.

Kama kweli wote tunasononeshwa na hali ya maisha ya mtanzania na tunataka kupata mabadiliko na tunaamini kwamba Chadema ndiyo inaweza kutukwamua hapa tulipo basi tuachane na siasa za mitandaoni twende tukafanye kazi, tujitokeze twende tukagombee nafasi mbalimbali za chama na zaidi tujitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za kitaifa.

mkuu naposema vijijini namaanisha maeneo yale ambayo ccm wamejiimarisha tangu enzi za mwalimu na bado hawajapata mwamko wa mabadiliko na kama mwamko wameupata wanakuwa wagumu kuyakubali, kwamfano songea vijjn, mbozi, maeneo walipo wasukuma kwa wingi (samahan lengo si kutaja kabila ila imebidi)hawa watu ni vigumu kuwabadili inahitajika nguvu ya ziada.binafsi napinga kutumia muda mwingi kaskazin, mie nimekuwa kwenye kizaz cha changes wakati napata fahamu mama yangu alikuwa upinzan wakati huo nccr mageuz ,so kwanin tusitumie rasilimal tulizonazo kuhamasisha maeneo mengine? Popote napokwenda nahamasisha vijana kwa wazee kuhusu mabadiliko so si kwamba ni siasa za keyboard tu mkuu!
 
Back
Top Bottom