CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015

Hili ni tatizo, hasa pale chama kinapokuwa hakina mvuto unaotokana na itikadi bali masuala ya mpito (mfano ufisadi) au mvuto wa wapiga kura unaotokana na personalities za viongozi kadhaa.

Yapo masuala ambayo chadema huwa na msimamo kama chama, lakini huwa inatokea mara nyingine individual leaders wanasimamia mambo ambayo mara nyingine yanapishana na mtazamo wa chama, au wa viongozi wengine.
Mkuu Mchambuzi, kwa kinaendelea Chadama sasa, nimekukumbuka!, haswa hapo kwenye bold!.
Pasco.
 
Kilichonipa hamasa ya kuja na mjadala huu ni kauli ya Mwenyekiti wa Chadema (Taifa), Freeman Mbowe, aliyoitoa hivi karibuni ambapo alitamka (nanukuu):

Iwapo CCM itashinda uchaguzi mwaka 2015, basi nitajiuzulu Siasa.

Kuna tofauti kubwa baina ya Doing the Right Things na Doing things Right, na ili ufanikiwe, nilazima kufanya yote mawili. Chadema has been doing the right things ambayo ni kutumia kikamilifu mapungufu ya CCM kujijenga kisiasa. Lakini tatizo linakuja kwenye doing things right ambapo, mbali na kutumia mapungufu ya CCM, kuna umuhimu wa kufanyia kazi viambato (ingredients) vinavyoiwezesha CCM kuwa na mafanikio ya kisiasa. Ushindi wa Chadema utatokana na umahiri wake kufanyia kazi mambo kuu tisa kama ifuatavyo:

  1. CCM ndio iliyoongoza mageuzi ya kiuchumi (political reforms) Tanzania;
  2. Umiliki na Udhibiti wa Vyombo Vya habari;
  3. Uchumi Mkubwa Wa CCM;
  4. Ujamaa Bado ni Relevant (unaendana) na Maisha ya Wengi Vijijini;
  5. CCM imejenga Coalition na Taasisi zote nchini zenye nguvu kiuchumi, kijamii na kijeshi;
  6. Katiba ya Sasa ya nchi inaipa CCM nguvu kubwa kisiasa;
  7. Mbinu za upinzani zinazotumiwa na Chadema Hazipo Consistent na Coherent;
  8. Tanzania inakabiliwa na Udhaifu mkubwa wa Civil Society; na
  9. Political Culture ya Tanzania ina matatizo.

Ni mambo haya tisa ambayo nadhani yakifanyiwa kazi na Chadema, basi yatazidi kujenga mazingira ya utayari kwa Chadema kushika madaraka ya nchi 2015 kwani mbali ya doing the right things, pia watakuwa wametekeleza dhana ya doing things right
Mkuu Mchambuzi, thread hii is always my reference thread katika kuitathmini Chadema kuelekea 2015. As times go by, naomba ufanye upadate ya hizo hoja zipi zimefanyiwa kazi na matokeo yake ni yapi?!, zipi zimepuuzwa na what are the consequences?!, na pia kwenda a bit further kwa kueleza, kuelekea 2015, Chadema ifanye nini and if should we keep our hopes and faith with Chadema kuwa they might make it, or its dead hopes we better get prepared for the worst!.
Pasco
 
Mchambuzi kama utakumbuka tulipozungumza swala la Zitto siku moja tuu baada ya kujulikana kwamba Zitto atavuliwa madaraka nilisema kwamba kama CDM hawajakurupuka hili jambo halitakuwa na maumivi, lakini kama wamekurupuka na hawana mpango endelevu wa kuzuia hili jambo basi moto wake ni sawa na moto wa nyikani utasambaa ndani ya sekunde.

Na muda siku zote ndio muamuzi wa mwisho, leo hii tunaona kwamba CDM hawakujipanga walipo fikia maamuzi ya kumfukuza Zitto, walikulupuka matokeo yake swala la Zitto mpaka leo miezi inakwenda sita na bado halina dawa na CDM nayo inaelekea kwenye Coma.

Kinachonifanya niseme CDM inaelekea kwenye Coma ni kwa kuangalia trend, mchambuzi (analyst) yoyote anaapotazama data huwa anangalia kama data zinaonyesha uwiano (correlation), na jee uwiano huu unaweza kuwa ni mwenendo (trend), na ukiangalia chaguzi zilizopita hivi karibu utaona regression trend, japokuwa semehu hizo ni maeneo madhubuti ya CCM, lakini utaona graoh inaonyesha ni negative slope kwa chadema.

Wapo wengi wanasoma CDM sasa inastahili kuwa na hadhi ya tasisi, lakini mimi nawaonya kwa kusema sio kwa haraka haraka hivyo (not too fast), bado safari ni ndevu kwa CDM na nilazima wajitambue kwanza
 
Miaka mitatu iliyopita, kwenye bandiko #1, among other things nilijadili yafuatayo:

"Ni muhimu Chadema ikafanya marekebisho ya maana kwenye itikadi yake, kwani nje ya uchovu wa wananchi na CCM, nje ya agenda ya serikali ya CCM kutokuwa na maamuzi magumu kutatua matatizo ya nchi, na pia nje ya agenda ya ufisadi, Chadema haina ammunition ya kutosha kisera kuitoa CCM magogoni.

Hivi karibuni, chadema imekuwa ikifananishwa na TANU, jambo ambalo ni la kheri kwa Chadema. Lakini ili Chadema iwe TANU iliyokamilika, inahitaji ije na ?new and a radical orientation? inayo challenge dhana ya soko huria (hasa mapungufu yake), na ambayo inahimiza umuhimu wa umiliki wa mageuzi (ownership of reforms kwa wananchi), badala ya sasa ambapo mageuzi yanafuata mtindo wa ?Top ? Down? (badala ya bottom ? up). Ni muhimu na ni lazima wananchi wahisi kwamba kuna chama ambacho kina nia ya kuwashirikishwa katika kila hatua ya mageuzi i.e. a bottom up and participatory process (badala ya top ? down), kwani tangia mwaka 1985 Tanzania ilipoachana na mfumo wa Ujamaa, wananchi wamekuwa wanatengwa na kuachwa wapigane vikumbo kivyao vyao na nguvu za soko (market forces). Hili linahitaji kubadilika na ndio kete kuu ya Chadema 2015 itakayowaletea mafanikio yenye mashiko zaidi mbali ya vita dhidi ya ufisadi ambayo sio mwarobaini (panacea) ya matatizo ya wananchi walio vijijini.

Tukumbushane tu kwamba CCM enzi za ujamaa ilijitahidi sana kuzuia ufisadi lakini hiyo haikutosha kumletea mabadiliko mwananchi wa kijijini."

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Pia katika sehemu mbalimbali za uzi huu, nilijadili kwamba Chadema inahitaji kubadilika na kuacha kutegemea criticisms kwa serikali ya CCM kama ndio silaha kuu ya kuungwa mkono na wananchi. Nikasisitiza kwamba bila ya kubadilika katika hilo, ipo hatari mbeleni ya kukwama hasa iwapo aidha CCM itaamua kufanyia kazi mawazo na Chadema au iwapo CCM itapata mgombea ambae atabeba agenda ya upinzani.

Vile vile nilihimiza kwamba ili kukabiliana vyema na CCM, kuna haja ya Chadema haraka sana kuanzia kuunganisha sera zake zote na criticisims zake kwa CCM, na itikadi yake (ya chadema), huku pia Chadema ikianza ku - challenge itikadi ya CCM kwamba it exists in the vacuum, hivyo CCM inaendesha siasa za matukio na kufanya maamuzi yanayoendana na ?personality? iliyopo madarakani badala ya ?institution?. Nikaonya kwamba hili ni tatizo kubwa sana kwa CCM lakini pia kwa taifa kwa ujumla wake.

Leo magufuli ametangazwa mshindi na NEC (not neccesarily ameshinda kihalali) na ameanza kutekeleza hoja zile zile za upinzani. Siasa zetu upinzani zimekuwa kama zimepigwa kidogo ?shoti?, huku wananchi wengi wanaotuunga mkono wakiwa wamepigwa na butwaa. Kwa vile upinzani hatukufanya kazi nzuri ya kuwashawishi kwa njia ya itikadi, ushawishi wa njia ya ?uwajibikaji? umeacha wafuasi wengi wa upinzani njia panda. Kuna haja ya Upinzani kuzingatia umuhimu wa kuunganisha sera zake, misimamo yake bungeni dhidi ya serikali with their ideological position (itikadi ya upinzani).

Nje ya hapo, huko mbeleni itakuwa vigumu kwa wananchi kutofautisha baina ya CCM inayowajibika kwa wananchi na Upinzani unaohimiza juu ya umuhimu wa serikali kuwajibika kwa wananchi.

Nawasilisha.
 
"Iwapo CCM itashinda uchaguzi mwaka 2015, basi nitajiuzulu Siasa."-Mbowe au wewe??

Mchambuzi nasikia hata form ya ubunge ulishindwa kurudisha unabaki kugombana na akina zitto mitandaoni??
 
mmetengeneza matabaka jukwaani, mmefukuza watu kwa kuwatenga,mmebaki wewe na nguruvi kujaza server ambazo hazina wachangiaji simply kwa sababu mli choose side.......mkakataa kazi ya kuwa analysts mkaruhusu mahaba yatawale! mmepotea, hamna nguvu tena, hamna la kusema...wakati yaka mengi mno
 
Mahaba kwa zito yatakuua
 
Mchambuzi.

Unasema kauli ya Mbowe ndiyo iliyokupa hamasa hii kauli.

"Iwapo CCM itashinda uchaguzi mwaka 2015, basi nitajiuzulu Siasa".

Vipi Mbowe kajiuzulu?

Naona umebakia kuwa mshauri wa Pro-Chadema.

Cc; Waberoya.
 
Last edited by a moderator:
?Iwapo CCM itashinda uchaguzi mwaka 2015, basi nitajiuzulu Siasa.?-Mbowe au wewe??

Mchambuzi nasikia hata form ya ubunge ulishindwa kurudisha unabaki kugombana na akina zitto mitandaoni??

Tatizo nini kama mwisho wa siku jimbo tumewapokonya ccm? ACT mna majimbo mangapi ukiacha la Kigoma mjini mlilopewa na CCM?
 
mmetengeneza matabaka jukwaani, mmefukuza watu kwa kuwatenga,mmebaki wewe na @Nguruvi kujaza server ambazo hazina wachangiaji simply kwa sababu mli choose side.......mkakataa kazi ya kuwa analysts mkaruhusu mahaba yatawale! mmepotea, hamna nguvu tena, hamna la kusema...wakati yaka mengi mno
Nani anaweza ,kufukuzwa katika jukwaa!
Kwani kuna ulazima kusoma tunachoandika.

Ninakuhakikishia wewe ni msomaji mzuri sana
Unaposemawatu hawachangii wakati unachangia, unavunja watu mbavu.Kwani wewesiyo mtu!

Hili ni jukwaa huru, kuna wanasoma,wanaochangia na wasiosoma.
Nawashukurusana wale wanaotutia moyo kupitia PM.

Kumpa mtukidogo ulicho nacho akashukuru ni Baraka.

Pili, hatuandiki kwa dhiki au kulamba watu miguu .
Tunaandika kama sehemu ya maisha yetuambayo huna sababu ya kuhoji au kujua

Hasirazako ni kutokana na Mh wa Kigomakuwekwa kati na nje ya wakati.

Kama umeamuakutualika tutoke likizo, hewala tupo hapa

Sikiliza, kauli ya Mh wa Kigoma kuhusu mikoa inayopendelewa na kuchangia kidogo tuliikomalia kwa kumkanya ni hatari. Nadhani umeona hatari tuiyoonya inavyotokea.

Siasa zaukanda na hasa kushambulia mikoa fulani ni uasisi wa huyu mh

Mbegu yakibaguzi na ubinafsi aliyopipanda imeachanua.

CCMwalipata hoja na mwisho wanamlipafadhila za kutulia mjengoni.
Ametuliaje baada ya kuchonganisha taifa?

Tuliposimamana kusema ule ulikuwa ni ujinga, wengihawakutuelewa.

Leo watuwanaona ukweli na wanatuelewa.
Na kwa jinsi gani umma umetuelewa ni jinsi alivyofutika katikamaongezi ya siasa za nchi hii.

Wengiwanamuona ni mwanasiasa muflsi

Kaendabungeni. kaamua kulamba viatu vya watawala badala ya kukemea ubabe.
Kasifiwa ili apewekamati.

Inafikirisha,hivi mtu anayewezaje kuridhia kusifiwana CCM.

CCMwalikataa kutumia jina lao katikauchaguzi, leo wanawezaje kumsifia mtu!

Walikataa jina lao lisinasibishwe na mtu leowanamsifiaje mtu

Kwaviileumetualika, tuanzie hapa kwa wikikadhaa!

O.P...............
 
mmh, unasema???

angalia matokeo ya urais jimbo la Lissu utachoka mkuu!

mshinde na wabunge 35?? u must be kidding

Matokeo urais jimbo la mwana mazingira Makamba ndio utachoka kabisa. Ni maigizo tu.

Wabunge 35? ACTCCM mlijitapa kuweka wagombea wengi kuliko chadema, Wapo bungeni? Zitto kama sio ccm kumpigia debe plus siasa za ubaguzi, asingepita.

Maeneo mengi ukawa Kura za ubunge zilichakachuliwa. Kesi nyingi zipo mahakamani. Lakini pia Kura za Urais, yapo maeneo walimpigia Lowassa Kura lakini kumpigia mgombea wa ccm ubunge. Kura za Urais hazijawahi kuwa na uhusiano wa Moja kwa moja na ubunge nchini in a general sense. Rudi kasome historia.

Mwisho:
Chama mama cha ACT, yani Chama cha mapinduzi (CCM) hakikushinda Urais. Kiliiba Kura kwa kuweka wataalam wake kutoka china, india, kenya... katika maeneo kadhaa to hack mtandao uliokuwa unatuma matokeo NEC. Wapo waliokuwepo double tree, mlimani city villas etc. Huo ndio ukweli!
 
same old fckn song

EL amekuwa miaka yote CCM
Sumaye PM miaka kumi na master minder
kingunge muiba kura mkuu wa CCM

EL ndiye kingmaker wa JK!

Hiwezekani hawa watu hawakujua mchezo mchafu, aidha wao nao walipanga kufanya hivyo, au wamezidiwa ujanja au wameshindwa kihalali?

2010 slaa alilia same faulo.......je waliokuwa timu ya ushindi ya JK ni akina nani? kama sio EL,sumaye na kingunge??

so aidha 2010 slaa alikuwa mwongo.......kama likuwa mkweli waliohusika kwenye huo wizi ndio hamo mliokuwa nao chadema

ebu uwe unafikiria basi mkuu, tutakusaidia mpaka lini?
 
Matokeo urais jimbo la mwana mazingira Makamba ndio utachoka kabisa. Ni maigizo tu.

Wabunge 35? ACTCCM mlijitapa kuweka wagombea wengi kuliko chadema, Wapo bungeni? Zitto kama sio ccm kumpigia debe plus siasa za ubaguzi, asingepita.

Maeneo mengi ukawa Kura za ubunge zilichakachuliwa. Kesi nyingi zipo mahakamani. Lakini pia Kura za Urais, yapo maeneo walimpigia Lowassa Kura lakini kumpigia mgombea wa ccm ubunge. Kura za Urais hazijawahi kuwa na uhusiano wa Moja kwa moja na ubunge nchini in a general sense. Rudi kasome historia.

Mwisho:
Chama mama cha ACT, yani Chama cha mapinduzi (CCM) hakikushinda Urais. Kiliiba Kura kwa kuweka wataalam wake kutoka china, india, kenya... katika maeneo kadhaa to hack mtandao uliokuwa unatuma matokeo NEC. Wapo waliokuwepo double tree, mlimani city villas etc. Huo ndio ukweli!

ona aibu mkuu

walid kaburu kamuulize kule.....kwa hiyo alikuwa boya?

unaaibika mkuu, achana na zitto na ACT

kwa kifupi hauna address wala any value kwenye siasa za kushindana na akina zitto

kama ulishindwa tu kurudisha form, unachoweza kufanya ni nini kama sio hatred??

call zitto any name, others they know him differently....very well, and their love toward zitto is so genuine!

utakufa kwa chuki

kwa akili hizi ndio ulikuwa unajadili utayari wa kuchukua madaraka? seriously?

wewe tu kuwapo chadema ndio kushindwa kwa chadema

I mean moja ya failure ya chadema ni kuwa na watu kama wewe ambao individually wameshindwa kila kitu, kuanzia shule, maisha, dini, mahusiano, familia na ulichobakiza ni kunyoosha vidole

kwa akili zako utasema CDM wameshindwa kwa sababu ya ACT, nakuangalia tu, utasema sasa hivi
 
Kuna nyuzi ukizipitia na kuangalia watu walisema nini na nini kinatokea, utakubaliana na mimi Chadema bado sana!.

Pasco
 
Back
Top Bottom