Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
- Thread starter
- #81
Mkuu wakati mwingine tunawalenga sana individuals na kuvilenga sana vyama. Kuna wakati naamini kuwa weakness kubwa tuliyonayo haiko kwenye individuals iko kwenye systems na institution. Ninaposema hili maana yangu ni kuwa hatuna mfumo (haupo) unaoweza kufanya mambo hapa Tanzania yaende, na hatuna institutions zinazoweza kutekeleza mambo.
Ukiangalia hapa Tanzania unaweza kuona kama Rais mzuri mambo mengi yanaenda vizuri, na kama si mzuri mambo mengi yanaenda hovyo. Ukiangalia wizara ni hivyo hivyo, kama waziri ni mzuri wizara inaenda vizuri na kama waziri si mzuri wizara inaenda hovyo...fuata utaratibu huo hadi ngazi ya chini kabisa.
Jaribu kuuangalia suala la msongamano wa magari hapa Dar, msongamano unaendelea kuwepo tangu JK aingine madarakani hakuna kilichofanyika (zaidi ya mipango na hatua ndogo ambavyo havitekelezeki), Angalia baraza la mawaziri limefanya nini, wizara ya ujenzi imefanya nini, polisi wa usalama barabarani wamefanya nini. Zaidi ya maneno hakuna chochote significant kimefanyika.
Au jaribu kuangalia akikatwa mwizi haadi kufikishwa mahakamani kusimewa mashatki na keshi yake kutolewa huku, utaona kuwa kuna mambo mengi sana hapo katikati hayafanyiki na hata kama yanafanyika ni kwa mwendo wa chura na kwa ubabaishaji mwingi.
Angalia kati ya serikali kuu, bunge, mahakama , civil society na media. Karibu kila moja haifanyi kazi inayostahili na kwa ufanisi, serikali kuu haiko united as one institution na haijui priorities zake ni zipi, bunge nalo liko kwenye sura ya kamati ya CCM zaidi kuliko bunge, mahakama ndio usiseme haina sautikabisa wakati kisheria ndio inatakiwa kuwa na sauti, civil society ndio njaa tu wao ni kama watu wanaoganga njaa, hakuna issue ya maana ambayo wameweza kupush kwa interest ya Tanzania, sana sana wanapush mambo ambayo hayana umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya Tanzania, media ndio kabisa....apart from hapa JF na gazeti moja au mawili, majority ya waandishi na watangazaji ni vilaza na vibonde, wamebaki kufanya kazi ya entertainment zaidi ya kuelimisha na kuongopea watu.
Kwa hiyo naweza kusema pamoja na kuwa tunsema chama hiki kina itikadi hiki hakina, au huyu ni mgombea mzuri au yule si mgombea mzuri...the bottom line ni kwamba ni lazima tuweze kuwa na instututions zinazokuwa imara bila kujali nani anakuja nani anatoka.
Civilized states zote zina idara zinazojua majukumu yake, na sio kufanya kazi za zimamoto kwa amri ya katibu mkuu, mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya. hata mkuu wa mkoa akifanya fyongo anachukuliwa hatua mwa mujibu wa rules na regulations zilizowekwa kwa taasisi ile kufanya kazi.
Upo sahihi kabisa juu ya hili, especially umuhimu wa institutions in development; institutions zinaweka framework kwa ajili ya shughuli zote za uchumi katika taifa; tukiwa na institutions nzuri, it means kuna mazingira mazuri ya ku promote economic activity kwa mfano wananchi/wafanyakazi wanakuwa na motivation ya kufanya kazi, inventiveness n.k, lakini kama kuna bad institutions, nothing moves; Kuna njia nyingi za kupima institutional quality in a country, ikiwa ni pamoja na uwepo wa rule of law na pia democracy;
Lakini tukija kwenye suala la watu (people), hawa bado ni muhimu sana kwani bila uwepo wa watu wenye ari, mwamko, uzalendo n.k, institutions alone sio lolote;