Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,197
Mkuu FortJeasus kwanza inabidi tuangalie maana rahisi ya neno itikadi kwenye muktadha wa siasa, na hasa siasa za Tanzania. Kwa ufupi inaweza kuwa mkusanyiko wa imani, nadharia, mawazo na misimamo ya chama kuhusu mambo fulani.
Pili tuangalie Tanzania iko katika mazingira gani, na tuangalie ni vipi hizo itikadi zinaweza kutekelezwa.
Nikianza kuangalia itikadi(ideology) ya CCM ya ujamaa na kijitegemea, ambayo wengi tunaifahamu, kimsingi haipo. Imebaki tu kwenye vitabu, lakini kwa uhalisia ni kuwa haitekelezwi na haifuatwi hata kidogo, hata ukiangalia mwelekeo wa sasa hakuna dalili inayoonesha kuwa CCM itaelekea huko siku moja. Remnants wa itikadi hiyo kama Kina Mzee Kingunge kwa sasa ni makabaila wakubwa kama si mabepari. Uki-unpack the whole ideology na kuchambua element moja moja huwezi kuona hata kidogo kuwa CCM inatekeleza itikadi ya Ujamaa na kujitegemea. Kwa sasa kwenye aspect nyingi sana tunaona Tanzania inaegeemea zaidi kwenye ubepari.
Hata tukiangalia sera(policies) za CCM za sasa na election manifesto, hata ukiangalia ile vision 2025 which is 'implemented' based on ideology and policies of CCM, haina element zinazoweza kumconvince mtu mwenye akili kuwa tunaekelea kwenye ujamaa na kujitegemea. Zote zinalenga zaidi kwenye utengano, ubepari na kujitajirisha. Kwa maoni yangu, nikiangalia nini kipo kwenye katiba ya chama, ilani yake ya uchaguzi na kile kinachofanyika on the ground naweza kusema sielewi itikadi ya CCM ni ipi. Ujamaa ni kujitegemea? ubepari na kujitajirisha? ufisadi, fitna nk hakuna unachoweza kukiona wazi. Hakuna anayeweza kusema sasa hivi chama cha mapinduzi kinafanya kazi hii. Nina hakika leo ukimuuliza Nape hili swali hana jibu, leave Nape aside, muulize Mukama pia hana jibu.
Tukiangalia CHADEMA wao at least wako more ralistic, kwa kuwa wanaangalia mazingira ya sasa wanako-operate. Hata kama wana sera au itikadi, hawana uwanja wa kuzitekeleza. Majimboni ambako wana wabunge wawili au watatu bado hawana uwezo wa kufanya tofauti na kinachofanywa na wabunge wa CCM. Sidhani kama mkazi wa kinondoni ana tofauti na mkazi wa Ubungo kunakota na kuwa na wabunge tofauti. Sasa hivi hata kama kuna kitu kinaitwa sera ya Chadema naweza kusema bado hatuwezi kukiona wazi hadi washike rungu. Kidogo tumeona bungeni kwenye suala la ufisadi, wao hawaungi mkono ufisadi kama CCM (japo sera na itikadi zake zinapinga kivitendo wanaruhusu). So if there is such a thing as CDM ideology, we have to wait and see what is it.
Inawezekana Chadema na CCM wana maoni tofauti kuhusu mambo madogo madogo ambayo haya umuhimu sana katika mambo ya maendeleo na usalama wa nchi. Hayo kimsingi ni kwa ajili ya kukusanya wapiga kura tu. Lakini kuna makubwa kama defence, economy national unity , integration, etc huko ndio tunataka kujua itikadi hasa ya Chadema. Ya CCM tumeiona nadhani wengi hapa JF tunajua kuwa haifai, kwa sababu matokeo yake yameonekana.
Kulingana na hali ya sasa ya dunia, chama chochote makini kitafuata sera inayolenga kuinufaisha nchi katika mazigira ya sasa, ndani na nje, kitafuata sera inayoendana na upepo unaovuma. Kwa hiyo kikiwa madarakani ndio tutaweza kujua ndani kikoje.
Sasa hivi Chadema wamevaa Gwanda hatujui wakivua gwanda ndani kuna nini, CCM ingawa wamevaa Gamba tayari tumeona ndani kuna nini. Kwa hiyo bado hatuwezi kusema wazi ideology ya CHADEMA ikoje, hadi pale watakaoweza kuitekeleza, naamini kuwa haitakuwa tofauti na itikadi halisi ya CCM (sio iliyoandikwa kwenye mnakaratasi na inayoimbwa).
I stand to be corrected.

Last edited by a moderator: