CHADEMA, tuelimisheni nini hasa Lissu alikusudia kukisema!

Lissu alimaanisha hiki;

MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Mheshimiwa Spika,
Tarehe 11 Machi 2011, Serikali ilichapisha Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba ya mwaka 2011 (The Constitutional Review Bill, 2011) katika Gazeti la Serikali la tarehe hiyo. Muswada huo uliletwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge hili tukufu kwa Hati ya Dharura. Hata hivyo, baada ya upinzani mkubwa dhidi ya Muswada huo kujitokeza karibu nchi nzima, Serikali ililazimika kuundoa katika ratiba ya shughuli za Bunge kwa maelezo kwamba itaufanyia marekebisho na kuurudisha Bungeni katika Mkutano huu wa Bunge. Hata hivyo, licha ya Muswada huo kuwepo katika ratiba ya awali ya shughuli za Bunge, baadae ratiba hiyo ilifanyiwa mabadiliko kwa kuuondoa Muswada kwenye ratiba hiyo.

Mheshimiwa Spika,
Dana dana yote hii inaonyesha jinsi suala la utaratibu wa namna ya kupata Katiba mpya kwa ajili ya nchi yetu lilivyo muhimu. Tofauti na kauli za awali za Serikali, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba sheria inayoweka utaratibu wa kupatikana kwa Katiba mpya ina umuhimu mkubwa wa karibu sawa na Katiba yenyewe. Utaratibu wa kidemokrasia, shirikishi wa makundi makuu ya kijamii na ulio wazi utapelekea nchi yetu kuwa na Katiba mpya ambayo sisi wote tutaweza kujivunia. Kwa upande mwingine, utaratibu uliojaa ukiritimba wa kirasimu, unaohodhiwa na watu au taasisi chache na unaofanyika gizani na/au kwa siri utaleta Katiba mpya kwa jina tu. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba katika hali ya sasa ya kisiasa ya nchi yetu, utaratibu huu hauwezi kukubalika na wananchi walio wengi na utasababisha machafuko makubwa ya kisiasa na kijamii.

Kwa bahati mbaya, Mheshimiwa Spika, Serikali inaelekea kufikiri kwamba inaweza kuwalazimisha Watanzania kukubali utaratibu wa aina hiyo. Hii ni kwa sababu Kambi Rasmi ya Upinzani imepata nakala ya Rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba, 2011 iliyofanyiwa marekebisho ambayo inatazamiwa kuletwa Bungeni kwa tarehe ambayo haijulikani bado. Rasimu ya Muswada huu inathibitisha kwamba Serikali haina nia yoyote ya kuweka utaratibu wa kidemokrasia, ulio shirikishi wa makundi makuu ya kijamii na kisiasa katika kupata Katiba Mpya. Kwa upande mwingine, Rasimu inapendekeza utaratibu wa kupata Katiba Mpya uliojaa urasimu na unaoendeleza hodhi ya Urais wa Kifalme ambayo ndiyo imekuwa hulka kuu ya mfumo wetu wa kikatiba na kisiasa.

Mheshimiwa Spika,
Rasimu ya Muswada inapendekeza kumpa mamlaka makubwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mashauriano na/au makubaliano na Rais wa Zanzibar ya kuteua Tume ya Kupitia Katiba yenye wajumbe wasiozidi thelathini. Aidha, Rasimu ya Muswada inapendekeza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mashauriano na/au makubaliano na Rais wa Zanzibar ataipatia Tume hiyo hadidu za rejea na muda wa kumaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa. Utaratibu huo huo wa mashauriano na makubaliano utatumika katika uteuzi wa Katibu wa Tume; na Sekretariati ya Tume ambayo itateuliwa na Waziri wa Katiba na Sheria kwa makubaliano na Waziri mwenzake wa Zanzibar. Katibu na wajumbe wa Sekretariati wanatakiwa kuwa watumishi wa umma ambao, hata kwa mujibu wa utaratibu wa sasa wa kikatiba, wanawajibika kwa Rais.

Mheshimiwa Spika,
Rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba inaendeleza pia mfumo wa Urais wa Kifalme kwa mapendekezo juu ya uwasilishaji wa taarifa ya Tume. Hapa inapendekezwa kwamba Tume ya Mapitio ya Katiba itawasilisha taarifa yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar. Aidha, "baada ya mashauriano na makubaliano na Rais wa Zanzibar na baada ya kumalizika kwa taratibu za ndani zinazohusu utungaji wa sera, Rais atamwelekeza Waziri kuwasilisha Muswada wa Katiba katika Bunge la Katiba kwa ajili ya kupitishwa kwa vifungu vya Katiba." Pendekezo hili ni la hatari kubwa. Kwanza, ‘kumalizika kwa taratibu za ndani zinazohusu utungaji wa sera' maana yake ni kwamba mpaka Baraza la Mawaziri liridhie Muswada huo ndio utapelekwa kwenye Bunge la Katiba! Kwa mujibu wa Katiba, wajumbe wote wa Baraza la Mawaziri ni wateuliwa wa Rais.

Mheshimiwa Spika,
Mfumo wa Urais wa Kifalme pia unaonekana katika mapendekezo yanayohusu Baraza la Katiba. Kwa mujibu wa kifungu cha 20 cha Rasimu ya Muswada, Rais – kwa makubaliano na Rais wa Zanzibar – na baada ya kushauriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na yule wa Zanzibar ataunda Baraza la Katiba na kuteua wajumbe wake. Baada ya kuundwa, Baraza la Katiba litateua Spika na Naibu Spika ambao watatakiwa kutoka katika sehemu tofauti za Jamhuri ya Muungano. Spika na Naibu Spika watatakiwa kula kiapo mbele ya Makatibu wa Baraza la Katiba ambao ni Katibu wa Bunge wa sasa na Katibu wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wa sasa. Wote hawa, kwa mujibu wa Katiba na Katiba ya Zanzibar ya 1984, ni wateuliwa wa Rais na/au wa Rais wa Zanzibar na wanatakiwa kula kiapo kwa Rais!

Mheshimiwa Spika, Rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba inapendekeza kwamba kazi ya Baraza la Katiba iwe moja tu: kutunga Katiba Mpya na mambo yanayohusiana nayo. Baada ya kufanya kazi hiyo, Baraza litakuwa limejifuta lenyewe, ijapokuwa kujifuta huko kwa Baraza hakutamzuia Rais kuliunda upya Baraza siku za baadae likiwa na wajumbe wale wale kwa lengo la kufanya mabadiliko ya Rasimu ya Katiba Mpya kabla Rasimu hiyo haijapitishwa! Rasimu inapendekeza kwamba ili Katiba Mpya ipitishwe ni lazima ipate ridhaa ya theluthi mbili ya wajumbe wote wanaotoka Tanzania Bara na idadi hiyo hiyo ya wajumbe wanaotoka Tanzania Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, Rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba inapendekeza pia kwamba Katiba Mpya ipatiwe nguvu na uhalali wa kisheria kwa kupitia kura ya maoni itakayoratibiwa na kusimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Tume hizi mbili – kwa mashauriano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar - ndizo zitakazotengeneza swali litakaloulizwa kwenye kura ya maoni. Utaratibu utakaotumika katika kura ya maoni ni ule unaotumika katika chaguzi za kawaida katika nchi yetu, yaani Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343, Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar, 1984. Ijapokuwa kura ya maoni itaamuliwa kwa wingi wa wapiga kura (simple majority), Rasimu ya Muswada inapendekeza kwamba ili kura hiyo iwe halali ni lazima angalau 65% ya wapiga kura wote waliojiandikisha Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar washiriki katika kupiga kura. Rasimu ya Muswada inapendekeza kwamba Rais ndiye atakayeamua, kwa namna atakavyoona inafaa, kuanza kutumika kwa Katiba Mpya!

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa kauli rasmi kama Rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba ndio inawakilisha msimamo wa Serikali juu ya mchakato wa kutungwa kwa Katiba Mpya. Kama ni hivyo, basi Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapenda kuweka wazi msimamo wake Muswada huu haukubaliki hata kidogo. Kwanza, Kambi Rasmi ya Upinzani haikubaliani na mamlaka makubwa yanayopendekezwa kupewa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar chini ya Muswada huu. Urais wa Kifalme kama kanuni kuu ya kikatiba na kisiasa ndiyo ambayo imetufikisha hapa tulipo leo: taifa lenye wananchi maskini, lililojaa ufisadi, lisilojali demokrasia na haki za binadamu na lenye kuongozwa na watawala wasiowajibika kwa wananchi au kwa vyombo vya uwakilishi vya wananchi. Mfumo huu hauwezi kutumika tena kulipatia taifa letu Katiba Mpya ya kidemokrasia itakayokidhi mahitaji ya karne hii na nyingine zijazo.

Pili, Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya Rasimu ya Muswada hayakubaliki kwa sababu yanaweka mchakato wa Katiba Mpya kwenye huruma na/au fadhila ya Rais wa Zanzibar na siasa za Zanzibar kwa ujumla. Kwa mapendekezo haya, Rais wa Zanzibar asipokubaliana na jambo lolote linalohitaji ridhaa yake basi mchakato mzima utasimama au kusitishwa. Aidha, endapo katika kura ya maoni inayopendekezwa, theluthi mbili ya Wazanzibari hawatakubaliana na Katiba Mpya basi Katiba hiyo haitapitishwa hata kama inakubaliwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa Tanzania Bara. Mustakbala wa taifa letu hauwezi kuwekwa tena rehani kwenye siasa za Zanzibar na kwenye matakwa ya Wazanzibari kwa kiasi hicho. Kuhusiana na jambo hili, Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kwamba Rais wa Zanzibar ahusishwe tu katika masuala ya kikatiba ambayo ni ya Muungano tu. Nje ya masuala hayo, Rais wa Zanzibar hana sababu yoyote ya kuhusishwa na mchakato wa kikatiba unaohusu mambo ya Tanzania Bara.

Aidha, wajumbe wa Tume ya Mapitio ya Katiba ambao watatoka Zanzibar wahusike tu katika mchakato wa masuala ya kikatiba ambayo ni ya Muungano tu. Vile vile, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza wananchi wa Zanzibar washiriki katika kura ya maoni inayohusu mfumo mpya wa Muungano tu. Hii ndio kusema kwamba, kama vile ambavyo viongozi, wawakilishi na wananchi wa Tanzania Bara hawajashirikishwa katika mchakato wa kikatiba wa Zanzibar kwa sababu ulihusu mambo yasiyokuwa ya Muungano, vivyo hivyo viongozi, wawakilishi na wananchi wa Zanzibar wasishiriki katika mchakato wa kikatiba wa mambo yasiyokuwa ya kikatiba kwa upande wa Tanzania Bara.

Mheshimiwa Spika, Kwa kuzingatia historia halisi ya Muungano wetu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba wakati umefika kwa wananchi wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kuamua - kwa mara ya kwanza katika historia yetu na kwa uhuru kabisa - kama wanataka kuendelea kuwa na Muungano na wa aina gani. Hili halijawahi kufanyika na ndio maana Muungano umeendelea kuwa kero kwa wananchi wengi wa nchi hizi mbili. Kambi Rasmi ya Upinzani inaamini kwamba suala la ridhaa ya wananchi ni la umuhimu mkubwa na ni lazima lishughulikiwe kwanza kabla ya mchakato unaopendekezwa na Rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba kuanza na/au kupitishwa.

Aidha, kwa kuzingatia historia yetu halisi ya kikatiba na kisiasa, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza mfumo mpya wa kutunga Katiba Mpya ambao hautatawaliwa na kivuli kirefu cha Urais wa Kifalme. Kikubwa hapa ni kwamba, badala ya wajumbe wa Tume ya Katiba kuteuliwa na Rais kama inavyopendekezwa na Rasimu ya Muswada, wajumbe hao wateuliwe kutokana na mapendekezo ya vyama vya siasa, hasa hasa vile ambavyo vina uwakilishi Bungeni, taasisi zisizokuwa za kiserikali na za kitaaluma, makundi maalum ya kijamii pamoja na Serikali yenyewe. Aidha, badala ya Sekretariati ya Tume kujazwa warasimu wa Serikali ambao ni wateuliwa wa Rais kama inavyopendekezwa, Sekretariati hiyo itokane na wajumbe watakaoteuliwa na Tume yenyewe na ambao watawajibika moja kwa moja kwa Tume yenyewe badala ya kuwajibika kwa Rais kama ilivyo sasa.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haina imani, sio tu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, bali pia na mfumo mzima wa kisheria na kitaasisi unaoendesha chaguzi za nchi yetu. Mfumo huu na watendaji wake wameonyesha wazi kutokuwa huru na kutumiwa na Chama cha Mapinduzi kuchakachua matokeo ya chaguzi mbali mbali hapa nchini. Kwa maana hiyo, Tume ya Uchaguzi ya Taifa, na ile ya Zanzibar, haiwezi kuachiwa jukumu kubwa la kuendesha kura ya maoni kwa ajili ya kupata Katiba Mpya. Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kwamba Serikali ilete bungeni muswada wa mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba na ya sheria husika za uchaguzi kwa lengo la kuiunda upya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha inasimamia zoezi la kura ya maoni kwa uhuru na bila upendeleo kwa chama tawala. Muswada huu vile vile utatoa fursa kwa Bunge hili tukufu kutunga vifungu vinavyowezesha Katiba Mpya kutungwa ambavyo havipo kwa Katiba ya sasa. Kutofanya marekebisho haya kutafanya sheria yoyote ya kuweka utaratibu wa kupata Katiba Mpya kuwa batili kwa kwenda kinyume na matakwa ya Katiba ya sasa ambayo hairuhusu Katiba Mpya kutungwa ila inaruhusu tu marekebisho ya Katiba yenyewe.

 
kweli kwa mtu makini hawezi kushangaa ukweli na hali halisi ya mambo yanavyotakiwa kufanyika hapa Tanzania. Kisheria Muungano wetu ni kama ni kidonda ambacho hakijapata tiba sahihi coz kuna upande wanalalamika zaidi ya wengine. Tatizo ni kutokuonekana kwa mambo ya Tanzania Bara ktk Muungano, lakini hili halizuii hoja kuwa ni kweli kuna mambo wazanzibar hawatakiwi kuamua juu ya mambo ya watu wa bara,,, thats what Lissu alijaribu kusema ktk hotuba yake.
Kama itatokea wazanzibar wataruhusiwa kujadili kila kitu basi wabara tutakuwa zuzu wa kujua mambo yatu,,hoja kuwa hakuna serikali ya Tanganika haitoi mwanya kwa Wazanzibar pekee kuwa na haki kila jambo ktk Muungano na wakati huo huo mambo ya Z'bar wanajadili wakiwa peke yao. Huo utakuwa ni uonevu mkubwa ambao unatumika vibaya kutokana na udhaifu wa sheria na mkataba wa Hati ya Muungano.
Kuna haja ya kuweka mipaka kwa uwazi kabisa kuwa Wazanzaibar na Wabara wajadili mambo kadhaa tuu katika Muungano na yaliyobaki yajadiliwe na serikali Zanzibar pekee while yale ya bara exclusively yawe chini ya Serikali ya Muungano bila kuingiliana na mambo ya Zanzibar.
Mkuu umeongea point nzuri - Huu muungano una udhaifu mkubwa yaani eti kwa sababu wazanzibari ni wachache na kwa kuogopa sisi wa bara tutawameza ndani ya muungano basi wawe na serikali yao na pili wawepo kwenye serikali ya muungano kujadili mambo yetu. in this case watanganyika hatuna mambo yetu binafsi ambayo tunaweza kuyajadili ya kuyatolea uamuzi bila wazanzibar. Na kukuhakikishia hilo waziri wa mambo ya ndani ambaye ni mzanzibar hupo hapa na anafanya kazi mbona hakuna hata mtanzania bara hata mmoja kuwa waziri au mwakilishi katika baraza la mapinduzi? kuna dhambi ipi wakati sisi ni wamoja?Mbona wanangangania mafuta ya nchini kwao ni ya wazanzibar pekee huo nao si ubaguzi tena wa hadharani? je huu umoja upo wapii?

Hata juzi wakati wanarekebisha katiba yao hakuna wa bara wowote walioshiriki - ya kwao yawe ya kwao then ya kwetu wao wawemo ndo maana tunasema muungano wa Tanganyika + Zanzibar = Tanzania + Zanzibar. Huu muungano muundo wake si sawa wananchi wenzangu. kuhoji chochote juu ya muungano huu si dhambi.

Tunadanganyana ndugu zangu, ni sawa na kuwa katika ndoa wakati mnalala vyumba tofauti, mkitoka nje mnacheka mkiwa ndani kila mtu kivyake na madukuduku kibao moyoni.
 
Narudia tena haiwezekani vitu viwili vikaungana halafu vikatoa vitu viwili! Tatizo ndipo lilipoanzia,sasa kwa mfano eti 2/3 ya wanzibar wakiigomea katiba basi haitapita! Hata kama nusu ya wa Tanganyika watakuwa wamekubali. Lakini zanzibar ingekuwa ni kanda tu yenye mikoa labda miwili ndani ya muungano tukawa na serikali moja haya tusingeyajadiri.
 
Mbunge alikuwa akiongea kwa hisia na sio akili, ukimsikiliza Lissu unafurahi maana kuna mambo nilitamani kuyasikia na kupata nafasi ya kuyasema na Mungu mkubwa nimelipata toka kwa kaka yangu msomi Lissu.Mungu amjalie Nguvu na baraka tele, miaka mingi yenye heri duniani.
 
Pole sn mh Lissu kwa ma2c ya mzenji huyo
Bt nakuamin ulitendea haki bajeti yako
Jipe pole wewe mwenyewe, Lissu ni mwanasheria na mbunge hivyo alikuwa antimiza wajibu wake. Anajua na ana uhakika wa yale aliyoyasema juu ya katiba na muundo wa muungano wetu. Leo hii mtambishia na kumbeza Lissu lakini nina uhakika 100% msipoyafuata haya mtafikia pahala mtakwama tu, tena si mbali hii migongano itaanzia kwenye hiyo katiba yenu mpya mnayoitaka wakati ni waoga kuongea wazi wazi -- FUNGUKENI WATANGANYIKA.
 
Narudia tena haiwezekani vitu viwili vikaungana halafu vikatoa vitu viwili! Tatizo ndipo lilipoanzia,sasa kwa mfano eti 2/3 ya wanzibar wakiigomea katiba basi haitapita! Hata kama nusu ya wa Tanganyika watakuwa wamekubali. Lakini zanzibar ingekuwa ni kanda tu yenye mikoa labda miwili ndani ya muungano tukawa na serikali moja haya tusingeyajadiri.
kaka ni kweli usemalo na huu muungano wa kiunafiki, mimi ningependa watu wote tukae chini tuamue muundo upi utatufaa kwa sisi wenyewe na vizazi vijavyo.
 
Mbunge alikuwa akiongea kwa hisia na sio akili, ukimsikiliza Lissu unafurahi maana kuna mambo nilitamani kuyasikia na kupata nafasi ya kuyasema na Mungu mkubwa nimelipata toka kwa kaka yangu msomi Lissu.Mungu amjalie Nguvu na baraka tele, miaka mingi yenye heri duniani.
<br /> <br / na amjalie moyo wa ujasiri na uvumilivu juu ya hawa wachumia tumbo
 
Naisubiri kwa hamu sana siku ya kuvunja muungano ili kila mtu aishi kivyake. Mimi mkulima wa alizeti hapa Haidom sijui na wala sijawahi kufaidika au kutofaidika na huo muungano wenu
 
kumbe wewe mpemba! Kwanini siku hizi cuf mnajifanya kutetea sana ccm haaaa!??
Kama wamezamishwa kwenye serikali ya MAFISI WA AHADI wa CCM kwa mgongo wa serikali ya umoja wa kitaifa hatuwahitaji.
Kama ni kwenda OIC na MAKA nendeni kama ni mahakama ya kadhi na serikali ya sharia nendeni Ruksa!!!
 
Jipe pole wewe mwenyewe, Lissu ni mwanasheria na mbunge hivyo alikuwa antimiza wajibu wake. Anajua na ana uhakika wa yale aliyoyasema juu ya katiba na muundo wa muungano wetu. Leo hii mtambishia na kumbeza Lissu lakini nina uhakika 100% msipoyafuata haya mtafikia pahala mtakwama tu, tena si mbali hii migongano itaanzia kwenye hiyo katiba yenu mpya mnayoitaka wakati ni waoga kuongea wazi wazi -- FUNGUKENI WATANGANYIKA.
Ni kweli mkuu!!
 
kwa hoja alizotoa lissu jana bungeni, basi kama ni kidonda basi kimepata mkunaji. Aliyoongea jana ni maneno ambayo wengi wetu tumetamani kuayasikia siku nyingi, ila kwa sababu watu na waoga wa kusema vitu black and white basi tunaona amekosea. Lissu ni jasiri, mpambanaji, mwerevu, open minded, etc.. Huyu mzenji kaja na hoja mdebwedo na anataka kila mmoja aaminia alischosema yeye ndo sahihi. Namuasa tu kwamba kama waliweza kuinunua CUF huko zenji wasifikir na CDM wanaweza kuinunua. Jipu limepasuka
 
kwa hoja alizotoa lissu jana bungeni, basi kama ni kidonda basi kimepata mkunaji. Aliyoongea jana ni maneno ambayo wengi wetu tumetamani kuayasikia siku nyingi, ila kwa sababu watu na waoga wa kusema vitu black and white basi tunaona amekosea. Lissu ni jasiri, mpambanaji, mwerevu, open minded, etc.. Huyu mzenji kaja na hoja mdebwedo na anataka kila mmoja aaminia alischosema yeye ndo sahihi. Namuasa tu kwamba kama waliweza kuinunua CUF huko zenji wasifikir na CDM wanaweza kuinunua. Jipu limepasuka
Safi sana mkuu - pia nimependa hiyo key word yako.
 
Wazee wa kizenj wana matusi wewe! Matusi ya kiurojorojo!
<br />
<br />
Halafu walalamishi sana! "Lissu alisema haiwezekani theluthi mbili 2/3 ya wazenji zizuie maamuzi ya wengi wa bara, hususan ktk suala la katiba" Hapa kwa maoni yangu Lissu alimaanisha "SIASA ZA ZANZIBAR NA BARA ZISIWE STUMBLING BLOCK KWA SERIKALI KUTOFANYA MAAMUZI"
 
CDM always ahead, thank you Lissu, thank you true God.

hivi wakati yule mdebwedo anaongea wabunge wa CCM walikuwa wanatumia masaburi (kupiga makofi) kusikiliza? if they, then take this.

Mbinu pekee ya CCM kuendeleza mfumo wake wa ubinafsi na uporaji wa mali za taifa hili ni kupata ushawishi/uwezo mdogo wa wabunge wa kule zenji kupambanua mambo ili tuwe na katiba mbofumbofu. take a good care you Tanganyika.
 
FUSO; "...Ninavyopendekeza mimi CHADEMA warudi kwetu watueleza nini hasa Lissu aliongea na nini hasa anamaanisha, sababu duniani kila mtu ana upeo wake wa kuelewa, kuna wengine pia ni wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau. Kuna wengine mpaka uongee kwa lugha nyepesi ili dhana nzima uliotarajia kueleza iweze kueleweka.

Kama ni pumba au mchelle sisi wananachi tutajua baada ya ufafanuzi kufanyika, siamini na sidhani LISSU ana nia mbaya juu ya Tanganyika, Zanzibar na Tanzania kwa ujumla laa hasa, nafikiri ni upeo wa kuelewana ndiyo kikwazo hapa...

CHADEMA nawaomba mrudi kwetu wananchi, kwa lungha nyepesi kabisa mtueleze ni nini hasa mantiki ya mawazo ya Lissu hasa katika masuala ya muungano sababu navyojua mimi huo ndio msimao wa CHAMA ila Lissu alitumika kuufikisha kupitia Bunge."


Mkuu FUSO, Heshima natoa; Hotuba ya Mh. Lissu ipo very clear, i mean black & white. Nimeipitia na kuitafakari, nikajiridhisha kuwa Mh. Lissu is my Hero of year.

Mengi yamesemwa na mengi yatasemwa but kiongozi aliwasilisha kile kinachostahili kuwasilishwa. Hao wanaomu-attack personally badala ya hoja wameishiwa hoja, kwan hoja hujibiwa kwa hoja.

Nawashauri watz wenzangu wapitie hotuba yake, waitafakari. Halafu wapime yale yaliyosemwa na wawakilishi wao bungeni, halafu wachanganye na zao.

Hata hivyo naunga mkono hoja, kwa kuzingatia ukweli kuwa % kubwa ya waafrika hawapendi kujisomea
 
Mhe. Tundu Lissu alikuwa sahihi sana kwani iweje tuwashirikishe wazanzibar kwenye mambo yasiyo husu muungano. Nasema NO capita N, O bolded NO. Hakuna kuruhusu watuamulie mambo yetu
 
Kwenye katiba Rais wa zanzibar anapaswa ashirikishwe kwenye mambo yanayohusu muungao tu asishirikishwe kwenye mambo mengine ya tz bara ikumbuje Wazanzibar wametunga katiba yao bila kumshirikisha mtanzania bara ht m1. NA kuhusu muungano wananch waseme km wanauhtaji muungano na wanahtaji muungano wa aina gani. Maneno haya aliyaongea TUNDU LISSU. Maoni yng: haiwezekani upande 1 utunge katiba yk bl kushrikisha upande wa 2 hlf wkt upande wa 2 unapotaka kutunga katiba yk upande wa 1 ung 'anie kushiriki kwa lazima, hii si sawa kbs kila upande utunge sheria zake kwa nch yk hlf kuwe na sheria/ katiba ya muungano ninamaa kuwe na katiba 3. wazanzbar wanamambo ya udini sn wanataka kuleta udini wao hk bara mf. Wanasema lazima sheria ya ndoa irekebishwe iruhusu watoto wakishapevuka waolewe kwa kawaida watoto wanapevuka 10-12yrs when they are std 5/6 hvy mchumba(mbakaji) akijitokeza sheria imruhusu kuoa, mi naona huu ni upumbavu,unyanyasaji na ukatili kwa watoto wa kike.
<br />
<br />
Nakuunga mkono %100 hawa watu wapuuzi sana,yaani mtoto mdogo aolewe?huo upumbavu wakaufanyie huko kwao sio huku.
 
Dhambi ya UKABURU tukiiendekeza, itatutafuna mpaka tutaparaganyika kabisa.

Leo hii ni Utanganyika na Uzanzibari

Kesho ni Uislam na Ukristo

Keshokutwa ni Usabato na Ukatoliki

Halafu utasikia wewe msukuma mimi mchagga.

Baadae kabisa itafikia wewe wa Kibosho na mimi wa Marangu.

Baadae itakua hawa ni akina Massawe na sisi ni akina Shirima.

Jamani tupunguze jazba ndugu zangu. Mwalimu alituasa tusiendekeze dhambi ya ukaburu...
ikishaanza kututafuna haina siku itakoma... kila siku tutakua tunaconcentrate kwenye tofauti
zetu, badala ya values gani zinatuunganisha na kuwa taifa.
 
Siku zote ukweli huwa unauma, na lissu alisimama kwenye ukweli na huyo kilaza chombo kama kawaida ya wazenj kwa jazba badala ya kujenga hoja yeye anajenga matusi. Sasa watu kama hawa uwashirikishe kwenye kutunga katiba c watachangia utumbo mtupu, kama udhaifu aliouonyesha chombo!
 
Wazanzibar hawaeleweki, elimu yao, uwezo wao wa kuelewa, matakwa yao nk.. Watu ambao wamekuwa wakipiga makelele kuwa kuna mambo yasiyokuwa ya muungano yameongezwa kinyemela, leo hii wanatoa mapovu kama mataahira wanapoambiwa kuwa wasishiriki ktk mambo yasiyo ya muungano!!! wazanzibar WAACHE UNAFIKI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom