CHADEMA tamkeni wazi kumtambua JK (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)

VGL, actions speak louder than words, Chadema hawana haja ya kusema wanamtambua, mambo mengine yanamalizwa kuitu uzima tuu. Nilishawaambia siku nyingi kuhusu hilo katika thread yangu ya "Chadema Wamtambua JK Kinyemela", that was then, now sio kinyemela tena bali ni mambo hadharani!.
Mkuu kule kwingine uliapa kuwa kikwete alivyo arrogant lazima atausani muswada kabla ya kukutana na Chadema! Vipi, ameusaini KINYEMELA bila shamrashamra yoyote?! Na mbona ikulu haijatoa taarifa kuwa umesainiwa? Au kwa sababu wanajua wewe ulishatoa tarifa kuwa atausani kabla ya kukutana na Chadema?!
 
Jabulani, huna haja ya kunitafuta popote as if sionekaniki. Mimi nipo tuu hapa jf 24/7 hivyo nipo sana.

Ni kweli nilikula kiapo kile na niliapa JK hakutani na yoyote kabla hajasaini!. Alipowaona Chedama jana aliwaambia hajasaini?.

Wewe hujawahi kulea mtoto au hata mdogo wako?. Hivi hujaona mtoto akililia sana kitu fulani, akipewa pipi hunyamaza?!.

Unazungumzia hizo pipi za Ikulu jana kwa jina la chai na vitafunwa?. Hivi hukuwaona walivyo kuwa wanatabasamu kwenye ile picha?. Unaijua sababu?.

Umeisoma taarifa ya Ikulu kuhusu mkutano wa jana, taatifa imesema hajasaini?.

Tarehe 1 sheria mpya in force!.

Pasco acha kumtusi jk, Unataka kusema kuwa ameshausaini mswada?
Hivi kama yeye amewaita ikulu kujadili mswada ambao yeye ameshausaini kwa siri ( if that is the case), nani msanii na mwongo kati ya CHADEMA NA kikwete? Unatupa siri zaidi za kumdhalilisha mkuu wako wa kazi au?
Hata hivyo, Chadema wameenda kutoa maoni yao, hawajenda kumlazimisha. Akikataa ni uamuzi wake.
 
tumkushuru na kumpongeza kikwete kwa kukubali kwake kukaa meza moja na wapinzani wake ambao kila kukicha wanamtukana na kumkejeli kama aweda alivyomkejeli na kumtukana kwa kumfananisha na baba mbakaji....kwa msomi kama aweda jinsi ninavomfaham sikutarajia atumie maneno ya dharau na yasiyoenda shule kama yale.....kikwete alipata asilimia 61 ya kura zote tanzania.chama chake kilipata wabunge zaidi ya 200 kati ya zaidi ya 350.takwimu za chadema na upinzani zinajulikana kwa idadi na asilimia.....sasa unapoandika kejeli apa kwenye forum ambayo inasomwa na watu wenye akili zao waliosambaa dunia nzima huoni kuwa unajidhalilisha?????????????nawapongeza makamanda wa cdm kuamua kukaa meza moja na kikwete kuzungumzia mustakabali wa taifa letu changa la Tanzania.

Mkuu pole kwa mfano wangu mgumu,
Nami niliutafakari lakini baadaye kutokana na jinsi ambavyo wanaoedesha propaganda za ccm kunizidi, nilizamika kutumia mfano huo.
Kila siku wanapotosha kwa makusudi na kuna watu wanaaminishwa upotoshaji huo. Mfano huu unamfanya mtu asisahau.
 
Nimesema na narudia kusema, kitendo cha magwanda kwenda kuonana na Rais ni cha kiuungwana na kisiasa nzuri sana, wangekuwa siku zote wanafanya haya wangetukonga nyoyo zetu, maandamano si siasa ni ujinga. Naona Mzee wa Maandano hakuwepo. Slaa daktari wa kanoni, hakuafikiana na wenzake au?

Sijamuona na Zitto pia, watendaji wakuu wawili, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu sijawaona walipooneshwa kwenye TV jana. Kulikoni?
 
Nimesema na narudia kusema, kitendo cha magwanda kwenda kuonana na Rais ni cha kiuungwana na kisiasa nzuri sana, wangekuwa siku zote wanafanya haya wanetukonga nyoyo zetu, maandamno si siasa ni ujinga. Naona Mzee wa Maandano hakuwepo. Slaa daktari wa kanoni, hakuafikiana na wenzake au?

Urahisi wa hoja zako ndio unakufanya uonekane huna lolote zaidi uswahili na maneno mengi yasiyo na msingi.
Aliyekwambia Zitto na Dr. Slaa wapo kwenye kamati iliyoundwa ni nani?
 
Mkuu kule kwingine uliapa kuwa kikwete alivyo arrogant lazima atausani muswada kabla ya kukutana na Chadema! Vipi, ameusaini KINYEMELA bila shamrashamra yoyote?! Na mbona ikulu haijatoa taarifa kuwa umesainiwa? Au kwa sababu wanajua wewe ulishatoa tarifa kuwa atausani kabla ya kukutana na Chadema?!

Pasco amekuwa anajaribu kujificha kwenye kivuli chake kwa muda mrefu sasa........naona ameshindwa.......jua limehama, yeye amesahau kugeuka.
 
VGL, actions speak louder than words, Chadema hawana haja ya kusema wanamtambua, mambo mengine yanamalizwa kuitu uzima tuu. Nilishawaambia siku nyingi kuhusu hilo katika thread yangu ya "Chadema Wamtambua JK Kinyemela", that was then, now sio kinyemela tena bali ni mambo hadharani!.

Pasco sielewi ni kwanini ung'ang'ania haya madai kwamba CHADEMA walikataa kumtambua rais! CHADEMA walitoa ufafanuzi wa kina kabisa kuhusu nini hasa hawatambui, lakini bado unaonekana kuendelea kuhubiri hii hoja potofu! Nakumbuka kuna mahali umeandika kuwa unasoma law of 'somesort' sasa ni kwa nini hueweli tofauti kati ya kutotambua 'mchakato - process' na rais- end product'? Kuna agenda gani hapa?
 
Jana tarehe 27/11/2011 JK alikutana na ujumbe wa CHADEMA Ikulu kwa mazungumzo ya mchakato wa kupata katiba mpya. Mazungumzo hayo yanaendelea leo tarehe 28/11/2011. Nakumbuka kwamba CHADEMA waliwahi kutamka kwamba hawatambui kama JK ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hoja yangu ni kwamba kama wamekutana naye kama Rais wa nchi, basi watoe tamko la kumkubali.

Are you serious?!

Last edited by a moderator:
Mtatoka nje lakini mtarudi ndani wapi? Hivi ndani una maanisha ndani ya jengo la Bunge au Ikulu. Hivyo vyote, hakuna ambacho kikwete ni mmliki wake au ni mali yake. Vyote alivikuta na ataviaacha. Hakuna kilichojengwa kwa mshahara wake. Vyote hivi ni ofisi za watanzania siyo ya Kikewte wala ccm.
Tunachofanya chadema ni kutumia hekima ili tusivuruge nchi yetu. Chadema siyo waajiriwa wa Kikwete, tuko kwa ridhaa ya watanzania na hakuna mtanzania mwenye haki zaidi ya mwingine. Wanachadema ni watz kama walivyo jk na wanaccm wote.

Hivi kuna neno 'ndani' kwenye post yangu?
 
Pasco acha kumtusi jk, Unataka kusema kuwa ameshausaini mswada?
Hivi kama yeye amewaita ikulu kujadili mswada ambao yeye ameshausaini kwa siri ( if that is the case), nani msanii na mwongo kati ya CHADEMA NA kikwete? Unatupa siri zaidi za kumdhalilisha mkuu wako wa kazi au?
Hata hivyo, Chadema wameenda kutoa maoni yao, hawajenda kumlazimisha. Akikataa ni uamuzi wake.
Michael P Aweda, mbona unataka kuleta uchonganishi?!. Nani kamtusi JK?. Kutusi maana yake kutukana matusi, hivi kweli kuna tukano lolote kwa JK?!.

Kitendo tuu cha kuandika eti tumemtusi JK kinatosha kuhatarisha amani na kuitia JF matatani?!. Why?!.
 
Nitakufuata popote Pasco unipe jibu, hata kama utakwepa. Ulikula kiapo kwamba KAMWE JK hatakutana na CHADEMA na LAZIMA atausaini muswada kabla ya tarehe 01/12/2011. Jambo mojawapo limeonekana ni UONGO wako (la kutokutana na CHADEMA kamwe!). Unatoleaje ufafanuzi uongo wa kiapo chako hicho? Mimi huwa sipendi watu waongo wachangie humu JF

Pasco anajifanya mzimu wa sheikh yahaya
 
Pasco sielewi ni kwanini ung'ang'ania haya madai kwamba CHADEMA walikataa kumtambua rais! CHADEMA walitoa ufafanuzi wa kina kabisa kuhusu nini hasa hawatambui, lakini bado unaonekana kuendelea kuhubiri hii hoja potofu! Nakumbuka kuna mahali umeandika kuwa unasoma law of 'somesort' sasa ni kwa nini hueweli tofauti kati ya kutotambua 'mchakato - process' na rais- end product'? Kuna agenda gani hapa?
FJM, waliposusia kutangazwa matokeo walifafanua kuwa wanasusia process?. Haya process ya uchaguzi inaisha kwa kuapishwa kwa rais, baada ya rais kuapishwa pale bungeni Dodoma aliposimama JK kulihutubia bunge wao walitoka nje, hapo napo walikuwa wanasusia process?.

Nawashauri mfike mahali muwe mna addimit mistakes!.

Sisi wote ni binadamu sio malaika, hivyo hakuna mkamilifu. Hata Nyerere anaetatajiwa kutangazwa mwenye heri, alifanya makosa!. CCM imefanya makosa mengi tuu, sasa nyie Chadema ndio nani?. Nyie hamkosei chochote, every move you do and every step you take is always the right step?!.

Kila anayepingana na Chadema humu mnamshambulia kama adui!. Mbona nimeandika mengi tuu kuhusu madudu ya CCM, mbona sijashambuliwa kama ukosoaji wa Chadema?!.

Kwangu Chadema ni chama chenye matumaini ila sio chama malaika!. Mkikosea mnakosolewa tuu kama tunavyo ikosoa CCM!.
 
jana tarehe 27/11/2011 jk alikutana na ujumbe wa chadema ikulu kwa mazungumzo ya mchakato wa kupata katiba mpya. Mazungumzo hayo yanaendelea leo tarehe 28/11/2011. Nakumbuka kwamba chadema waliwahi kutamka kwamba hawatambui kama jk ndiye rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania.

Hoja yangu ni kwamba kama wamekutana naye kama rais wa nchi, basi watoe tamko la kumkubali.

wewe unaishi wapi? Ni lini chadema walisema hawamtambue kikwete kama rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania? Usilete hoja ambayo haina ukweli hapa.
 
Nimesema na narudia kusema, kitendo cha magwanda kwenda kuonana na Rais ni cha kiuungwana na kisiasa nzuri sana, wangekuwa siku zote wanafanya haya wanetukonga nyoyo zetu, maandamno si siasa ni ujinga. Naona Mzee wa Maandano hakuwepo. Slaa daktari wa kanoni, hakuafikiana na wenzake au?

Sijamuona na Zitto pia, watendaji wakuu wawili, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu sijawaona walipooneshwa kwenye TV jana. Kulikoni?

Makamu wa Rais, rais wa Zanzibar na Waziri mkuu wao walikuwepo kwenye kikao??
 
FJM, waliposusia kutangazwa matokeo walifafanua kuwa wanasusia process?. Haya process ya uchaguzi inaisha kwa kuapishwa kwa rais, baada ya rais kuapishwa pale bungeni Dodoma aliposimama JK kulihutubia bunge wao walitoka nje, hapo napo walikuwa wanasusia process?.

Nawashauri mfike mahali muwe mna addimit mistakes!.

Sisi wote ni binadamu sio malaika, hivyo hakuna mkamilifu. Hata Nyerere anaetatajiwa kutangazwa mwenye heri, alifanya makosa!. CCM imefanya makosa mengi tuu, sasa nyie Chadema ndio nani?. Nyie hamkosei chochote, every move you do and every step you take is always the right step?!.

Kila anayepingana na Chadema humu mnamshambulia kama adui!. Mbona nimeandika mengi tuu kuhusu madudu ya CCM, mbona sijashambuliwa kama ukosoaji wa Chadema?!.

Kwangu Chadema ni chama chenye matumaini ila sio chama malaika!. Mkikosea mnakosolewa tuu kama tunavyo ikosoa CCM!.

Nimegundua kuwa tunatofaviana malengo ya kupost humu jamvini. Kwamfano wewe unalengo la kupotosha watu. Naamini hivyo maana hata jambo ambalo wachangiaji walidhani hujui au umesahau, wamejaribu kukufafanulia lakini kwakuwa unamalengo tofauti umeamua kukataa bila sababu.

Sasa, upende usipende, elewa au endelea kujifanya huelewi, cdm walifafaeua vizuri wakati ule kwamba wabunge wake walitoka bungeni wakati wa hotuba xa rais kuonesha kutokukubaliana kwao na mchakato mzima uliopelekea yeye kutangazwa mshindi. Hawajawahi kutamka kutokumtambua rais. Hilo hatukubembelezi kukubali. Kama inazuia malengo yako yasitimie, pole!

Endelea kuwadanganya wajingawajinga wasiokuwa na kumbukumbu na kuwafurahisha wapuuzi wa ccm mnaofarijika na uongo wako!
 
Asante, thanks.
 
Mkuu kule kwingine uliapa kuwa kikwete alivyo arrogant lazima atausani muswada kabla ya kukutana na Chadema! Vipi, ameusaini KINYEMELA bila shamrashamra yoyote?! Na mbona ikulu haijatoa taarifa kuwa umesainiwa? Au kwa sababu wanajua wewe ulishatoa tarifa kuwa atausani kabla ya kukutana na Chadema?!
Kikao kimemalizika, matokeo ndio hayo!.
 
Back
Top Bottom