CHADEMA tafadhali nawaomba...

Nimekubali hili TZ hakuna udini hi ni propaganda ya CCM wakamatwe basi hao wadini watu tumezaliwa mama muislam baba mkristo na hawabaguani udini uko wapi huko ni kuomba huruma wakati wewe ndo mtesaji ukombozi daima TUSIKUBALI KUGAWANYWA aluta continuaaaa!
 
Wanachohitaji watz sasa ni utekelezwaji thabiti wa dhana ya USAWA WA BINADAMU, hivi naomba niulize ni: Ni Chama gani cha kisiasa hapa TZ ambacho wafuasi wote (100%) ni wa DINI moja? Kama kipo naomba mnijuze na kama hakipo kwa nini basi tufikie hatua ya kuogopa na kukimbia vivuli vyetu wenyewe?
 
Jamani mi naogopa, vita iskie kwa nchi jirani ndugu zangu, i wish mgekuwepo kwenye vita au mauaji ya kimba' au burundi na kongo enzi za wanyamurenge guyz si kitu cha kuomba, inatisha acheni tu.
 
Tafuteni muislam vocal hata wakununua. I smell trouble. Nina ndugu yangu ustaadh ni mstaarab na mpole sana ila mambo aliyoniambia yaliyoko kichwani kwa waislam wengi ni hatari kwa taifa. Uongozi wa CDM tumieni inteligensia yenu tafadhali kwenye hili.

Nisingeunga mkono kuhusu hilo la kutafuta sijui watu kwa ajili ya dini fulani wajiunge CHADEMA. Kitu kama hiki kinatoka rohoni sio unalazimishwa. Mimi sioni kama kuna tatizo mbona CUF kuna mtatiro peke yake. CHADEMA muwe macho mnaweza kuchukua moto mkashindwa kuuzima. Angalieni yaliyoko CCM sasa hivi kiutendaji hakuna, watu wapo kule kama mapambo tu jiulize ni kwa nini ndugu. yangu.
 
Chama cha siasa sio bendi kwamba inapotumbuiza kila mtu lazima afurahi. Mambo ya chama ni mambo ya sera na itikadi. Hivi ukabila umeshaisha? Maana CDM ilisemekana kuwa ya wachaga. Sasa hivi CDM ina udini! Hivi shida zetu zinaangalia dini? Mabomu ya gongolamboto yalifuata mfumo wa kidini? Huyu Slaa udini amejifunza baada ya kugombea urais? Mbona wakati wa kuibana serikali bungeni hakuwa mdini? Kwa hiyo watu wote wanaomsikiliza ktk mikutano ni wadini? Wa-zanzibar wako honeymoon kwa sasa waache na sisi tufanye kazi huku bara!
 
Waislamu si watu wajinga. Wanajua zuri na baya. CHADEMA ni chama kizuri, hivyo watajiunga hata bila kushawishiwa. Kwani ZITTO, ARFI, HALIMA sio Waislamu? Mwanzisha mada ni mbumbumbu wa CCM.
 
Mkeshaji comment yangu ya kuhusu kusilim ilikuwa iwe taken lightly. Shangaa ni wewe tu ulieshupalia hivyo jiulize nani mjinga.
Kashaijabutege is on another level,bahati mbaya hatupimwi akili kabla ya kuingia JF.
Kwa wale mliopinga hoja kibusara naombeni mfanye kauchunguzi kidogo tu na sio kukimbilia kuita watu wajinga na hawapo hio ni denial mbaya. Nami nilikua kama nyie nabish kua udini hauko kwasbabu upande wa mama wakristo baba waislam na there is harmony. Lakini kuja kutitoa kwenye hio narrow view na kuingia circles za waislam na wakristo mtaani,nimeanza kuamini sumu walioanzisha CCM itaanza changanya. Sasa watu humu wanakubali ccm wameanzisha cancer hii lakini eti watanzania tunapendana sana haliwezi tokea. Kutoa tahadhari sio kuchochea jambo. Kwa wenye akili i.e. excluding a significant few above fanyeni utafiti. Mpaka ulivyoitishwa mkutano wa viongozi wa dini pale Mengi alikua mgeni rasmi waTZ werevu lazma muanzi kutafakari kua something might not be right wandugu. Nyie mnaopinga ongeeni kistaarab na masheikh na wachungaji japokuwa kuna wengine sidhani akili zenu zinaweza undertake such a task. Na badala ya kurusha matusi kisa tu hupendi udini ni kufanya utafiti na kuchukua hatua. Wasiwasi ndio akili yenyewe!
 
Hawa wametumwa kuchochea mgawanyiko wa kidini. Ni mkakati na mbinu ya ccm, hakuna lolote katika mjadala huu. We, as great thinkers, hatupaswi kuendekeza majadiliano haya yasiyo na tija. watanzania wanajitambulisha kwa utanzania wao, wala si kwa dini zao. ukimuona mtu anatamani sana kujipambanua kwa dini yake, basi, huyo kafirisika ki fikra na ni wa kuogopwa kama "ukoma". Watanzania wote wanaandamana na kupinga ufisadi na ugumu wa maisha (wakristo + waislamu+ wapagani". Katika maandamano yote ya mwanza, shinyanga, bukomba, kulikuwa na watu wa dini mbalimbali na wasio na dini. Hivyo achanane na mtu hapa jamvini anaye pandikiza mkanganyo wa hoja za kidini kujaribu kuficha ukweli wa mambo. Nani aliye sema kuwa serikali ya Mkapa ilikuwa safiiiiiiiiii?? na kwamba ya kikwete ndo mbaya?? wote ni wale wale -"mafisadi tu"
 
uwezi kutafuta solution ktk tatizo ambalo haliko mjomba, udini hakuna hizi ni siasa tu waislamu na wakristo wananishi kama ndugu hao wanaoidai kuna udini ni wanasiasa uchwara kama kikwete ambao wanatumia udini kujipatia kura. mashekhe wengi wanaoubiri udini wakati wa uchaguzi ulipwa na wausika kwa ajili ya kufanya kazi hiyo lakini hawawaambiii wanaowaubilia kuwa wamechukua pesa mfano mzuri ni shekhe Halifa wa kariakoo ni maarufu kwa kazi hiyo. ukitaka kujua anachokisema KIKWETE NI PUMBA fikiria kwanini hawachukulii hatua watu anaodai kuwa wanaeneza udini, yeye kama raisi anayo mamlaka makubwa ya kisheria kwanini hawachukulii hatua anakaa pembeni kulalamika kama mwananchi wa kawaida? mdini ni yeye JK akienda kusini anailalamikia CUF kuna udini akienda Kaskazini analalamikia CHADEMA. alipokuwa Lindi aliuliza kwenye mkutano wa hadhara aliwalalamikia CUF kuwa wana mbagua kwani yeye ni john?, hebu fikiria kwahiyo John ndio anastahili kubaghuliwa JK ndiye MDINI MKUBWA na siyo watanzania wengine.
Politiki soma post yako tena. Kwenye red unasema udini hamna TZ unainsinuate pia kuwa hauwezi tokea. Lakini kwenye blue unatoa vidhibitisho kua kuna watu wanauchochea. Sasa ndugu ni hatari kuamini kuwa watu wengi wanawapuuzia hawa wachochezi kama wewe.Utashangaa ni kinyume kabisaa.An increasingly number of TZ are starting to take sides. Kikwete alivyoenda Lindi na kusema yeye sio John,walimzomea au walimshangilia?
Tafakarini wandugu.
 
Mbona hawaizungumzii kafu Iliyojaa waislamu kibao,kwa mwenye akili timamu ataelewa lakini propaganda hizi zikatumiwe kwa watu wajinga kwakuwa hizi dini hapa nchini kwetu zimegawanyika kutokana na maeneo husika.Mbona hatushangai serikali ya zanzibar haina mkristo hata mmoja?na si ccm na cuf ndio wanaoounda hiyo serikali?kwani hamna wazenji wakristo?Sasa huu udini ni sere ya ccm wakishirikiana na wake zao cuf lakini hawana hoja za msingi huwezi kumshutumu Dr Slaa kuwa ni padre ile hali tunafahamu Ukiwa muislamu tu unaweza kuwa na Title ya Shekhe?sasa tatizo lipo wapi hapo kwa chadema?
"Akinyakuku sawa lakini akinya Bata kaharisha"
CCM na CUF acheni kuwagawa wananchi kwa propaganda za kidini nyie kwani hawa mafisadi hata wakiwa ni dini yako utaathirika na madhara yake bila kujali dini yako.
 
Hili la CDM na ukristo lisiwasumbue kwani waislam walio CDM wanajidhihirisha ZITO,HALIMA,MUSTAFA,AFRI na hata wakiondoka haisumbui kwani JK alipalilia udini wakati wa kampeni.
Hivi nani aliyewapa waislam majengo ya shirika la umma TANESCO ili walifanye kuwa chuo kikuu chao-MUSLIMS UNIVERSITY MOROGORO?
Wazanziba waligawanywa hivyo hivyo CUF cha wapemba,CCM cha waunguja baadae itakuja washia/wasunii
Bara waislam /wakristo tena CCM wakimweka mkristo 2015 itaanza wakatoliki/walutheran
Hizo zote propaganda ila JK aliingiza propaganda ngumu isiyofutika kirahisi
 
the way topic ya udini inavyospread like a wild fire ndipo napomuona kikwete ni mbaya kuliko shetani,katuletea balaa nchii hii,..moses kilaini alisema ni chaguo la mungu mi naona the other way round,..speaking of kilaini,kila zinapoonyeshwa misa za katoliki jpili kwny tbc1,basi litaonyeshwa jimbo la bukoba analoliongoza kilaini sijui kwa nini??mkapa alikuwa fisadi so was mwinyi lakini hawkuwahi kuingiza sumu ya udini
 
Kwa kiasi kikubwa naweza kuunga mkono hoja ya mtoa mada, kwa nchi kama Tanzania ambapo asilimia kubwa ya Raia wameleweshwa Dini ni busara kwa uongozi wa chama chochote au kiongozi yeyote kuwa makini katika namna ya ku-organize mambo ili kuepusha malalamiko kutoka upande wowote. Kwa kifupi huwa ni ngumu na inakera pale unapojaribu kutetea haki za watu bila kujali itikadi zao za kiimani na kikabila, lakini mwisho wa siku bado ukapata malalamiko kutoka upande mmoja kwamba unapendelea upande mwingine.

Hivyo ni baadhi ya vizingiti ambavyo chama/kiongozi yeyote atakumbana navyo kwenye kutekeleza majukumu yake. Cha muhimu kufanya ni kutafuta solution ya haraka kabla hii sumu haijaenea zaidi. Wakati mwingine huwa naamini kuwa sisi watanzania tu wavivu wa kufikiri na hatupendi kushughulisha akili zetu kutafakari mambo, kwa mantiki hiyo huwa ni rahisi sana kwa mtu kupotoshwa na mtu yeyote atakayeamua kupotosha pale anapoonekana kuturahisishia mambo, hasa hawa wanaojiita/wanaoitwa viongozi wa dini aidha kwa makusudi (kulinda maslahi) au kwa bahati mbaya (kwa uelewa wao mdogo).

Tukirejea kwa walengwa, nashauri ninyi wana-CHADEMA mliopo humu ndani, mchukue ushauri wa mtoa mada na mara moja muanze kueneza Propaganda misikitini na kwa waumini wa Uislamu kuwa ukombozi wa Mtanzania hauna uhusiano wowote na CHADEMA kama chama bali unawahusu watanzania wote. CHADEMA wanatekeleza jukumu lao kama sehemu ya watanzania, wengine nao watekeleze kwa upande wao, mradi lengo ni moja, basi tusihitilafiane bali tupeane moyo na ushauri pale mmoja atakapohitaji. Iwepo au isiwepo CHADEMA, ni lazima mtanzania akombolewe kutoka kwenye makucha ya wanyonyaji wachache. Uislamu na Ukiristo ni imani zenu, ziheshimuni, zipo, zilikuwepo, na mtakufa mtaziacha, tuweke imani zetu kando pale tunapodai maisha mazuri, huduma bora za afya, punguzo la bei za sukari, nauli na mchele, kuondoa kero za foleni za magari, kuchelewa kwa mishahara pamoja na kero mbali mbali ambazo zinachangiwa na uongozi wetu kutupuuza waislamu na wakristo na wapagani wa Tanzania. Waambieni kuwa akina mama wajawazito wanaokufa kwa kukosa huduma za afya ni waislam na wakiristo kwa pamoja, vibaka waliopoteza matumaini wanakaba watu wote kwa pamoja, masheikh na wachungaji. Waambieni wakati yote hayo yakitokea Viongozi wao wakuu wa dini wanapewa huduma zote muhimu na Serikali, hawabugudhiwi!!!

Ndg Yangu TANMO ulicho sema ni kweli, mbegu za chuki zimekwisha pandikizwa hivyo yahitajika jitihada za maksudi kungoa hayo mapando ya udini. Juzi hapa Mto wa Mbuu watu walishikana mashati, kupigana kuchoma nguo za watu kubomoa kanisa, mwishowe kupelekana POLICI hadi mahakamani Kijana mmoja alilazwa Hospitari Monduli. Hivyo kuna haja ya kuwa na busara kwa mambo tufanyayo, tupime matamshi yetu, maana watu tumeishi pamoja kama majirani, tumesoma pamoja shule, tunashiriki pamoja hata kwenye harusi na misiba, vipi hizi siasa za maji taka zitutenganishe????????? Hebu wote tufikiri, tusiwe na jaziba, twende kwa hekima tuondoe huu utando unao anza kuenea kwa kasi, turudishe imani na kuheshimiana. Tuwapime watu kwa uwezo wao bila kujali dini zao kama ni Mwislam au Mkristo akishindwa kazi au wajibu ameshindwa, mbona Misri Mubarak ni Mwislam na wamemwondoa kwa sababu kashindwa kazi ya kutawala!!!!!Tusinganganie kwenye moto eti kwa sababu anayetuchoma ni dini yetu, tunaungua!!!!!!!!!
 
Mdini ni kikwete, na safu yake ya vibaraka. We dont give a damn, we need results. Awe mwislam, mkristo,Hindu, pagani tunachohitaji ni RESULTS.
Ishu za dini ni propaganda za JK na vibaraka wake, anazodhani ndo silaha ya kupambana na Chadema.
Waislam wakristo waTZ wote ni marafiki, tunakula bia pamoja, ndugu, tunaoleana, tunafanya kazi pamoja, tunapanga nyumba moja tunaishi vizuri, ijumaa mi msikitini, jpili mwenzangu chach. Udini nin siasa. sumu inayotumiwa na JK kutuchonganisha na ndugun zete wakristo.
JK anadeviate from the real problem, na kutafuta solution ya matatizo yake kwa sympathy za kidini.
 
Chama cha siasa sio bendi kwamba inapotumbuiza kila mtu lazima afurahi. Mambo ya chama ni mambo ya sera na itikadi. Hivi ukabila umeshaisha? Maana CDM ilisemekana kuwa ya wachaga. Sasa hivi CDM ina udini! Hivi shida zetu zinaangalia dini? Mabomu ya gongolamboto yalifuata mfumo wa kidini? Huyu Slaa udini amejifunza baada ya kugombea urais? Mbona wakati wa kuibana serikali bungeni hakuwa mdini? Kwa hiyo watu wote wanaomsikiliza ktk mikutano ni wadini? Wa-zanzibar wako honeymoon kwa sasa waache na sisi tufanye kazi huku bara!

Ilikuwa ya wachaga kipindi kile coverage yake ilikuwa limited kwa Arusha na Kilimajaro. Na kwa kuwa sasa kimekubalika nchi nzima namna ya kukidhoofisha ni DINI propaganda.
 
Kwa kiasi kikubwa naweza kuunga mkono hoja ya mtoa mada, kwa nchi kama Tanzania ambapo asilimia kubwa ya Raia wameleweshwa Dini ni busara kwa uongozi wa chama chochote au kiongozi yeyote kuwa makini katika namna ya ku-organize mambo ili kuepusha malalamiko kutoka upande wowote. Kwa kifupi huwa ni ngumu na inakera pale unapojaribu kutetea haki za watu bila kujali itikadi zao za kiimani na kikabila, lakini mwisho wa siku bado ukapata malalamiko kutoka upande mmoja kwamba unapendelea upande mwingine.

Hivyo ni baadhi ya vizingiti ambavyo chama/kiongozi yeyote atakumbana navyo kwenye kutekeleza majukumu yake. Cha muhimu kufanya ni kutafuta solution ya haraka kabla hii sumu haijaenea zaidi. Wakati mwingine huwa naamini kuwa sisi watanzania tu wavivu wa kufikiri na hatupendi kushughulisha akili zetu kutafakari mambo, kwa mantiki hiyo huwa ni rahisi sana kwa mtu kupotoshwa na mtu yeyote atakayeamua kupotosha pale anapoonekana kuturahisishia mambo, hasa hawa wanaojiita/wanaoitwa viongozi wa dini aidha kwa makusudi (kulinda maslahi) au kwa bahati mbaya (kwa uelewa wao mdogo).

Tukirejea kwa walengwa, nashauri ninyi wana-CHADEMA mliopo humu ndani, mchukue ushauri wa mtoa mada na mara moja muanze kueneza Propaganda misikitini na kwa waumini wa Uislamu kuwa ukombozi wa Mtanzania hauna uhusiano wowote na CHADEMA kama chama bali unawahusu watanzania wote. CHADEMA wanatekeleza jukumu lao kama sehemu ya watanzania, wengine nao watekeleze kwa upande wao, mradi lengo ni moja, basi tusihitilafiane bali tupeane moyo na ushauri pale mmoja atakapohitaji. Iwepo au isiwepo CHADEMA, ni lazima mtanzania akombolewe kutoka kwenye makucha ya wanyonyaji wachache. Uislamu na Ukiristo ni imani zenu, ziheshimuni, zipo, zilikuwepo, na mtakufa mtaziacha, tuweke imani zetu kando pale tunapodai maisha mazuri, huduma bora za afya, punguzo la bei za sukari, nauli na mchele, kuondoa kero za foleni za magari, kuchelewa kwa mishahara pamoja na kero mbali mbali ambazo zinachangiwa na uongozi wetu kutupuuza waislamu na wakristo na wapagani wa Tanzania. Waambieni kuwa akina mama wajawazito wanaokufa kwa kukosa huduma za afya ni waislam na wakiristo kwa pamoja, vibaka waliopoteza matumaini wanakaba watu wote kwa pamoja, masheikh na wachungaji. Waambieni wakati yote hayo yakitokea Viongozi wao wakuu wa dini wanapewa huduma zote muhimu na Serikali, hawabugudhiwi!!!

Well said! Ni mawazo mzuri kwa watu wasikivu na wale wanaotakia mema nchi hii, UDINI upo na unatakiwa ukemewe na watu kuelimishwa ili waondokane na UDINI. CDM watakna hadharani lakini sina shaka wanalijua tatizo hili, wachulue hatua kulitatua kabla halijakomaa.
 
kwa hali hii bora nchi ikatawaliwa na mpagani tu. Kazi yake kubwa kuwaletea wananchi maendeleo na kuwashughulikiwa wanaoleta machafuko kwa kisingizio cha dini zao za mashariki ya kati.
 
Suala ni kuwa pamoja kama taifa kupigania masuala muhimu ya taifa (bila kujali dini, maeneo tutokayo na rangi zetu)na si kuwa kama vikundi vya kidini. Tuangalie kwanza common interests, mengine yatakuja baadaye.
 
CDM angalieni nchi hii kwa upeo wa miaka 150 kutokea sasa! tusidanganyane kwa kuangalia UDINI na UKABILA kama vyanzo vya kuondoa amani ya nchi, wanaovitumia wanajua wanachotaka! Hivi viko 'inseparable' na binadamu sio Tanzania tu bali pote duniani. Dawa yake ni wahusika kuwa na uelewa na kujitambua pamoja UBORA WA MAISHA ya jamii husika badala ya kuwapanga 'waumini' wake kwenye uongozi. Haya mambo ndiyo yametufikisha hapa. Kwa waliosoma CITIZEN ya tarehe 28/02/2011 waliona jinsi TZ ilivyo ya kwanza Africa kwa imani za ushirikina (most likely duniani pia). Badala ya kuongelea udini kwa kupanga safu za waislamu na wakristo ni bora kupanga safu wa wawajibikaji ambazo zitabadilisha maisha ya watu na watasahau dini zao, makabila na ushirikina .
 
Back
Top Bottom