Elections 2010 CHADEMA: Synovate wahini mahakamani

Chadema wanahitaji kupiga kura na si kuimba kuhusu Synovate. Muda unapotea hivi hivi kwa kupiga kelele zisizo na kichwa cha kura ya maoni. Shawishini watu wawapigie kura na si kupiga kelele za kipuuzi kila siku.
 
Chadema wanahitaji kupiga kura na si kuimba kuhusu Synovate. Muda unapotea hivi hivi kwa kupiga kelele zisizo na kichwa cha kura ya maoni. Shawishini watu wawapigie kura na si kupiga kelele za kipuuzi kila siku.

Chagua wakali wa Chadema wanaotumia vichwa kufikiri.

Usichague vilaza wa CCM wanaotumia makalio kufikiri.
 
Ubaya wa kuchakachua huishia kujichakachua mwenyewe kama siyovyetu walivyofanya
 
kama kweli questionnaire yao ilikuwa na swali hili...!

'uchaguzi ukifanyika sasa hivi nani utampigia kura kuwa rais wa Tanzania?

MAJIBU YAKE YAPO WAPI..?
 
kwenye viti maalum chadema napingana na nyie haiwezekani wanaume ndiyo mkae kuwachagulia wanawake watu a kuwawakilisha hii si demkrasia ya kweli yote nawaunga mkono lakini hili hapana. Otherwise wanaume waeleze wazi wanatumia nafasi hizo kuwaendesha wanawake

najua shida salumu (mama zitto) alikuwepo na katika hili hapa wamezingatia utaalamu katika jopo la uteuzi ndio maana mkumbo na wataalam wengine wametumika. Tunachoangalia hapa ni utaalam utakaowezesha kupata wawakilishi bora na sio idadi ya wanawake wanaoingia kwenye jopo la kufanya uteuzi
 
Synovate waambiwa wawahi Mahakamani!

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeivaa kampuni utafiti ya Synovate kikisisitiza kuwa kina matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni hiyo ya kupata matokeo yaliyotoa ushindi wa asilimia 45 kwa chama hicho na mgombea wake wa urais, Dkt. Willibrod Slaa.

Synovate hivi karibuni ilikanusha habari kuwa haijawahi kufanya utafiti wala kuficha matokeo hayo yaliyodaiwa kuipa CCM na mgombea wake Rais Jakaya Kikwete asilimia 41, huku ikitishia kulishtaki gazeti moja liliwakariri viongozi wa CHADEMA wakieleza utafiti huo.


Akizungumzia matokeo hayo jana, Dkt. Slaa alisema "Synovate wakimbie haraka mahakamani, tunazo document (nyaraka), hata gazeti lililotishiwa kushtakiwa lisiwe na wasiwasi, huu ni wakati wa kuvunja heshima ya Synovate kitaifa na kimataifa.


"Walifanya utafiti na katika swali namba GP 06 waliuliza, 'uchaguzi ukifanyika sasa hivi nani utampigia kura kuwa rais wa Tanzania?' na majina yote yaliweka pale ya wagombea, sasa wanakanusha nini, waende haraka sana mahakamani, vinginevyo credibility (heshima) yao tutaivuruga nchi nzima na kimataifa, alisema huku akionesha nyaraka hizo kwa mbali.


Dkt. Slaa alisema katika nchi nyingine taasisi za maoni zinakuwa huru, hazipendelei chama chochote kile. [Chanzo kutoka Darhotwire
]
 
Back
Top Bottom