CHADEMA sasa yawaadhibu wananchi: NAPE

tatizo sio cdm tatizo watoke waende wapi? Kuna market ya kuuza bidhaa zao? Tuwe wwa kweli mtu anapotafuta ridhiki yake unamwingilia, wakaibe? Hahao mnawadai ushuru wa serikali mbona sasa mnachanganya watu, wananchi wana hasira na ukali wa maisha huku serikali imeakaa kimya , plz think twice kabla hujasema maana ndio mnaansha hisia nyingine
 
Mkuu wa mkoa ambaye hakuchaguliwa na wananchi, aliyeteuliwa na Rais mithili ya magavana wa iliyokuwa Tanganyika, anawafukuza wananchi kufanya shughuli zao! Yeye sio mkazi wa mbeya! Mbunge wa mbeya anaenda kusuluhisha halafu mjinga mmoja anasema CDM inatesa wananchi, we need a new katiba! Futilia mbali wakuu wa mikoa!
 
Hii katiba mi naona bora ipelekwe pale kwenye kaunta ya bilicanas ikarekebishwe na chapombe.
 
Tatizo ni kwamba hakuna mtu anayewasikiliza na kuwaamini CCM kwa sasa. Kauli kama hizi hazitaisaidia CCM hata kidogo bali zitawasaidia watoaji kwa kujionesha wanafanya kazi za Chama ili waendelee kupeleka mikono yao kinywani.

Serikali na CCM wanaiona hali halisi sasa wakati wakiliingiza taifa katika maigizo ya kutafuta wanayosema katiba mpya. Hili linawatisha kwelikweli na kwa maana hiyo lazima kauli za kupanic zitolewe bila mpangilio.
 
Ndiyo maana watu wakizungumza ukweli hapa jamvini watu wanasema wanaJF na JF ni wanaCDM which is not true. Ukweli ni kwamba kuna vitu ambavyo viongozi wetu wa chama tawala wamejisahau na wanadhani propaganda walizowahi kuzifanya huko nyuma zikawasaidia hata miaka hii itawasaidia.
 
Kama kaongea nape haina tatizo maana huyu mtu hakuna asiyemuelewa ni mtu wa kubwabwaja tu,mtu wa kutema pumba hana tofauti na risasi mwaulanga au tambwe hizza au paul makonda ni wale wale wakisema kitu ni propaganda/siasa za majitaka
 
Tatzo la huyu Mmakonde (Mmakonde au Mnyakyusa? mnanichanganya) ana mtindio wa KIFIKRA,ameshindwa kuelewa tatzo lililotokea Mbeya limegusa maisha ya wakazi wa mji ule,Nadhani kama Prof.Mwandosya angelikuwepo akaenda kuongea na watu wana Mbeya wangemsikiliza on behalf of SUGU kwani yeye ni mtu wa kujishusha sana kwa Wananchi kwahiyo na hapo tungesema chanzo ni CCM?Mara ngapi JK amezomewa Mbeya lakn akaokolewa na Mwandosya?Na hapo Nape ameshndwa kutambua kuwa tatzo ni wao CCM na badala yake atupia mpira kwa CDM.Serikali ya CCM endapo itaendeleza utawala wa KIIMLA itambue fika kuna watoto wadogo hawajafikisha umri wa kupiga KURA na hao 2015 kwa hasira wataiadhibu CCM,kama vile watoto wa shule moja ya secondary walotendwa vibaya na polisi kwa kupigwa na kuwekwa lumande.NAPE OPEN YOUR EYES,leo Wazanzibar wanataka kujitenga na MUUNGANO but kuna siku SOUTHERN HIGHLAND watataka kujitenga.
......penye red
 
Kumjadili nape ni kushushiana heshima. I will never take his word my consideration.
 
Amani kwenye sera ya "wapiganaji"? Highly contradictory.
Mafisadi CCM lazima wavue gamba

Kutoka Gazeti la Habarileo

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, amesema yeye ni sawa na mtu aliyeteuliwa kufanya kazi ya kunyonga mkosaji aliyehukumiwa adhabu hiyo na Mahakama, hivyo hawezi kuogopa kutekeleza hukumu hiyo.

Akifafanua kauli hiyo jana mjini Morogro, Mukama alisema uamuzi wa ngazi za juu wa CCM ukishatolewa kuhusu kuvua gamba watuhumiwa wa ufisadi, hakuna kiongozi atakayepuuza kuutekeleza.

"Ufisadi unasemwa dhahiri na wananchi kwa kuwataja watuhumiwa hadharani wakiwahusisha ana EPA (Akaunti ya Malipo ya Nje ya Benki Kuu), Dowans, ununuzi wa rada na Richmond … na vikao vya chama vimetoa uamuzi.

"Kilichobaki ni utekelezaji tu…na hukumu ikishatolewa na Mahakama hakuna njia nyingine isipokuwa kutekeleza agizo hilo," alisema Katibu Mkuu huyo alipokuwa akizungumzia madai, kwamba anaogopa kutoa barua za kujivua gamba kwa watuhumiwa wa ufisadi.

Akihutubia mahafali ya wanafunzi wanachama wa CCM wanaomaliza Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, Mukama alisema hataogopa kusimamia kikamilifu uamuzi wa chama hicho wa kuwatosa watuhumiwa hao.

Alisema vitendo vyao vimesababisha CCM na Serikali ichafuke mbele ya Watanzania.

Mbali na kuwavua gamba, Mukama alisema CCM pia itashughulikia suala la wafanyabiashara wasio waadilifu wanaojipenyeza ndani ya chama hicho, na itapambana na saratani ya kujilimbikizia madaraka na kukiondoa chama hicho katika utegemezi wa matajiri na wahisani wanaokiweka pabaya.

Alisema, hakuna mwananchi asiyejua kuwa ndani ya CCM wapo viongozi wenye nyadhifa kubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi kuanzia wa EPA, Richmond, Dowans, Rada na kashfa nyingine.

Katibu Mkuu huyo alisisitiza kwamba ili kukisafisha chama hicho mbele ya jamii na kukifanya kikubalike katika uchaguzi wowote, ni lazima watuhumiwa hao watoswe ili kurudisha imani kwa Watanzania.

Mukama alionesha katuni aliyodai imemchora hivi karibuni, akiwa na barua mkononi ikionesha kuwa ameshindwa kutoa uamuzi na kusisitiza kuwa uamuzi huo ni wa chama, hivyo utatekelezwa kama ilivyopangwa.

Awali katika risala ya wanafunzi hao, walitaka viongozi wote wa CCM kujikita kuwaletea maendeleo wananchi, ili baadaye wapimwe kwa kazi zao.

Wanachama hao waliwataka viongozi wahubiri amani badala ya kuendeleza malumbano na vyama vya upinzani na kuwataka watumishi wa Serikali kuachana na siasa wakati wakiwa watumishi wa umma.​

Hii katiba mi naona bora ipelekwe pale kwenye kaunta ya bilicanas ikarekebishwe na chapombe.
[h=1]Wasaliti CCM Kuwajibishwa[/h]Kutoka Uhuru

KATIBU wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema Chama kitawawajibisha waliohusika na uchakachuaji kura ya maoni katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Amesema hatua itachukuliwa kwa kuwa uchakachuaji huo uliigharimu CCM kwa kupata matokeo mabaya katika baadhi ya kata na majimbo. Hata hivyo, amesema Chama katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka jana, kilipata kura nyingi za urais na viti vingi vya ubunge na udiwani. Nape alisema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Fisi, Manispaa ya Lindi. Kwa mujibu wa Nape, wasaliti wa Chama wakati wa uchaguzi pia hawatasalimika, kwani hatua zitachukuliwa dhidi yao. "Tunatambua tunao viongozi na wanachama wengi waadilifu na wasiothubutu kukisaliti Chama, hawa tutawaenzi, lakini wenye tabia za usaliti na wachakachuaji wa kura ya maoni kwa faida ya matumbo yao hawa lazima tutashughulika nao katika uchaguzi mkuu ujao wa Chama," alisema.

Nape alisema hatua za kuwashughulikia ni miongoni mwa maazimio yaliyopitishwa na kikao cha NEC, kilichofanyika mjini Dodoma, Aprili, mwaka huu. Katika kikao hicho pia yalifanyika mabadiliko makubwa ya uongozi wa ngazi ya juu ya CCM kwa lengo la kukirejesha Chama katika kutekeleza matakwa ya kuasisiwa kwake.
Alisema Chama kinachukua hatua hizo, kwa sababu kinatambua kuwa bila usaliti wa viongozi wachache kisingeweza kupoteza baadhi ya majimbo na kata, katika uchaguzi mkuu uliopita.
Nape alitoa mfano wa jimbo la Lindi Mjini, ambalo lilikwenda mikononi mwa wapinzani, licha ya kuwepo wanachama wengi wa CCM ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.
"Baada ya matokeo kutangazwa, wakati huo nikiwa mkuu wa wilaya nilipita hapa Lindi mjini nikaona watoto wakishangilia kushindwa kwa CCM.
"Nikauliza mbona wanaoshangilia ni watoto, wakubwa waliopiga kura wako wapi? nikajibiwa na wenyeji waliopiga kura za kuiwezesha CUF kushinda ni wanachama wa CCM, hivyo hawawezi kutoka barabarani kushangilia kushindwa Chama chao," alisema.
 
Amani kwenye sera ya "wapiganaji"? Highly contradictory.

Tunisia,Libya, misri, madarasca ,Kenya na Zanzibar wayajua kuwa ilianzaje.?
Je watu walikufa na kuwa wakimbizi.?
Nini kimetokea sasa zanzibar ?
Atumaini amani ujui maana yake
 
Jamaa anasema ukweli, CDM wanafikiri siasa za fujo ndio zitawaendeleza. Hii serikali inawaendekeza sana. Wao wanahamasiha fujo halafu mambo yakicharuka wanatia mbio huku wakiwaacha wanachama wao wale bakora. Mfano mzuri ni yalio tokea Arusha. Viongozi wao walipotea ghafla wakati bakora zikitembezwa. Mmoja karuka ukuta na mwingine kajificha kama panya kwenye sanduku.

Unapoongelea Chadema ujue unaongelea Uma...!! grow up and pretend to be patriotic even if u cant be one
 
Nimekaa na kufikiri nimegundua kitu ambacho nakiona JK ametumia akili sana kumchagua Nape. Nape haaishi kuongea hovyo tena mambo magumu yenye utata. Katika hilo, watu wanasahau kuongelea mambo ya msingi wanabaki kutupiana lawama juu ya kauli za Nape. Ni bora Nape akapuuzwa ili tuweze kuona na kujadili makosa ya serikali.
 
[h=1]Wasaliti CCM Kuwajibishwa[/h]Kutoka Uhuru

KATIBU wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema Chama kitawawajibisha waliohusika na uchakachuaji kura ya maoni katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Amesema hatua itachukuliwa kwa kuwa uchakachuaji huo uliigharimu CCM kwa kupata matokeo mabaya katika baadhi ya kata na majimbo. Hata hivyo, amesema Chama katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka jana, kilipata kura nyingi za urais na viti vingi vya ubunge na udiwani. Nape alisema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Fisi, Manispaa ya Lindi. Kwa mujibu wa Nape, wasaliti wa Chama wakati wa uchaguzi pia hawatasalimika, kwani hatua zitachukuliwa dhidi yao. "Tunatambua tunao viongozi na wanachama wengi waadilifu na wasiothubutu kukisaliti Chama, hawa tutawaenzi, lakini wenye tabia za usaliti na wachakachuaji wa kura ya maoni kwa faida ya matumbo yao hawa lazima tutashughulika nao katika uchaguzi mkuu ujao wa Chama," alisema.

Nape alisema hatua za kuwashughulikia ni miongoni mwa maazimio yaliyopitishwa na kikao cha NEC, kilichofanyika mjini Dodoma, Aprili, mwaka huu. Katika kikao hicho pia yalifanyika mabadiliko makubwa ya uongozi wa ngazi ya juu ya CCM kwa lengo la kukirejesha Chama katika kutekeleza matakwa ya kuasisiwa kwake.
Alisema Chama kinachukua hatua hizo, kwa sababu kinatambua kuwa bila usaliti wa viongozi wachache kisingeweza kupoteza baadhi ya majimbo na kata, katika uchaguzi mkuu uliopita.
Nape alitoa mfano wa jimbo la Lindi Mjini, ambalo lilikwenda mikononi mwa wapinzani, licha ya kuwepo wanachama wengi wa CCM ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.
"Baada ya matokeo kutangazwa, wakati huo nikiwa mkuu wa wilaya nilipita hapa Lindi mjini nikaona watoto wakishangilia kushindwa kwa CCM.
"Nikauliza mbona wanaoshangilia ni watoto, wakubwa waliopiga kura wako wapi? nikajibiwa na wenyeji waliopiga kura za kuiwezesha CUF kushinda ni wanachama wa CCM, hivyo hawawezi kutoka barabarani kushangilia kushindwa Chama chao," alisema.

wanaweweseka na mabadiliko yanayotokea sasa,wananchi wamechoka kudanganywa kila siku na single yao ya kujivua gamba leo wanaleta kichagizo kingine.maisha yanazidi kuwa magumu baadala ya wao kufikiri ni jinsi gani wataboresha uchumi wao wanakalia propoganda za kuvuana gamba ina msaada wowote kwa wananchi?shame on u magamba
 
Haya masuala ya msingi kuyawekea siasa ndo yametufiksha hapa tulipo,sasa cdm sijui ndo waliwatuma mgambo wakamwage bidhaa au ilikuwaje?badala ya kutatua tatzo wapo wanawaza kwa kutumia masaburi
 
Back
Top Bottom