CHADEMA: Ole wenu mkiipokea Mizoga ya CCM!

Nadhani mengi yamesemwa mengine kwa jazba nk...lakini hebu tuutazame ukweli wa mambo? kwa nini hawa waheshimiwa wanapotoswa ndio wanahama vyama? na huko wanakokimbilia kitu cha kwanza ni kutaka kugombea? hivi wamekaa na kutafakari kwa nini wameshindwa walikotoka?na je wameshazijua vema sera za chama wanachoingia? na je wameshakubalika miongoni mwa wanachama wa vyama vyao vipya?(yaweza kuwa sio relevant ila ni muhimu kukubalika). Nahisi iko haja ya kuwapa uanachama wa kawaida kwa miaka mitano ndipo wagombee coz nina hofu yasitokee ya 1995 watu walipodhani Mrema and Co wangechukua nchi kumbe wametumwa kuvuruga upinzani.

Hao wanaoenda upinzani toka CCM nadhani baadhi yao ni waroho wa madaraka,kwani wanaona kwa kukosa nafasi CCM basi hawawezi kukaa bila madaraka ndio maana wanaona ni bora wakajaribu kupata madaraka haya kupitia vyama vingine..wachekiwe nia zao kabla ya kupewa nafasi kuwakilisha upinzani kwani nahofu kuwa iko siku wakitoswa upinzani watarejea CCM na mifano mingi tumeiona. yawezekana wana uchungu kweli wa kuleta maendeleo ila nadhani wakae kwanza wakijue chama walichokwenda au la watakuwa ni sawa na wale waliohama CCM 1995 na badae kurudi baada ya kuua iliyokuwa NCCR-Mageuzi ya kumsukuma mrema na kumbeba.

Ni maamuzi ya Chadema kuwapa nafasi wagombee ila kwa mtazamo wa kisiasa hilo laweza kuwa kosa kwa namna moja au nyingine kwani hawa bado ni wageni sana..nadhani tumeona waliokosa Chadema wameenda CUF kama alivyofanya Mwera na hii inaonesha kuwa kuna watu wao wanachotaka ni madaraka tu na si kingine,bila kujali ni wapi anakopatia madaraka hayo. mtu kakaa CCM miaka20 au 30 leo anadai chama kimeoza wakati angepita kwenye maoni sidhani kama angesema hayo yote...

Kazi kwa Chadema kupembua pumba na mchele kabla ya kuwapa nafasi waheshimiwa hawa ambao kama si mbinu ya CCM basi wachunguzwe utashi wao wa kujiunga Chadema, what is their motive? watu wanaweza kudanganyika nao au kwa umati unaotokea pindi CHADEMA wakifanya mikutano lakini kumbe ni yale yale ya Mrema and company ya 1995 yakabaki yakiumiza watu mioyo na kulia kuwa matokeo hayakuwa halali. chonde wanajamii tuwachunguze wote wanaohama baada ya kutoswa wawe wa CCm au Upinzani na nia zao huko waendako . hapo ndipo tutajua wanaimarisha au kubomoa upinzani...

Binafsi siungi mkono hawa jamaa kupewa nafasi za kugombea kwa tiketi ya upinzani bali wapewe muda ndipo wagombee..ni mtazamo tu
 
mizoga huwa imepata muda saa ngapi wa kuzijua sera za chama wanachohamia?


hata selelii aichaguliwa ubunge kwa tiketi ya chadema atakuwa ana represent chadema kweli au mawazo yake binafsi? ( if not mawazo ya ccm aliyoyazowea)

upiganiaji wa haki za wananchi sio lazima uwe mbunge tu, wangeweza pia kutumia umaarufu wao walionao kuwanadi hao wagombea waliowekwa tokea mwanzo na chama.......................hapo nafikiri tungelijua kuwa kweli wana nia thabiti, vinginevyo tunaona ni kuwakosea heshima wananchi.

je ingekuwa wewe ungechukua mda gani kuzijua sera za chadema?
au ungechukua mwaka mzima....
du hata kuzijua sera za chama unaona ni kitu kikubwa

ukiwa mbunge wa chadema lazima uzijue baadhi ya sera na itikadi za ccm na uweze kuwaambia wanachi wako kuwa sera kadhaa za ccm ni mbaya na za kwenu chadema ni nzuri,. halikadhalika ukiwa mbunge wa ccm unatakiwa ujue ya chadema ili uweze kuzipinga.. lazima ujue chadema watafanya nini na wewe uweze kuwaambia hawawezi kufanya. kwa maana hiyo hao watakojiunga na chadema tiyari wanajua what chadema stands for na itaitajika siku 1 au mbili za kupitia mambo kidogo ambayo hawayajui....
 
Wait a minute, hawa mateka wa CCM si ndio hao hao walikaa kimya kama watunga Sheria Bungeni kufikisha muswaada wa mgombea binafsi na kurekebisha sheria na katiba ambayo ingemruhusu mtu kuhama chama na asipoteze Ubunge?

Sasa kwa nini mnawaonea huruma na kuwashangilia wattu ambao walikula yamini ya kulinda ile ibara ya 15.1 ya CCM? Kama walishindwa kutengeneza mazingira mazuri kwa Watanzania wote hata kuifanya katiba kuwa ni huru isiyolinda mfumo au chama kimoja kuongoza nchi kibabe, leo hii iweje tuseme hawa wanafaa kwa kuwa watatuongezea kura?

Je kama walishindwa wajibu mdogo wa kukikatalia chama chao bila woga, iweje leo tuwe na tumaini wataliongoza Taifa vyema katika chama kipya?

Narudia tena, Mizoga=Makapi=Pumba=Mokombo=Gharasha!
 
Mkuu Rev nafikiri mawazo yako ni mazuri sana ila tusiwakatae moja kwa moja tuwape uwanachama tuwapime ifikapo 2015 kama watakuwepo then tunaweza kuamua. Kibaya ambacho mimi niko nawe ni kuwapa nafasi za kugombea wote moja kwa moja wapo baadhi tunaweza kuwapa kutokana na mazingira lakini isiharibu utulivu ndani ya chama.

Nafikiri hili ni la msingi, nilishawahi kusema hapa, kwa kuchukua mfano wa dini, kwamba hata Wakatoliki ukitaka kujiunga nao wanakupa muda kujifunza "kateki Ama sivyo unaweza kuwa mpinga kristo unayetaka kuingia katika system yao kuchunguza vitu tu.

Wapeni miaka mitano hii, itatupa muda wa kuwapima kama kweli wanakipenda chama au wanataka ubunge tu.
 
Kuna wengine wanadai ati hawa makapi walionewa, wamedhulumiwa, wamehujumiwa; swali je wao walipoafiki kwa kura zao kila kitu ambacho kimeendeleza dhuluma kwa Mtanzania hata vyama vya Upinzani ili kunufaisha CCM hamkuliona hilo na kulilalamikia?

Iwe ni kura zao za ndio ndani ya Bunge au Mkutano Mkuu wa CCM, je kwa nini kama waoni CCM Taifa na si CCM 15.1, kwa nini basi hata kwenye kumteua mgombea wa CCM ni Kikwete alipitishwa kwa kura nyingi takriban asilimia 99.99%?

Wao walinufaika na kuneemeka kwa kuwa washika hatamu ya Chama chenye kudhulumu na kuhujumu Watanzania, basi wabakie hukohuko na tuwaone wakifanya mapinduzi ndani ya Chama chao CCM na si kujidai kwa kuhamia Upinzani, ndipo wataleta mafanikio na maendeleo kwa mtanzania na kujenga mfumo wenye haki sawa.
 
Nafikiri hili ni la msingi, nilishawahi kusema hapa, kwa kuchukua mfano wa dini, kwamba hata Wakatoliki ukitaka kujiunga nao wanakupa muda kujifunza "kateki Ama sivyo unaweza kuwa mpinga kristo unayetaka kuingia katika system yao kuchunguza vitu tu.

Wapeni miaka mitano hii, itatupa muda wa kuwapima kama kweli wanakipenda chama au wanataka ubunge tu.

Kateki ni kitu gani bro!
 
Katika mapambano ukiokota silaha ya adui hata kama inarisasi moja ichukue na uitumie huenda ikakuokoa
 
Katika mapambano ukiokota silaha ya adui hata kama inarisasi moja ichukue na uitumie huenda ikakuokoa

Lakini angalia usiokote bomu litakalokulipukia, hawa watu wengi ni mabomu yanayotick, ukifika muda wake yatalipuka.
 
Mimi naweza kutabiri (kwa urahisi bila kutumia mbinu za jadi) hawa wanaokimbiliia sasa Chadema wakishindwa hawatadumu ndani ya cHadema. Ila wakishinda ndio watabakia hadi mwisho wa bunge lijalo au ndio yatakuwa ya kina Lamwai au Dr. Kaborou. Vyovyote vile ilivyo iwe ni case on case basis. Sipendi Chadema iwe ni kimbilio la waliokataliwa CCM. TEna ingekuwa vizuri sana kama Chadema ingekuwa imetangaza wagombea wake a month before ili kuweka presha kwa watu waliosalia CCM. Lakini sasa inaonekana CHadema imewapigia mahesabu watakaotoka CCM.

Kwa hiyo ni lazima tupime na gharama yake vile vile kwa sababu wakipoteza nafasi hizo na wakajirudi CCM na kuanza kusema "chadema haichaguliki" au "Sera za Chadema ni mbaya".. kuna watu watajisikia wameuzwa bure!
 
Nadhani hili lafaa liangaliwe vizuri kwa makini. Ni kweli si vizuri kuwapapatikia hawa watu kwani wanaonekana ni maopportunist ambao ugali wao umeingia mchanga wanatafuta ugali mwingine, lakini pia ikumbukwe kuwa CCM ni chama kikongwe, hivyo wanachama wake wanaweza kuleta chachu fulani katika upinzani na kuipa CCM a run for its money. Haitakuwa business as usual kwani wanafahamu fika siri zao na pia wanazo networks na connections ambazo zinaweza kuisaidia CHADEMA.
CCM wameshaamua nani watawawakilisha kwenye Ubunge, wamechuja chuya, wametupa makapi na mizoga.

Sasa natoa tahadhari kwa CHADEMA; Ole wenu mkiipokea hii mizoga ya CCM na kuipa kadi na hata kuwafanya wagombea wenu kwenye majimbo, mtajishushia hadhi na kuonekana chama kisicho na maana na ni hifadhi ya mizoga na makapi.

Jiulizeni kwa nini hawa mizoga, makapi na pumba kwa nini walisubiri kuenguliwa na CCM ndipo wakakimblia kwenu? Kwa nini tangu awali hawakufanya uamuzi wa kuhamia CHADEMA kabla ya kushindwa ndani ya CCM na hivyo baada ya kutalikiwa wanakuja kwenu nanyi mnawapa Ufestiledi kwenye majimbo?
 
Wait a minute, hawa mateka wa CCM si ndio hao hao walikaa kimya kama watunga Sheria Bungeni kufikisha muswaada wa mgombea binafsi na kurekebisha sheria na katiba ambayo ingemruhusu mtu kuhama chama na asipoteze Ubunge?

Sasa kwa nini mnawaonea huruma na kuwashangilia wattu ambao walikula yamini ya kulinda ile ibara ya 15.1 ya CCM? Kama walishindwa kutengeneza mazingira mazuri kwa Watanzania wote hata kuifanya katiba kuwa ni huru isiyolinda mfumo au chama kimoja kuongoza nchi kibabe, leo hii iweje tuseme hawa wanafaa kwa kuwa watatuongezea kura?

Je kama walishindwa wajibu mdogo wa kukikatalia chama chao bila woga, iweje leo tuwe na tumaini wataliongoza Taifa vyema katika chama kipya?

Narudia tena, Mizoga=Makapi=Pumba=Mokombo=Gharasha!

Baniani mbaya kiatu chake dawa.......We si mchungaji?? unasahau ya mtume Paulo?? alikua nani kabla ya kumgeukia kristo.......? Hakatazwi mtu kutubu na kugeuka kwenye mambo ya msingi kama ya Dini...sembuse siasa..!?

Hawa si makombo wala makapi hawa ni wana wapotevu walioamua kubadilika na kuzaliwa Upya....! Kwanini tuwahukumu kabla ya wakati..! time will tell ila kwa sasa tunawapa benefit of the doubt..!
 
Kuna wimbi sasa hivi la waliobwangwa na CCM kwenye kura zao za maoni kukimbilia CHADEMA. Ni haki yao kikatiba lakini tahadharini wakuu wa CHADEMA epukeni kuwa kokoro na kubeba hata visivyofaa. Mnaweza kufikiri kwamba mumepata mtaji wa kukuza chama chenu kuelekea uchaguz mkuu, lakini kwa watu makini watawadharau sana na kupoteza imani na nyinyi kama mtapokea ovyo ovyo bila kuchuja taka taka zilizotupwa.



"Moringe wote ni wamasai lakini sio kila mmasai ni Moringe".
 
Asante Inkoskazi, mwenyewe hilo nimekuwa nikilifikiria sana na kuanza kukosa imani na Chadema, manake inakuwa kama walikuwa hajajipanga vya kutosha na kuwa na uhaba wa wagombea makini, haina sababu ya kung'ang'ania watu walioshindwa huko watokako ati tu kwa sababu ya uzoefu na umaarufu wao. Tusipoziamini na kuzijaribu damu mpya tutapataje vijana makini kama kina ZITO, MDEE, MNYIKA na wengine?

Hebu Chadema amkeni achaneni na hao watu walioshindikana huko watokako, wapeni watu wapya nafasi za uongozi, naamini kuna watu wengi makini wenye sifa na uwezo mkubwa wa uongozi ila hawapewi nafasi. Hayo mambo ya zoa zoa yaliiponza NCCR-MAGEUZI enzi za Mrema. Chadema kumbukeni watanzania wameanza kuamka kwa kasi ya ajabu na wanataka mabadiliko na uongozi mpya ulio makini na wameanza kujenga imani kwenu.
 
Labda nigeuze mchakato wa mada hii tena kwa upande mwingine. Leo hii, magazti yanamnukuu Zitto akidai kuwa wanamtaka Bashe agombee huku CCM wamemkata kwa hisia si raia. Bashee alipaa kura nyingi sana za wana CCM< lakini je anaweza pata kura ngapi za Watanzania wa jimbo lake?

Ama, ikiwa leo CHADEMA au upinzani unakimbilia kuteua mateka kuwa wagombea katika majimbo, hili linaashiria nini kuhusu uhai wa Chadema katika majimbo Tanzania? Je hakuna hata mwanachama mmoja mwenye mvuto au uwezo katika jimbo kugombea mpaka tegemeo liwekwe kwa mateka kutoka CCM? Kama ndivyo, je mnalipokeaje sasa suaal hili la kukosa hata watu imara kugombea Ubunge, je kuongoza Serikali watakuweza?
 
jamani kuna baadhi siyo mizoga na chadema inawajua na si tunawajua ila wale mizoga wapigwe chini wabaki huko mtaani
 
Bashee alipaa kura nyingi sana za wana CCM< lakini je anaweza pata kura ngapi za Watanzania wa jimbo lake?

Hili halijibiki mpaka uchaguzi ufanyike ila hizo 14,000 alizopata kutoka kwa wana CCM ni mtaji mzuri kuanzia

Ama, ikiwa leo CHADEMA au upinzani unakimbilia kuteua mateka kuwa wagombea katika majimbo, hili linaashiria nini kuhusu uhai wa Chadema katika majimbo Tanzania?
Hii inaashiria kukua na kukubalika, Siasa mtaji wake ni watu na huwezi kubagua wanachama wako as long as wana sifa zinazokidhi katiba ya chama.

Je hakuna hata mwanachama mmoja mwenye mvuto au uwezo katika jimbo kugombea mpaka tegemeo liwekwe kwa mateka kutoka CCM?
Wangekuwepo wangegombea na kuchaguliwa, hao unaowaita mateka pindi wanapojiunga na chadema wanakuwa wana Chadema na si vinginevyo..!

Kama ndivyo, je mnalipokeaje sasa suaal hili la kukosa hata watu imara kugombea Ubunge, je kuongoza Serikali watakuweza?
Kuongoza Serikali si shida maana Chadema ishaliweka wazi hili kuwa haiwezi kuongoza peke yake Kutakua na Serikali ya umoja wa kitaifa..watu makini kutoka CCM,CUF na wengine makini watashirikishwa..!
 
Rev. Kishoka,
Mkuu wangu pengine umesahau au huelewi kwamba vita ya Chadema ni kuwaondoa CCM madarakani. Dhamira hii haijabadilika kwani hii ni Vita baridi ya kisiasa..Na kutokana na kutoelewa huku ndiko kumewafanya wengi wenu msijiunge na Chadema ktk vita hii toka awali. Chadema will use all means hata iwe vifaa vya CCM wenyewe kupata ushindi kama Nyerere alivyompiga Idd amin na mizinga yake mwenyewe kushinda vita.

Kwa hiyo mnashindwa kuelewa kwamba hapa sii swala la demokrasia at it's best, ila ni kuitumia demokrasia hiyo hiyo inapowezekana kutumika kwani Mungu katukataza kuua lakini ukiwa vitani huwezi kuweka silaha chini ukisema ati Mungu alikataza kuua na haitakuwa haki kkuua ili upande kumshinda adui yako..

Strategy ya Chadema ni ya Ushindi by all means hayo ya Demokrasia na Itikadi huu sio wakati wake na ndio maana hadi sasa hivi mnashindwa kuwaelewa Chadema kwani kama ingebidi kuchukua silaha ingekuwa hatuzungumzii tena demokrasia wala usalama wa Taifa isipokuwa kwa uzito wa hatua walizochukua.

Alichofanya Zitto ni kuchekecha hao mizoga ili kupata kinachoweza kulika. Zitto baada ya kutopa taarifa za hao waliojiunga wale wenye woga na kujificha wamekimbilia kukana kujitoa CCM. na kama nilivyowahi kusema siku za nyuma kutoka CCM na kujiunga Chadema haitakuwa kazi ndogo kwao. Watatangazwa magazetini na hakuna Usiri, watavikwa majezi na penbgine hata kupewa wajibu ambao hawatapenda kuufanya ili mradi wanapimwa Uaminifu wao kwa chama na hasa vita hii.

Kwa Chadema hili swala lipo beyond maslahi ya Chama au matakwa ya demokrasia - ni swala la Mustakabali wa Taifa letu ambao uko hatarini. Uhatari ambao pengine nyie mnashindwa kuusoma au kukifikiria isipokuwa mnaona tu sheria na taratibu za demokrasia ambayo haipo nchini to begin with..Tukishindwa sasa hivi, they will be no 2015...Take my word for that!
 
Back
Top Bottom