CHADEMA: Ole wenu mkiipokea Mizoga ya CCM!

Wenye kuelewa siasa wameelewa nilichokisema, wasiojua siasa ndio mwakimbilia kuangua vilio. Jibu langu ni moja, kama hukuhama chama ulichokuwa mwanzonii kwa hiari, ukasubiri kuangushwa kwenye kura za maoni au maamuzi ya vikao cha chama wewe ni sawa na Mzoga=Makapi=Pumba=Makombo!

Hufai kwenda kwingine ila huko huko walikokukataa!
 
Hello Kishoka
watu wote wanaokatiliwa ni mizoga?
support jibu lako!

Mutu,

Kwa heshima na taadhima kubwa, naomba urudi usome kila nilichoandika kuhusiana na hili la wahamiaji waliokosa kura za CCM, kisha uoanishe mwenyewe ninachokimaanisha kabla ya kuingia hamaki kama klorokwini alivyoingia kichwa kichwa!
 
Si kweli kuwa wote walio temwa na CCM ni makapi au Mizoga! Kwanza tangu lini binadamu aliye hai akawa mzoga? Hebu wana jamii tuchaguwe maneno yakuandika.

Mtu kuhama kutoka CCM baada ya kuenguliwa kwa mizengwe na kuhamia chama kingine bado hiyo ni haki yake kufanya hivyo,na hiyo haimfanyi aonekane kuwa ni makapi ya CCM,kila mmoja ukimuuliza alihamaje kutoka chama kile na kujiunga na chama kingine; utapata majibu tofauti na sababu tofauti.

Hivyo walionasifa na kweli bado wanakubalika kwa wapiga kura sioni sababu ya kuwanyima haki hiyo.
 
CCM wameshaamua nani watawawakilisha kwenye Ubunge, wamechuja chuya, wametupa makapi na mizoga.

Sasa natoa tahadhari kwa CHADEMA; Ole wenu mkiipokea hii mizoga ya CCM na kuipa kadi na hata kuwafanya wagombea wenu kwenye majimbo, mtajishushia hadhi na kuonekana chama kisicho na maana na ni hifadhi ya mizoga na makapi.

Jiulizeni kwa nini hawa mizoga, makapi na pumba kwa nini walisubiri kuenguliwa na CCM ndipo wakakimblia kwenu? Kwa nini tangu awali hawakufanya uamuzi wa kuhamia CHADEMA kabla ya kushindwa ndani ya CCM na hivyo baada ya kutalikiwa wanakuja kwenu nanyi mnawapa Ufestiledi kwenye majimbo?

La Hasha! Si kweli kabisa kuwa kila aliye enguliwa na vikao vya juu vya CCM ni makapi. Kuna watu wengi tu wamej engewa zengwe na CC japo wamepita kwenye kura za maoni na ni candidates wanaouzika na kukubalika kwa wananchi. Je hao wakihamia CHADEMA na kupeperusha bendera ya CHADEMA kuna ubaya gani kwani haja ni kupanua representation ya Upinzani Bungeni. Au?
 
Katiba ya CHADEMA haisemi mkatalie muomba uanachama kama katoka kugombea chama kingine.

Akiingia chamani, akafata mchakato wa demokrasia ndani ya chama, akawapiku wanachama wa siku nyingi katika kupata tiketi ya chama, basi mwache awe mgombea.

Vinginevyo ni kuiga mfumo wa CCM ambao vikao vya juu vinaamua nani agombee hata kama wanachama hawamtaki.

Katiba ya CHADEMA pia haisemi kwamba mtaka ugombea akisubiri katikati ya mkutano mkuu na kujivua serawili (ashakum si matusi), na kunyesha mashonde meza kuu, akataliwe kugombea ubunge, lakini hii haimaanishi kwamba ukienda kufanya hivi, to forward an understatement, utapewa nafasi kugombea ubunge. Katiba ni muongozo wa mambo kijumla na haiwezi ku address kila swala, kuna mambo mengine watu inabidi waende kwa pragmatic principles tu.

Kama mtu alikuwa na muda wote huo kujiunga CHADEMA, na hakujiunga mpaka alipokataliwa na chama chake, anatuonyesha mapenzi yake yapo kwenye ubunge zaidi kuliko CHADEMA. Kama mimi ndiye mtu wa CHADEMA nitakuwa naogopa sana watu wenye mapenzi na ubunge kuliko CHADEMA.
 
Let me see, who are the classic example of Makapi: Masumbuko Lamwai, Tambwe... umm...
 
Kuna maswali ya msingi kweli yanayohitaji tafakari. Mojawapo ni swali ambalo nimeuliza mara nyingi huko nyuma "waing'oe CCM ili kiwe nini?" Swali hili kwa wengine limekuwa ni kikwazo na wengine wanaona halistahili hata kuulizwa. Lakini tukilipeleka kwenye suala la wagombea hatuna budi kujiuliza:

a. Chadema inataka kusimamisha wabunge wengi wanaochaguliwa;

b. Wabunge hawa wataingia madarakani ili wafanye nini?

c. Kama lengo ni kupata TU wabunge wengi wanaochagulika basi Chadema ipokee mtu yeyote na kumpa nafasi ya kugombea katika Ubunge ili wapata hilo jimbo.

d. Lakini mwisho swali litakuwa ni lile lile, itakuwaje kama wanaoingia wameingia kwa ajili ya kupata nafasi ya kushinda tu waende Bungeni hata kama hawaamini itikadi, ajenda na malengo ya chama?

Binafsi ningependa Chadema iweke masharti kwa wabunge wake wote kuwa asilimia 15 ya mapato yao yote ya Ubunge (mshahara na marupurupu) yatachangia mfuko wa chama. Lakini nafahamu upande mmoja kutakuwa na faida ya kuwa na wabunge wengi (hata wasioamini sana chama) kwani ruzuku kubwa itapatikana kwa wabunge wengi na hapo Chadema itaweza kujijenga.

Sasa upande mmoja kuna suala la demokrasia na mwonekano; na upande mwingine ni faida zinazoweza kupatikana.

Hivyo maoni yangu mimi ni kutokuwa na msimamo wa ujumla (kama unaopendezwa na Reverend hapa); binafsi ningependa Chadema ifanye mambo yale "case on case basis" yaani kila anayekimbilia Chadema ahukumiwe kwa mambo yake. Kwa mfano Selelii akitaka kugombea kupitia Chadema yawezekana ana kesi nzuri zaidi ya kumrudisha Bungeni.

Matatizo mengine inabidi niyameze tu maana wengine wanaweza kuona siwatakii mema Chadema. Inabidi nipunguze ukosoaji wangu.
 
So MM, let me get this straight, if Seleli is to be selected over Regia Mtema let say in Kilombero, you will bless the move?
 
mizoga huwa imepata muda saa ngapi wa kuzijua sera za chama wanachohamia?


hata selelii aichaguliwa ubunge kwa tiketi ya chadema atakuwa ana represent chadema kweli au mawazo yake binafsi? ( if not mawazo ya ccm aliyoyazowea)

upiganiaji wa haki za wananchi sio lazima uwe mbunge tu, wangeweza pia kutumia umaarufu wao walionao kuwanadi hao wagombea waliowekwa tokea mwanzo na chama.......................hapo nafikiri tungelijua kuwa kweli wana nia thabiti, vinginevyo tunaona ni kuwakosea heshima wananchi.
shukrani G, nahisi baadhi ya wachangiaji hawaelewi maana ya mzoga wa kisiasa... Achilia mbali kwamba si lazma uwe mbunge kusaidia nchi yako na ndugu zako. What i see ni hawa mizoga kutegemea siasa kama ajira pekee hivyo kuwa tayari kufanya chochote wasipoteze ajira
 
Rev Kishoka
Kwa mara ya kwanza natofautiana nawe. Hao walioachwa na CCM siyo mizoga kwa concept yako bali kuna mchezo unaoendelea ndani ya CCM (unaujua) kuwaweka pembeni wale wote ambao wana nia ya dhati kuitumikia nchi kwa misimamo isiyitiwa maji. Pia CCM inakumbatia matajiri na wapiga filimbi wa hamelin hivyo usitegemee mtu makini atapenya kule. Ingawa sikatai kuna ambao hata uwaoshe na kuwasugua kwa brush ya dhahabu hawasafishiki.

Kishoka, hebu nieleze kisa cha CCM kumkumbatia Lowasa, Rostam, Chenge na Kikwete ilihali wameshaprove kuwa hawafai kwa matendo yao...?
Nadhani CHADEMA wanaweza kuchuja na kupata waliomakini ili kuendeleza dhana ya upinzani wa kweli bungeni.
 
THANKS REV

post number 11 tells it all, kama wana uoendo na nchi, wasubiri five years from now... one can not transform in 3 weeks to know sera za chama, watu wake culture yao na pia kuwawakilisha kwenye uchaguzi

down with political prostitutes

Lakini kama una UWEZO wa kumtumia prostitutes vizuri kwa faida yako, sioni kwa nini usiwatumie. Hivyo yote yatabakia kwa CHADEMA kuonyesha busara na ubingwa wao namna wawezavyo kutumia na kudhibiti hao PROSTITUTES, kama prostitute atashinda jimbo basi itakuwa sifa kwa CHADEMA na akikosa itakua kinyume chake.
 
Lakini kama una UWEZO wa kumtumia prostitutes vizuri kwa faida yako, sioni kwa nini usiwatumie. Hivyo yote yatabakia kwa CHADEMA kuonyesha busara na ubingwa wao namna wawezavyo kutumia na kudhibiti hao PROSTITUTES, kama prostitute atashinda jimbo basi itakuwa sifa kwa CHADEMA na akikosa itakua kinyume chake.
it is immoral and if that is the way we want to build our nation basi tumekwisha.... maana atakuja mwenye fungu azidi atamchukua huyo malaya wa kisiasa na unabaki kama breeding site ya hao vibwengo... NI SAWA NA KUJENGA NYUMBA KWA KUTUMIA TOFALI LA BARAFU, JUA LIKIWAKA LINAYEYUKA... PERIOD

the bottom line, siasa za kujenga nchi haziandaliwi kwa short term strategies, na ndio tatizo la wapinzani, they want cheap popularity!!!!
 
Wenye kuelewa siasa wameelewa nilichokisema, wasiojua siasa ndio mwakimbilia kuangua vilio. Jibu langu ni moja, kama hukuhama chama ulichokuwa mwanzonii kwa hiari, ukasubiri kuangushwa kwenye kura za maoni au maamuzi ya vikao cha chama wewe ni sawa na Mzoga=Makapi=Pumba=Makombo!

Hufai kwenda kwingine ila huko huko walikokukataa!

Waliotemwa CCM wamiminika Chadema
Boniface Meena
BAADA ya kukosa ridhaa ya kugombdea ubunge kwa tiketi ya CCM kutokana na chekeche la mwisho la halmashauri kuu ya chama hicho, waliokuwa wagombea ubunge na wanachama waandamizi watano wamekitema chama hicho na kuhamia Chadema.

Baada ya kumalizika kwa kura za maoni ndani ya CCM ambazo ziliripotiwa kuwa zilijaa rafu, ukiukwaji wa taratibu na wagombea kukamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), tegemeo la mwisho la wagombea wote lilikuwa kwa halmashauri kuu ambayo ilimaliza kikao chake Jumamosi.

Chombo hicho chenye nguvu ndani ya CCM kilibatilisha ushindi wa wagombea watatu tu na kuidhinisha ushindi kwenye majimbo mengine yote licha ya kuwepo malalamiko na rufaa nyingi kupinga ushindi.

Naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe aliiambia Mwananchi kuwa wanachama wa CCM waliojiunga na chama chake kuwa ni Dk Raphael Chegeni, John Shibuda, Alatanga Nyagawa na Thomas Nyimbo.

Alisema kuwa kwa sasa tayari wameshawachukua hao na wanafanya jitihada za kumpata aliyekuwa mshindi kwenye kura za maoni jimbo la Nzega, Hussein Bashe ili aweze kugombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema. Bashe alimuangusha mbunge aliyemaliza muda wake, Lucas Selelii kwa kura nyingi, lakini CCM imemteua mshindi wa tatu kugombea ubunge.

Kabwe alisema kuwa tayari wameshampitisha Shibuda agombee ubunge wa jimbo la Maswa Mashariki kwa tiketi ya Chadema, huku Chegeni akipitishwa kugombea jimbo la Magu, Nyagawa jimbo la Njombe Kaskazini na Nyimbo jimbo la Njombe Magharibi.

"Hao wanne tayari tumeshakubaliana nao na tunazidi kuwatafuta wengine kama aliyeshindwa jimbo la Nkenge ambaye sitamtaja jina kwa sasa ila tuna matumaini ya kumpata pamoja na mwingine wa Shinyanga Mjini," alisema Kabwe.

Alisema kuhusu Bashe, Zitto alisema wanataka kumchukua ili kuwaonyesha Watanzania kuwa hawana ubaguzi wa rangi kwa CCM wanamjua Bashe kwa muda mrefu na inashangaza kwamba wakati huu ndio wamemgeuka kwa kigezo cha uraia.

"Tuko katika mazungumzo na Bashe tunajitahidi tumpate ili akasimame kwa niaba ya chama chetu huko Nzega... kwanza alipitishwa kwa kura nyingi ikimaanisha kuwa ataweze kukitetea chama ipasavyo," alisema Kabwe.
Alisema kuwa CCM si mamlaka ya kusema mtu fulani ni raia au si raia hivyo walichokifanya si sawa bali wameingilia mamlaka nyingine.

"Baba yake Bashe yuko Nzega pale, kwa nini wasiende kumfuata na kumuuliza? Hawa CCM wamekuwa na Bashe kwa muda mrefu iweje wanamgeuka sasa," alihoji Kabwe.

Aliongeza kusema: "Tunapinga ubaguzi kwa mtu yeyote, kwa hiyo tunamtaka."


chegeni%20mp.jpg
Dk Chegeni

Alipoulizwa kuhusu habari za kuhamia Chadema, Dk Chegeni (Pichani) alikiri kufanya mazungumzo na viongozi wa chama hicho lakini akawaeleza kuwa alikuwa safarini na alitarajia kumalizia mazungumzo, ingawa alisema mpaka jana jioni hakuwa amefikia uamuzi.

Alisema kuwa hawezi kuzugumzia kwa kina suala hilo kwa sasa kwa kwa sababu bado hajafanya uamuzi wa kujiunga na Chadema.

Kabla ya kujiunga na Chadema, Shibuda alikuwa katika ziara za kuaga wazee na marafiki zake wa siku nyingi ndani ya chama hicho tawala.
Shibuda, mwanasiasa mwenye historia nzito ndani ya CCM tangu enzi za Mwalimu, alifafanua kwamba asingeweza kufanya maamuzi magumu bila kuagana na wazee waliomlea katika chama.

Mbunge huyo wa zamani wa Maswa, alifafanua kwamba wapo wazee ndani ya CCM ambao anawaheshimu kwa kuwa ndio waliomtoa gizani na kumpandisha chati katika siasa.

Katika safari hiyo ya kuaga wazee, Shibuda alisema wiki iliyopita alikuwa visiwani Zanzibar alikokuita kuwa ndiko alikokulia na kukomaa kisiasa.

"Mimi niko Zanzibar nakutana na kuagana na wazee wangu. Nimelelewa Zanzibar ambako ndiko nilikokulia na kulelewa katika mazingira mazuri ya kisiasa," alifafanua.

Dk Chegeni, ambaye alikuwa mbunge wa Busega aliangushwa kwenye kura za maoni na Dk Titus Kamani Mlengenya, wakati Shibuda ambaye aliangushwa na Martine Makondo kwenye jimbo la Maswa Mashariki.

Naye Nyimbo alishinda kwenye kura za maoni lakini jina lake lilienguliwa na kupitishwa Gerson Lwenge na kwa upande wa Nyagawa atapambana na mwenyekiti wa CCM mkoani Iringa, De Sanga (Jah People) akiibeba Chadema.

Katika kura za maoni za CCM, zaidi ya wabunge 60, wakiwemo mawaziri watano, waliangushwa na halmashauri kuu haikuwa na huruma kwa mawaziri hao na wabunge wa muda mrefu, akiwemo mwanasiasa mkongwe na waziri wa zamani, John Malecela ambaye aliangushwa kwenye kura za maoni za jimbo la Mtera.

Mbali na kigogo huyo ambaye alianza kuitumikia nchi tangu nchi ilipopata uhuru, wabunge wengine walioanguka ni Joseph Mungai (Mufindi Mashariki), Jackson Makweta (Njombe Kaskazini), Prof Philemon Sarungi (Rorya) na Dk Ibrahim Msabaha (Kibaha Mjini).

Wengine ambao wameshaanguka ni Bujiku Sakila (Kwimba), William Shelukindo (Bumburi), Raphael Mwalyosi (Ludewa) na Zainab Gama (Kibaha Mjini).

Wabunge wengine ambao hawajakitumikia chombo hicho kwa muda mrefu, lakini wameanguka kwenye kura za maoni ni Ludovic Mwananzila (Kalambo), Ponsian Nyami (Nkasi Kaskazini), Yono Kevela (Njombe Magharibi), Felix Mrema (Arusha Mjini), Ramadhan Maneno (Chalinze) na George Lubeleje (Mpwapwa).

Mawaziri walioshindwa vibaya kwenye kura za maoni ni pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Diodorus Kamala, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera (Korogwe Mjini) na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, James Wanyancha.
 
CHADEMA tuko makini, ndio maana hata mwaka 1995 , tulimkatalia Mrema kuwa mweyekiti wetu baada ya kukimbia CCM, TULIMWAMBIA, taratibu lazima zifanywe, si tu umaarufu wako, hilo pia limemkumba mzee wa CCJ, amekwama Segerea, kwasababu tunaamini katika utaratibu na demokrasia.
 
Kwa nini hatutaki kujifunza kutoka kwa jirani zetu? Wao waliazimia kumtoa KANU kwa namna yeyote ile na walifanikiwa, kwa mchango mkubwa wa hao mercenaries. Leo hii wananuka kuliko hata KANU!

Kuna jamaa nimesoma kuwa wameingia CHADEMA lakini wakati wakiwa katika nafasi za uongozi walishiriki kikamilifu katika kuendeleza libeneke la dhulma kwa wananchi. Leo tunategemea kuwa watabadilika kwa sababu tu wako CHADEMA? Hao so-called wapiganaji walirukia ishu ambazo walizileta wenzao na kuzipunguza makali.

Kumkemea Mkapa ni rahisi lakini nani kati yao alikuwa tayari na kupambana na mzizi mzima wa huo uozo? Nani kati yao alisimama kidete na wakina Slaa walipokuwa wakihoji maovu ya vyama vyao? Hao walikuwa opportunists, dyed in the wool populists. Wanakimbilia CHADEMA kwa sababu ndio flavour of the month. Upepo ukibadilika watawatosa. CHADEMA lazima wawe makini nao.

Amandla.....
 
CCM wameshaamua nani watawawakilisha kwenye Ubunge, wamechuja chuya, wametupa makapi na mizoga.

Sasa natoa tahadhari kwa CHADEMA; Ole wenu mkiipokea hii mizoga ya CCM na kuipa kadi na hata kuwafanya wagombea wenu kwenye majimbo, mtajishushia hadhi na kuonekana chama kisicho na maana na ni hifadhi ya mizoga na makapi.

Jiulizeni kwa nini hawa mizoga, makapi na pumba kwa nini walisubiri kuenguliwa na CCM ndipo wakakimblia kwenu? Kwa nini tangu awali hawakufanya uamuzi wa kuhamia CHADEMA kabla ya kushindwa ndani ya CCM na hivyo baada ya kutalikiwa wanakuja kwenu nanyi mnawapa Ufestiledi kwenye majimbo?

Nani kakwambia ndani ya Chadema hakuna mizoga, mizoga ipo kila mahali na ndani ya kila chama. Kinacho matter ni namna gani mtaidhibiti
 
Kuongezea alivyosema Kichuguu, hivi CHADEMA itakuwa ina send message gani kwa wanachama wake waadilifu wa miaka mingi wanaotaka kugombea ubunge kama kizito mmoja aliyekataliwa na CCM anakuja na kuchukua ugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA katika muda wa siku chache? Hii haitakuwa na effect ya kuua morale kwa watu waliomenyeka kutafuta wanachama na ku fanya grassroot campaigns miaka yote hii?

Mimi kama niko katika position ya kugombea ubunge, nimweweka muda mwingi katika kuhughulikia mambo ya CHADEMA, halafu anakuja kigogo mmoja kutoka CCM anapewa ugombea ubunge just like that nitaona kama nimetukanwa.

Kiranga

Naona Concern yako!Kimsingi naiafiki lakini...,

1. Kama ilivyosemwa sio lazima "Kigogo" akija CHADEMA apewe jimbo ...anaweza akachangia Ukigogo na uzoefu mwingine bila kuwa Mbunge.
2. Swala la kuja kwa mwanachama mpya na HAKI ya yeye kupewa jimbo itategemea Maamuzi ya Chama na sio lazima apewe nafasi hiyo kama kuna mtu mwingine tayari anonyesha kila hali ya kufanya vizuri kwenye nafasi hiyo!
3. Kama amekuja mwanachama mpya ... na inaonekana wazi anaweza kuleta ushindi wa jimbo fulani ... ambalo akipewa Mwanachama wa siku nyingi inaonekana litapotea.... Definetly Busara ianaonyesha Kigogo/mwanachama wa kuja apewa nafasi for the sake of the CHAMA!
4. Kwa vyovyote vile anachosema Mchungaji na wachangiaji wengine kuh "Mizoga" ni sawa lakini ni sawa zaidi Kuangalia maendeleo ya chama na si kwa kuangalia fadhila ya wanachama waliokaa muda mrefu CHADEMA sasa iwe ni zamu yao kuutwaa Ubunge ...hata kama inaonekana wazi kuwa atashindwa na huku Rejct from CCM anaonekana kabisa atashinda.
5. Ni kweli lazima kuwa na vigezo kadhaa ambavyo kila chama kimejiwekea kuwapata wagombea ubunge wake. Hata CHADEMA wana vigezo vyao. Kigezo cha kuangalia muda wa mwanachama kuweko Kwenye chama na muda wa mchango wake ni muhimu ili kutowavunja moyo wakongwe. Lakini kwa kuwa vigezo hivi ni ili kuwezesha ushindi...then, Mkongwe akubali na ajisikie vizuri kama jimbo analotaka kogombea uongozi linaweza kupatikana na mwanachama mpya. Ni Kama tu Alivyofanya Mwenyekiti Mbowe, alikuwa radhi kabisa Kutokogombea kwa nafasi ya RAIS kulingana na hali halisi ilivyokuwa na ninafikiri angetokea Mwanachama mwingine Hata "KOGOGO" kutoka CCM au kwingine anayekubalika akaja na Chama kikatathmini kikaona angefaa ..... nafikiri ingekuwa sawa! Na angekuwa amewaacha wanachama wengi wa siku nyingi ndani ya CHADEMA!nafikiri ingekuwa sawa. Na wanchama wote wangeungana na Kufurahia ushindi wa Chama na wa jamii yote.
 
Mkuu Rev nafikiri mawazo yako ni mazuri sana ila tusiwakatae moja kwa moja tuwape uwanachama tuwapime ifikapo 2015 kama watakuwepo then tunaweza kuamua. Kibaya ambacho mimi niko nawe ni kuwapa nafasi za kugombea wote moja kwa moja wapo baadhi tunaweza kuwapa kutokana na mazingira lakini isiharibu utulivu ndani ya chama.
 
CHADEMA ni vema muwe makini kuchunguza wanachama wapya hasa wale ambao wamekosa nafasi SSM na wanakuja kuomba hifadhi ya kisiasa kwenu. Kumbuka hawa ina maana hawana uzalendo na chama chao, wanachotaka ni uongozi tu. Hata hivyo kuna wachache ambao wao wemeenguliwa kwa kuwa wanatofautiana na uozo ndani ya chama chao na walipopayuka basi wakaambiwa wanakwenda kinyume na maadili ya chama. Walijua tu rungu la kuwamaliza ni kura za maoni, na hata kama wakipita basi utasikia oooh amekwenda kinyume na maadili ya chama!! Ni maadili gani chama hiki kinayo? Chakachueni wale wanachama waliokuwa na nyadhifa ssm kama kweli wanafaa kukimbilia kwenu na kupewa nafasi za kugombea ubunge kwa tiketi yenu.

Kwa upande wangu kama Selelii atakubali kujiunga kwenu, huyo atafaa na kwa hakika jimbo la Nzega mtalichukua. Kule Tarime, inabidi muwe makini sana. Kumbuka Mwera amehamia CUF na baadhi ya wanachama wenu watahama naye hivyo mtapunguza kura. Sasa sielewi mmejipangaje wakati wa kampeni mridhishe wapambe wa Mwera na waendelee kuwa pamoja nanyi. Msipoangalia mtalipoteza jimbo kwa SSM.
 
Kuna kitu unasahau ndugu Mchungaji nacho ni "jiwe walilolikataa waashi tazama limekua jiwe kuu la pembeni...!"
 
Back
Top Bottom