CHADEMA njooni vijijini uza sera kwenye jamii watu wana kiu na CHADEMA

Kaka nia na ya chadema sio kuchukua dola bali ni kurise ruzuku.sasa wanapata ruzuku ya milion280 kutoka serikalini tayari wamesha kipata walichokua wanakitaka ndio maana sasa wameacha operation sangara ambayo ilikua inasambaza chama vijijini na sasa wanadeal na maandamano ili wagawane posho na kulipana madeni hewa.kwa sasa wameamua kugawana posho kwa kisingio kwamba wanakwenda kutoa elimu kuhusu katiba.wananchi wameichoka ccm lakini hawana kimbilio mwisho wa siku wanajikuta wako chadema,chadema wanasambaza chama kwa kutoa matamko makao makuu ndugu zangu wanachadema kuchukua nchi2015 kwa kusubili matamko ya mnyika makao makuu ni ndoto za mchana na Dk slaa kuwa rais haiwezekani maana kwa sasa hana hoja zaidi ya maandamano na kukesha viwanja vya NMC arusha?mwanachadema jenga chama mwenyewe huko uliko ukisubili wakujengee hao wachaga unapoteza mda wao wako kumaximize profit sasa wanapataprofit ndio maana Dk slaa analipwa mshahara wa milion saba na nusu kwa kuongeza ruzuku Umeandika upuuzi

Shauri yako,nape hana fungu tena,uhuu?!
 
Hapo Mkuu Patriote umesema kweli watu wote tukiwa na moyo huo basi itakuwa kazi nzuri, inatakiwa kila mtu mahali alipo ahamasishe watu!!!! Swala kubwa ni kadi na bendela za chama zisambazwe nchi nzima, watu waone kuwa CHADEMA wapo kazini, nakwambia wengi watajiunga na chama kuimalisha upinzani, matokeo yake yatakuwa mazuri!!!!!!!!!

Unajua kamanda mimi kwa kupitia hoja mbali mbali humu nimegundua kuwa kunawanasiasa wengi sana humu ambao hawajagundua kuwa wanaweza kuwa Viongozi wazuri tu wa Taifa hili. Tatizo wote wanataka kuanza kufanya siasa katikati ya miji na ndo mana wanakata tamaa. Wamuulize Mbunge Mbozi wa CDM alihonga nini kupata Ubunge. Hakuna! Vijinin watu wanataka mabadiliko sana sana sana ila hakuna anayejitokeza na kuonesha nia ya kuwakwamua. Vijana turudi vijijini mana watu wa vijijini ndio tunaoambiwa kuwa wanakura nyingi zinazowapaga CCM ushindi. So far sisi wa mjini hatuhitaji tochi kuelekezwa ilipo njia. Chama kingeelekeza nguvu vijijini. Tena kukonvince watu wa vijijini ni kazi rahisi sana. Mana wameshadanganywa sana na wabunge na madiwani wa CCM kwani wanatumia udhaifu wao wa elimu na uelewa wa mambo kuwadanganya miaka nenda rudi.

Kwa mfano mwaka 2010 CDM haikusimamisha wagombea Ubunge na Madiwani katika Majimbo/Kata mengi sana vijijini kwa sababu tu hakuna aliyejitokeza kutaka kugombea. Hii inaonesha ni jinsi gani vijana tupo nyuma kwenye mapambano ya kweli ya ukombozi. Kama nguvu ya kumchagua Rais tumewaachia watu wa vijijini ndio watuchagulie Rais watu wa mjini, hivi tukipata Rais mbabaishaji, hapo wa kulaumiwa nani???wa mjini anayejua mambo yanavyoenda au wa kijijini anayejua kuwa jina ''Nyerere'' ni sawa na ukiita ''Rais''???? Na hivyo wakitembelewa na Kikwete wanasema Nyerere Kikwete leo katutembelea.

kwanini tusiende kuchukua hayo majimbo km Wabunge au Kata km madiwani???? kwani unahitaji kwenda chuo cha ubunge/udiwani ili uwe Mbunge/Diwani???Je ni kweli wewe ungekuwa mbunge huwezi fanya vizuri zaidi ya Ngereja, Lusinde, Kingwangala au Anne Makinda??? Tatizo hatujitokezi kwenye kutaka nafasi za uongozi then badae tunakuwa wa kwanza kutupa lawama kwa waliojitokeza kutuongoza. Binafsi Nimesha identify jimbo la CCM lililojificha sana kule kwetu kusini la kuhangaika nalo 2015. Mi nadhani kuna haja ya kufanya mabadiliko MAKUBWA. Ukitaka mbinu za kuchukua jimbo ushauri wa bure unapatikana tena mwingi tu kwenye ofisi za chama/kwa wabunge wetu wa CDM, kwa kweli vijana tuchange our mind sets na tupambane kuingia kwenye nafasi za uongozi na sio tubaki tu kama washabiki. Humu JF tutatoa povu hadi litufunike na tutalaumu sana tu, lakini hata tukilaumu vipi mambo hayabadiliki, hivyo kikubwa ni kuingia humo humo ndani kama walivyofanya vijana wenzetu akina Zito, Kafulila, Mkosamali and the like. Mizee inawaza matumbo yao na familia zao tu, tukiiacha iendelee kutuongoza tunaoangamia ni sisi vijana.

Ushauri wangu, Tuanze sasa kufikiria namna ya kuchukua Kata/Majimbo ya vijijini yanayoshikiliwa na CCM, kwa kufanya hivyo itabidi uanze kuandaa mazingira. Kitendo hicho kitakufanya uwe karibu na wapiga kura wako watarajiwa na utawajua vizuri na kuweza kuwaconvice kujiunga na chama huku mdogo mdogo unatoa ushauri wa kitaalam juu ya shughuli zao mbalimbali za maendeleo. kama wewe si mtaalam mchukue hata rafiki yako atakusaidia ktk hilo. Badala ya kunywa mibia na mijimbuzi break point pub, nenda kijijin kaanzishe mashindano ya kugombea bata baada ya mavuno ili kupitia hayo makusanyiko ujuane na vijana wa vijijini. Ukitaka kuwafahamu kiundani zaid unaweza fanya kautafiti kadogo ambako katakufanya siku ya kampeni ujue pa kuanzia, watafiti wapo bwelele. We onesha nia tu uone. Ukifanya haya yote, watakufwata wenyewe kukuomba ugombee ubunge au udiwani. Kwa kweli in this the sky is our limit, unless tumeamua kuongozwa na watu wababaishaji kama kina Ngereja, Wasira, Nundu, Lusinde, etc......"Together we can" take CCM out of the CCM as Zambians did.
 
Ukweli ndio huo. Siasa za mjini haziwezi kukupa ushindi irahisi. Cdm ikubali gharama za kwenda vivivni
 
Hiyo ni dalili kuwa wapo wapambanaji hata kwenye vijiji, lakini mimi nakwambia Mkuu Jackbauer bado tunahitaji jitihada zamakusudi ili moto wa CDM uwake nchi nzima hadi ukombozi upatikane!!!!!!!!!!


usiamini sana kwenye propaganda amini uhalisia wa mambo kama nilivyokuonyesha hapo juu,zamani ulikuwa ukipita vijijini unakuta bendera za kijani sasa hivi mambo yamebadilika sana na tusiendelee kudanganyika eti upinzani haujafika vijijini.
 
Kwa mujibu wa ratiba ya CDM TAREHE 28 . 12 . 2011 Makongamano ya kuhamasiasha chama vijijini itafanyika fuatilia wapi makongamano haya yatafanyika ktk kijiji chako na uhudhulie pasi kukosa maana miutano ya hadhara imekatazwa
 
Mpango uliopo kuimalisha chama kuanzia ngazi ya tawi na chaguzi za mashina ( aka mabalozi) viongozi wa kata zote zitafanyika mwakani [2012]
 
Back
Top Bottom