Chadema nje wanaalani udikteta lakini ndani ya chama chao kuna udikteta wa kutisha

Chadema wanataka vyombo vya ulinzi vifanye kazi yao kwa matakwa yao badala ya matakwa ya taaluma mpaka sasa hivi hakuna hata kiongozi mmoja wa Chadema aliefungwa kwa sababu za kisiasa halafu wanasema wananyanyaswa..

Kama policcm wanaweza kuzuia mkutano wa Chadema Iringa lakini wakajipanga kwa wingi kulinda mkutano wa ccm Bububu, na wewe kwa kutumia kichwa chako cha kuku huwezi kuona kwamba huo ni ushahidi tosha kwamba policcm hawatumii sheria wala taaluma katika kufanya kazi zao basi hata hiki unachojaribu kukilalamikia hapa ni pumba tupu.

Watu wasiofuata sheria na kanuni za uendeshaji wa chama lazima wawajibishwe kwa mujibu wa katiba, kanuni na taratibu zilizopo. Chadema si sawa na ccm msiokuwa na uwezo wa kuwajibishana kwakuwa wote ni ni wezi na kwahiyo hakuna wa kumnyooshea mwenzake kidole.

Hapa tulipofika tunahitaji sana viongozi wanaosema na kutenda wanayoyasema, si viongozi wanaozurura kila siku na kuacha nchi ikiyumba bila mwelekeo na hawawezi kuchukua maamuzi magumu kwakuwa wao wenyewe ni dhaifu sana.
 
Chadema ni watu wa porojo Dr Slaa, hajafikia msimamo mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema, mwaka 1995.

Augustino Mrema hawezi kuwa role model wa mwanasiasa yeyote mwenye akili ya kawaida achilia mbali mtu yeyote anayetumia akili yake vizuri.

Mrema atabaki kuwa ni role model wenu ninyi visebengo wa mabwepande.
 
Mtu yoyote aliye makini na mwenye akili timamu ni lazima ahoji, serikali iwauwe viongozi wa Chadema kwa sababu ipi na kwa manufaa ya nani?
Mtu huyohuyo makini na mwenye akili timamu ni lazima atahoji, serikali dhaifu ya Kikwete ilimuua kikatili mwandishi wa habari Daud Mwangosi kwa sababu ipi na kwa manufaa ya nani?
 
Hakuuliwa mrema na saif sharif itakuja kuwa Slaa,unakumbuka hawa walivyo vuma? Vyama vya upinzani ni kama bongo fleva,wanakuja kwa mkwara halafu wanafifia. Wanaendelea kuwepo lakini hawavumi.

Usifananishe hao waganga njaa wa cuf na tlp na makamanda wa Chadema. ccm ingewauaje vibaraka wake?
Cuf pamoja na kujinadi kwamba wao ni ngangari lakini hawajawahi kuendesha operation kabambe na ya muda mrefu kama ya Chadema; Operation Sangara ikienda sambamba na M4C.

Chadema imebadilisha siasa za vyama vya upinzani kutoka kuwa vyama vya msimu wa uchaguzi hadi kuwafanya watawala wasipate usingizi kwani uwepo uchaguzi, usiwepo Chadema inakwenda mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya, jimbo kwa jimbo, tarafa kwa tarafa, kata kwa kata, kijiji kwa kijiji na mtaa kwa mtaa.
 
Ina maana demokrasia ni kumruhusu kila mtu abwabwaje anavyotaka?CDM ni taasisi yenye katiba na miongozo yake,ukienda kinyume na maazimio au katiba lazima upate stahiki yake au ujiengue mwenyewe kwa kutokukubaliana na sera au maazimio husika.Kinyume na hapo hicho kitakuwa si chama bali genge kama SAIGON.Yani mwanachama asimame mbele ya umma na kukitusi chama kilichompa jukwaa alilosimamia kwa kujiita yeye ni taasisi kisha aachwe tu ati democracy!kesho tukishika dola akawa kiongozi mkubwa si atasema yeye ni nchi inayojitegemea?CDM kuelekea kushika dola yapo makapi mengi ya kuyatema.Kwa mtazamo wangu kiongozi bora lazima awe japo na chembe ya udikteta si kila kitu ni cha ku argue.
 
Wanabodi,

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kimekuwa kilaani udikteta lakini inasikitisha wanalaani kwa maneno tu ndani ya chama hiki kuna udikteta wa kutisha.

Chadema walitaka kumvua uanchama mbunge wao, Zitto Kabwe alipolikataa kusudio lao la kususia hotuba ya rais na kutoka bungeni, Chadema pia walitaka pia kumfukuza John Shibuda alipotofautiana na maagizo yao.

Chadema wameshindwa kuwavumilia hao wanaokaidi maagizo yao na kuwatimua lakini cha achabu wao wanataka wakaidi maagizo ya serikali halafu wasiguswe,.

Chadema wanataka vyombo vya ulinzi vifanye kazi yao kwa matakwa yao badala ya matakwa ya taaluma mpaka sasa hivi hakuna hata kiongozi mmoja wa Chadema aliefungwa kwa sababu za kisiasa halafu wanasema wananyanyaswa..

Mkuu, umenichanganya kidogo.
Kwa muhtasari umezungumzia udikteta, kutovumiliana, ukaidi na polisi kuogopa kuwatia ndani viongozi wa CDM?
Kwa kawaida dikteta huwa ni mtu mmoja tu katika jumuia yoyote, kwa maana kwamba kauli yake ni ya mwisho na hashauriani na yeyote katika jumuia hiyo.
Kukisha kuwa na mjadala wa nani afukuzwe au aadhibiwe katika jumuia hiyo huo tena sio udikteta, na ninaamini TZ haiwezi kulea chama cha aina hiyo.

Kama mijadala inakuwepo halafu mmoja wao akashindwa kuvumiliwa hadi kutoswa ujue kosa lake ni kubwa na laweza kuleta athari kwa jumuia hiyo. Ndiyo maana kuna hata mahakama za kiraia na huhukumu watu wasiovumilika katika jamii.

Kama kuna udikteta CDM, wameshindwaje kuwatosa Wahe. Zitto na Shibuda?

Kwa sheria za nchi yoyote ikiwemo TZ, anayekaidi amri halali ya serikali iliyomo madarakani, huchukuliwa hatua kali. Kama ndivyo na kama ni kweli kwamba viongozi wa CDM wanakaidi amri hizo halali, basi kuna walakini katika vyombo vinavyotakiwa kuzisimamia. Vinginevyo itabidi uhoji uhalali wa amri hizo.
 
Dr Slaa, hajaufikia hata nusu ya umaarufu aliokuwa nao Christopher Mtikila mwaka mwaka 1992 na chama chake cha DP alipohubiri kwa nguvu ya uzawa akileta msamiati mpya katika siasa wa "magabacho'li" na "walalahoi" mbona hakuuwa...Dr Slaa bana.

Dr. Slaa hatafuti umaarufu, umaarufu unamtafuta wenyewe, anachofanya ni kupambana na huu mfumo dhalimu unaowanyonya na kuwakandamiza watanzania, anachofanya ni kutoa elimu ya uraia kwa watanzania ili kwa pamoja watambue haki zao, watambue ni kwa kiasi gani ccm ni janga kwa maisha yao, watambue dhulma wanazofanyiwa na ccm na watambue ufisadi unaofanywa na ccm na serikali yake.

Mtikila hajawahi kuwindwa na uslama wa taifa, mtikila hajawahi kuwekewa vifaa vya kunasa mawasiliano yake nyumbani kwake ama hotelini, sasa hadi hapo utamlinganisshaje Dr. Slaa na mtikila huyu huyu anayepewa na rostam shilingi milioni moja tu anachanganyikiwa na kusahau ufisadi wa rostam na ccm!!??
 
Chadema ni watu wa porojo Dr Slaa, hajafikia msimamo mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema, mwaka 1995.

dah mkuu umenikumbusha jana tulikuwa nae hapa HIMO anatuhutubia wananchi wake
 
Hiyo ndio CDM ni sawa na jeneza muonekano wa nje mzuri kumbe ndani kuna mzoga wa ubabe, ukabila, udini na kujifanya malaika wasio kosea
 
Wanabodi,

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kimekuwa kilaani udikteta lakini inasikitisha wanalaani kwa maneno tu ndani ya chama hiki kuna udikteta wa kutisha.

Ndani ya Chadema hakuna demokrasia hakuna uvumilivu wowote Chadema imewatimua madiwani wa Arusha, Chadema imewatimua madiwani wa Mwanza, Chadema walitaka kumvua uanchama mbunge wao, Zitto Kabwe alipolikataa kusudio lao la kususia hotuba ya rais na kutoka bungeni, Chadema pia walitaka pia kumfukuza John Shibuda alipotofautiana na maagizo yao.

Chadema wameshindwa kuwavumilia hao wanaokaidi maagizo yao na kuwatimua lakini cha achabu wao wanataka wakaidi maagizo ya serikali halafu wasiguswe, je nchi yetu itakuwa nchi ya namna gani endapo Chadema itaachiwa kufanya lolote walitakalo pasipo kufuata sheria za nchi, Chadema kijumla upinzani kwao una maana moja tu ya "antagonism" kwamba serikali ikisema ndio wao ni kusema hapana, ni upinzani usio na manufaa yoyote kwa watanzania.

Chadema wanataka vyombo vya ulinzi vifanye kazi yao kwa matakwa yao badala ya matakwa ya taaluma mpaka sasa hivi hakuna hata kiongozi mmoja wa Chadema aliefungwa kwa sababu za kisiasa halafu wanasema wananyanyaswa..
Wewe sio mwanachama wa chadema, udikteta wa chadema unaaujuaje kama sio kukaa vijiwe vya kahawa na kupeana umbea tu
 
Dr Slaa hajaufikia hata nusu ya umaarufu aliokuwa nao Christopher Mtikila mwaka mwaka 1992 na chama chake cha DP alipohubiri kwa nguvu ya uzawa akileta msamiati mpya katika siasa wa "magabacho'li" na "walalahoi"

Inakuwaje sasa anawasumbua hadi mnamuwekea vinasa sauti?

TUMBIRI (PhD, University of HULL - United Kingdom),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Wanabodi,

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kimekuwa kilaani udikteta lakini inasikitisha wanalaani kwa maneno tu ndani ya chama hiki kuna udikteta wa kutisha.

Ndani ya Chadema hakuna demokrasia hakuna uvumilivu wowote Chadema imewatimua madiwani wa Arusha, Chadema imewatimua madiwani wa Mwanza, Chadema walitaka kumvua uanchama mbunge wao, Zitto Kabwe alipolikataa kusudio lao la kususia hotuba ya rais na kutoka bungeni, Chadema pia walitaka pia kumfukuza John Shibuda alipotofautiana na maagizo yao.

Chadema wameshindwa kuwavumilia hao wanaokaidi maagizo yao na kuwatimua lakini cha achabu wao wanataka wakaidi maagizo ya serikali halafu wasiguswe, je nchi yetu itakuwa nchi ya namna gani endapo Chadema itaachiwa kufanya lolote walitakalo pasipo kufuata sheria za nchi, Chadema kijumla upinzani kwao una maana moja tu ya "antagonism" kwamba serikali ikisema ndio wao ni kusema hapana, ni upinzani usio na manufaa yoyote kwa watanzania.

Chadema wanataka vyombo vya ulinzi vifanye kazi yao kwa matakwa yao badala ya matakwa ya taaluma mpaka sasa hivi hakuna hata kiongozi mmoja wa Chadema aliefungwa kwa sababu za kisiasa halafu wanasema wananyanyaswa..
Ritz unashangaza kidogo, unaposema Chadema wanakataa maagizo ya serikali, halafu wanataka wasiguswe, ndipo unapoonyesha jinsi unavyojitahidi kutetea uharamia wa magamba, bila kuzingatia facts. Kuna swali moja limekuwa likiulizwa mara kwa mara, baada ya tukio la Nyololo, kuwa iweje kama kulikuwa na zuio la mikusanyiko ya aina yoyote, siku hiyo hiyo, magamba walifanya mkutano wa hadhara mkubwa huko Bububu, ndiyo maana inaelezwa Polisi wanafanya mambo yao kwa double standards na hawafanyi hivyo kwa bahata mbaya, bali ni kwa maelekezo maalum toka kwa uongozi wa juu kabisa wa nchi. Na ndiyo sababu ushahidi wote unaonyesha mauaji ya Mwangosi yaliamrishwa na RPC Kamuhanda, lakini hadi leo, hajapandishwa kizimbani wala hajafikiria kuwajibika kujiuzuru, na wakubwa wake waliomteua wanagwaya kumfukuza kazi!!
 
Kila mtu anyepinga chadema akipost thread JF lazima amtaje slaa au mbowe. Ritz,rejao,tume ya katiba,majebere na wengineo chadema haina viongozi wengine zaidi ya hao ambao kila kukicha madongo tuu.
 
Mbona unajichanganya kaka mkubwa,nakuaminia sana kwa uwezo wako wa kutotereka pindi unaposhambuliwa humu jamvini na wana CDM ila hapa hoja zako hujazipanga.

Ona hapa ''Chadema wameshindwa kuwavumilia''
Ukajijibu bila kujua "Chadema walitaka kumvua uanchama mbunge wao, Zitto Kabwe alipolikataa kusudio lao la kususia hotuba ya rais na kutoka bungeni, Chadema pia walitaka pia kumfukuza John Shibuda alipotofautiana na maagizo yao.''

Kama wangekuwa hawana kuvumiliana basi usingeandika hiyo sentensi hapo juu.

Ona tena mistari yako hii "Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kimekuwa kilaani udikteta lakini inasikitisha wanalaani kwa maneno tu ndani ya chama hiki kuna udikteta wa kutisha."

ukajijibu hapa " Chadema imewatimua madiwani wa Arusha, Chadema imewatimua madiwani wa Mwanza"

Umeyajibu maswali yako mwenyewe bila kujua ,Kapitie upya nini maana ya demokrasia pale ambapo mwanachama/raia/kiongozi anapokiuka masharti /kanuni na sheria walizojiwekea kujiongoza/ziwaongoze anatakiwa afanywaje. Demokrasia haisemi kiongozi anapokosea asihukumiwe bali inatoa mwanya wa kumsikiliza mkosaji ili apewe hukumu stahiki.Hivyo waliofukuzwa walionekana wana makosa na adhabu kulingana na demokrasia ya chama ni kuvuliwa uwanachama,kama ambavyo Shibuda na Zitto walivyohukumiwa kulingana na Demokrasia ya chama.

Mbona ujajibu hoja ulichofanya hapa ni kuonesha ustadi wako mkubwa wa kupamba harusi.
 
Chadema mnajiita chama cha demokrasia, sijui demokrasia gani ambayo mnayo haiwezekani mnakaa kikundi cha watu wachache mnatoa maamuzi bila kuwashirikisha wananchi wa Mwanza, mnawavua uanachama madiwani wa Mwanza, wenye haki hiyo walikuwa wapiga kura wao sio Dr Slaa, Lema na Mbowe, huo ni udikteta.
 
Mtu yoyote aliye makini na mwenye akili timamu ni lazima ahoji, serikali iwauwe viongozi wa Chadema kwa sababu ipi na kwa manufaa ya nani?

Baada ya kijiuliza swali la msingi jiulize pia kwa nini ilikuwa viongozi wa chadema wawindwe?!, jiulize pia, kama Mwangosi ameweza kuuwawa mbele ya maofisa wa jeshi la polisi wanao linda amani na usalama wa raia na bado wako makazini, je wangewauwa viongozi wa chadema wanao ichachafya serikali wangefanywaje?!

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
hao uliowataja wamesoma lakini hawakuelimika! chenge amegraduate Harvard ila vitendo vyake havina tofauti na wewe ulimaliza primary ya kata!Daud Balal sina cv yake ila naye kukubali kudanganya amekufa ili kulinda mafisadi wakati yupo hai naona hata wewe una akili kidogo kumshinda maana bado hujafikia kudanganya umekufa pamoja na kuwa kuna mambo mengi sana huyajui!

Nadhani hapo tunaenda sawa kwa faida ya JF naomba unitajie elimu ya Lema pamoja na Mbowe, tuendelee na mjadala mkuu wangu.
 
Back
Top Bottom