CHADEMA ni sawa na 'Simba mfa maji'

Mods hebu wekeni hili debe pembeni kwanza kwa mwezi mzima maana linapika kelele mno ni tu na lina distruct kwa kweli .
 
Mods hebu wekeni hili debe pembeni kwanza kwa mwezi mzima maana linapika kelele mno ni tu na lina distruct kwa kweli .

Ndugu yangu Linyungu mbona unapanda Temperature. Tena uko juu chini, ni dakika chache tu zilizopita ulinialika kirafiki katika Thread nyingine, ukidai mnanisubiri. Uliandika hivi... #79 "Kuna mada huku tunakutafuta acha utumbo huku njoo pale onyesha kama unaweza kuaminika .Acha unusu akili na kutawaliwa kwa masaburi" Nilifikiri tutajibizana hoja kwa hoja..... Mara leo unapeleka maombi kwa Mod nifungiwe mwezi mmoja.

Ninachoamini mimi ni kwamba CHADEMA ni chama kinachokuwa kwa nguvu ya soda kwa sababu Propaganda inazotoa kamwe haitaweza kuzitekeleza. Ni nini adhma ya chama kama hicho.. wananchi kukatishwa tamaa na chama hicho na kukikimbia na kuhamia vyama visemavyo ukweli japo unauma. Na kwa historia ya Tanzania CHADEMA si chama cha kwanza kukua kwa nguvu ya soda, vipo vyama vilivyoanzishwa na Mrema kweli nilijua kuwa sasa tumepata mkombozi. Lakini mkombozi akawa mkimbizi na hali hiyo inanukia CHADEMA.

Tanzania si nchi pekee ya Afrika ambayo ni masikini na wala si nchi pekee Afrika yenye rasilimali nyingi, lakini tukija kwenye umasikini wote letu ni moja. Umeyasikia ya Swaziland, sijakwambia ya Zaire, Liberia , Siera leone n.k. Ninachotaka kusema ni kwamba adui mkuu wa umasikini Afrika ni mmoja, kama hatukukaa na kuambiana ukweli basi tutapiga kelele majukaani bila kuondoa umasikini ambae ndie mlengwa mkuu katika chaguzi zote.

Kwa hiyo naomba CHADEMA wajipange upya kama wanataka kushika Dola La Tanzania. Sitoruhusu kamwe kukiruhusu chama chochote kile kushika madaraka Tanzania kama hakiathibitisha kuwepo kwa amani nchini. Haka kaamani kadogo tulikonako ni muhimu sana kwangu kuliko kushabikiwa kuingia vitani eti kwa jina la kutoa umasikini. Nchi zote zilizoingia vitani Afrika, mwananchi wa kawaida bado hajaona faida yake baada ya vita kwisha na Tanzania sio Exceptional. Chukulia LIberia na Siera Leon kama mfano.

Hivyo ndivyo ninavyoamini mimi Zawadi Ngoda, sitaki kajumba kangu kaUdongo kabomolewe kwa vurugu zenu na ndio maana nimeshikia bango hoja. Hiyo ndio silaha yangu pekee. Kama unataka nifungiwe kwa hilo OK.
 
Hatuna haja na mzazi fisadi anayeua watoto wake kwa njaa. Hivi TANU ilivyochukua nchi, ilikuwa mzee au mtoto? acha sera cha kifisadi za CCM. Angalieni, mtakuja ondolewa madarakani kama misri na Libya.
 
Wewe ndio mfa maji.

Wewe na chama chako cha Magamba mnaotukanana wenyewe kwa wenyewe hadharani ndio mtadumu.? Huna kazi nyingine ya kufanya? Unalipwa sh ngapi kuleta thread za kipuuzi hivi? Vipi yale matusi mliyotukana wananchi wa Mwanza ndio sera yenu mpya.?
kaka na wewe kama unalipwa unavyoitetea CDM??? cha msingi ni kusubiri kama utabiri wake utakuwa kweli au la. Kama unataka mabadiliko nia tu inatosha sio mpaka uwe shabiki wa CDM kwani kumbuka nao ni wanasiasa, mwisho wa siku yatakuwa yale yale. Mabadiliko yako juu yako na wala sio juu Ya CDM kwani wao wanataka uongozi km hao magamba ambao unawachukia.... UENDA SIKU MOJA UTANIKUMBUKA
 
Kama sera za CHADEMA zingekuwa nyoofu, Watanzania wangeshafahamu ni wapi chama kinatupeleka. Lakini mpaka leo hii hakuna hata mtanzania mmoja anaweza kuthubutu kusema anaelewa ajenda za CHADEMA. CHA AJABU NI KWAMBA HATA WALE, wanachama wakereketwa wa chama hicho nao hawafahamu. Katika mazingira hayo hayo unategemea hatima ya chama hichi ni ipi.

Baada ya kuisoma CHADEMA nikaelewa kuwa hiki ni chama cha nguvu ya SODA kinachotapatapa sawa na Simba mfa maji anayehangaikia survival yake. Hii inaonyesha wazi kuwa mfarakano ndani ya chadema ni sambamba na kukuwa kwa chama hicho. Hii ni kwa sababu CHAMA hicho hakina DIRA.

Utabiri wangu ni kwamba kama CHADEMA itavuka salama uchaguzi ujao mkuu basi kifo chake kitakuwa mwaka 2017. Tuombe uhai!

Mbona hujazungumzia CUF?
 
Back
Top Bottom