CHADEMA ni mti wenye maembe, lazima utupiwe mawe - Mbowe

Kujenga demokrasia ni ngumu, mimi nampongeza sana Mboe mpaka hapo alipofikisha CHADEMA, ndo maana alipoulizwa kuwa makosa waliyofanya ndani ya uongozi wake akukataa, alisema yapo.

Swala la kumshauri mgombea kujitoa kumwachia mwingine ni la kawaida ndani ya vyama. Hilary Clinton alishauriwa hivyo, na aligundua hivyo kuwa kuendelea na kinyanganyiro na Obama ni kuumiza Chama chake, hivyo alikubali kujiondoa kabla ya mkutano mkuu wa Democrat ili amuunge mkono Obama na kuomba wafuasi wake wamkubali Obama.
Hivyo kufanya hivyo kwa namna moja ni kujenga demokrasia kwani mgombea anabaki na uhuru wa kuamua kuendelea au kuachia.
Naitakia Mboe na CHADEMA mafanikio zaidi.

Kuna watu haya maandishi mekundu hawataki kuyasoma na kuyatafakari, wao wanaona tuu kwa jicho moja hawataki kuona upande wa pili .well articulated.
 
Katiba ya CHADEMA Inatambua uwepo wa kundi la wazee na inatamka wazi kuwa ni washauri ndani ya chama , tena imeenda mbali zaidi kwa kutambua kokasi ya wazee ndani ya chama , hivyo kusema kuwa ni kwenda kinyume na katiba ya chama inaonyesha huijui katiba ya CHADEMA.

- Mkuu Kieleweke, kwanza heshima yako mkuu sasa mkuu mbona umeruka mengi sana mpaka kufikia hapa, si ungeanza mwanzo kama kweli unataka kujadili haya, anyways hebu tujadili hoja yako,

- Unasema kwamba katiba ya Chadema, inaunda kundi la wazee as a kokasi ambayo inatambuliwa kikatiba na kupewa uwezo wa kumlazimisha au kumuomba mwanachama au kiongozi yoyote wa Chadema, kujitoa kwenye kinyang'anyiro chochote cha uongozi ndani ya chama, na tena kwa wakati wowote ule,

- Mkuu Kieleweke, unasema kwenye katiba ya Chadema kuna kipengele kinachoruhusu haya? Are you serious? au labda kiweke hicho kifungu hapa kutoka katiba ya Chadema mkuu, na kwa nini Mwenyekiti wa Chadema asitumie hicho kifungu kuwajibu critics kwenye mahojiano yake? Maaana angemaliza ubishi mara moja, wala tusingefika huku, infact bado anaweza kukiweka hapa tukaacha mara moja hii discussion.

Respect.

FMEs!
 
Kujenga demokrasia ni ngumu, mimi nampongeza sana Mboe mpaka hapo alipofikisha CHADEMA, ndo maana alipoulizwa kuwa makosa waliyofanya ndani ya uongozi wake akukataa, alisema yapo.
Swala la kumshauri mgombea kujitoa kumwachia mwingine ni la kawaida ndani ya vyama.

Hilary Clinton alishauriwa hivyo, na aligundua hivyo kuwa kuendelea na kinyanganyiro na Obama ni kuumiza Chama chake, hivyo alikubali kujiondoa kabla ya mkutano mkuu wa Democrat ili amuunge mkono Obama na kuomba wafuasi wake wamkubali Obama.

Hivyo kufanya hivyo kwa namna moja ni kujenga demokrasia kwani mgombea anabaki na uhuru wa kuamua kuendelea au kuachia.
Naitakia Mboe na CHADEMA mafanikio zaidi.

- Mkuu Orche, heshima yako ndugu yangu, unasema kwamba Mama Clinton, alichukua fomu ya urais, halafu kabla hajairudisha akaombwa na wazee wa Democratic Party kuirudisha fomu na kumuuunga mkono Obama, na akakubali eti unasema this is what happened? Halafu Mkuu Kieleweke, eti unasema haya ni maneno mazito sana, no wonder hili taifa linaendelea kurudi nyuma, ulikuwa una make a lot of sense ulipokuwa umenyamaza, kuliko hizi maneno!

- Chadema mnaposhindwa chaguzi huwa tunajiuliza kulikoni?, kwa majibu kama haya ndio unapata jawabu rahisi sana, kumbe hakuna tofauti na CCM!

- Unajua mnaharibu sana mnapojaribu kutumia uongo uongo wa kitoto kama wa CCM, kuhalalisha nonsense! Sometimes muwe mnalionea huruma kidogo hili taifa, hivi wananchi wa taifa hili watadanganywa mpaka lini?

Respect.

FMEs!
 
Mzee FMEs
Unajua mimi ni shabiki wako na sioni soo kusema hilo.
Lakini kwa hili la demokrasia ndani ya CHEDEMA napingana nawe.
Kusema wazee walimlazimisha Zitto unakosea maana hata Zitto mwenyewe hajawahi kujilazimisha akafanikiwa, sembuse kulazimishwa! We jaribu leo umlazimishe Zitto tuone kama atakukubalia.

Zitto alikubali ushauri, kwa maslahi ya chama, halii hii hutokea katika vyama vyote hata ndani ya CCM yetu. Kama huu ni mfano mbaya, si wa kwanza, tuendelee na maisha. Nijuavyo mimi CCM wamechukia kwa hatua ya Zitto na hiyo ni haki yao.
 
- Mkuu Orche, Mama Clinton aligombea urais as opposed na maneno yako, soma hapa chini infact kuna wakati hata alishinda kura za some of the states:-

Hillary Clinton presidential campaign, 2008

From Wikipedia, the free encyclopedia


Jump to: navigation, search
Hillary Clinton for President CampaignU.S. presidential election, 2008CandidateHillary Rodham Clinton
Senator 2001–2009AffiliationDemocratic PartyStatusAnnounced January 20, 2007
Suspended June 7, 2008HeadquartersArlington, VirginiaKey peopleMaggie Williams (Manager)
Terry McAuliffe (Chairman)


Howard Wolfson (Communications Director)SloganSolutions for America!ChantYes We WillWebsitewww.HillaryClinton.com
The Hillary Rodham Clinton series v • d • e



United States Senate career, 2001–2009
Campaign for the Presidency, 2007–2008
Political positions · Awards and honors
List of books about Hillary Rodham Clinton

Hillary Clinton campaigning for the Democratic nomination for President of the United States. South Hall, San Jose, California, February 1, 2008.


New York junior Senator and former First Lady Hillary Rodham Clinton had expressed interest in the 2008 United States presidential election[1] since at least October 2002, drawing media speculation on whether she would become a candidate.[2] No woman has ever won the nomination of a major party in the history of U.S. presidential elections.[3]
On January 20, 2007, she announced that she was forming an exploratory committee and filed with the Federal Election Commission to seek the nomination of the Democratic Party. Subsequently she began fundraising and campaigning activities. For several months Clinton led opinion polls among Democratic candidates by substantial margins until Senator Barack Obama pulled close to or even with her. Clinton then regained her polling lead, winning many polls by double digits; by autumn 2007 she was leading all other Democratic candidates by wide margins in national polls.[4] She placed third in the Iowa caucus to Barack Obama and John Edwards,[5] and trailed considerably in polls shortly thereafter in New Hampshire before staging a comeback and finishing first in the primary there.[6]
She went on to win a plurality of votes in Nevada, but won fewer delegates in Nevada than Obama, then lost by a large margin in South Carolina.[7] On Super Tuesday, Clinton won the most populous states such as California and New York, while Obama won more states total. The two gained a nearly equal number of delegates and a nearly equal share of the total popular vote. Clinton then lost the next eleven caucuses and primaries to Obama, and lost the overall delegate lead to him for the first time. On March 4, his consecutive wins increased to twelve when Vermont went his way. After an increasingly aggressive round of campaigning, Clinton broke the string of losses with wins in the Rhode Island, Ohio and Texas primaries. [8]
Clinton subsequently lost in Wyoming, Mississippi, Montana, North Carolina and Oregon, and won in Pennsylvania, Indiana, West Virginia, Kentucky, Puerto Rico and South Dakota. On the final day of primaries on June 3, 2008, Obama had gained enough pledged- and super-delegates to become the presumptive nominee;[9] she then suspended her campaign on June 7, 2008 and endorsed Barack Obama.
 
Mzee FMEs
Unajua mimi ni shabiki wako na sioni soo kusema hilo.

- Mkuu BB, ni maneno kama haya ndio huwa mwenyewe unaniambia wewe ni nani, hebu tizama in the last four days umetumia haya maneno mara ngapi ndugu yangu, mjumbe wa NEC ya CCM, kama ulivyosema mwenyewe? Ni nini hasa unachonitakia na kunitafuta tafuta mkuu kwa nini usiseme shida yako nikakusaidia? Utahangaika hivi mpaka lini? ndio maana nilisema hivi unatia kinyaa sana lazima kila wakati urudie matapishi yako, vipi ndugu!

Lakini kwa hili la demokrasia ndani ya CHEDEMA napingana nawe.
Kusema wazee walimlazimisha Zitto unakosea maana hata Zitto mwenyewe hajawahi kujilazimisha akafanikiwa, sembuse kulazimishwa! We jaribu leo umlazimishe Zitto tuone kama atakukubalia. Zitto alikubali ushauri, kwa maslahi ya chama, halii hii hutokea katika vyama vyote hata ndani ya CCM yetu. Kama huu ni mfano mbaya, si wa kwanza, tuendelee na maisha. Nijuavyo mimi CCM wamechukia kwa hatua ya Zitto na hiyo ni haki yao.

- Hapa unapingana na wewe mwenyewe sio mimi, haya maswali ameulizwa Mwenyekiti wa Chadema, hakutoa majibu kama yako sasa vipi na huko nako wewe ni mjumbe wa NEC kama CCM nini, labda ndio maana una majibu ya kweli kuliko Mwenyekiti mwenyewe wa Chadema, acha kupoteza muda wangu mkuu, hebu nenda usome tena majibu ya Mwenyekiti wa Chadema alipoulizwa swali la Zitto.

- Sasa unaona unasema CCM wamechukia, wakati wewe mwenyewe kwa maneno yako ni mjumbe wa NEC, sasa unaona unavyojichanganya mkuu? Kwa hiyo huyu Muandishi aliyemuhoji mkuu wa Chadema naye ni CCM na amechukizwa sana na Zitto kukosa cheo? Waste of my time mkuu!

- Na JF hatujawahi kuwa na free pass, hata siku moja wala kuangalia sura au kuogopa jina, you know that!

Respect

FMEs!
 
Just joking: Kama CHADEMA ni mti wenye maembe, na lazima utupiwe mawe. Basi si vibaya tukakiita CHAMA CHA DEMOKRASIA ZA MAEMBE.
 
it is BB v/s fmes!

i hope ni mjadala wa kawaida tu,NO CONFLICTS OF INTERESTS btn the two parties
 
it is BB v/s fmes!

i hope ni mjadala wa kawaida tu,NO CONFLICTS OF INTERESTS btn the two parties

- Wala hakuna sababu mkuu just come out as you are, si unajua hapa kwangu ni mtakuja na mtasuuzika! ila tu stick kwenye hoja na sio viroja! Sasa labda useme hiyo conflict of interest maana ni wewe ndiye uliyeyaleta hayo?

Respect.

FMEs!
 
it is BB v/s fmes!

i hope ni mjadala wa kawaida tu,NO CONFLICTS OF INTERESTS btn the two parties

Kumbe ndivyo? Wengine tumekatazwa na nani?

Halafu hii conflict iko wapi? Mimi siioni hata moja.
 
- Mkuu Orche, Mama Clinton aligombea urais as opposed na maneno yako, soma hapa chini infact kuna wakati hata alishinda kura za some of the states:-

Kama sikosei hamna aliyesema mama Clinton hakugombea urais. Ulikuwa unafananishwa mchakato mzima wa uchaguzi wa Democrats na Chadema. Kwamba mama Clinton alikuwa ni mgombea mmojawapo mwenye ushawishi mkubwa na kwa kutaka kugombea MPAKA MWISHO chama kikawa kinapasuka kutokana na vijembe walivyokuwa wanatupiana. Obama alikuwa anashinda hivyo haikuwa busara chama kuendelea kuumizana wakati adui wao ni McCain. Zitto naye ana ushawishi mkubwa ndani ya chama chake. Kitendo cha kuchukua fomu kikaibua makundi yenye uhasama ambao haujawahi kutokea tena kwenye chaguzi za Chadema na baya zaidi ukichochewa kwa kiasi kikubwa na watu nje ya chama. Makundi haya yote mawili yakashindwa kudhibitiwa na Zitto, Mbowe na chama. Hivyo busara za wazee wa chama, ambao kikanuni wanapaswa kuchambua na kutoa ushauri kwa kamati kuu kuhusu wagombea, zikawatuma kumshawishi Zitto ajitoe. Ilikuwa ni tahadhari kwani suala la kampeni zinafanywaje ndani ya chama bado halijawekwa vizuri kwenye kanuni kwavile bado ni jambo jipya. Zitto nimjuavyo sio mtu anayekubali kuonewa. Kama angeona haki yake inadhulumiwa angekataa ushauri na kuendelea MPAKA MWISHO, ila naye alitumia busara zake na kwa maslahi ya chama akaamua kujitoa.
 
Kama sikosei hamna aliyesema mama Clinton hakugombea urais. Ulikuwa unafananishwa mchakato mzima wa uchaguzi wa Democrats na Chadema. Kwamba mama Clinton alikuwa ni mgombea mmojawapo mwenye ushawishi mkubwa na kwa kutaka kugombea MPAKA MWISHO chama kikawa kinapasuka kutokana na vijembe walivyokuwa wanatupiana. Obama alikuwa anashinda hivyo haikuwa busara chama kuendelea kuumizana wakati adui wao ni McCain. Zitto naye ana ushawishi mkubwa ndani ya chama chake.

- Tofauti ya Zitto na Mama Clinton, ni kwamba Mama Clinton aligombea na akashindwa, Zitto hakuruhusiwa kugombea kwa sababu aliombwa na wazee wa Chadema, asigombee.

- Democratic Party, haijawahi kutaka kupasuka, kwanza haina wanachama wenye kadi mtu yoyote yule unaweza kuamka na kugombea tu on Democratic ticket, hakuna mtu yoyote wa kukuomba ujitoe hata kabla hujagombea, Mama Clinton simply alishindwa uchaguzi, hata angebaki hesabu hazikuwezekana ndio maana alijitoa, hakuwa na wajumbe wa kumpa kura wa kutosha kumshinda Obama, aliyekua amemshinda kwa state nyingi sana ndogo ndogo,

- Mama Clinton aligombea akashindwa, Zitto hakugombea kabisa!

Respect

FMEs!
 
FMES kama nilivyosema hapo juu kilichokuwa kinafananishwa ni MCHAKATO MZIMA WA UCHAGUZI. Na mchakato huo unaanza kwa mgombea kuchukua fomu au kuonyesha nia yake ya kutaka kugombea. Zitto alichukua fomu hivyo alishaingia kwenye mchakato wa uchaguzi kama mgombea mtarajiwa kwa nafasi ya uenyekiti.

Vilevile kingine kilichokuwa kinafananishwa ni timing ya kujitoa ya Mama Clinton kwenye mchakato mzima. Angeendelea MPAKA MWISHO damage ingekuwa kubwa zaidi na hivyo ingekula kwao.
 
I love JF, lakini hapa ndio tunapotofautiana na wengi. Bwana Mbowe ameikwaza democrasia. Hakuna swala hata moja kwenye democrasia ambalo linasema kwamba kama mgombea mwingine atagombea na incumbent then anaweza kutishia usalama wa kichama. CHADEMA ni ya Watanzania, kwa nini wasiachwe waamue nani awe mwenyekiti wao? Instead ya kuimpose system ya kura ya ndio?

Bado naamini kwamba Mbowe ni tatizo ndani ya CHADEMA, na tupo wengi ambao tuna hari ya kujiunga na CHADEMA lakini Mbowe ni kikwazo sababu ya maono yake ya kisiasa.
 
Big up Mheshimiwa Mbowe.Una uelewa na upeoo mkubwa .Jamani naomba hiyo namba ya kuchangia CHADEMA tuanze au bado kuanza?
 
I love JF, lakini hapa ndio tunapotofautiana na wengi. Bwana Mbowe ameikwaza democrasia. Hakuna swala hata moja kwenye democrasia ambalo linasema kwamba kama mgombea mwingine atagombea na incumbent then anaweza kutishia usalama wa kichama. CHADEMA ni ya Watanzania, kwa nini wasiachwe waamue nani awe mwenyekiti wao? Instead ya kuimpose system ya kura ya ndio?

Bado naamini kwamba Mbowe ni tatizo ndani ya CHADEMA, na tupo wengi ambao tuna hari ya kujiunga na CHADEMA lakini Mbowe ni kikwazo sababu ya maono yake ya kisiasa.

CHADEMA ni ya wanaCHADEMA. WanaCHADEMA wameamua nani awe mwenyekiti wao kwa kutumia mchakato walioamua wao wenyewe. Kama wewe unasubiri Mbowe atoke ndio ujiunge na chama ni bora uende kujiunga na vyama vingine. Wanaoitakia mema CHADEMA wanajiunga nayo na kuiboresha wakiwa ndani ya chama.
 
Back
Top Bottom