TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
- Thread starter
- #21
Mara zote ninapojadiliana juu ya suala fulani lengo la majadiliano yangu ni kufikia solution na kuelewesha kwa kufikisha ufahamu.Ama kweli CCM puppets are now on air. Ngoja tukutoe tongotongo machoni na threads zako zisizo fanyiwa utafiti pamoja na nduguyo maralia sugu.
1. Dhamira ya dhati ya kupambana na rushwa na ufisadi sio nyimbo za majukwaani, ama machozi bungeni bali ni kwa vitendo. Rushwa ni kosa la jinai ambalo kwa mujibu wa sheria mtuhumiwa hushitakiwa mahakamani na mwendesha mashtaka wa jamii (Public Prosecutor).
Huyu ni mteule wa Rais aliye madarakani, ingawa anapaswa kufanya kazi kwa mujibu wa katiba. Katiba haijatoa uhuru kwa mtu mwingine kuendesha kesi za jinai. Tueleze ni kwa namna gani CDM watamwagiza DPP awakamate mafisadi na kuwafungulia mashtaka?
Kazi ya kushughulikia rushwa, kuanzia kupeleleza, kukamata na kufikisha mtuhumiwa kwa DPP ni ya TAKUKURU na POLISI (Mkurugenzi wa PCCB na IGP ni wateule wa rais na wanawajibika kwa rais), CDM watatumia njia gani na kwa sheria ipi kumwagiza Hosea au Mwema kutafuta ushahidi kuhusu ufisadi, kuwakamata na kuwafungulia mashtaka mafisadi?
Haiyumkini mahakama zetu pamoja na kuzionesha kama ni vyombo huru, lakini si huru abadani. Jaji Mkuu, Jaji kiongozi na majaji wengine wote ni wateule wa Rais (CCM), mishahara yao na marupurupu inapangwa na serikali, bajeti yao inapangwa na serikali (Celina Kombani), hata kiutendaji ni sehemu ya serikali (Rejea semina elekezi Dodoma na Hotuba toka kwa Jaji mkuu).
Unategemea CDM wataweza vipi kupambana na ufisadi kwa njia mbadala zaidi ya kushitaki kwa wananchi? Katika mfumo ambao Serikali, Bunge na Mahakama zinafanya kazi kama kitu kimoja (Mapacha watatu, baba mmoja CCM), unategemea kundi la wananchi na asasi nyingine watapata wapi haki zao wanazoamini zimenyang'anywa?
2. CDM haijapinga matokeo bila kufanya study kama unavyotaka Dunia iamini. Wana ushahidi wa wazi na waliutoa, lakini CDM ni chama cha wapenda amani kupita kiasi, ndio sababu hawakutaka kuingia barabarani kuandamani kupinga kuporwa ushindi wao. Na kwa kukupa ushahidi dhahiri si tume ya uchaguzi wala CCM ama JK waliokanusha madai ya CDM. Na mpaka leo tume ya uchaguzi haijatoa matokeo kamili ya kura za urais (Tembelea tovuti yao uone).
3. Nadhani hujui unachokiongea unakurupuka tuu. Mwelekeo wa uchumi wa nchi hautolewi na vyama vya siasa ama asasi za kiraia. Mwelekeo wa uchumi wa nchi hutolewa na serikali iliyo madarakani kupitia tume za mipango, wizara ya fedha, Benki kuu na vyombo vingine vya kifedha kama TRA. Hivi ni chombo gani kati ya hivi CDM wanaweza kuvitumia kutoa mwelekeo wa uchumi?
Dunia nzima kushindwa kwa uchumi wa nchi ni kushindwa kwa serikali iliyo madarakani. Jamani, muwe mnaangalia hata TV, fuatilia yanayoendelea sasa Ugiriki, Uturuki japo ufunguke akili kidogo. Na kudorora kwa uchumi wa Tanzania ni matokeo ya kushindwa kwa serikali ya JK na si visingizio vingine.
4. Suala la undugunisation fanya utafiti usikurupuke.
5. Thread yako haijafanyiwa utafiti, kwa wakati huu CDM ndicho chama kinachoungwa mkono na watanzania wengi zaidi kuliko chama chochote cha siasa. Tafiti za sasa zinaonyesha wazi, na matokeo ya Igunga ni sehemu ya ushahidi tosha. Licha ya CCM kununua shahada, kugawa pesa, kupeleka viongozi wake wote wanaoungwa mkono na watanzania wengi, wamerudisha jimbo kwa tofauti ya kura 3000, CDM imenyang'anya kura za CUF 9000, CCM 9000 na kupata nyingine 4000.
Na hii ni tishio kwa CCM ndio maana hawaishi kutisha watu na kubambikiza kesi viongozi wa CDM. Ikiwemo hii ya kizushi kabisa ya Mh. Lema.
6. Siasa ni propaganda, lakini hii yako ni unafiki uliokithiri. CDM wana mgogoro gani? Vipi dhana ya kuvuana magamba na kukatazana kutangaza nia ya kugombea urais? Vipi makundi yanayotafunana ndani ya CCM?
Umesahau mkutano wa wenyeviti na makatibu wa mikoa ulivyoisha kwa kuwa na misimamo inayosigana (Kundi la Makongoro na la Mwenyekiti wa mkoa wa DSM?), kauli ya Sita kuhusu kuenguliwa uspika kwamba ni njama za mafisadi? Je, uamuzi wa chama chenu ulitoka kwa mafisadi?
Vipi kuhusu CCJ vs Magamba? Mgogoro ndani ya CCM ni wa maangamizi, CDM hawana mgogoro wowote ila CCM wanajaribu kuipandikiza bila mafanikio. Wanaweza kufanikiwa kuisambaratisha NCCR na si chama makini CDM.
PUNGUZA UNAZI JADILI HOJA ZA KWELI NDUGU.
Na sina lengo la kuonekana mshindi kwa kupayuka kwingi..,unaweza kudhani kuwa i'm too harsh in critique but believe me kama nisingelikuwa modest basi post yako yote ningeliijaza rangi za makosa ila nimejitahidi sana kuwa fair..,kwa kifupi haujui yafuatayo;
1; utawala wa sheria na namna unavyofanya kazi.
2; haujui nini maana ya "study" ikiwa ni neno ulilolitumia katika hoja yako juu ya kupinga matokeo na pia neno "ushahidi";
3; haujui misingi na kanuni zinazoongoza sera za kiuchumi na namna ya upatikanaji wake, haujui ni nini "uelekeo wa uchumi"
4&5; haujui ni nini "utafiti" usingelisema kuwa CDM ni chama kinachoungwa mkono na watz wengi na takwimu zako ni irrelevant kuhusu igunga.
6; haujui, aidha maana ya mgogoro ama haujui nini kinaendelea ktk chama chako;
Hayo ni katika baadhi ya usiyoyajua..,jaribu kuleta yale unayoyajua tujadiliane..,kwa haya hakuna mjadala....!