CHADEMA ngoma mbichi Arusha

Nashukuru walau nina mwanga kidogo na hoja walizong'ang'ania hao madiwani.

Juzi nilibanwa na mwana-CCM mmoja kwa hoja kwamba wale madiwani walitumia akili sana kuangalia maslahi ya Arusha.

Sikai Arusha lakini akanipa mfano unaoweza kumvuta mtu yeyote kwamba hata mikutano sasa haiendi tena AICC ndiyo maana wanakuja MLIMANI CITY.

Ni kweli kwa mtu asiyejiandaa hoja hizi ni kali na nilitoka pale sina hoja ya kumbishia ndipo nikajaa kichwani maswali kutaka kujua hoja zao.

Kuna mmoja amesema tuunge thread. Nimeileta topic hii makusudi ili tupate kujitumbukiza kwenye viatu vya CC-CHADEMA tukiwa na hoja zao jamvini na nzuri zaidi kama kuna kauli zao zilikwenda hewani bila kupitia any sort of reporter or asseror.
Nikupateje,
Ama kweli umenishika pazuri..Wewe ulipoulizwa swala na huyo mtu wa CCM nadhani hukutaka kukiumiza kichwa chako zaidi ya kutafuta jibu sawa na kile alichotaka yeye kukuonyesha.

Ebu fikiria Meya ni wa CCM na naibu ndiye wa CDM, team yao sii imekamilika? lakini mbona mikutano na vikao vya kimataifa vimehamishwa toka AICC wakiwa kazini?. Kwa nini wao ndio wasiwe sababu ya kutokea haya yote, wakati tunajua fika kwamba mikutano ya kimataifa sio swala la kupanga siku moja, linahitaji maandalizi ya muda mrefu na wakati mwingine venue kuchaguliwa na Taasisi au Jumuiya zinazoshiriki kulingana na mapendekezo.

Mara nyingi vitu kama hivi hutokea tender na ushindani baina ya venues ku host mikutano kama hii.. Sasa kama Meya wa jiji na serikali yake hawana mahusiano mazuri, hawezi kujihusisha kikamilifu kutafuta madeal iweje liwe kosa la CDM.

Labda niulize kitu kingine, wakati wa Nyerere ndege za Air France, Alitalia, SAS, Aeroflot, na nyingine nyingi sana za bara la Ulaya zillikuwa zikitua Dar na Kilimanjaro. Lakini toka tumeingia vyama vingi Ndege hizo zimekoma kuja Tanzania, Je utasema tatizo limetokana na Upinzani wa NCCR, CUF na Chadema maanake nchi hizo wameona hakuna usalama? Na tukifanya muafaka fulani na CCM basi mashirika hayo yatarudisha ndege zao!.

Mkuu tafadhali usipende kuwasiliza watu wanaofikiria wakiwa ndani ya kabati la UCCM maana hawajui yaliyoko nje na hakuna kilicho bora zaidi ya kabati lao...
 
Wakuu mimi ni mmoja wa wanaounga mkono kutimuliwa kwa wale madiwani wa Arusha on the basis kwamba walitakiwa wasome "Disclaimer" ya CDM kabla ya kukurupukia majigambo na kutunishiana misuli na uongozi wao.

Ushauri wangu kwa viongozi wa CDM ni kwamba baada ya mkutano wao huo wa Alhamisi, hiyo SAGA iachwe huko huko Arusha Mwenyekiti wa CDM na katibu wa mkoa ndiyo wawe responsible na kuongea na vyombo vya habari, kudeal na kesi kama watafunguliwa na hata kujibu tuhuma za hao madiwani kama zitatolewa.

Kuna kila dalili kwamba CCM itatumia hii ishu kuhamisha attention ya wananchi kutoka kwenye masuala muhimu ya nchi kama ukosefu wa umeme, mafuta na ufisadi. Yo must understand CCM has been struggling to steal the show for sometimes na ishu hii kwao could be the way. Sasa CDM should play smart on this na kuwaonyesha CCM kwamba wao ni zaidi. Just stay local and leave it local
 
Madiwani watano wa CDM, waliovuliwa uanachama na Kamati kuu ya chama hicho mwishoni wa wiki iliyopita wanakwenda mahakamani kupinga uamuzi huo.

Diwani wa Kata ya Elerai, John Bayo, alieleza kwa njia ya simu akiwa njiani kutokea Dodoma walipokwenda kuhojiwa kabla uamuzi wa kutimuliwa kufikiwa.

Bayo alisema kabla ya kuchukua uamuzi wowote watazungumza na wapiga kura kwenye kata zao kuwaeleza yaliojiri na kuacha nafasi ya uamuzi wa hatua zinazostahili mikononi mwa umma uliwaamini na kuwapa dhamana yb uongozi.

"Binafsi sina kinyongo na chama changu nimepokea nimepokea uamuzi huo, lakini nakuhakikishia nitaendelea na nafasi ya udiwani hadi uchaguzi mkuu ujao, kuna njia nyingine ya kupinga uamuzi huo kupitia vikao au mahakama" alisema Bayo.

SOURCE: www.mwananchi.co.tz
8 August 2011
 
"Binafsi sina kinyongo na chama changu nimepokea nimepokea uamuzi huo, lakini nakuhakikishia nitaendelea na nafasi ya udiwani hadi uchaguzi mkuu ujao, kuna njia nyingine ya kupinga uamuzi huo kupitia vikao au mahakama" alisema Bayo.
Kumbe kuvuliwa uanachama kuna maana zaidi ya ninavyofahamu ! Bayo anaapa kuwa, kwa kutumia vikao (vya Chadema ?) au mahakama, atahakikisha anaendelea na nafasi ya udiwani hadi uchaguzi mkuu ujao - duh !
 
Kumbe kuvuliwa uanachama kuna maana zaidi ya ninavyofahamu ! Bayo anaapa kuwa, kwa kutumia vikao (vya Chadema ?) au mahakama, atahakikisha anaendelea na nafasi ya udiwani hadi uchaguzi mkuu ujao - duh !

Ufahamu kumbe ndiyo tatizo la hao madiwani, sijui wanadanganywa na nani!!!!!!!! Unatumiaje vikao wakati umeshafukuzwa uanachama?????? Kama ni appeal wanatakiwa wakaifanye CDM na sio mahakamani!!!!!!!!!! Hawa jamaa kama ndiyo hivi basi walikuwa ni mzigo kweli kweli!
 
Shughuli ya Arusha ni nzito, CDM hawawezi kutetea viti vyote hivyo. Madiwani walichagliwa kw anguvu ya Umma, leo wanatolewa kwa nguvu ya CDM CC.
you wish, mamgamba bwana. kwa taarifa yako watu walikuwa wanachangua chadema kuliko mtu... na tutateta kata zote
 
Usiwe na wasi wasi tupo Arusha na tunasafisha chama kama ccm mnafikiri kuwahongo wanaopenda pesa basi mkalale nao hao walezi wenu. Wananchi siku zote tuko macho na hatutaki mchezo hii ni generation yetu to make difference Tanzania

[quote="MAFILILI, post: 2330124" ]

Mtafaruku wa kisiasa ndani ya CDM halmashauri ya manispaa ya ARUSHA unazidi kuendelea. Madiwani waliofukuzwa na CDM wameandaa kikao jioni ya leo mjini Arusha kwa lengo la kuwapa wananchi hali halisi kuhusiana na sakata zima la CDM hapo A town.

Tunaomba kwa mwenyezi mungu, sakata la CDM liishe salama ili chama kizidi kuchanja mbuga na kushiriki vizuri mchuano wa IGUNGA wasije kupata kisingizio watapopata kipigo cha mbwa mwizi jimboni IGUNGA wasije na kisinngizio cha mtafaruku wa A town.
 
Shughuli ya Arusha ni nzito, CDM hawawezi kutetea viti vyote hivyo. Madiwani walichagliwa kw anguvu ya Umma, leo wanatolewa kwa nguvu ya CDM CC.
#

Sheria inasema mgombea hatoki mtaani anapitia chama .Chama kina namba kinavyo endeshwa .NEC hawatambui mgombea binfasi bado.Sasa hao huko waendako wanenda kupinga nini ? Haki ipi wanayo ? Walidhaminiwa na Chama kwa wananchi na si zaidi .
 
I wish kama ungemfahamu huyo jamaa usingemjibu,kikulacho ki nguoni mwako..................!Sema tu sheria za JF zinakataza watu kutoa ID ya mtu hadharani.Watu wa aina hii ni wa kuwaumbua tu hadharani wakati mwingine

Hili suala limeamuliwa na CC,kama ni kupinga mtu angeweza kufanya lobbying na kuppinga ndani ya CC hata kama haingii. Tusonge mbele.....!

Ben ebu ni PM nami nimfahamu tafadhali sana.
 
Kumbe kuvuliwa uanachama kuna maana zaidi ya ninavyofahamu ! Bayo anaapa kuwa, kwa kutumia vikao (vya Chadema ?) au mahakama, atahakikisha anaendelea na nafasi ya udiwani hadi uchaguzi mkuu ujao - duh !

Naona CCM na waliomdanganya bado wanaendelea kumdanganya kachanganyikiwa huyo anadhani kwa watawala wanapokutumia ukiwa hauna nafasi bado utaendelea kuwa na nafasi mbele yao, hapo ndio mwisho wake kama kondom waliomdanganya sasa soon watamdamp kwenye dust bin na kutafuta mwingine tena wakudanganya.

Yeye alichagua kukengeuka chama chake kwa kusikiliza Upuuzi wa Nape, sasa labda wanamdanganya kuwa wanaweza kuchelewesha uchaguzi hadi 2015, kitu ambacho CCM haitakubali hata siku moja namshauri aachane na siasa wamejiaribia na kuchafua rekodi yako milele maana katika wakati huu ambapo wananchni wanahitaji watu wa kusimama mbele kuwangoza wao walitaka kuwa vigeugeu wa kupotosha wana-CDM kwa mshahara wa Unafki waende sasa wagombee kwa ticket ya CCM
 
Hao wadiwani 5 wanasema walifikia muafaka na CCM kwa manufaa ya wananchi waliowachangua ili wapeleke maendeleo kwenye kata zao - sasa mimi nasema waendelee kuwapelekea hayo maendeleo waliyokuwa wanayahuburi.

Hawakujua ni kwa tiketi ya CDM tu ndiyo wangeweza kufanya hayo maendeleo waliyoyaota, sasa hapa ndipo tamati ya safari yako ya kisiasa unless warudi CCM. Tena kabla hawajarudi Arusha nawashauri wamtafute NAPE wafanye naye mazungumzo ya awali ili wakatete hizo kata zao kama watakuwa na ubavu huo.

Pia kama wanaona hawajatendewa haki basi waende mahakamani maana walishasema hata wakikata rufaa hivyo vikao vya juu vya chama yaani Balaza kuu na mkutano mkuu hautawasikiliza.

Wewe Mallya acha kuwaburuza wenzako - umeona matokeo ya kupiga NGUMI ukuta wa ZEGE?
 
maji yakimwangika hayazoleki na hii ndio mwisho wao kama kunamtu aliwadanganya kutotii ni chama kiliwataka watajiju
 
mkuu freedom of flag, tunachojaribu kukiangalia ni kwanini hawakutii mapendekezo ya kamati kuu pamoja kushauriwa na watu mbalimbali mfano mzee mtei..

Aliye watuma alikuwa anawapa moyo na kuwarubuni kudhara maamuzi ya CC, hii inaonyesha dhahiri kuwa hawa hawafai kuwa sehemu ya CDM kwa wakati huu acha waende huko waliko danganywa sikio la kufa halisiki dawa
 
Shughuli ya Arusha ni nzito, CDM hawawezi kutetea viti vyote hivyo. Madiwani walichagliwa kw anguvu ya Umma, leo wanatolewa kwa nguvu ya CDM CC.

Hoja hapa sio viti vya udiwani ni uadilifu. CCM ndio wanaoweka kipaumbele katika kutetea viti badala ya uadilifu. CDM imekaa muda mrefu tu bila ya viti vyovyote na chama kilikuwepo.

Je CCM leo hii ikikosa nguvu za kidola inaweza kuendela kuwepo katika hali ambayo hata viongozi wake wa ngazi za chini kukutana ni lazima ufanyike ufisadi ndani ya serikali za mitaa, vijiji n.k?
 
Saharavoice,
Afadhali tukose viti in the short term ili tujenge uongozi bora in the long term.

Mkuu Jasusi hapo umenena mkuu. Hawa wanaonekana walikuwa wachumia tumbo. Hawawezi kabisa kutetea walalahoi wakati CDM iko kwa ajili ya maslahi ya umma kwa ujumla wake.
 
Shughuli ya Arusha ni nzito, CDM hawawezi kutetea viti vyote hivyo. Madiwani walichagliwa kw anguvu ya Umma, leo wanatolewa kwa nguvu ya CDM CC.


it is better to remain with few and stable leaders than to have many leader who are traitor of Democracy..I know they will create rumors but let we focus ahead.....njia kufikia ukombozi wa kweli si rais kama wengi tunavyofikiri, self sucrification, devotion and tolerance is needed...........wana chadema dont think that eversyday good thing will always be on your tracks, the fact is that there many peoples who have been planted to your part, what you are supposed to do is to identify them and chase them away............................democracy is expensive if and only real you mean what you stand for..........viva CDM.. please show the path to my friend Nnauye that action speaks louder than being chatter box
 
<br />
<br />
ni kweli kabisa Mkuu, hawa jamaa walishauriwa sana kabla ya maamuzi, lakini walisimamia hata wasichokiamini. Hii inanipa imani kwamba Mallah na wenzake walikuwa na agenda za siri kuivuruga chadema, bahati mbaya kakwaa kisiki, nadhani hata aliyemtuma atakuwa ICU kwa maamuzi ya chadema. Watalipa hela za magamba pumbavu zao. Nina hasira nao sana hawa jamaa, nakumbuka siku Akina Marando walipokuja Arusha mmoja wao alinipigia simu asubuhi, akaniambia endapo nitaulizwa na akina Marando kuhusu suala la muafaka nimjibu kuwa sisi viongozi wa chama tunaukubali muafaka, lakini eti tunamshangaa Lema. Nami nikamwuliza kama ataniambia walichoafikiana ni nini, masharti yao yalikuwa yapi, na vipi kuhusu kesi, mauaji ya watu ya januari 5, na watu waliopata vilema? Hakunipa jibu, japo sipendi kutukana lakini nitoa dongo.
hayo maswali niliyauliza siku nipoaambiwa mwafaka umepatikana na swali lingine ambalo nililiuliza ni kuhusiana na Mary Chitanda mbunge mkoa wa Tanga kuwa mpiga kura halali mkoa wa Arusha...alicho nijibu wameona bora kwanza waanze na mwafaka halafu baadae ndiyo watajadiliana na juzi jumamosi nilipowapigia waliniambia eti masharti ya CHADEMA yalikuwa hayatekelezeki.

Mfano Serikalikutoa mkono wa pole kwa wafiwa na majeruhi eti serikali ingepelekwa mahakamani kudaiwa...nikajiuliza hawajamaa wako kwa masilahi ya nani, je wanaionea huruma serikali yao kupelekwa mahakamani, je wanaona aibu serikali yao kuonekana ilivunja sheria kwenye swala la Arusha...lakini jibu nililo lipata kichwani mwangu ni kuwa kuna rushwa hapa ilitumika kuwabadilisha hawa jamaa siyo bure.....
 
Back
Top Bottom