CHADEMA ndiyo walioshinda uchaguzi mdogo wa Igunga

Kushinda au kushindwa huwa hakuna maelezo ni suala la wazi.

My take : opposition hawahitaji kutolea maelezo ya kushindwa, they just have to take note if there is a stead growth in their popularity else they have to rework their way of doing political business.

This country needs a strong opposition, I MEAN WISE OPPOSITION not trouble makers to discipline whoever is rulling not by causing problems but by critically challenging them.

You really think you have credibility to advise anybody? Just stay and hang on your dreams until the wind shows the direction.
 
Marwa,
Wewe kama Senior, chambua hoja na uikosoe, acha thihaka. Uchambuzi huo ni kweli au sikweli; maana wengine hatujapitia takwimu kwa undani nawe tupe wako kinzani na anayosema. Kama CDM walipeleka watu 2,000, ni kosa lipi? Walipiga kura katika vituo vipi?
 
Na wasiwasi wakati unaandika hii thread ulikuwa una hara kwani haina kitu na waonekana hata mambo ya uchaguzi huyajui ww. Kwa taarifa yako CDM kwenye huu uchaguzi wametumia Tshs 1.345 bn ambazo zingetosha kufungua ofisi za wilaya au hata kata zipatazo 300 na zaidi. Na mmeambulia patupu na wengine wamezimia jana viongozi wenu, taarifa ziko wazi kabisa

From 70% win nine months ago to 50% win. The GeniusBrain calls it a win my foot. Possibly it is Geniusbrain under masaburi yardstick
 
FoolishBrain,
Ok CDM wametumia Tshs.1,345 bn. Well and good. Haya CCM wametumia Tshs.10 bn+! Kwa hiyo unataka kusema kuwa CDM ndiyo wametumia pesa nyingi kuliko CCM???
Hoja yako kuwa CDM wangelizitumia hizo pesakufungua ofisi za wilaya au hata kata zipatazo 300 na zaid ni dhaifu sana!
Wewe ulipashwa KUWAHOJI HAO MAGAMBA WENZAKO kwanini hizo 10 bn+ hawajataka kuziingiza kwenye MIRADI YA MAENDELEAO YA WILAYA YA IGUNGA KAMA MAJI,AFYA,SHULE,BARABARA na DARAJA kubwa lililiokuwa likipigiwa makelele na kina MAGUFULI kuwa watalijenga baada ya Uchaguzi wa juzi.

Kama miaka yote 50 tangu uhuru CCM wameshindwa kujenga miundo mbinu na kuboresha hali ya maisha ya wana-Igunga ndiyo wataweza sasa kupitia huyo FISADI WA MADINI Dr. Kafumu? Jibu ni HAPANA.

Mimi nawapa pole sana Wana-IGUNGA kwa uelewa mdogo na ufinyu wa mawazo wa kushindwa kupambanua ULAGHAI WA CHAMA TWAWALA na kukipa ridhaa ya kuwaongoza tena kwa miaka 4 ijayo. Hii itakuwa ni miaka ya mateso,njaa,maradhi,ujinga na ukosefu wa maji.

Poleeeeeeeeeeeeeeni sana kwa kutapeliwa na ri-CCM lenu. Bakong'wanzoka bing'we banadakama!

Hizo pesa za kujenga barabara , maji nk kwa wana igunga nyie ndio mgezipata wapi ? isssue bado iko pale pale mlikuwa mnawategemea wakina magufuli kuwapigia magoti wajenge, na ingekuwa aibu kwa watu wa igunga kuchagua mbunge wa cdm ambae anakuja kutekeleza ilani ya ccm.
 
Igunga ina kata 26 na sio Kata 17! Mbona hujasema habari ya wapiga debe 2000 wa Chadema kwenda Igunga?

Kwani wapiga debe wa eneo tofauti wanaruhusiwa kupiga kura!!!?John Marwa na akili mbovu Kama hizi!!!!?
 
From 70% win nine months ago to 29% win. The GeniusBrain calls it a win my foot. Possibly it is Geniusbrain under masaburi yardstick

Soma taarifa ya tume ya uchaguzi ccm wameshinda kwa asilimia ngapi? acha kupotosha watu na takwimu uharo hz. Nyie twajuam mmechanganyikiwa na hata Dokta jana alizimia, hizi taarifa mbona tunazo, hali ni mbaya kwa cdm hv sasa
 
Soma taarifa ya tume ya uchaguzi ccm wameshinda kwa asilimia ngapi? acha kupotosha watu na takwimu uharo hz. Nyie twajuam mmechanganyikiwa na hata Dokta jana alizimia, hizi taarifa mbona tunazo, hali ni mbaya kwa cdm hv sasa
Ahsante kwa matusi inazidi kuthibitisha ugenious wa kimasabauri. Huoni kama 20% drop in nine months ni issues?
 
Uchaguzi wa Jimbo la Igunga umemalizika J2 na mshindi kutangazwa jana 3 Oktoba,2011 na msimamizi wa Uchaguzi. Kwa kufanya tathmini ya haraka haraka tu baada ya Uchaguzi na matokeo kutangazwa CHADEMA kwa uhakika kabisa ndiyo Walioshinda Ubunge huko Igunga. Nitaeleza.
  1. CHADEMA wamepata kura 23,260 dhidi ya kura 26,484 za CCM.Tofauti ya kura 3,224! Tukumbuke kuwa Uchaguzi Mkuu 2010 CDM hawakuwa wamesimamisha mgombea Ubunge jimbo la Igunga. Lakini mgombea Urais wa CDM Dr.Slaa alipata kura 8,000+. Hii inaashiria kuwa CDM inapendwa na ina uhakika wa kufanya vizuri zaidi 2015.
  2. CHADEMA wametumia gharama ndogo ukilinganisha na CCM chama twawala. Gharama elekezi ya Uchaguzi toka msajili wa Vyamailikuwa Tshs.80m. CCM wametumia NGUVU na GHARAMA kubwa sana kulipata jimbo hili. Tunaambiwa CCM wametumia Tshs.10 Billion!Gharama hizi lazima ziwe juu kwa vile Serikali yote ilihamia Igunga.
  3. CHADEMA wametumia HELIKOPTA MOJA tu wakti CCM wametumia HELIKOPTA MBILI.
  4. CHADEMA hawakutumia SERA ya UDINI kama walivofanya CCM kwa kumgeuza DC wa Igunga kuwa mtaji wa siasa za UDINI. Pamoja na siasa CHAFU za udini za CCM bado hazikufaulu. Tumeona Masheikh wakihimiza Waislamu kutoipigia CDM kura kwasababu ya kumdhalilisha DC ambaye ni Muislamu fake!
  5. CHADEMA kupata KURA 23,260 dhidi ya CUF iliyopata kura 2,104 ni ushindi tosha kabisa dhidi ya SIASA CHAFU ZA UDINI(Uislamu).
  6. CHADEMA wamepata kura 23,260 kwa mjini tu yaani KATA 5! Huu ni wastani wa kura 4,652 kwa kata! CCM amepata kura 26,484 toka KATA 17! Huu ni wastani wa wapiga kura 1,557 kwa kata.Kwa maana hiyo kama CDM kikianza kujiimarisha vijijini CCM wajue watakuwa na hali mbaya sana na hawatakuwa na kitu tena Igunga 2015! CDM lazima wajifunze toka hapo kwamba KUANZISHA MATAWI YA CHAMA VIJIJINI NI KITU CHA LAZIMA NA UTAKUWA MTAJI MZURI SANA KWA GE-2015.
  7. CHADEMA hawajatumia DOLA(Serikali kwa maana ya Polisi,UWT na MAWAZIRI) kujinadi Igunga. CCM wametumia POLISI,UWT na RASLIMALI za SERIKALI.
  8. Kwa CHADEMA hii ni INDICATOR kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2015 utakuwa ni UCHAGUZI MKUU WA KUIMALIZA NA KUINYAMAZISHA CCM KWENYE ULINGO WA SIASA ZA TANZANIA.
Kwa vipengele hivi inadhihirisha kabisa CHADEMA ndiyo washindi wa jimbo la Igunga na siyo CCM. Kwa mara nyingine CHADEMA wameithibitishia serikali ya CCM kuwa ndicho Chama pekee cha upinzani chenye nguvu Tanzania kwa sasa! Huo ndiyo ukweli wenyewe bila kujali CCM kama watakubali au la.

Nawasilisha.

totally crap + wasted... kushindwa hata kwa kura moja.. ni ishahidi tosha cdm they have a long way to go .. inshort watu wa igunga wamevote for no confidence .. kushindwa ni kushindwa tu it ain't matter kwa kura ngapi.
 
Igunga imewashinda mnawaza kushinda Nchi nzima 2015! Tatizo la kuvaa magwanda akili yote ina hamia kwenye magwanda!
Hahaaaaa, kweli umenena John Marwa, Je tatizo la kuvaa mashati, vilemba na vitenge vya kijani akili inahamia wapi???? Kwenye Makalio (a.k.a Masaburi)

Take care
 
Uchaguzi wa Jimbo la Igunga umemalizika J2 na mshindi kutangazwa jana 3 Oktoba,2011 na msimamizi wa Uchaguzi. Kwa kufanya tathmini ya haraka haraka tu baada ya Uchaguzi na matokeo kutangazwa CHADEMA kwa uhakika kabisa ndiyo Walioshinda Ubunge huko Igunga. CHADEMA ndiyo washindi wa jimbo la Igunga na siyo CCM. Kwa mara nyingine CHADEMA wameithibitishia serikali ya CCM kuwa ndicho Chama pekee cha upinzani chenye nguvu Tanzania kwa sasa! Huo ndiyo ukweli wenyewe bila kujali CCM kama watakubali au la..

Sawa mkuu.
CHADEMA ndio wameshinda uchaguzi....tumefurahi sana kusikia CHADEMA wameshinda uchaguzi Igunga.
Mbunge aliyechaguliwa anatoka chama kipi?
Tume ya uchaguzi ni ile ya Lewis Makame na Kivaru?

Kama tume ndio hiyo ya Kivaru basi CHADEMA kimeshinda...Kama ni Tume huru basi CHADEMA hawawezi kushinda uchaguzi.

Tuendelee kushiriki chaguzi bila ya kuwa na Tume huru na bila ya kuidai Tume huru kwa nguvu zetu zote na matokeo yatabaki haya ya kujifajiri na kujisemea tutashinda next time, tutashinda 2015.

Kwa Tume ipi ya uchaguzi?...yes , CHADEMA ndio chama dume, ndio chama pekee cha upinzani!!!

Nimefurahi sana kusikia CHAMA CHA UPINZANI kimeshinda uchaguzi wa Igunga. Tujipongeze!
 
sammosses:ukweli utabaki palepale siku zote,magamba kitathimini wameshindwa.watumishi wa umma wamekaa siku ngapi bila kulipwa mishahara yao?!!!!!eti kisa mishahara imekwenda kwenye kampeni!!hivi kweli tutafika?miaka hamsini bado chama tawala kinatumia mbinu chafu za kununua haki za wananchi wake,bila kujali wavuja jasho.Ipo siku watakuja kulipa deni la usaliti.

Walitaka kuchakachua Kata ya Masekelo mjini Shinyanga ,mbona walishindwa na nguvu ya umma.siku zao za kula bata zinahesabika lakini kila jasho la mnyonge linahesabika.Big up kwa sana wana wa Igunga mliogundua zipi mbivu na zipi mbovu.leo hii mmeona umuhimu wa mabadiliko mmeichagua CDM kwa kura nyingi na ndio bwana mkubwa Sindbad baharia ana wabeza kuwa vyama vya msimu,kama ni vya msimu kulikoni kutumia nguvu kubwa za dola ikiwa pamoja na kufisidi kodi zetu walalahoi kwa kuwalipa posho mawaziri wa serikali bila idhini ya waajiri wao yaani wana wa nchi hii.ALUTA CONTINUA ..........................
 
Tufahamu CCM Ni chama dola,kinamiliki serikali na maamuzi yake.Suala la kukitoa madarakani ni suala la kishabiki kwa sasa lkn tunashindwa kujua tunataka nini kwa wakati huu na hata hao CHADEMA bado hawajatupa uhakika kama tukiwapa mamlaka hawatafanya kama CCM.Suala lililotakiwa kufanyiwa kazi ni utungaji wa KATIBA ambayo itatuongoza jinsi ya kumpata rais na serikali,chama kitakachomtoa raisi kisiwe ndio serikali na Rais wa nchi asiwe juu ya sheria(kinga ya kutokushitakiwa iondolewe).Mamlaka makubwa aliyopewa rais yapunguzwe na sheria za uhujumu uchumi zirudishwe,uadilifu makazini na kila mmoja ajue nafasi yake makazini na tabia za khanga(kama cdm)zisiwepo.Unajua m2 anapopata muda wa kupiga majungu ujue sio muadilifu,kwaiyo suala la nani aongoze nchi sio muhimi ila muhimu ni nchi iongozwe kwa kufuata misingi hii na ile hilo ndio muhimu kwa sasa sio ooh ccm,ooh cdm ushabiki 2ume2jaa na siasa za vijiweni,mshindi kashinda mwacheni ale vyake.

Mkuu chama dola?! Unamaanisha state party?! Kama ndivyo, hakuna kitu kama hicho kwa TZ. CCM ni chama kinachoongoza serikali ya JMT tu; tafadhali husichanganye habari za serikali na dola, ni vitu viwili tofauti.

Dola linamilikiwa na wananchi wenyewe!
 
Mkuu Makoye uko juu sana!!! Achana na hao FOOLISHBRAIN wanapima mafanikio kwa tukio moja tu (kushinda au kushindwa uchaguzi wa IGUNGA). Ukweli ni kwamba UCHAGUZI WA IGUNGA umetoa VERY RELEVANT POLITICAL SNAPSHOT kwa vyama vikuu vitatu yaani CCM, CDM, na CUF. Analysis yako iko very clear....kwamba kwa kutazama mbele yafuatayo yako dhahiri kabisa, bila kujali itikadi za vyama:
-CCM Supremacy is declining. Bado mtaji mkubwa wa CCM uko vijijini. Perhaps, had election process be conducted in a level playing field...CCM would be history.
-CHADEMA is steadily gaining momentum. Ushahidi uko wazi kwamba sehemu za mijini tayari CDM wanakubalika sana...ila wana changamoto ya kueneza elimu ya uraia kwa wananchi wa vijijini ambao wanarubuniwa kirahisi na CCM.
-CUF is getting off the track. Wanatakiwa kufanya a lot of restructuring laa sivyo chama kitakufa!!!
 
Chadema walienda Igunga kushinda au kufanya political analysis? Kushindwa kuna umiza sanaa! Poleni sana magwanda!
 
Chadema walienda Igunga kushinda au kufanya political analysis? Kushindwa kuna umiza sanaa! Poleni sana magwanda!

Mujitathmini kupungua kura kwa 20% ukilingamisha na gain ya kura 23,000 kutoka 0. Usiangalie ushindi angalia taarifa na mantiki katika takwimu. Nitakupa true story ya kweli, wanangu walimpa mmoja wa bibi zao noti mbili za elfu kumi kumi, akakataa akataka mapene (coins) akapewa coins tano za ishirini ishirini akamwaga baraka zote zote kabisa. Hali hiyo hiyo ikajitokeza kwa baadhi ya wajomba na akina shangazi zangu.

Hayo ndiyo mafanikio ya ccm kwenye takwimu siyo kwenye maana ya takwimu
 
Back
Top Bottom