CHADEMA ndicho chama makini kilichobaki Tanzania

Mkondakaiye

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
838
174
Katika vyama vya siasa vilivyopo hapa Tanzania CDM ndicho chama pekee kilichobaki kuwa chama makini na kinachoshughulika na matatizo ya watanzania kwa sababu zifuatazo:
  1. CDM Toka uchaguzi umalizike wamekuwa msitari wa mbele kupigania haki za wananchi na kuibana serikali kwa kusababisha uchumi wa Tanzania kushuka na kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu. Na hata ilipofukuza wanachama hakuna malalamiko yaliyotolewa.
  2. CCM wao toka uchaguzi umalizike wamekalia kulalama kuvuana magamba ambayo yameshindikana kuto na huku wananchi wakiumia na hali ngumu ya uchumi na wala hawajali.
  3. NCCR-MAGEUZI na CUF Toka uchaguzi uishe wamebaki kuwatukana CDM kwa kufadhiliwa na CCM na wananchi kuwaita CCM B na laana iliyowapata wameanza kufukuzana.
  4. TLP na UDP Toka uchaguzi umalizike wamejikita kutafuta maslahi yao binafsi huku wakiunga mkono CCM na kuacha kutetea wananchi
  5. Vyama vingine ni vya musimu wakati wa uchaguzi kuitibulia CDM

CDM kazeni buti, Msikae mjini nendeni vijijini mkawaamushe watu waliolala ili magamba wasiwaibie kura tena.

Tujadili
 
Maelezo yako, yako wazi ni ukweli mtupu na iyo haina mjadala ivyo basi tushikamane dumu na chadema yetu, mpaka 2015 na kuendelea ili tuwasurprise magamba, mafisadi wa ccm na washirika wao inshallah
 
Haikuwahi tokea chama kingine tofauti na CDM kikawa makini.
Labda unikumbushe lini CCM au CCB-B vilikuwa makini?
 
Ebu ngoja tuangalie sifa za chama makini Chadema.

1. Chadema inawalazimisha wabunge wake kususia mijadala ndani ya Katiba.

2. Chadema haikujali kwamba wabunge hao hawakufikishwa bungeni kwa kadi za Chadema bali kwa kura za wapigakura.

3. Chadema waliwafukuza kwa nguvu Madiwani wake ambao ni wawakilishi halali wa wananchi.

5. Chadema wanataka kutuendesha wananchi kama maroboti, ndio maana wanatarajia kuungwa mkono kirahisi watakopoanza kuuza siasa nyepesi za kuwataka Watanzania wasusie mjadala wa katiba.

6.Narudia kusema tena Chadema, Wananchi sio misukule kiasi cha kuburuzwa kirahisi kwani wanajua kupembua kati ya dhamira njema na dhamira mbaya.

Hizo ni baadhi ya sifa za chama makini Chadema
 
Hapo Ndo naona sasa wewe Ritz ni fake kwelikweli ,hayo yote unayajua mwenyewe pia ,wewe ni Gamba kweli hujuwi kucompare na contrast ,hayo ni negativity zako juu ya CDM huijuwi CDM na usomi Katika yake.Unaendesha ushabiki tu ambao hauna jipya zaidi ya kutunga vitu vya upande mmoja au ndo wewe uliyepoteza kiti cha uchanguzi 2011 kwa CDM nini?
 
Nakwenda kukusanya data za chama makini Chadema tarudi kuziweka humu jamvini tuwe na subira.
 
Ebu ngoja tuangalie sifa za chama makini Chadema.

1. Chadema inawalazimisha wabunge wake kususia mijadala ndani ya Katiba.

2. Chadema haikujali kwamba wabunge hao hawakufikishwa bungeni kwa kadi za Chadema bali kwa kura za wapigakura.

3. Chadema waliwafukuza kwa nguvu Madiwani wake ambao ni wawakilishi halali wa wananchi.

5. Chadema wanataka kutuendesha wananchi kama maroboti, ndio maana wanatarajia kuungwa mkono kirahisi watakopoanza kuuza siasa nyepesi za kuwataka Watanzania wasusie mjadala wa katiba.

6.Narudia kusema tena Chadema, Wananchi sio misukule kiasi cha kuburuzwa kirahisi kwani wanajua kupembua kati ya dhamira njema na dhamira mbaya.

Hizo ni baadhi ya sifa za chama makini Chadema

1. CCM inawalazimisha wabunge wake kuunga mkono hoja za kimasabuli.
2. Bila kuwa mwanachama wa chama chochote huwezi kupitishwa kuwa mgombea kupitia chama hicho
3. Walifukuzwa lakini hakuna wananchi waliolalamika. ona kafulila na HR watu wanavyolalamika.
4. Watanaznia ni watu wenye akili, siasa za zidumu fikira za mwenyekiti unazotaka kuziendeleza zimepitwa na wakati.
5. Watanzania sio misukule unatakiwa uwaombe radhi.

Kwajinsi usivyo makini hata kuhesabu hujui. ona ulivyopanga umasabuli hapo juu
 
Mkuu Mkondakaiye,

Tanzania inahitaji mabadiliko makubwa hili iweze kukabiliana na chanagamoto za karne ya 21 bahati mbaya mpaka sasa hakuna chama chochote cha siasa ambacho kimejipanga kimkakati kuwakomboa waTanzania dhidi ya madui wanne wakubwa UJINGA,UMASIKINI,MARADHI na UFISADI.Narudia tena vyama vyote vimejikita zaidi kupata madaraka lakini havina ajenda ya maana ya kuondokana na hao maadui watatu wakubwa.
 
Nithibitishie, isije kuwa unatumia kauli ya samaki mmoja akioza wote wameoza.
 
Mkuu Mkondakaiye,

Tanzania inahitaji mabadiliko makubwa hili iweze kukabiliana na chanagamoto za karne ya 21 bahati mbaya mpaka sasa hakuna chama chochote cha siasa ambacho kimejipanga kimkakati kuwakomboa waTanzania dhidi ya madui wanne wakubwa UJINGA,UMASIKINI,MARADHI na CCM aka UFISADI.Narudia tena vyama vyote vimejikita zaidi kupata madaraka lakini havina ajenda ya maana ya kuondokana na hao maadui watatu wakubwa.

Adui namba nne ni CCM ufisadi ni chembe tu ktk adui CCM. Bado kuna undugunization,udinization,ukoonization,urithinization nk
 
A plan is not a litany of complaints...
Ikiwa Chadema kazi yake kubwa ni kubwabwaja tu..then it is a useless party..

Ndio maana wenzenu waligundua hili kule Zanzibar, wakaona hawawezi kuwaambia wananchi same stories everyday..
malalamiko.. malalamiko..malalamiko..
Huwezi kujenga nchi kwa kulalamika tuu..

Wananchi wanahitaji maendeleo sio MAANDAMANO!

Sijuwi umakini wa Chadema una upimaje?
  1. Chama ni NGO ya watu wachache wa Kaskazini
  2. Inaendeshwa kama family property
  3. Iko religiously polarized..
  4. Haina national agenda..bali ni Zonal agenda..
 
Hofu yangu ni kwamba pindi CHADEMA watakapochukua utawala wa nchi hii, hakutakuwa na chama makini cha upinzani, kwani wakati huo CCM na wakala wake watakuwa wamezikwa.
 
katika vyama vya siasa vilivyopo hapa tanzania cdm ndicho chama pekee kilichobaki kuwa chama makini na kinachoshughulika na matatizo ya watanzania kwa sababu zifuatazo:
  1. cdm toka uchaguzi umalizike wamekuwa msitari wa mbele kupigania haki za wananchi na kuibana serikali kwa kusababisha uchumi wa tanzania kushuka na kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu. Na hata ilipofukuza wanachama hakuna malalamiko yaliyotolewa.
  2. ccm wao toka uchaguzi umalizike wamekalia kulalama kuvuana magamba ambayo yameshindikana kuto na huku wananchi wakiumia na hali ngumu ya uchumi na wala hawajali.
  3. nccr-mageuzi na cuf toka uchaguzi uishe wamebaki kuwatukana cdm kwa kufadhiliwa na ccm na wananchi kuwaita ccm b na laana iliyowapata wameanza kufukuzana.
  4. tlp na udp toka uchaguzi umalizike wamejikita kutafuta maslahi yao binafsi huku wakiunga mkono ccm na kuacha kutetea wananchi
  5. vyama vingine ni vya musimu wakati wa uchaguzi kuitibulia cdm
cdm kazeni buti, msikae mjini nendeni vijijini mkawaamushe watu waliolala ili magamba wasiwaibie kura tena.

tujadili
wameiga sasa wametepeta....tulienda ikulu wakapiga copy..tukawatimua wanachama ambao sio waaminifu sasa wameiga wamepotea vibaya..big up chadema sasa tusonge mbele kwa kasi ....watakuwa wamejifunza hawataiga tena...tunawategemea mtakuja na mbinu kabambe itakayotusaidie tutoke hapa tulipo..viva chadema
 
Sina la zaidi la kusema,kwani matendo ya CHADEMA yanasema yenyewe na wananchi wanaona!CCM wapo Ikulu,lakini Dr Slaa na CHADEMA wapo mioyoni mwa watanzania wengi!
 
Hofu yangu ni kwamba pindi CHADEMA watakapochukua utawala wa nchi hii, hakutakuwa na chama makini cha upinzani, kwani wakati huo CCM na wakala wake watakuwa wamezikwa.

Maneno yako nimeyakubali kabisa mkuu .Idumu Chadema
 
Hofu yangu ni kwamba pindi CHADEMA watakapochukua utawala wa nchi hii, hakutakuwa na chama makini cha upinzani, kwani wakati huo CCM na wakala wake watakuwa wamezikwa.

Yaah,umeongea jambo la msingi mno!Unapendekeza nini mkuu?
 
Back
Top Bottom