CHADEMA ndani ya Sumbawanga

Nami ndo narejea toka katika mkutano,wacha kabisa watu walifurika katika viwanja vya Msakila sekondari haijapata tokea.Mkutano umeisha saa 07.49.wanachama zaidi ya 600 wamejiunga na CHADEMA!Wengine wamerejesha kadi za Magamba,lililonifurahisha zaidi wazee muhimu sana wa kifipa,mzee Zeno Nkoswe mzee Mtuka nao pia wamerejesha kadi za chama cha Magamba na kujiunga na CHADEMA.kumbuka hawa wazee ndio walihamasisha sana wananchi wa Sumbawanga kuchagua viongozi wadilifu katika nkoa huu!Hii naona ni hatua moja kubwa sana katika mkoa wa Rukwa kuelekea mageuzi juu ya nchi hii.T-Shirts,holders na promotools zimenunuliwa kama njugu.Jamani CHADEMA inatisha,Mbowe,Slaa,Zitto,Mpendazowe wachache walioongea wakati nafika kwa mkutano.
 
Nimepigiwa simu na bibi (ambaye ni mwenyekiti wa mtaa kupitia CCM),hali iliyotokea leo imeushangaza mji wa Sumbawanga. Anasema waanzilishi wa TANU wamerudisha kadi zao. Kuna Mzee anaitwa Nkoswe na mwingine Mtuka, walikuwa ni wanachama prominent w CCM miaka mingi sana. Wameamua kurudi kundini (CHADEMA).
 
Mkuu tunashukuru sana kwa updates na mafanikio hayo. Hivi kamanda Arfi alikuwepo?
 
attachment.php
 
Nimepigiwa simu na bibi (ambaye ni mwenyekiti wa mtaa kupitia CCM),hali iliyotokea leo imeushangaza mji wa Sumbawanga. Anasema waanzilishi wa TANU wamerudisha kadi zao. Kuna Mzee anaitwa Nkoswe na mwingine Mtuka, walikuwa ni wanachama prominent w CCM miaka mingi sana. Wameamua kurudi kundini (CHADEMA).

Yaa Mzee Mtuka namfahamu sana ni mpiga picha maarufu Sumbawanga, alikuwa CCM humwambii kitu, yaani ni wale wazee waliokunywa maji ya kijani, kama ni kweli nae ameondoka CCM, kazi wanayo. Atabaki JK na Riz1 na Salma huko
 
tujuzeni zaidi yanayojiri huko na waliokuwa kwenye front line huko, na km inawezekana tupostieni hayo ma foto ya wapambanaji!

Sugu:- Uchumi mdogo ni muhimu kwa ustawi wa Taifa, mama ntilie na wamachinga waandaliwe mazingira bora kuimarisha hilo. Wasibughudhiwe. Chiku:- Watanzania wawe na ujasiri kulinda na kutetea mambo ya msingi ikiwa ni pamoja na matokeo wakati wa uchaguzi. Hili pia kalisema Mch. Msigwa. Zito:- CDM kuwasilisha bajeti kivuli inayoonyesha njia ya kupunguza makali ya maisha kwa mtanzania wa chini, hii ni katika bunge lijalo. Dr. Slaa:- CDM ina waraka wa siri wa ccm wenye tathimini ya uchaguzi mkuu ulopita. Amewashukuru wana swanga kwa mwitikio thabiti kwenye sanduku la kura 2010. Mbowe:- Shukrani za cdm kwa wana swanga, wabunge wa cdm ni wa kitaifa na watafanya kazi popote bila kuchoka, watasemea ulazima wa kupunguza ukali wa maisha mda wote bila kuchoka. Katiba mpya si sera ya ccm na hivyo wataonyesha njia ya kufika huko chini ya uimara wa Lissu. Regia alikuwepo na wabunge kadhaa ambao sikuwapata majina yao maana napita tu. Kesho ni mpanda pengine ntawajuza zaidi.
 
Nimejifunza kuwa Watanzania wengi hawana shughuli za kufanya, hivyo kuwa tayari kujiunga kwenye tukio lolote litakalowachangamsha na kuwasaidia kuupoteza muda wa siku husika.

Hapa chini ni wana Sumbawanga walipoenda kumsikiliza Kikwete mwaka jana.

Francis Godwin ni mzee wa matukio daima: MGOMBEA URAIS WA CCM DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE APATA MAPOKEZI MAKUBWA SUMBAWANGA LEO

Nasema, mwitikio wa wananchi ni mkubwa na umeanza kuondoa dhana ya chama tawala. Amka wewe!
 
Mambo poa kabisa. Walisema CDM ni chama cha msimu sijui sasa watasema nini? Tuzidi kusonga mbele hadi kieleweke. CDM oyeee, Magamba ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Yako mambo ambayo kila mtu anapaswa` kujiuliza sasa ingawa sina uhakika kama majibu yatapatikana. Kama ni kweli na kama inavyoeleweka duniani kote kuwa uchaguzi popote pale duniani hutoa kiu ya mahitaji ya kisisa katika kipindi fulani, sasa kwa Tanzania iweje leo wananchi waliokata kiu ya kisiasa miezi minne iliyopita mwezi moja baadaye wawe na njaa kubwa ya kisisa na kutaka mabadiliko kiasi hicho? wingi wa watu hao na wasiwasi alioonyesha JK katika hotuba ya mwezi wa tatu inaacha maswali elfu moja yasiyoweza kujibiwa kwa ufasaha, kukidhi kiu hii ni kuwambia wananchi waliibiwa kura zao. Had it been election was organized fairly CDM wouldnt be a crowed puller in a period less than two months after election results were out.
 
Nipeni raha mie nipeni raha, aaaaeeeee. Kombe ni swaga za kuleeeee! Mwisho utaelezea namna, mwenye akili haambiwi tazama n.k
 
Hizi picha zihifadhiwe sana na CDM kama kumbukumbu ya uhamasishaji wa Watanzania ulivyofanyika. Tumetawaliwa na kikundi kile kile kwa miaka 50 bila kupata maendeleo (na hata kuwa na maisha magumu zaidi). Sasa CDM inahamasisha wananchi ili tuanze upya.

Hizi picha zitakuwa sehemu ya vielelezo muhimu vya historia ya taifa letu.
 
Masikini CCM, Mukama anagandisha gamba na super glue, sasa sijui itakuwaje. Nape anajaribu kutoa superglue inakataa. CCM ifanye nini sasa. Labda nape aanze kuzungumzia Tanganyika.:israel:
 
Tunaomba sasa kuona ofisi na matawi yanasimikwa kila mahali mnapoweza kufika..we shall leave no stone unturned,mwabeja mno bangosha!
 
Binafsi nimeishuhudia hii, Hakika Chadema Wanakubalika wana JF kama hukubali utakuja shuhudia na kuthibitisha hili, sikutegemea kabisa CDM wakakusanya watu wengi kiasi kile tena watu wa rika zote Sumbawanga, Nauomba uongozi wa CDM waendelee na moto huu mikoa yote na kanda zote.

Unaweza kupotosha watu wengi kwa muda lakini kamwe huwezi kuwadanganya watu wote milele yote.
 
Back
Top Bottom