CHADEMA ndani ya Songea mjini

Makamba anapong'atuliwa alishamwandaa mwanae na ameshika sehemu nyeti ya secretarieti, Mwinyi mwanae ni waziri, Nape baba yake alikuwa kiongozi mwandamizi, Kikwete mwanae kiongozi umoja wa vijana nk. huu ndio uongozi wa ukoo anaotakiwa Nape auongelee na una mizizi miaka mingi kulilko kuhangaikia chama ambacho hata hakijashika dola.
 
ni kweli kabisa ufasadi ni tatizo kubwa, mkuu wa kaya hawezi kufanya kitu hapa maana anausika moja kwa moja

headline_bullet.jpg
ukiritimba uliokithiri
headline_bullet.jpg
ufisadi wa mabilioni
headline_bullet.jpg
ubovu mitaala ya elimu
chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), kimesema dawa pekee ya kumaliza tatizo la umaskini uliokithiri miongoni mwa watanzania wengi nchini ni kuondoa ukiritimba na ufisadi. Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama hicho taifa, wilfred lwakatare, alisema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha mgazini, kata ya kilagano, wilaya songea vijijini, mkoani ruvuma jana. Mkutano huo ni wa kwanza kati ya mikutano mitatu ya hadhara iliyofanywa na lwakatare, uliofuatiwa na ule alioufanya katika kituo cha mabasi cha mjini peramiho na katika uwanja wa shule ya msingi ya lilambo, songea mjini.

Lwakatare ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa chadema walioko katika timu sita zinazoendesha operesheni maalum ya chama hicho nchini inayohusisha maandamano na mikutano ya hadhara, kwa lengo la kuishinikiza serikali kusikiliza kilio cha wananchi, ukiwamo umaskini na hali ngumu ya maisha. Operesheni hiyo, ambayo ni muendelezo wa ile iliyofanyika katika mikoa ya kanda ya ziwa, inayohusisha mikoa ya mwanza, shinyanga, kagera na mara mwezi uliopita, ilianza mei 6, mwaka huu, katika mikoa ya nyanda za juu kusini, mkoani mbeya. "dawa ya umaskini ni ndogo. ni kuondoa ukiritimba na ufisadi," alisema lwakatare, ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu taifa na mwenyekiti wa chadema mkoa wa kagera.

Alisema ukiritimba unaonekana katika serikali ya chama cha mapinduzi (ccm), ni pamoja na kushindwa kutengeneza barabara nyingi vijijini na hivyo kuwafanya wananchi kupata tabu ya kusafirisha mazao wanayoyalima kuyapeleka kwenye masoko. Pia alisema sh. Bilioni 133 zilizokuwa kwenye akaunti ya madeni ya nje (epa) ndani ya benki kuu ya tanzania (bot) kama zisingeibwa na wajanja wachache, zingeweza kutumika kujenga vyumba 19,000 vya madarasa na kusaidia watoto wa maskini kupata elimu bila tabu.

alibainisha kuwa, chini ya ccm kamwe umaskini hauwezi kuondoka nchini kwani badala ya kushughulikia tatizo hilo, imekuwa ikiendekeza propaganda kupitia nyimbo za kikundi chake cha burudani cha tanzania one theatre (tot) kuwahadaa watanzania kwamba, 'wanapendeza', huku wengi wao wakiishia kuusikia mlo wa asubuhi (chai) redioni. Lwakatare alisema chama hicho kimekuwa kikiulea umaskini na imekuwa ikiutumia kama ndoano ya kuvuna kura za wananchi nyakati za uchaguzi.

alizifananisha shule za sekondari za kata sawa na vituo vya kukulia watoto kutokana na kukosa nyenzo za kufundishia, kama vile maabara. Lwakatare alisema mbunge wa peramiho, jenista mhagama, ni miongoni mwa wabunge wa ccm, ambao wamekuwa wakipitisha bajeti za mabilioni ya shilingi bungeni kwa ajili ya kujenga shule za kata lakini zikishajengwa wabunge hao awawapeleki watoto wao kwenda kusoma kwenye shule hizo. "wanajua shule hizi hazitatoa madaktari na wataalamu wengine. Badala yake wanawapeleka watoto wao kwenda kupata elimu nzuri ulaya. Matokeo yake imekuwa akiondoka kawawa anakuja kawawa, akiondoka mwinyi anakuja mwinyi," alisema lwakatare.

alisema ccm imekuwa na tabia ya kuwahitaji wananchi wakati wa uchaguzi tu, mithili ya kuku wa kienyeji, ambaye mmiliki wake akihitaji kitoweo, humdanganya kwa mahindi ili amkamate na kumchinja. "kama tanzania bila ukimwi inawezekana, basi tanzania bila ccm pia inawezekana," alisema lwakatare. Aidha, alisema vijiji vinavyoongozwa na ccm, havina maendeleo, na kuwataja wananchi kujiunga na chadema kwa sababu inauwezo wa kuleta mabadiliko nchini.

lwakatare alisema ndani ya ccm kuna makundi matatu; kuna 'ccm tafuta kivuli', 'ccm maslahi' na 'ccm kiherehere'. Alisema miongoni mwa wanaoteseka nchini, ni askari polisi, ambao wengi wao wamekuwa wakiishi katika nyumba za mateso. "kule kwetu kagera askari wamejengewa nyumba, juu bati, pembeni bati. Likija jua mnaokwa kama mikate, ikija baridi utadhani mochwari gani sijui.
sasa haya ni maisha gani?" alihoji lwakatare.

kabla ya kuhutubia mkutano huo, lwakatare akiongozana na viongozi wa chadema mkoa wa ruvuma, alifungua matawi matatu ya chama likiwamo tawi la mapambano kata ya majengo, londoni na kichangani, yaliyoko mjini songea na songea vijijini.
ippmedia
 
timing bom
Makamba anapong'atuliwa alishamwandaa mwanae na ameshika sehemu nyeti ya secretarieti, Mwinyi mwanae ni waziri, Nape baba yake alikuwa kiongozi mwandamizi, Kikwete mwanae kiongozi umoja wa vijana nk. huu ndio uongozi wa ukoo anaotakiwa Nape auongelee na una mizizi miaka mingi kulilko kuhangaikia chama ambacho hata hakijashika dola.
 
attachment.php


Kijana Nape ndiye msiri mkubwa ambaye CCM hawakumjua alivyowasaliti alipokuwa mmoja wa waanzilishi wa CCJ na kuiba Katiba ya ANC kwa mzee Madiba, Mpendazone mwanzilishi mwenza katoboa siri hiyo kwanye mwendelezo wa mikutano ya Chadema - Ruvuma -Mbambabay. Nape anaubavu bado?
 
peoples power itawaondoa ccm miaka si mingi, kila kona imeshachoshwa, wakulima wamechoka, walimu wamechoka, wanafunzi wamechoka, wawekezaji wa ndani wamechoka, ila hawa watu wa usalama, polisi na wanajeshi wachini chini ambao hawanufaiki na serikari ya kirafiki tupo pamoja, hao wengine wanalinda maslahi yao binafsi.
 
May 14



2.JPG

1.jpg


KATIKA kile kinachoonekana kuwa ni kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kutekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni za urais mwaka jana, Chadema kimesema kitatumia kura za maoni kumwajibisha ikiwa atashindwa kuzitekeleza.Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliwaambia maelfu ya wakazi wa Mji wa Songea mkoani Ruvuma kuwa wamegundua kwamba katika nchi nyingine, akitolea mfano, Japan, kama waziri mkuu wao akishindwa kutimiza ahadi zake, wananchi hupiga kura za maoni.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kibulangoma, Dk Slaa alisema chama chake kilipoanza kuandamana, Rais Kikwete alisema kuwa wanapanga njama za kumwondoa madarakani na kutokana na hilo, kiliamua kuchunguza sababu za Rais kutoa kauli hiyo.

"Serikali ikichaguliwa si lazima akae miaka mitano ikiwa ni kama hajatekeleza ahadi za wananchi na kama hatupi elimu bora na bure kushusha bei ya sukari na mabati. Kama ameshindwa hilo tutamwondoa kwa kura za maoni," alisema Dk Slaa."Tutaandamana na kupiga mchakamchaka ili hoja zetu tulizoahidiwa zitekelezwe kupitia Bunge kwa kuwa nchi itakalika kama wananchi wana amani na maisha mazuri," alisema Dk Slaa.

Alidai kuwa Rais Kikwete amekuwa hawajali wananchi ikiwa ni pamoja na kutokuwashukuru kwa kumpigia kura, akidai kwamba tangu aingie madarakani katika awamu hii, amekuwa akisafiri nje ya nchi badala ya kuwatembelea wananchi wake."Kikwete atueleze alichaguliwa na Ulaya au Tanzania, anasafiri nje kila mwezi badala ya kuwashukuru wananchi waliomchagua," alisema Dk Slaa.

Katika hatua nyingine, Dk Slaa alisema kuwa CCM kimekuwa kikiishambulia Chadema kuwa kinafanya ufisadi kwa kununua magari yaliyotumika, akisema walishasema kwamba watanunua malori ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwa kuwa wamekuwa wakiyatumia tangu yakiwa mapya

Haya ndo matokeo ya songea?
 
hapa cdm ninawashangaa, kushangaa pinda kushindwa kuwawekea umeme majirani zake. Sasa kwanini cdm isiamue genereta hili kusambazia umeme kwa baadhi ya wananchi wa madaba?? Kumbe ubinafsi upo katika kila chama!


Nadhani iq yako inaweza kuwa na matatizo. Hili gari ni maalum kwa ajili ya kampeni na shughuli nyingine za mikutano mbalimbali. kumbuka hili gari lina sehem ya jukwaa, na jenerator kwa ajili ya kuwezesha system nzima ya sound. Kwa hiyo tukiwapa hili generator Madaba halafu shughuli za mikutano ziindeshweje? Si unajua TANESCO walvyo na hila kwenye mikutano ya CHADEMA?
 
Back
Top Bottom