Chadema ndani ya Bukoba

This is so good! Watanzania wanaonyesha mwamko wa hali ya juu! Sipati picha CDC wakifanya maandamano Dar itakuwaje, manake wa mbagala wataibuka, wa GOMS nao watafurika, waliobomolewa mahakama ya ndizi ndio usiseme kabisa, acha wazee wa EA ambao hawajalipwa mpaka sasa, madaktari yaani the list goes on and on!
 
attachment.php

Picha hizo zinaanza kuja

Je inawezekana kumtoa mtu aliyewekwa madarakani kwa wingi wa kura za wananchi na kuapishwa kisheria. Chadema lazima mtumie japo akili kidogo kujua kuwa hamtaweza kumng'oa JK mpaka miaka mitano yake imalizike. sasa msituletee balaa kwa maneno yenu ya uchochezi na kufarakanisha watu ili damu imwagike.

Sisi tunazidi kuomba amani itawale na wenye nia tofauti na hiyo Mola awaadhibu sana.
 
Wakuu.Habari!!!

Yale Maandamano ya CHADEMA katika Kanda ya Ziwa yanatarajiwa kuhitimishwa leo kwa maandamano makubwa na ya aina yake Bukoba Mjini. Maandamano hayo yanatarajiwa kuanza saa 7 mchana.Maandalizi yameshakamilika na msafara wa Vikosi Kazi ndio unajiandaa kutoka Kahama vilipotia nanga kuelekea Bukoba. Kazi kamili itahitimishwa kesho kwa kufanya mikutano ya hadhara kwenye Wilaya za Mkoa wa Kagera. Baada ya hapo Vikosi vitarudi Dar es salam kwa maandalizi ya Kanda nyingine baada ya Bunge la Aprili. Habari ya matukio baadaye kazi ikianza.

Kutoka Kahama
Reagia E Mtema
Waziri Kivuli- Kazi na Ajira.

Ahsante Mh. Mtema kwa taarifa za mara kwa mara kutoka kanda ya ziwa. Unaweza kutwambia viwanja gani vitatumika kesho kwa mikutano katika wilaya zote za wilaya zote za mkoa huo wa Kagera? Logistics zikoje kaatika mkoa huo? maana kuna umbali mkubwa kutoka Bukoba kufikia wilaya zote mf. Ngara iko mbali sana na Bukoba.

Mungu azidi kuwatangulia katika kazi nzuri mnayoifanya.
 
Je inawezekana kumtoa mtu aliyewekwa madarakani kwa wingi wa kura za wananchi na kuapishwa kisheria. Chadema lazima mtumie japo akili kidogo kujua kuwa hamtaweza kumng'oa JK mpaka miaka mitano yake imalizike. sasa msituletee balaa kwa maneno yenu ya uchochezi na kufarakanisha watu ili damu imwagike.

Sisi tunazidi kuomba amani itawale na wenye nia tofauti na hiyo Mola awaadhibu sana.

Msindanganye watu hapa. Hakuna cha damu kumwagika wala cha amani kuvunjika. Swala ni UFISADI NA KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA. Period. Sasa huo mtaji wenu wa amani kuvunjika ushapitwa na wakati. Hivi unafikiri watu wote hao unawaona wanakwenda kwenye maandamano unafikiri wanafuata nini huko?? Kama huna jibu basi ujuwe kuwa hawana matumaini na serikali yao na wanatafuta tumaini jipya!! Dr. Silaa na CDM.
 
Hongera dada yangu na Mungu awatangulie daima tupo pamoja nanyi. Ninaomba nifahamu mikakati ya kuimarisha ofisi za CDM wilaya na mikoa kwa kweli nguvu inahitajika kufanikisha hili ninaamini hata ikiitishwa harambee tutafanikisha hili, kwa mfano ofisi ya CDM mkoa wa Dodoma inatia huruma ninaamini hata wewe dada yangu unapokuwa dodoma huwa haikupi hata hamu ya kwenda kupumzika au kufanyia kazi zako mahali pale. Mimi nipo tayari kulitetea hili la uimarishaji au ujenzi wa ofisi hizi

Kweli kabisa.
 
Kazi kamili itahitimishwa kesho kwa kufanya mikutano ya hadhara kwenye Wilaya za Mkoa wa Kagera. Baada ya hapo Vikosi vitarudi Dar es salam kwa maandalizi ya Kanda nyingine baada ya Bunge la Aprili..
Hizi habari kama vile sizielewi au sijazitegemea...!?
Inamaana hamtafika Arusha mpaka baada ya bunge la April???????
 
Wakuu.Habari!!!

Yale Maandamano ya CHADEMA katika Kanda ya Ziwa yanatarajiwa kuhitimishwa leo kwa maandamano makubwa na ya aina yake Bukoba Mjini. Maandamano hayo yanatarajiwa kuanza saa 7 mchana.Maandalizi yameshakamilika na msafara wa Vikosi Kazi ndio unajiandaa kutoka Kahama vilipotia nanga kuelekea Bukoba. Kazi kamili itahitimishwa kesho kwa kufanya mikutano ya hadhara kwenye Wilaya za Mkoa wa Kagera. Baada ya hapo Vikosi vitarudi Dar es salam kwa maandalizi ya Kanda nyingine baada ya Bunge la Aprili. Habari ya matukio baadaye kazi ikianza.

Kutoka Kahama
Reagia E Mtema
Waziri Kivuli- Kazi na Ajira.

:flame:
let the fire go on and BIG UP CDM
 
Eeee MWENYENZI MUNGU uwalinde kwa neema yako hawa ndgu zetu ''Watanzania wakweli'' wapenda haki,wanaharakati wakweli i.e CHADEMA kwa mchango mkubwa wanaoonesha kuleta mabadiliko ya kweli nchini TZ.

CHADEMA TUPO NYUMA YENU.

DR.NENDA,NENDA,SEMA,SEMA,USIOGOPE,USIFADHAIKE.MUNGU YUPO NAWE.

Dada yetu MTEMA.Thank u a lot 4 hot news.Keep it up.

Thank u CHADEMA.
 
Wanajamvi naomba mniweke sawa katika hii move ya CDM. Je, lengo ni kuindoa madarakani serikali inayotawala?! Ni mkakati mzito kujipanga na uchaguzi mkuu 2015?! Je, ni kuifungua macho serikali iliyoko madarakani kuhusu maeneo yanakwenda ndivyo sivyo? Msaada tafadhali.
 
rejao hapana....nchi teyari iko pabaya, chadema wanaongoza kupiga u turn igeuke ielekee kuzuri......just be part of the progress it does not matter how long it will take!
 
CHADEMA mkirudi bungeni sasa nadhani mtakuwa na nguvu hata zaidi kwani wale wazomeaji washauona moto wenu, walidhani watu wamewatupa baada ya uchaguzi sasa wameona kinachomaanishwa na PEOPE'S POWER
 
Sisi tunazidi kuomba amani itawale

amani ya k*i*s*e*n*g*e anaitaka nani?

kikwete lazima ang'oke kwa maana dhambi alizotenda nchi hii ni kosa sawa na kosa la uhaini dhidi ya serikali yake mwenyewe.

nchi kama china RA na AL wangekuwa wamenyongwa.

lakini jk na genge lake wanamuandaa AL kuwa Rais.

this is purely ridiculous
 
Kikosi kazi cha CDM kilichokuwa kinatalajiwa kutua Bukoba mjini leo hii majira ya saa 7 kimewasili hapa bukoba mjini majira ya saa kumi hivi. Hivi sasa kinahutubia mkutano wa hadhara katika uwanjawa kaitaba. Mahudhurio ni makubwa sana haijapata kutokea. Maandamano yalikwenda vizuri. Polisi hawakuwabugudhi hata kidogo waandamanaji.
 
amani ya k*i*s*e*n*g*e anaitaka nani?

kikwete lazima ang'oke kwa maana dhambi alizotenda nchi hii ni kosa sawa na kosa la uhaini dhidi ya serikali yake mwenyewe.

nchi kama china RA na AL wangekuwa wamenyongwa.

lakini jk na genge lake wanamuandaa AL kuwa Rais.

this is purely ridiculous

Hahahahahaha,duh kweli una hasira angalia usija haribu computer basi
 
Je inawezekana kumtoa mtu aliyewekwa madarakani kwa wingi wa kura za wananchi na kuapishwa kisheria. Chadema lazima mtumie japo akili kidogo kujua kuwa hamtaweza kumng'oa JK mpaka miaka mitano yake imalizike. sasa msituletee balaa kwa maneno yenu ya uchochezi na kufarakanisha watu ili damu imwagike.

Sisi tunazidi kuomba amani itawale na wenye nia tofauti na hiyo Mola awaadhibu sana.

...inFamous last Words! Mubarak wa Misri naye alijaribu kujitetea kwa maneno yanayofanana na hayo. sasa yuko mahututi kitandani na BP!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom