chadema nayo kujivua gamba juu ya hizi kashfa??

Mujumba

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
853
306
sio siri chadema ndio chama kikuu cha upinzani kwasasa lakini kimekuwa kina kashfa nyingi sana kama vile swala la udini,ingawa walijaribu kumuita kundini prof safari ili kufuta dhana ya udini lakini bado swala la udini halijafutika mioyoni mwa watu,pia liko swala la kupewa fedha na mataifa ya nje,liko swala la ukabila,pia liko swala la vurugu,mfano hai ni pale mbunge machachari Godbless Lema alipotamka live bungeni kuwa milango ifungwe watu wapigane!(mwananchi ya leo) hivi kweli mtu aliyepewa dhamana na wananchi anaweza kutamka maneno kama hayo katika chombo kikuu cha maamuzi nchini?? sasa je chadema kuvua gamba na kuwa na sura mpya katika macho ya watu?
 
Acha upuuzi ndio mana watu hawachangii thread yako..wanaiangalia wanakupuuza....
 
Baada ya ccm kujivua gamba ni zamu yako Kashaga kujivua gamba kwa kashfa zinazokukabili. Uliupotosha umma wa watanzania kuhusu jimbo la karatu. Tunaoifahamu karatu tukakuumbua. Hata baada ya kuomba radhi bado umekuwa ukiendelea kutuletea thread zenye mambo ya uzushi na propaganda za ccm. Sasa ni wakati wako wa kujivua gamba ili kurudisha imani ya jukwaa hili kwako. Kwa kifupi cdm haina gamba. Hizo unazoziita kashfa ni uzushi na propagana zinazoenezwa na wajijinga wajinga kama wewe wanaotumwa na ccm baada ya kuishiwa hoja.
 
sio siri chadema ndio chama kikuu cha upinzani kwasasa lakini kimekuwa kina kashfa nyingi sana kama vile swala la udini,ingawa walijaribu kumuita kundini prof safari ili kufuta dhana ya udini lakini bado swala la udini halijafutika mioyoni mwa watu,pia liko swala la kupewa fedha na mataifa ya nje,liko swala la ukabila,pia liko swala la vurugu,mfano hai ni pale mbunge machachari Godbless Lema alipotamka live bungeni kuwa milango ifungwe watu wapigane!(mwananchi ya leo) hivi kweli mtu aliyepewa dhamana na wananchi anaweza kutamka maneno kama hayo katika chombo kikuu cha maamuzi nchini?? sasa je chadema kuvua gamba na kuwa na sura mpya katika macho ya watu?
<br />



Ulishawahi Kuumwa Degedege wewe?
Heri kukaa kimya kuliko kuandika Utumbo!!!
 
Hata hao wanaosema wamevua gamba hakuna cha maana walichofanya. Ni kama wamepulizia mavi manukato eti kitanukia vizuri!
 
Chadema si chama cha bendera fuata upepo. Endeleeni kujivua magamba yenu huko CCM.
 
The following member has groaned Kashaga for this useless post
genekai (Today)
 
Waislamu wampinga Mufti kuibeba CCM
na Abdallah Khamis, Dodoma

UMOJA wa Kiislamu (Istiqama) Mkoa wa Dares Salaam, umemtaka Sheikh Mkuu nchini, Mufti Shaaban bin Simba, kuacha kuvishambulia vyama vya siasa vinavyoikosoa serikali na badala yake ashughulikie masuala yanayohusu maslahi na matakwa ya Waislamu hasa katika kipindi hiki cha vuguvugu la madai ya Katiba mpya.
Msimamo huo ulitolewa jana na Sheikh Yasin Bahama, kwa niaba ya umoja huo wa mringano wa Kiislamu, wakati akitoa tamko kuhusu mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya na nafasi ya Waislamu katika mchakato huo.
Tamko hilo limekuja ikiwa ni wiki chache tu zimepita tangu Mufti Simba ayalaumu maandamano yaliyofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika mikoa ya Kanda ya Ziwa akisema yanahatarisha amani ya nchi.
Ajenda ya maandamano hayo ilikuwa ni kuishinikiza serikali kuchukua hatua za dharura za kulinusuru taifa liondokane na maisha magumu hasa baada ya kupanda kwa bei za vyakula, bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo umeme, gesi na mafuta.
Sheikh Bahama alisema mufti kama kiongozi wa waislamu wote nchini anapaswa ahakikishe kuwa katiba ijayo inawapa Waislamu fursa na haki za kutosha ikiwa ni pamoja na kuwa na Mahakama ya Kadhi.
"Haya maisha magumu tunayapata wote sasa wanapotokea watu wanaishinikiza serikali ili hali iwe nafuu halafu anatokea mtu anawapinga (Mufti), kwa kweli ni jambo la kushangaza," alisema.
Sisi kama Waislamu hatuoni tatizo lolote linalofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kuwa ni chama cha siasa cha upinzani, na lengo la vyama vya upinzani ni kuikosoa serikali kwa kuwa ni haki yao kisheria.
Tunawasihi Waislamu wote kwa pamoja tuhakikishe Katiba mpya inakuwa na Mahakama ya Kadhi. &#8230;.tushughulike na kudai haki zetu ziingie kwenye Katiba. Tuachane na kutetea CCM na serikali yake, tuachane na kushambulia vyama vya siasa kwani vipo kwa mujibu wa sheria", alisema Sheikh Bahama.
Walisisitiza kuwa suala la kuwa na Katiba mpya ni muhimu kuliko kuangalia ni chama gani kinaongoza nchi kwa wakati huu, kwani chama kinachoongoza sasa kitafika mwisho wake lakini kama Katiba itakuwa mbovu basi haki na maslahi ya Mwislamu vitaendelea kudhulumiwa siku zote.
Alisema kuwa Waislamu wana madai mengi na ya msingi wanayopaswa kuhakikisha wanatimiziwa kuliko kuangalia kwanini serikali ya CCM inasemwa.
Waliwataka viongozi wote wa kidini nchini kuachana na masuala ya kisiasa na badala yake wawaongoze watu wao katika kufanya mema kwa ajili ya mwenyezi Mungu.


Waislamu wampinga Mufti kuibeba CCM
 
Back
Top Bottom