CHADEMA na Udikteta Makao Makuu

mmeshawahi kusikia kumpigia mbuzi gitaa?

chadema kuwa na wachagga kadhaa kwenye nafasi za uongozi basi ni Ukabila
CCM kuwa na waislamu wengi kwenye nafasi za juu za uongozi siyo udini ni historia

CCM inaongozwa na Ibara 15:1 na hakuna chochote ambacho kinaweza kuwafanya CCM waone tofauti. Wao wana "standard" yao halafu wana standard ya "wengine wote".
 
kama kawaida yako.

mara ngapi tumesikia ccm ni chama cha mafisadi just because mafisadi wawili watatu wametoka ccm na hao wengine wamebaki kama mafisadi wa "midomoni" yaani hakuna kinachoonyesha ufisadi wao ?

vivyo hivyo chadema, chama cha wachaggas ! mnabisha nini ? kilianzishwa based on "uchagga". na wengi waliodandia basi njiani hata historia yake hawaijui !
 
Kama CCM ina madhaifu na kuweza kukosolewa inakueje ikifika kwenye CHADEMA watu humu wana ng'aka?Haya majeshi ya humu ndani vipi?Hawapendi Jemadari wao akosolewe?
 
nafikiri ikifika zamu ya chadema, watu hukosa mafuta hivyo kuishia njiani na kutembea, lakini ikifika zamu ya ccm watu wapo tayari kutembea maili kadhaa kuchukua mafuta hata kwenye vidumu ili mradi ipondwe !

mhm...........(thinking) kama nawaona vile watu wamebeba vidumu ..........whistling !
 
Kubwajinga

1. Matangazo ya gazetini pekee ya mwaka mmoja hayatoshi kuweka sura ya ruzuku kusambazwa kwa kuwa hayawezi kutaja orodha ya wilaya zote zilizopokea ruzuku. Si unajua kwamba huwa zinachapwa audited statements ambazo ni summary? Sheria ya vyama vya siasa inasema msajili anawajibu wa kuchapa mahesabu ya vyama. Sasa kamuulize msajili kwa nini hachapi wakati CHADEMA inampelekea kila wakati? CHADEMA wakati wote inaweka wazi matumizi yake kwa wanachama kupitia vikao ikiwemo kiasi kilichosambazwa na jina la eneo. Mimi ya kwetu niliyapata Zanzibar. Lakini baada ya baraza kuu unakumbuka Tamko la CHADEMA lilionyesha kwamba wajumbe walijadili na kupitisha ripoti ya fedha ikiwemo mgawanyo wa ruzuku?

2. Hilo la Uchagga wa sekretariati acha kuwasingizia. Mbona iliwahi kusemwa hapa kwamba Wasukuma ni wengi kuliko wachagga? Kama wasukuma ni zaidi ya 30% katika makao makuu ya CHADEMA kwanini unawataja wachagga tu wakati mwenyewe umesema ni 25&, au unafanya spinning? Na ni kiongozi gani wa sekretariati au mbunge ambaye amechaguliwa kwa shinikizo la Freeman kutokana na mchango wake ambao amechangia chama yeye kama Freeman?

Hebu Mods tuleteeni tena hapa tamko la CHADEMA walilolitoa kujibu suala la Uchagga, au tupe link ambapo suala hili lilishajadiliwa na kujibiwa na Zitto, Mnyika, Kitila na wengineo.

Wallah napata uchungu haya mambo kurudiwa rudiwa ili hali yalishajibiwa mpaka makada wa CCM wakasalimu amri wakati huo

Asha

Asha,
Inaelekea wewe ni mndani kabisa wa Chadema, jambo ambalo ni zuri na litasaidia kufikisha haya malalamiko.

Lakini ningekushauri usiwe mshabiki asiyedadisi, kama walivyo wa Simba na Yanga. Kama tunavyowachamba CCM, tusione kichefu-chefu kuhitaji fafanuzi za yale yasiyoeleweka kwenye upinzani, iwe ni CHADEMA au hata TADEA.

Kwa hiyo, ukweli unabaki pale pale kuwa, CHADEMA inatakiwa kujibu malalamiko ya wanachama wake, bila kuzunguka-zunguka otherwise hawatakuwa na tofauti yoyote na wanamtandao.

Kama kuna wanachama mikoani wanaolalamikia malipo, jibu ni kuchapisha tu mgawanyo na kuwaumbua kuwa mbona walipewa kiasi husika? Ila kama makosa yalifanyika katika ugawaji, CHADEMA bado ni wachanga kwa hiyo wangeeleza tu wanachama wake kuwa kuna makosa yaliyofanyika na hayatarudiwa. Lakini kumuingiza au kumlaumu msajili wa vyama, sidhani kama ni solution.

Kuhusu ukabila, hili sio la ajabu. Vyama vilipoanzishwa vilianza kwa milengo ya kikabila, kimajimbo na kidini, hasa kwa kutokana na waanzilishi au viongozi wake wa juu. Ni NCCR pekee ambayo ilikuwa kwa kiasi si ya kijimbo kwa vile base yake ilikuwa pale mlimani, mpaka Mrema alipoingia ndio ikaanza kuwa na mwelekeo wa kikabila.

Kwa kifupi ni kuwa vyama vyetu vyote vilianza kwa misingi isiyo mizuri ambayo ni tofauti na maandiko ya katiba zao. Kwa hiyo image za hivyo vyama zinatakiwa zibadilike kama vinataka kukua na kutwaa nchi. Kuficha kichwa mvunguni wakati kiwiliwili kiko nje ni mchezo wa kitoto.
 
Jamani kuna mtu mwenye ile makala ya Mzee Mtei aliyoandika "CHADEMA ni nini, CHADEMA ni nani?" ambapo aliweka wazi historia ya kuanzishwa kwa CHADEMA na wakina nani alianzisha nao na katika maeneo gani? Iliwahi kuwekwa hapa JF na kati ya Zitto au Mnyika; hebu toeni link basi

Asha

Asha,
Ile article ya Mzee Mtei niliisoma. Lakini tuliokuwepo wakati hivi vyama vinaanzishwa na kama wakereketwa wa awali, tunafahamu kuwepo kwa hizi elements za ukabila na udini kwa baadhi ya vyama. Na Chadema haikuwa immune. Lakini vyama hukua na kubadilika, ila kama havitabadilika, basi vitabaki nyuma na mvuto wao utakuwa mdogo hasa kwa walioelimika na kwa hiyo kushindwa kuipiku CCM. Let's face the issues, not shy away from them.
 
Hebu tuangalie kwa mbali kinachosemwa... halafu tuone kama ipo haja ya kujaribu kutoa majibu:

KILA JUMAPILI
Na Mzee Yusuf Halimoja

......Imedaiwa kwa haki kabisa kwamba kundi la kwanza la CHADEMA lililoko Makao Makuu ya chama ni kundi linaloundwa na viongozi wa Makao Makuu na watendaji wakuu wa chama hicho, wakiwamo wakurugenzi. [/quote]

Inaonekana kuwa lengo kuu la kundi hili ni kulinda maslahi binafsi. Furaha kubwa ya kundi hili ni kuhakikisha kuwa ruzuku ya shilingi milioni 66 inayopata CHADEMA kila mwezi haifiki mikoani. Badala yake inatumiwa nao kwa mishahara na posho za safari za magari na helikopta zisizokwisha na zisizo na manufaa yoyote kwa chama.

Kuna habari kwamba baadhi ya wale walioko makao makuu wamenufaika na fedha za CHADEMA, kiasi cha kuanzisha miradi na biashara ambazo hawakuwa nazo kabla hawajajiunga na CHADEMA.

Kwa jumla kundi la kwanza la CHADEMA lililoko makao makuu linatuhumiwa kwa ubadhirifu, ufisadi, udikteta, matumizi mabaya ya fedha ikiwa ni pamoja na matumizi ya helikopta ambayo hayana tija yoyote katika ujenzi wa chama.

Juu ya yote, kundi hili linaaminiwa kuwa lina mawakala wa chama tawala ambao wamekaa pale kukomba tu fedha ya chama zinazowapeleka mikoani, huku wakiuacha Mkoa wa Dar es Salaam ukiwa hauna uhai wa chama kwa sababu safari ndani ya Dar es Salaam hazina posho.

Kwa kifupi kundi la kwanza la CHADEMA lililoko makao makuu ni kundi la wababe wasio na uchungu wowote na chama na wanaoendesha chama kama vile ni kampuni yao binafsi. Kiongozi au mtendaji yeyote anayethubutu kupambana na maovu yanayoendelea kutendwa na kundi hili la kwanza anahatarisha nafasi yake. Atafukuzwa bila kupewa nafasi ya kujieleza, hata kama atakuwa ameitwa kwenye kikao hicho ili ajieleze. Hiyo ni demokrasia kwa staili ya Makao Makuu ya CHADEMA. Nani anabisha?

Anapokuja kuzungumzia kundi la pili; angalia matumizi ya maneno (very factual and matter of point)

Kundi la pili la CHADEMA ni lile lililoko mikoani.
Lengo kuu la kundi hili ni kuhakikisha kuwa lengo la chama cha upinzani la kushika madaraka ya utawala linatimia. Hili ni kundi lenye uchungu wa kweli na chama. Ni kundi linalotaka nguvu zote za chama zielekezwe kwenye kujenga chama ngazi zote.

Ni kundi linalotaka kujenga mtandao wa chama nchi nzima. Kundi hili linataka chama kiwe na ofisi mikoani kote na wilayani ili wanachama wapate mahali pa kukutana, kupata wanachama wapya, kufundishana sera za chama, na kubadilishana mawazo juu ya ujenzi wa chama utakaosaidia kuleta ushindi katika chaguzi mbalimbali. Kwa kifupi hili ni kundi linalotaka chama kiwe cha watu wote badala ya kugeuzwa kuwa kampuni ya watu binafsi.

Kundi hili la pili lililoko mikoani ambalo ndilo lenye uchungu na chama linapinga vikali matumizi ya helikopta wakati wa kampeni za uchaguzi, wakati wagombea ubunge na udiwani hawapewi hata shilingi moja ya kuwawezesha. Kundi hili pia linataka ruzuku ya chama isiishie kufujwa makao makuu, bali ifike mikoani ili kusaidia kufungua matawi na kuwafikia wananchi wa vijijini ambao hawana habari zozote za CHADEMA.

My take:

you make your own mind!
 
Asha,
Inaelekea wewe ni mndani kabisa wa Chadema, jambo ambalo ni zuri na litasaidia kufikisha haya malalamiko.

Lakini ningekushauri usiwe mshabiki asiyedadisi, kama walivyo wa Simba na Yanga. Kama tunavyowachamba CCM, tusione kichefu-chefu kuhitaji fafanuzi za yale yasiyoeleweka kwenye upinzani, iwe ni CHADEMA au hata TADEA.

Kwa hiyo, ukweli unabaki pale pale kuwa, CHADEMA inatakiwa kujibu malalamiko ya wanachama wake, bila kuzunguka-zunguka otherwise hawatakuwa na tofauti yoyote na wanamtandao.

Kama kuna wanachama mikoani wanaolalamikia malipo, jibu ni kuchapisha tu mgawanyo na kuwaumbua kuwa mbona walipewa kiasi husika? Ila kama makosa yalifanyika katika ugawaji, CHADEMA bado ni wachanga kwa hiyo wangeeleza tu wanachama wake kuwa kuna makosa yaliyofanyika na hayatarudiwa. Lakini kumuingiza au kumlaumu msajili wa vyama, sidhani kama ni solution.

Kuhusu ukabila, hili sio la ajabu. Vyama vilipoanzishwa vilianza kwa milengo ya kikabila, kimajimbo na kidini, hasa kwa kutokana na waanzilishi au viongozi wake wa juu. Ni NCCR pekee ambayo ilikuwa kwa kiasi si ya kijimbo kwa vile base yake ilikuwa pale mlimani, mpaka Mrema alipoingia ndio ikaanza kuwa na mwelekeo wa kikabila.

Kwa kifupi ni kuwa vyama vyetu vyote vilianza kwa misingi isiyo mizuri ambayo ni tofauti na maandiko ya katiba zao. Kwa hiyo image za hivyo vyama zinatakiwa zibadilike kama vinataka kukua na kutwaa nchi. Kuficha kichwa mvunguni wakati kiwiliwili kiko nje ni mchezo wa kitoto.

Hakuna kusema inaelekea Asha ni mwana ndani wa Chadema no ila amesha sema yeye ni mndani wa Chadema na kajibu kama Chadema si kama mimi Lunyungu sasa hadithi za kazi gani tena?Majibu ya Chadema yako wazi toka kwa wana Chadema bado unataka Chadema wake kujibu hoja .Unataka Chadema Mnyika ama Mbowe ? Lini Makamba ama JK ama hata kiongozi mmoja wa CCM alifika hapa JF kujibu hoja ?
 
Hivi mkjj una uwezo wa kujibu humu wakati wewe mwenyewe unashutuma nzito kuhusu Chadema katika moja ya threads humu JF? Ama kweli unamoyo, duhh, wala huoni haya?

oh no sir!.. nakuthubutisha uoneshe tuhuma nilizotoa dhidi ya Chadema... labda nilipitiwa.... nisaidie kuona hiyo/hizo tuhuma.
 
Lete thread tusome ili tukomae naye mwanakijiji kama kweli unajua usemalo vingenvyo muombe msamaha yeye na sisi wote wana JF maana uongo si sehemu ya kundi hili .
 
oh no sir!.. nakuthubutisha uoneshe tuhuma nilizotoa dhidi ya Chadema... labda nilipitiwa.... nisaidie kuona hiyo/hizo tuhuma.

Aidha kiswahili kinakupiga chenga au unataka kunipiga mimi chenga, na maanisha unashutumiwa au unashutuma nzito zinakukabili. Usibabaishe. Zimo humu JF tena niliziona jana au juzi kama hazijafutwa sijui.
 
DeS, sasa wewe ni mswahili iweje kiswahili kikupige chenga tena.. au ndio tungo tata..!? sasa nilidhani unamaanisha ni mimi nashtumu Chadema au unaweza kujaribu kujiweka sawa kidogo.
 
Aidha kiswahili kinakupiga chenga au unataka kunipiga mimi chenga, na maanisha unashutumiwa au unashutuma nzito zinakukabili. Usibabaishe. Zimo humu JF tena niliziona jana au juzi kama hazijafutwa sijui.

Hii inaitwa man to man, maana mzee naona umekuja special kuakikisha mwanakijiji analeveal ID yake auna utani katika hili, jitahidi kidogo atajitokeza
 
Aidha kiswahili kinakupiga chenga au unataka kunipiga mimi chenga, na maanisha unashutumiwa au unashutuma nzito zinakukabili. Usibabaishe. Zimo humu JF tena niliziona jana au juzi kama hazijafutwa sijui.

Mwaka thread ref .Ndiyo utaanmika unalia lia nini na una uwezo wa ku prove maneno yako ? Hakuna hadihi hapa wala dana dana ngoma unayo weka thread link tujimwage kama huna sema umekurupuka maana ni sehemu ya maisha kwa watu wa aina hii kukurupuka .Kakurupuka Sitta na Ristamn utakuwa wewe bwana?
 
Hii hapa: http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=11397

Na kichwa cha habari: Mwanakijiji Awagombanisha Chadema
 
achana nao hao Dar-es-salaam hawa Lunyungu na kundi lake la spinners na whinners. Wanataka kugeuza walichosema kwa kukusingizia hujui kinyerere wakati wewe ni mzawa halisi !

Naona baada ya kuwakandamizia hiyo thread umewashuka.
 
ebu endelea kumbipu huyo Lunyungu halafu tuone kama atapokea. dola zitaisha upande wetu iweje asipokee ?

halafu chunga mkuu maana utaambiwa wewe ni mmoja wa wale waliomo kwenye "kada na kundi lake"/"Kundi la kada".
 
Back
Top Bottom