Elections 2010 CHADEMA na kampeni kwa njia ya Mtandao

Mimi naona pamoja na utumbo mtupu anoutoa huyu Malaria Sugu kuhusu hoja mnazozitoa, nadhani ni bora zaidi mngeachana nae. Ukibishana na mpumbavu itakuwa vigumu kutambua nani mpumbavu zaidi -- nyinyi au yeye. Tangu leo mimi naachana naye!
 
chadema wabunge 3 ,2005 cuf 20 wa kuchaguliwa ndani ya dodoma duhu sijui nani zaidi

Soma hoja ya Counterpunch vizuri. Anasema CUF bara haikuambulia kitu mwaka 2005. CUF ni chama cha Wapemba tu, kule ambako walikopata viti vingi na hivyo kujiongezea idadi ya vile vya upendeleo!
 
duh, kwani mrema kaishia wapi vile hebu nikumbushe

hii sio sehemu ya kuulizia watu walio fulia kama huyo Mrema,we jaribu kufikiria wiki moja nyuma anamsifia Kikwete alivyo kiongozi bora wiki inayofuata anasimamimia mkutano wa kumchagua sijui profesa nani hivi? eti agombee urais jamani huko si zaidi ya kufulia jamani?
 
Kwa busara zako unadhani unachohangaika kusambaza huku na kule ni kwa manufaa ya nani kama sio mafisadi?Kumbuka kuwa ujira mdogo wanaokupatia unatokana na jasho lako kama mlipa kodi (unless nawe uwe fisadi usiyelipa kodi).Fikiria idadi ya baba na mama zetu wanaokwaza na ufisadi,watoto na wadogo zetu wanaoathiriwa na ufisadi na namna walalahoi wanavyoteswa na mafisadi.

Sawa,Kikwete ni Muislamu mwenzio lakini try to think outside the box.When it comes to Tanzania,mafisadi hawaangalii victims wao kwa misingi ya dini.Uwe Juma au Peter,as long as si mmoja wao,basi lazima watakukalia kooni.

Weka mbele maslahi ya taifa lako badala ya ubinafsi wako

Anyway,najua natwanga maji kwenye kinu kwa vile UKO KAZINI
 
Kwa busara zako unadhani unachohangaika kusambaza huku na kule ni kwa manufaa ya nani kama sio mafisadi?Kumbuka kuwa ujira mdogo wanaokupatia unatokana na jasho lako kama mlipa kodi (unless nawe uwe fisadi usiyelipa kodi).Fikiria idadi ya baba na mama zetu wanaokwaza na ufisadi,watoto na wadogo zetu wanaoathiriwa na ufisadi na namna walalahoi wanavyoteswa na mafisadi.

Sawa,Kikwete ni Muislamu mwenzio lakini try to think outside the box.When it comes to Tanzania,mafisadi hawaangalii victims wao kwa misingi ya dini.Uwe Juma au Peter,as long as si mmoja wao,basi lazima watakukalia kooni.

Weka mbele maslahi ya taifa lako badala ya ubinafsi wako

Anyway,najua natwanga maji kwenye kinu kwa vile UKO KAZINI
 
Maneno yako ni kweli kabisa ila kwa CUF sio tatizo wao wanamikakati iliyo invinsible na wanaweza kuikwamua nchi hii within a matter of months wanasema siku 99 tu ,Tanzania nzima itanusa mabadiliko ,CUF sio mchezo na huwezi kabisa kuilinganisha na Chadema ,kama ulivyosema ,watu wanajaa kuishangaa helikopta ,mikutano ya CUF watu wanajaa kusikiliza sera.
 
Jina lako malaria sugu linatosha kukujibu kwa hoja adhimu ya "ugonjwa wa malaria sugu"
 
Kwa wale waliofatilia kwa makini uchaguzi wa Marekani wa 2008 watakumbuka jinsi matumizi ya internet yalivyomsaidia rais wa sasa Barack Obama kushinda. kwa wale waliokuwa na access waliweza kupata taariza za kampeni, hotuba, ratiba za ziara na hata videos hii ilisaidia sana kukusanya wanachama wengi na ilikuwa ni nafasi ya kuwafikia wale ambao muda mwingi wako ofisini na hawakuwa na muda kuangalia TV au kusikiliza redio wala kuhurudhuria mikutano ya kampeni.

CHADEMA inapaswa kuona umuhimu wa kuitumia nyezo hii muhimu sana katika dunia ya leo ya utandawazi. Japo wale wenye access ya internet Tanzania si wengi kama Marekani, lakini ni ukweli kwamba wengi wao ni wasomi au ni watu ambao muda mwingi wako oficini na sirahisi kuwaona mikutanoni.


Ukiangalia kwenye website ya CHADEMA utaina taarifa ya mwisho ni ya July 12, inamaana ni karibu ya mwezi hawaja-update taarifa zao.
Najua jamvini JF kuna viongozi wengi ya CHADEMA, bila shaka hata Mkurungenzi wa Habari yupo humu. Ushauri wangu kwa CHADEMA waweke kwenye website yao daily update za safari za mgombea urais, taarifa za wagombea ubunge, picha,Videos, hotuba n.k. Hii itawasaidia hata wale wafanyakazi wanaobanwa au kukosa muda wa kuhudhuria mikutano kupata taarifa na sera za mgombea huyu.

Wanapaswa pia kuitangaza website ili watu waijue hii itawasaidia sana CHADEMA katika kueneza ujumbe kwa wanzania walioko ndani na hata nje ya nchi hii ambao magazeti wala redio zetu haziwafikii na njia pekee ya kuwafikia ni kwa njia ya mtandao.


kwa mtazamo wangu,njia ya mtandao ni garama nafuu au hata sawa karibu naa bure kulinganisha na njia zingine.hivyo pamoja na kutumia njia zote,kama tv,fm radio,mabango,sms,posters,na zingine zote zitakazo tumika,mtandao usisahaulike kwani gharama yake ni sawa na bure.

njia zote zitumike,kwani kila njia inamatokeo yake.tusizarau njia yoyote
 
hivi kwa nini Mgombea wa CCM hataki mdahalo naye ni graduate wa univarsiti ya darisalama, tena wauchumi si anaweza kujibu vizuri tu maswali ya kiuchumi na kiutawala, ambayo ni wasifu wa mwanzo kiongozi yoyote anatakiwa kuwa nayo????xxx
 
Mnadhani kwa nini serikali ya CCM iliwalazimisha watu kusajili namba zao kabla ya julai mwaka huu?????
 
Wana JF, nadhani umefika wakati wa kuacha kuchangia mada za MS kwani most of the time anaongea PUMBA, Kwanza ni MDINI kupita kiasi, hana Vision na wala sijui kama ni mtanzania.

Kwa taarifa yako, hutofanikiwa katika kile unachokitafuta, Dr. Slaa anakubalika si kwa sababu ya dini yake, bali ni kwa jinsi alivyojipambambanua kupambambana na WEZI wala rasilimali za nchi hii. Elewa kuwa wewe ni kibaraka wa CCM na huna nafasi katika Forum hii.
 
Nikiangalia Cuf bara haina mvuto wa kuunda serekali 2010 kwani haina viongozi shupavu wa kuweza kuongoza, viongozi wengi wa cuf sio maarufu katka nyanja za siasa ,wengi either fkutoka siasa za chini hadi kuwa cuf. hii tofauti na Cuf zenj ambapo baada ya wengi kungatuka kutoka ccm cuf zenj imekuwa na nguvu na ushawishi mkubwa, maalim seif aliwahi kuwa waziri kiongozi, hamad rashid waziri wa mambo ya ndani, abubak khamis mwanasheria wa gov, Juma duni , machano khamis, Nassor Khamis, marehemu sudi Yussuf Mgeni , ali hajji pandu ni mwanasheria mKuu na wengine ,kama cuf zenj isingekuwa na viongozi mashuhuri na maarufu wanaozijua siasa za tz basi ngalikuwa dhaifu sana na isingeweza kuleta changamoto za siasa za tz kama vile vyama vyengine vilivyopo


kwa chadema nako ndiko hivyo hivyo haina wanasiasa mashuri angalau 50 ambao wanaoweza kuwa mawaziri , manaibu au hata wakuu wa mikoa ambazo wanazijua siasa za tz, wanaoweza kupambana na ccm katika chaguzi lkn wengi wa viongozi wao ni kutoka chini.
kama utaangalia chadema inaviongozi wa 3 tu maarufu kama mbowe, slaa, zito Wengine watz waliochini wanaweza kuwafahamu.
watu wengi sasa wanakimbilia mikutanoni kuangalia helikopa jinsi inavyoruka na kutua na sio kuvutia kwa sera.
ili kiingie ikulu chadema kuna haja ya kuwa na viongozi wengi maarufu kutoka chama tawala, hivi ndivyo ilivyo nchi nyingi duniani kama vile kenya na sio kutegemea wanasiasa wasiomaarufu kama vile chadema
najua wapo wanachadema watakaoukataa ukweli na kuamini wananguvu lkn kila mtz makini anajua hizi ni nguvu za soda zikipoa mwanyaji atakunywa kiulaini

haya ni maoni yangu tu, unahaki ya kuyapinga lkn kwa hoja adhimu

Tanzania ina watu zaidi ya milioni 40, na wana CCM ni milioni 4 tu. Sasa kwa akili zako fupi na finyu unafikiri hakuna watu makini wa kuongoza nchi toka katika hilo kundi la watu milioni 36?. Hivi unajua Chadema ina wasomi mahili na waliobobea wangapi?. CCM imejaa vilaza tupu ndiyo maana nchi inaendeshwa kinyumenyume.
 
Malaria Sugu,
Unachosema ni kweli tupu. Kwa hiyo kuanzia leo nakuomba uache kutujazia hapa makala kuhusu CHADEMA.
 
Malaria Sugu,
Unachosema ni kweli tupu. Kwa hiyo kuanzia leo nakuomba uache kutujazia hapa makala kuhusu CHADEMA.
 
Maleria Sugu ANA MALARIA kweli ila hajui!!!!!!! Huwezi kutuambia habari za CCM humu kwenye JF, huna chako humu we kula pesa za waliokutuma. Jiandae kumpokea Ikulu Dr. Slaa na Siyo KIWETE mwenye UDAKTARI FEKI!!!!
 
waasisi wa chama cha taa na baadaye tanu walikuwa na umaarufu gani?? ulipozaliwa ulijikuta ukiwa mkubwa kama ulivyo au ulipita kwenye malezi kama wanaadamu wote??? kwako maarufu ni kingunge,tingatinga na wenye mvuto ni ra, el nk nk nk.pole na ugua salama na malaria sugu
 
Back
Top Bottom