Elections 2010 CHADEMA na kampeni kwa njia ya Mtandao

Badala ya kuwa na uchungu na maendeleo ya nchi, eti kila chama kina kimbilia kusimamisha mgombea urais kisa ruzuku, tunaenda wapi wapinzani? yaani ruzuku ni bora kuliko mapinduzi ya kimaendeleo. Na huko kwenye usimamizi wa kura sijui itakuwaje ili wasije kutuibia kura na haki yetu tutakayo pewa na wananchi.

Mkuu ungalia kwanza nani ameweka post hii,unaweza kujua lengo lake ni nini huenda haina ukweli.
 
Mbona Lipumba anapata HOMA mapema hivi? Yeye amegombea mara ngapi katika hiyo ngazi ya Urais??????
Umefika wakati Lipumba naye katuliza kichwa chake. Unagombea mara nne, ina maana humo kwenye CUF hakuna wengine zaidi ya yeye. Ukweli unajulikana, hata Sikonge wanaelewa wazi mchango wa Dk. Slaa kwa taifa, tuache majungu.
 
Watu wazima mnakaa mnabishana,mmatoa matusi na kejeli dhidi ya Rais ambaye amejitahidi katika kipindi kifupi kurekebisha hali ya nchi na kuiweka katika mstakabali mzuri kwa siku za baadaye.

Mnadhani Tanzania hii inafuata maoni ya wna JF na Chadema tu?Kwa kuwa wana forum wengi humu ni Chadema unategemea JK apate kura ngapi za maoni?

Kama ingekuwa Slaa anataka kuwa Rais wa Karatu,hapo nadhani angepita lakini nchi hii ni kubwa na kuungwa mkono kwa Cahdema na Slaa kunaishia katika sehemu chache sana.

Ofcourse politics zinachemka sasa hivi kwa sababu ni mwaka wa uchaguzi na wna Chadema na JF najitahidi kupiga kelele ili msikike.Sawa lakini kwa mtindo wa majibu ninayoyasoma humu,CCM itaendelea kutawala hadi 2100! Haya anzeni kutoa majibu yenu.
 
mimi mtanzania maskini, napigania uhuru wangu
Uhuru ambao haujaupata since 50 years back...!!. Haya mwakwetu, unapigania uhuru wako kwa kuwaombea mema wakoloni weusi (ccm) waendelee kukaba uhuru wako?? Kama wewe ni maskini, unaweza kututabanaisha chanzo cha umaskini wako? waweza kutupatia clues za elimu yako pia?
Huwa nawaambia watu kuwa "unaweza kushindana na kila kitu ila huwezi asilani kushindana na SAIKOLOJIA yako"

Kama unaweza kumshambulia na kumfitini MTANZANIA mwenzako kwa hoja za KIBAGUZI na KIDINI, je mpaka sasa haudhani kuwa UMEFILISIKA kichwani?
Nitafute nikupe DAWA
 
Lipumba ameona uzezeta wa CHADEMA na ni kweli kabisa kwa wewe Mtanzania uliepo nje utaona CHADEMA kama ni chama chenye mvuto na kufahamika sana katika TZ ,lakini ukweli sio huo CHADEMA ni Chama kidogo sana na ni chama zaidi kilichojikita katika udini ,maana mara utasikia wakiimba nyimbo za kanisani ile wanaiita kwaya wakimalizia na haleluya .

Chama mnajiandaa kugombea uraisi halafu eti unahitajia watu kutoka Chama fulani ili wawe wasaidizi au sijui ndio siku izi wanaitwa wagombea mwenza ,jamaini hivi Chama aina hii huwa kimekamilika kwa nini msiwape wagombea mwenza akina Shaibu na Lwakatare au Zitto ,Mbowe au yeyote ndani ya chadema ?
Mnaenda kuomba watu wa chama kingine kama si utaahira ni kitu gani ? Ipo kasoro ndani ya Chadema au kwa luga ingine naweza kusema kuna tatizo ndani ya Chadema na lazima mlitatue kabla hamjafika mbali ni aibu kabisa kwenda kudai eti Juma Duni au Hamad waipe tafu Chadema ,watu wa Chadema mnahuzunisha sana ,na hapa ndipo nilipoona udhaifu wenu na kuwa hamfai kabisa kusimamisha mgombea uraisi ikiwa hamjiamini na hamjakamilika ,maana huku ni kutokujiamini ,mbele ya jamii .

Chadema mnakuzwa na vyombo vya habari vinawasifu sana na inakuwa kama mnavishwa kilemba cha ukoka tatizo mnavyotoka kwenye magazeti sivyo mlivyo ,mtu atashangaa akifanikiwa kuona live mambo yenu.mnatia huruma sana hapa kwa jinsi mnavyojipa moyo mnadanganyana wenyewe kwa wenyewe ,likianguka sijui atalaumiwa nani ?

Hawa akina Slaa Mbowe Zitto si walikuwemo humu jamii forum mbona wameingia mitini ? CUF wataongoza tena katika ushindi na wataendelea kuwa ni chama hiki tu kinachoweza kuwasiliza CCM na si vinginevyo.

Nikiongezea CHADEMA mnajiona ni nyinyi tu kwa vile mnaendesha hicho Chama kikabila ,na mtu hawezi kuona mpaka awemo ndani humo ndio ukaona kunatokea mizozano ya hali ya juu ndani ya CHADEMA kwa sababu za kuongozana kimila na kuwemo kwa ukabila katika sehemu nyeti kwamba akina hawa tu ndio wanaoweza kushika nafasi hizi. Ukimaliza uchaguzi huu au kabla basi Chadema itasambaratika ,jamani hiki Chama hakina muelekeo ni wababaishaji tu. tusiandikie mate bado ka miezi miwili unusu ,mtaelewa popo nundu sio ndege.
 
Uhuru ambao haujaupata since 50 years back...!!. Haya mwakwetu, unapigania uhuru wako kwa kuwaombea mema wakoloni weusi (ccm) waendelee kukaba uhuru wako?? Kama wewe ni maskini, unaweza kututabanaisha chanzo cha umaskini wako? waweza kutupatia clues za elimu yako pia?
Huwa nawaambia watu kuwa "unaweza kushindana na kila kitu ila huwezi asilani kushindana na SAIKOLOJIA yako"

Kama unaweza kumshambulia na kumfitini MTANZANIA mwenzako kwa hoja za KIBAGUZI na KIDINI, je mpaka sasa haudhani kuwa UMEFILISIKA kichwani?
Nitafute nikupe DAWA

Kuna watu ambao ni mufilisi kimawazo, kisera kwa hiyo wanapojiita maskini ni vizuri kuwaelewa. Kote ambako wanashindwa kutangaza sera wanajaribu kutumia dini kama njia ya kuwakoroga watu ili wao wafanikiwe. Dini ni mbinu rahisi sana ya kuwarubuni watu wasio na elimu, unaweza kushangaa kuona mtu hana viatu hana elimu lakini anapigania kujenga kanisa, msikiti au sinagogi. Ukiona mtu wa namna huyo jua upstairs kuna tataizo.
 
Wewe na huyo Lipumba wako mumeshajichokea, hamna jiya, udini,chuki,usaliti, Lipumba mbona tunamjua siku nyingi kuwa ni CCM-B, anataka huruma ya JK ili aje amkubuke kwenye vile viti kumi maarufu kama MTAMA KWA WATOTO( soma wapinzani)


Hivi jamani nielewesheni, inakuwaje inapoguswa CUF inaungtanishwa na udini sana, na CHADEMA inaonekana si ya udini, yaani ghafla akitajwa Lipumba inakuwa udini lakini slaa ambae 80% ya CV yake ni Kanisa Katoliki.

Nashauri kwa wanaTZ wote tuache kuingiza udini katika kumuua mtu kisiasa maana mwisho wake na madhara yake yataturudia wenyewe, hili ni jambo baya sana kwa mwelekeo wa mbele wa nchi hii yetu ambayo ina wakristo , waislamu, wabahai, wabudha, wahindu, na wengineo kina sisi ambao hatupo kwenye dini hizi za kwenu, tusikubali ukoloni mpya jamani.
 
Hivi jamani nielewesheni, inakuwaje inapoguswa CUF inaungtanishwa na udini sana, na CHADEMA inaonekana si ya udini, yaani ghafla akitajwa Lipumba inakuwa udini lakini slaa ambae 80% ya CV yake ni Kanisa Katoliki.

Nashauri kwa wanaTZ wote tuache kuingiza udini katika kumuua mtu kisiasa maana mwisho wake na madhara yake yataturudia wenyewe, hili ni jambo baya sana kwa mwelekeo wa mbele wa nchi hii yetu ambayo ina wakristo , waislamu, wabahai, wabudha, wahindu, na wengineo kina sisi ambao hatupo kwenye dini hizi za kwenu, tusikubali ukoloni mpya jamani.

Malizia Ukitaja CCM unaimanisha mafisadi!
 
Kumfananisha Prof Lipumba na Mchungaji Slaa ni ukosefu wa akili na udadisi, simply:

@ Lipumba ni msomi anae fahamika, Mchungaji Slaa anaelimu ya kanisa
@ lipumba anauzoefu wa siasa na kiuchumi wamuda mrefu, Slaa hanauwezo hata wa kuongoza kondoo waliopotea ndio maana kashidwa kuendeleza kanisa

@ Lipumba utaalam wake wakisomi unatambulika na unakubalika duniani, Slaa hatambuliki nje ya TZ na hakubaliki pia ndani ya nchi
Slaa ni celeberaty na media za wachanga ndizo zinazo mtaja marakwa mara, Kashindwa kuondoa udini na ukabila ndani ya Chadema. Mchungaji Slaa Proooooooo fuu
 
Kama alisema hayo maneno, then he is becoming irrelevant. Ukiwauliza waswahili watakwambia huo ni wivu.......
 
Huyu naye anaota aliyekuambia SLAA hawezi kushindana na Kikwete ni nani? Kwani sasa hivi anafanya nini si ndio ushindani unavyoanza!!!acha kutuchanganya na siasa zako.
 
Hata akivalishwa kanzu na kilemba na wahehe akawa kama mimi,waislamu wameshajuwa siri zake na wakatoliki,hatutompa kura zetu.
Tutaangalia nani nafuu kati ya Lipumba na Kikwete.

Dah!

Hivi siasa za Tanzania ni baina ya wakatoliki na waislamu? Ina maana kwa vile CCM na CUF zina wagombea ambao ni waisilamu tu, kwa hiyo hivyo ni vyama vywa wasilamu?

Nadhani inabidi tukomae kiakili na kimawazo tuangalie utaifa zaidi ya udini. Dini ni kitu cha kuchagua, kwani mtu anaweza kuhama kutoka dini nyinge kwenda dini nyingine, lakini utaifa siyo jambo la kuchagua.
 
Samahani umewahi kuanalyse neno lipumba? LIPUMBA 0 yaani ni kikomo cha PUMBA, do you need more explanation? just beep!
 
Ingefaa ianzishwe thread maalum jf kuhusu mgombea yupi utampa kura yako ya urais
KURA YA MAONI

Mgombea yupi utampa kura yako ya Urais 2010?


Jakaya Kikwete 7%


Willbrod Slaa 88%


Ibrahim Lipumba 4%


Mutamwega Mugahywa 0%


Hashim Rungwe 1%


Paul Kyara 0%


Christopher Mtikila 1%


Peter Kuga Mziray 0%


Total votes: 339
 
Back
Top Bottom