Elections 2010 CHADEMA na kampeni kwa njia ya Mtandao

Nicky82

JF-Expert Member
Mar 14, 2009
941
64
Kwa wale waliofatilia kwa makini uchaguzi wa Marekani wa 2008 watakumbuka jinsi matumizi ya internet yalivyomsaidia rais wa sasa Barack Obama kushinda. kwa wale waliokuwa na access waliweza kupata taariza za kampeni, hotuba, ratiba za ziara na hata videos hii ilisaidia sana kukusanya wanachama wengi na ilikuwa ni nafasi ya kuwafikia wale ambao muda mwingi wako ofisini na hawakuwa na muda kuangalia TV au kusikiliza redio wala kuhurudhuria mikutano ya kampeni.

CHADEMA inapaswa kuona umuhimu wa kuitumia nyezo hii muhimu sana katika dunia ya leo ya utandawazi. Japo wale wenye access ya internet Tanzania si wengi kama Marekani, lakini ni ukweli kwamba wengi wao ni wasomi au ni watu ambao muda mwingi wako oficini na sirahisi kuwaona mikutanoni.

Ukiangalia kwenye website ya CHADEMA utaina taarifa ya mwisho ni ya July 12, inamaana ni karibu ya mwezi hawaja-update taarifa zao.
Najua jamvini JF kuna viongozi wengi ya CHADEMA, bila shaka hata Mkurungenzi wa Habari yupo humu. Ushauri wangu kwa CHADEMA waweke kwenye website yao daily update za safari za mgombea urais, taarifa za wagombea ubunge, picha,Videos, hotuba n.k. Hii itawasaidia hata wale wafanyakazi wanaobanwa au kukosa muda wa kuhudhuria mikutano kupata taarifa na sera za mgombea huyu.

Wanapaswa pia kuitangaza website ili watu waijue hii itawasaidia sana CHADEMA katika kueneza ujumbe kwa wanzania walioko ndani na hata nje ya nchi hii ambao magazeti wala redio zetu haziwafikii na njia pekee ya kuwafikia ni kwa njia ya mtandao.

nishapoke forwarde sms kibao ziwahusuzo hawa jamaa... !!sidhani kama ni wazembe kiasi hicho!! wafikirie kuingia ktka mabango na kusambaza vipeperushi kwa sana!!!
 
you can not compare internet penetration in tanzania ( both broadband and wap ) with the USA. a decent inquiry on the use of media in tanzania whether traditional or non traditional will show that as an election strategy, the internet in tanzania is not up to the task yet, hence there will be little value added. however, by the next general election in 2015, there will be a critical mass of voters existence in cyber space to make a big difference.
 
KWANGU NATUMIA CRANK BOX NI TA SOMAJE HUO MTANDAO,Mambo ya Marekani usifananishe na bongo jamani,wapiga kura wengi ni watu wasio na uwezo wala elimu ya mambo ya mtandao
 
Ni wazo zuri tuuu. Tukumbuke kuwa hawa wapiga kura wenye access ya internet ni wachache lakini ni wenye ushawishi mkubwa sana katika jamii. Binafsi naamini inaweza kusaidia sana. Mfano mimi mwenyewe ukiniuliza sasa Daktari Slaa sasa (leo tarehe 4 August 2010) yuko wapi na ameongea nini na watanzania wa huko aliko sijui.........
 
KWANGU NATUMIA CRANK BOX NI TA SOMAJE HUO MTANDAO,Mambo ya Marekani usifananishe na bongo jamani,wapiga kura wengi ni watu wasio na uwezo wala elimu ya mambo ya mtandao
kweli unachosema ni kweli japo wanapata kupitia mtanadaoni sio wakubeza pia na ushawishi walio nao pia! Ila mbona nikipita facebook watz kibao wageni, i mean unregistered member wa jf kwa siku nao si haba, kwa anko michuzi bado tunabeza tu kampeni za mtandaoni!
 
Kwa wale waliofatilia kwa makini uchaguzi wa Marekani wa 2008 watakumbuka jinsi matumizi ya internet yalivyomsaidia rais wa sasa Barack Obama kushinda. kwa wale waliokuwa na access waliweza kupata taariza za kampeni, hotuba, ratiba za ziara na hata videos hii ilisaidia sana kukusanya wanachama wengi na ilikuwa ni nafasi ya kuwafikia wale ambao muda mwingi wako ofisini na hawakuwa na muda kuangalia TV au kusikiliza redio wala kuhurudhuria mikutano ya kampeni.

CHADEMA inapaswa kuona umuhimu wa kuitumia nyezo hii muhimu sana katika dunia ya leo ya utandawazi. Japo wale wenye access ya internet Tanzania si wengi kama Marekani, lakini ni ukweli kwamba wengi wao ni wasomi au ni watu ambao muda mwingi wako oficini na sirahisi kuwaona mikutanoni.

Ukiangalia kwenye website ya CHADEMA utaina taarifa ya mwisho ni ya July 12, inamaana ni karibu ya mwezi hawaja-update taarifa zao.
Najua jamvini JF kuna viongozi wengi ya CHADEMA, bila shaka hata Mkurungenzi wa Habari yupo humu. Ushauri wangu kwa CHADEMA waweke kwenye website yao daily update za safari za mgombea urais, taarifa za wagombea ubunge, picha,Videos, hotuba n.k. Hii itawasaidia hata wale wafanyakazi wanaobanwa au kukosa muda wa kuhudhuria mikutano kupata taarifa na sera za mgombea huyu.

Wanapaswa pia kuitangaza website ili watu waijue hii itawasaidia sana CHADEMA katika kueneza ujumbe kwa wanzania walioko ndani na hata nje ya nchi hii ambao magazeti wala redio zetu haziwafikii na njia pekee ya kuwafikia ni kwa njia ya mtandao.

Obama alitumia internet kukusanya michango kwa sipidi kubwa sana, lakini ushindi wake haukutokana na interent sana. Ndugu yetu yule alikuwa wakata mbuga wengi sana waliokuwa wakipita nyumba hadi nyumba. Kwenye ofisi zao walikuwa na ramani ya eneo lote kuonyesha nani anaishi wapi, na ni yupi ni Republican damu, na yupi yupi ni democrat au hajulikani msimamo wake. Wale wakata mbuga wa Obama walikuwa wakifika mlangoni kwa yeyote ambaye hakuwa republican damu na kukuomba kura. Mimi nilipigiwa hodi mpaka nikaamua kuweka bango la McCain kwenye mlango wangu kwa vile ninaishi eneo lenye conservative wengi sana.

Chadema wanatakiwa wasivuje raslimali zao kusudi waweze kuwa na wakata mbuga wa kutosha nchi nzima kuhakikisha kila anayeweza kupiga kura anapatiwa ujumbe wa CHADEMA na anaufahamu vizuri sana. Watanzania wengi leo hii wanaweza kuamua kula na CCM na kura kwa CHADEMA kama watakuwa wanajua vizuri sera za CHADEMA.
 
Ni bora wakajihimarisha kwa kutumia Radio za FM, ambazo zipo kila mkoa wa Tanzania, kuliko kupoteza muda mwingi kwenye tovuti, tovuti ambazo si Watanzania wengi access nazo.
 
You can reach opinion makers through the internet. You reach news writers, talk show hosts, teachers, politicians and quite a few other influential people through the net. If you influence them, you influence the nation through them.

Vita vinapiganwa kwa kila nyenzo. Chadema itumie internet kama njia ya kukifikia kikundi Fulani ambacho ni chumvi ya Tanzania.

Naamini kuna Mungu. Naamini Mungu ni mwenye huruma, Naamini atakuwa amesikia sala na kilio cha Watanzania, kwamba wamechoka kutawaliwa na watu wale wale kwa miaka 50 bila ahueni. Nadhani Mungu katuchagulia Slaa atukuomboe toka makucha ya CCM. Kama hivyo ndivyo, lazima tutashinda. Kama wasemavyo KUG, "Vita vyake Mungu nani atashinda?"
 
Naamini kuna Mungu. Naamini Mungu ni mwenye huruma, Naamini atakuwa amesikia sala na kilio cha Watanzania, kwamba wamechoka kutawaliwa na watu wale wale kwa miaka 50 bila ahueni. Nadhani Mungu katuchagulia Slaa atukuomboe toka makucha ya CCM.
Kama hivyo ndivyo, lazima tutashinda.wasemavyo KUG, "Vita vyake Mungu nani atashinda?"
Mkuu wewe una tofauti gani na Maaskofu walio dai kuwa Rais Kikwete ni chguo la Mungu...!?
 
jf tayari imeshatumika kama nyenzo ya chadema....michuzi ccm.....an-nuur cuf.......
 
Kweli kabisa website ya chadema inatia aibu! Jamani tullitegemea kwamba taarifa za uhakika updates picha za matukio hasa ya mikutano hii tutayakuta huko? Ugumu uko wapi? Huyo anayehusika na hiyo site ni nani na anafanya nini?
Cammon chadema kama kuna wakati unaohitajika kumshambulia adui kila kona ni sasa? Flood the internet about chadema funika kabisa hayo manguo ya kijani
 
Mkuu wewe una tofauti gani na Maaskofu walio dai kuwa Rais Kikwete ni chguo la Mungu...!?

"Nadhani" Maaskofu walikuwa sahihi. Mungu alitaka tumrudie, akatupa pain ya JK. Imeandikwa "In you pain you will look for me". I think in their pain, Tanzanians have looked for the Lord, and He is answering them. Slaa is, in my humble opinion, that answer.
 
Tunarudi pale pale - WATU na MAZINGIRA...
Huwezi kuchukua ya Marekani ukayatumia Bongo haiwezekani wakuu zangu. Ndio yale ya kuwafanya Masai wawe wakulima wa Pamba na mahindi badala ya Ufugaji.

Kinachotakiwa tufanye ni kwanza kutazama WaBongo wanapashana vipi habari, Je wananchi wengi wanahabarishana kwa njia zipi zaidi kulingana na mazingira yetu kisha tumia njia hizo zaidi. Hadi leo hii Watanzania wengi hasa mikoani wameyajua ya Ufisadi kupitia magazeti, redio na TV na kikubwa zaidi UDAKU (kutoa maneno hapa na kuyapeleka kwingineko) - Hivi ndio vifaa tulokuwa navyo sisi leo ktk utamaduni wetu ulopitwa na wakati miaka kama 100 nyuma.

Chadema hawawezi kubadilisha mfumo ghafla kwa kutegemea Mtandao (internet) watafulia. Ikumbukwe tu kwamba kwa miaka mingi sana ya chaguzi zetu na dunia nzima wazee ndio wamekuwa wapiga kura wakubwa kuliko vijana na hakika njia alotumia Obama kuwafikia vijana wengi huko Marekani sisi hatunazo nchini. Sidhani kama zaidi ya asilimia 10 ya vijana wetu wana access ya mtandao lakini ni wazuri wa kusoma magazeti, matangazo, TV hasa wakati wa michezo ya kuigiza na ligi ya Uingereza.

Na nitarudia tena kikubwa zaidi ni UDAKU - hili pekee linapatikana kwa njia ya kisasa yaani utumiaji wa simu. Asilimia kubwa ya Watanzania leo hii wana simu za mkononi na mazingira yanaruhusu upokeaji wa sms kona zote nchini. Ujumbe wowote wa kitaifa unaweza kupitia njia za simu na ukasambaa nchi nzima na kwa haraka sana.
 
Nadhani umeenda mbali sana kuchukua mfano. ccm wanatumia hii mbinu. Nimeshatumiwa sms kadhaa
 
Hakuna njia bora kwa Tanzania Kama 'soga'

hakikisha Chana kinazungumziwa kila penye mkusaniko wa watu Kama wanavyofanya cuf zanzibar......kila sentensi mbili za mazungumzo moja itaponda ccm au itasifia cuf

inachosha lkn inafikisha ujumbe mpaka subconcious level nafikiri....... Atakaeliweza hili bara atachukua nchi
 
Mbinu zote zitumike, na hasa ya kutumia sms. Watz wengi wana simu za mkononi!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom