CHADEMA na harakati za kupinga posho; msimamo wa wananchi

Viongozi wa CCM wanaendeleza sarakasi kwenye swala la posho. Nape akisema msimamo wa chama chao no to posho, makinda anasema Dodoma maisha ni magumu kwa wabunge kama vile wananchi wengine ni nyoka, Kashilila anasema hakuna posho, JK hasemi kama ameruhusu posho zilipwe au la, wabunge hawakubali kama tayari wamekula CHA JUU AU la habari ni fully kizunguzungu kama vile viongozi wote ni majuha. Maelewano na jinsi nchi inavyoendeshwa inabidi wananchi wachukue nchi yao. Haiwezekani viongozi wote wa juu wasijue ni jinsi gani wanatuibia.

Posho ni laana na itamsumbua Anne Makinda siku zote. Angalia wananchi wa dodoma walivyo na maisha magumu halafu anayelipwa milioni zaidi ya saba kwa mwezi unamtetea kwa kusema maisha magumu, wakati kutoka bungeni ni hatua chahce kwenda vyuoni, shule za msingi na sekondari, kuna waalimu, wanajeshi,polisi, madaktari nk walio wengi wanalipwa chini ya laki nane kwa mwezi kwenye mji huo huo halafu leo unawaambia eti wabunge wasiozidi 370 ndio wenye shida zaidi.

Natamani kutokuwa na bunge, natamani kulifunga halina maana. Natamani wananchi wangejua na kutompa kura kila mbunge anayeshabikia posho na kuipokea. Natamani tungewakimbiza hata kwa viboko. Natamani watanzania siku moja waende dodoma na viboko wakaonyeshe hasira zao za ugumu wa ukweli wa maisha. Siku inakuja na hiyo siku sio mbali. Kwa wenye uelewa tuendeleeni kuwaelimisha wananchi.
 
posho kwawabunge siosawa kwa wananchi ambao wanapata mlo mmoja tuu kwa siku nivyema spika awajibike kwa hili kwa kujiuzulu na wale wabunge wanaosapoti posho kipindi kingine cha uchaguzi wa siwaami tena maana hawafaam maadili ya kazi waliotumwa na wananchi waliowachagua
 
ninawapongeza sana wabunge wa chadema kwa msimamo wenu juu ya swala laposho nyie ndio mnao ona masha magum kwa mtanzania wa kipato cha chini simamen katika msimamo huo huo
 
Tukumbuke kuwa vita dhidi ya posho siyo vita ya CDM bali ni vita inayofanywa ma mbunge mmoja tu wa CDM ambaye ni Mhm Zitto. Kama CDM wenyewe wameshindwa kuwa na msimamo mmoja kama chama, sisi wananchi wa kawaida tutaweza vipi?

Acha kupotosha kama rais wako, issue ya kupinga posho specifically seatting allowance iko kwenye manifesto ya CDM ya 2010. Kawadanganye masaburi wenzako au wale wote wavivu wa kutafuta ukweli
 
Back
Top Bottom