Chadema na diaspora njia bora ya kukuza uchumi na demokrasia tz

kinepi_nepi

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
869
235
Diaspora ni njia ambayo imetumiwa na nchi nyingi sana duniani kukuza uchumi wa ndani na demokrasia ya ndani ya nchi husika hasa pale inapokuwa ina wananchi wake wengi nje ya nchi mama. wananchi hawa hushiriki kataika maendeleo ya nchi zao kwa njia mbali mbali hasa kwa fedha za kigeni kusaidia ndugu na jamaa na kuhifadhi fedha bank za ndani kuziongezea mtaji. Kujenga nyumba, kufungua biashara na kuwekeza kwenye nyanja mbalimbali. kuingiza teknologia mbali mbali na kushirikiana na nchi wanazoishi/kufanya kazi/ kusoma nk kuzisaidia nchi zao.

Chadema kikiwa kinaungwa mkono na wana-diaspora wengi hasa ikiwa sababu zao nyingi kuwa nje ya nchi ni uchumi mbovu, elimu duni na huduma duni za jamii TZ wameamua kuwaunga mkono CDM wakiwa na matumaini kwamba kiingiapo madarakani kitasaidia kufikia njozi za wengi pamoja na hawa diaspora.

Sheria za nchi yetu kwa sasa zinakumbatia wageni kwa jina la wawekezaji na kuwatenga wazawa hata wakiwa na uwezo sawa na wageni hawa wawekezaji. SIo rahisi mtanzania kupata huduma anazopata mgeni ndani ya nchi yake. Serikali yetu inaheshimu wageni sana na kusahau kuwa hakuna nchi duniani imejengwa na wageni.

Kama serikali ingethamini mchango wa wazawa wa ndani na nje ya nchi na kuwajenga mazingira bora ya ushindani na kulinda bidhaa za ndani tanzania ingepiga hatua kubwa sana ya kiuchumi.

Leo tuna wana diaspora wanaofanya kazi kwenye kampuni kubwa za gas/oil , uchumi na fedha, science na technologia, udaktari, nurse, nuclear science, maabara, nk na vile vile tunao wafanyabiashara wakubwa na wenye ujuzi mkubwa wa kuiwezesha nchi. Kwa makusudi makubwa nchi yetu haina viongozi wenye uwezo wa kuwa vutia wazawa wapende nchi yao ama kuifanyia kazi ama kufanya biashara. Rushwa imekuwa kizingiti kikubwa kwani wageni wanakwepa kodi kwa kiasi kikubwa na kuifanya nchi jalala la bidhaa mbovu. Haina maana kuwa wazawa hawakwepi ila kwa kiasi kikubwa wageni wanaongoza.

Leo hii viwanda kama Tanzania machines tools, sido, nyumbu, auto asssmbly viwanda vya nguo, nk havipo tunaagiza wheelbarrow kutoka nje, betri, redio, tairi, sahani, touchi, nk wakati tulikuwa tukizalisha vipuri na hivi vifaa ndani ya nchi leo ingetakiwa uchumi unakuwa kwa kuongeza uzalishaji wa raw material kwa ajili ya viwanda vyetu vya ndani.

Nakumbuka nimevaa viatu vya mafundi wa vibambazani ambao wangewezeshwa leo tungekuwa tunauza viatu nje, leo hawapo kwani soko lao ama limeliwa na soko la viatu vya china vibovu au mtumba na kuwaacha maelfu hawa bila ajira.

Tanzania leo inaagizia kuku mboga, samaki, mchele, nk wakati wananchi wangeweza kuzalisha kwa kuwezesha na barabara bora. Leo hii tunatumia tomato sourse kutoka nje na zile za kwetu zikishindinishwa au hakuna .

Mifano hii ni michache sana kati ya mingi ambayo ingezingatiwa TZ ingekuwa kama ulaya na hakua mtu ambaye angelia ajira wala mlo mmoja. Achilia mbali madini, gas, utalii bandari usafirishaji. nk.

Tukae tutafakari tuandike historia bila kumumunya maneno wote tumjue aliyetufikisha hapa na tuseme hapana.

Chadema wananafasi kubwa ya kufufua njozi zilizozimwa za watanzania na watawala walioamua kwa mkusudi kuuwa watanzania kwa tamaa zao. Watawala waliomamua kwa makusudi kuwateka na kuwatesa wale wote wanaotetea ukweli. Kuwafungulia mashitaka na kuwadhalilisha wote wanaosema hapa si sawa.

Serikali ijui hakuna anayepigania kwa ajili yake zaidi ya watawala wadhalimu bali ni kwaajili ya vizazi na tanzania yenye neema kwa wote.
 
Chadema ni nyota inayowaka itakayowaangazia watanzania wote na kututoa kwenye utumwa wa watanzania wenzetu waitwao viongozi wasio na uchungu na nchi yao wala pesa za watanzania.
Tuungane pamoja na tusema basi inatosha. We need change now.
 
Back
Top Bottom