CHADEMA na CCM wagombea msiba Morogoro

kazikubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
598
143
Wanachama wa CDM mjini Morogoro wamefanikiwa kuuteka msiba wa mtoto wa kiongozi wa CCM na kugharamia chakula, sanduku na gari la kubeba mwili. Mfiwa alikubali msaada huo baada ya CCM wenzake kutomjali kwa kumpa msaada. Baada ya CCM kupata taarifa kuwa CDM wamekwisha umiliki msiba na mfiwa ameridhia, wana CCM wakavamia msiba huo na kutaka kuvuruga mazishi.

Viongozi wa Serikali ya mtaa walitumia mamlaka yao kuamuru jeneza lisiwekwe bendera ya CDM. Mwili ulipelekwa mazikoni bila ya sanduku kufunikwa bendera yoyote.

Siasa misibani zitatupeleka pabaya.

Source:ITV- Taarifa ya habari saa 2 usiku ambayo inaendelea sasa.
 
tukio hilo limetokea leo mjini morogoro ambapo wafuasi wa chadema walifika na kutoa pesa kwa ajili ya chakula na maandalizi ya mazishi, ambapo CCM walipoona chadema wameteka msiba hawakukubali ndipo walipovamia msiba na kusema kuwa mama wa marehemu ni kada wa CCM, My take, Hichi ni kioja cha mwaka hamuwezi kufanya siasa mpaka mteke msiba? source taarifa ya Habari ITV.
 
Huku tunakoelekea siko ndiko, hebu tupite huku jamani, uccm na uchadema hadi kwenye misiba
 
ha ha ha ha nacheka mie hivi sasa ndio siasa zimekolea mama wa mtoto aliyefariki kada wa CCM alisemaje ha ha alitoa ushuhuda wowote
 
Chadema kama mnataka kuwa taasisi ya misiba kwa nini msiwaliane hospitali ya taifa Muhimbili? Kuna maiti wengi tu hawana wazikaji!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
huo mtaa ninaufahamu ni jirani na home. Unapozungumzga CDM Morogoro basi unazungumzia kichangani, kuna kipindi CCM walikuja kufanya mkutano lakini wakaambulia patupu mpaka jioni. Ndipo wakaamua kuanzisha mpango wa siri wa kununua baadhi ya vijana waiache CDM na mmoja wapo namjua ila namuhifadh na jamaa huwa haishiwi kupewa pesa. Hivyo swara la vituko vya CCM na CDM kichangani kwa sisi wenyeji hatushangai maana yapo zaid ya hayo. Japo c nzuri ki-democrasia.
 
Hilo la kuzika kila mtu na bendera ndio linalonitatoza. Ila kugombea msiba ni sawa tu, wangeshusha magunia ya michele na nyama ili wafiwa wasihangaike kuhemea walau mwezi.
 
Chadema kama mnataka kuwa taasisi ya misiba kwa nini msiwaliane hospitali ya taifa Muhimbili? Kuna maiti wengi tu hawana wazikaji!

Chama
Gongo la mboto DSM

Pia nchi hii kuna Raisi wa Misiba he can't aford to miss msiba. Unamjua?
 
Chadema kama mnataka kuwa taasisi ya misiba kwa nini msiwaliane hospitali ya taifa Muhimbili? Kuna maiti wengi tu hawana wazikaji!

Chama
Gongo la mboto DSM

haha haha kaka wape ukweli wao
 
Siasa zimekamatwa na wasio wanasiasa.Mnagombea maiti kesho Kikwete na Mbowe wanazungumza huku wakicheka kwa furaha. CCM kama waliona CDM imetangulia na hakuna kilichoharibika ingewagharimu nini kukaa pembeni na marehemu akazikwa?
 
mtu mzima ana maamuzi yake ya kufuata ya kufuaata idadi gani issue siyo kuwa ni mtoto wa kada bali alikuwa mwanachama hivyo alipaswa kuzikwa kwa heshima zote na chama chake
 
Hivi wewe chama.....nyie mpaka mwenyekiti wenu kutwa yuko kwenye mahitima na misiba sasa kipi chama cha misiba...usiwe unabwabwaja tu hapa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom