CHADEMA na CCM Mnaiharibu JamiiForums

Status
Not open for further replies.
Waliotufikisha hapa ni hao wanaojiita Mods, wao ndio walioanza kuweka ushabiki na mapenzi yao juu ya chama chao. Huku wakiacha kundi jingine likisulubiwa kwa dharau, matusi na vijembe.
 
Mkuu, tatizo si kuwa wewe ni mwana Chadema, Mwana CUF au mwana CCM au wa chama kingine chochote kile. Kiinachotakiwa ni kupingana kwa hoja, na si kutumia matusi na kejeli. Mimi naamini kuwa hakuna chama au serikali isiyopingwa duniani.

Sasa sisi wengine tusiokuwa na vyama, mnatuogopesha na siasa zenu za visasi. Mi natarajia watu washushe nondo za uhakika na waeleze mazuri ya vyama vyao, na ikiwezekana waielekeze serikali nini cha kufanya, pale linapotokea tatizo na si kuleta matusi....! Tanzania ni yetu sote, sasa msituhatarishie amani yetu.

Mtakapoanza kuwatukana kuwa wanachama wa chama fulani i.e CHADEMA/CUF/CCM kuwa ni wajinga au kuwaita wapumbavu, unaye mtukana hapa kama si nduguyo ni nani!?

Mimi binafsi nina ndugu kwenye vyama vyote hivyo, na tunaheshimiana, na wakati mwingine wananishawishi kujiunga na vyama vyao, lakini kwa bahati ghafi mimi si mpenzi wa vyama vyote hivyo, nipo neutral na ninaheshimu mapenzi ya kila mmoja.

Mkuu kwanza wengi hana hiyo neutral! hawaamini hilo!

Pili nimesema sana hata kutuma post kwa mods kusema kuwa

CREDIBILITY YA JF HIVI SASA IME-SLUMP DOWN kwa kasi ya ajabu, na si ajabu kuwa wahuni wameisabottage na wengi wanajifanya chadema, wanachojua ni matusi tu.

Chadema si chama cha matusi wala ushabiki wa usio na maana! kikubwa mchadema mmoja akitukana mwingine ana-support bila kujali kwa kufanya vile ina repel watu kujiunga na chadema!!

Mpaka viongozi wa chadema members wa humu wengi ni ziro tu, maana kwa nafasi zao wangetoa onyo chadema si chama cha matusi!!

Kibaya si hadhi ya chadema, la! wanatumia uwanja wa JF, uwanja uliotukuka wenye hadhi na historia ya kutukuka!!!

Kama ambavyo standard ya elimu imeshuka kwa shule za kata
Kama ambavyo hadhi ya elimu mlimani ilivyoshuka wa kuongeza wanafunzi bila infrastructure
Kama ambavyo uhalisia wa maziwa upotea kwa kuongeza maji

ndivyo ilivyo JF, hata kama mods na founders watajisifu kwa kuongeza watu ili kupata ufadhili wa hapa na pale , lakini ukweli unabaki palepale this is not JF we used to have here!!!

Balantanda ametoa list ndogo sana ya watu tuliowapoteza, humu yamebaki matangazo ya chadema na ccm na si uwanja wa kufikiri na kupose challenge na kuzijibu!! leo ukitoa topic kinyume na matakwa ya wengi utatukanwa mpaka uone rangi zote!!!

Personally naona bora niseme ukweli nisiondoke kwani hata nikiondoka JF itakuwepo! lakini kama nasema ukweli na we have tangible proof why not change???

majibu ya siku hizi humu ni crap, umetumwa, ......n.k this is absurd!

wengi wa waliojiunga kuanzia may 2010 mpaka February 2011 ni stubborn!!!! wachache sana wenye busara zao!

Kuna siku nilianzisha topic kama hii nikasema tulikuwa tunalazimika ukasome kitu kwanza ndio ujibu hoja......waliotukana walitukana kwa kuona kama vile nina jivuna au ninadharau wageni wa JF , but I was right.
 
Ni bora wake ban wanapoteza maana ya jamvi hili kabisaaa
 
Umenena XP,naimiss sana ile JF ya enzi zile kabla ya June 2010.......Natamani Mods wairudishe ile JF ambayo ilifikia kipindi ikaitwa 'The Home of Great Thinkers......

Dah.....................

Mama,Kyoma,Dilunga,Kuhani,YournameisMine,bht,Charity,Game Theory,Icadon,Pundit,Bluray?,Ibrah,Kana Ka Nsungu,Nemesis,Next Level(anategea tegea siku hizi huyu),Sipo,Penny,Mbogela,Baba Mkubwa,Original Pastor,Ladislaus Modest,Asha Abdallah,Mwafrika wa Kike,Mwazange,Hauxtable,Kevo na wakuu wengine kibao ama wamepotea kabisa ama wanaingia JF kwa kusuasua kutokana hali ya hewa kuchafuka mara kwa mara kikubwa kikiwa ni u-CCM na u-CHADEMA....
Mimi siasa sio zangu ila naingia hapa jukwaa la siasa kuchungulia kwa vile nipende nisipende siasa inaathiri sehemu kubwa ya maisha yangu nikiwa kama raia.

Hata mimi hilo la kutukanana ovyo nimeliona, kwa kweli pre-2010 kulikuwa na memba (kama hao uliowataja) ambao michango yao ilikuwa tunafaidika nayo sana na ilikuwa ni kwa manufaa ya Mtanzania regardless of his/her political and religion affiliation, lakini hivi karibuni na zaidi memba wengi walojiunga katika vuguvugu la uchaguzi wamekuwa too confrontational, matusi na kebehi zimezidi, hata hivyo bado tunao watu kama Kiranga, Mkandara, Mzee Mkjj nk ambao michango yao mimi huwa inanifurahisha.

Maxence, Invincible and all Mods please weeds out those rotten apples before it is too late.
 
Hapo umenena ndugu.kuwa shabiki wa chama sio vibaya ila kuna watu wamezidi humu ndani,matusi ndo yanatawala.hii forum ni ya great thinkers ina maana inabidi tufanye mambo yetu in an intelectual manner
 
Sijasoma hata kumaliza hii thread ya kada wa ccm inaupungufu mwingi ila naona huyu kada hajajua umuhimu na mchango wa JF kwa Taifa la Tanzania. Waeleze tbc, daily news, itv na wengine wote katika hii journalism sectors Tanzania wafanye kazi zao then you will see less and less work in JF and other socials media outlets.

We never or fear inferior words for purposes of pushing ccm agendas here. We are seeking true freedom until all Tanzanians enjoy every bit of it....
 
Mkuu nakuunga mkono pia. Hali imekuwa mbaya hivi karibuni. Watu wanaandika tuu for the sake of it. Wanapost without thinking, no critical analysis. Hasa jukwaa la siasa linaanza kuboa.
 
Nakumbuka kipindi hicho hasa 2008,
Kwanza nilikuwa najua JF ni uwanja wa uchambuzi wa matukio ya kijamii,
Zile picha za wazee Jenerali Ulimwengu na Daniel Simbaye) pale kwenye homepage,

Zilikuwaga zinanifanya nione kama naingia kwenye eneo makini sana, na hata ndani yake ilikuwa hivyo kweli,
Ilikuwa ngumu kwangu kutifautisha kati ya mtoa hoja na wachangiaji, wote walikuwa wanapiga nondo tu,
Nakumbuka marakadhaa nimetumia JF kama referrence kwa baadhi ya material muhimu sana kwenye career yangu,

Na supervisor wangu alipopitia kweli akakubali na yeye akawa mpenzi sana wa jukwaa hili,
Hii ni sehemu ya kumbu kumbu zangu tamu kuhusiana na JF,
Leo nimekuwa member, sioni tena ule utamu japo siwezi kuacha coz JF ni kitu ninachopenda sana,

Ni muda muafaka kwa kupitia mjadala huu ambao Mh X-Paster umefungua mjadala ambao lazima ufungwe kwa "KIELEWEKE"
Kwamba ni muda muafaka sana kwa kila kuwekwa sawa ili kuendeleza makali ya JF....
Naamini Mods mnajua kazi yenu vizuri na mnaielewa vizuri sana JF kuliko wengi wetu hapa,

Tafadhali Mods turudishieni JF yetu ya kipindi hicho (kama alivyosimulia Balanatanda)
Kama umepitia mitandao mingi ya kijamii hapa kwetu, hamna jukwa ambalo linatoa sauti kali sana kama JF,
Tukirekebisha hii hali ambayo inaelekea kuporomosha zaidi hadhi ya JF, watu makini wengi watarejea.

Sikubaliani na idea ya kutajana majina (japo kuna watu specifically wananiboa sana)
Wala kunyooshea wanachama wa chama fulani ndio wagomvi,
Kila mtu ambaye anafanya ndivyo sivyo anajijua na nadhani atajirekebisha.
Tukianza kutajana kutaondoa maana ya thread hii sababu tena itajenga dhana "kwamba kumbe iliandikwa kwaajiri yetu"
Na wao next time watajibu..... then yaleyale......!

Sure lets save JF!
 
majina na sura za ajabu zilizoko humu zinaonyesha kuwa huu mtandao haupo makini,na most of them ni waoga thats why wanajificha.eg.picha ya hitler inafanya nini hapa?au kwa nini uweke picha ya jini wakati we ni binadamu.kama unaamini unachokisema hupaswi kujificha na unatakiwa uwe tayari kwa lolote litakalokufika.nashauri ufanyike usajili wa information za watu wote wanaotaka kuchangia humu or else discussion zetu zitachakachuliwa kila siku na hatufiki popote!

CCM tangu imeanzishwa inaogopa kupingwa, itafanya kila lilnalowezekana kuwanyamazisha wapinzani wake. kwa uhuru na msimamo wa Great thinkers, CCm inaamini kuwa Jamii Forum ni mpinzani wake kama ilivyo CHADEMA kwa hiyo iko kwenye list ya kuuawa kama vile ni chama cha upinzani!!! Makachero wake wamejazwa humu kuharibu mijadala na kutufanya wengine tukione kijiwe hiki kama kitu kilichokosa muelekeo ili tuondoke!!!
 
Wakuu all in all lazima tuadmit kwamba JF ni forum na si Blog. Kiasi kwamba civility na wisdom lies in the mind and fingers of wachangiaji. Mods ni mpaka wapitie hiyo michango ndiyo wanaweza kufanya intereference. Kifupi ni kwamba hii influx ya wachafuzi haijaanza leo wala mwaka jana. Nakumbuka mwanzo kabisa wa uchafuzi wa hoja ilikuwa ni kuingiza masuala ya kidini kwenye siasa wachangia hoja wakuu kwenye jukwaa la dini wakawa wakija kwenye jukwaa la siasa wakikutana huko basi wanaingiza vijembe vya huko jukwaani kwao. Mfano mzuri wa hao watu ni X-Paster na Max-Shimba (I am sorry if this sounds offending, lakini I am daring to talk openly). Hii ilipelekea kuzichujisha mada nyingi maana njia rahisi ya kuipoteza hoja ikawa ni kuingiza comments za dini.

Jkwaa la siasa enzi hizo ilikuwa ni majadiliano ya mustakabali wa nchi yetu, historia ya nchi yetu, scandals kubwa kubwa, udhaifu wa demokrasia yetu, udhaifuwa CCM na serikali yetu, what can we do to move on etc. Ikumbukwe kwamba toka enzi hizo CCM ilikuwa alwayz challenged na kulikuwa na very strong supporters wa CCM in the forum kama Masatu, Kada Mpinzani, Kasheshe, Mtu wa pwani, FmES etc. Lakini hazikuwahi kusikika lugha na matamshi yanayoonekana leo. Lingine muhimu ni kwamba those day it was much of CCM and the Other side (Wapinzani). Viongozi wa Chadema walikuwemo humu kama Zitto, Mkumbo, na baadaye Dr. Slaa na Mtei and others. Mara nyingi hawa viongozi wa Chadema na viongozi wao enzi hizo walikuwa wanaleta hoja mbadala asa to why they could do this or that better than CCM. Yes kulikuwa na kejeli,ubishi, uzushi etc hata enzi hizo za JF lakini yote yalifanyika with civility. Hata enzi hizi kulikuwa na kuparurana kwa hoja na vijembe lakini si kwa kiwango hiki cha leo.

Nini kimepelekea kutufikisha hapa tulipo? Narudia tena hii ni FORUM na sio BLOG. Kadri JF ilivyozidi kupata umaarufu ndivyo kadri members walizidi kujiunga na ni wakati huo huo CDM nayo ikawa inazidi kuwa maarufu. Kuelekea Uchaguzi 2010 lile kundi la the other side (wapinzani - Mainly CF na CDM) likazidi kukua na pia washabiki wa CCM wakazidi kuongezeka. Kipindi hiki ndi waliingia akina Malaria Sugu (what a character?) Huu ukawa sasa ni muda wa vijembe na kejeli kwa kwenda mbele upinzani ukiwa as a united force Vs CCM. Hapo kwenye upinzani namaanisha hata wale wasiokuwa na vyama. Zilipoanza kampeni ndiyo kabsaaaa na kuna something unusual kilitokea wakati ule maanana mashabiki wa CUF humu JF wakahamishia support yao CCM (Ni haki yao kidemokrasia though). Ngoma ikawa ni CDM, CCM mara hoja za kidini, personalities, Slaa amepora mke, JK ameanguka etc. Mods walikuwa bize mno kuregulate the forum at this time lakini bado kila aina ya takataka ililetwa hapa. Uchaguzi ukaisha with such a big rift in between supporters. Mashabiki wa CDM humu JF hasa wale wapenda vijembe ikawa ndiyo kama wamejeruhiwa kila wakati na kila hoja ni vijembe na kejeli, sometimes beyond sane-minded propotions. Ban zikaendelea pia na nadhani hiki ni kipindi kilichokuwa na ban nyingi kuliko wakati wowote JF. Baadaye ndugu zetu wakajivua magamba kukatokea influx ya masupportes wa CCM, a good thing though. Lakini most of them hawachangii hoja ni mwendo ule ule wa vijembe, kejeli
supporting anyhing done by JK, Nape, Msekwa etc and demonizing every move or person in the CHADEMA.

Tatizo tulilonalo wengi wetu ni kufikiri by the time uko nyuma ya hiyo pen name basi u r safe na unaweza kutukana, kuzodoa, kuzusha ili mradi tu kutetea hoja yako. Ni uchanga katika dunia hii ya mitandao, ulimbukeni, kutawaliwa na hisia zaidi ya hoja. Ikumbukwe kuwa humu tunakutana watu mbalimbali wenye backgrounds mbalimbali, umri mbalilimbali na wengine ni walewale kwa majina tofauti tofauti.
Unaweza kupitia kwenye michango mfano ya hizi sort of blogs au news panels uone utofauti wake

WAY FORWARD
Baada ya kusoma michango kadhaa iliyotangulia kuna sauti moja naisikia, wote tunakerwa na uchafuzi wa forum unaoendelea. Sasa tufanyeje? Maoni yangu.

1. It begins with you,It begins with me, kila mmoja wetu ajitwange ahadi kwamba hatatukana, hatakejeli beyond civility proportions, na hataweka thread, post avatar au post inayodharau au kudescredit imani ya mtu mwingine iwe ya kidini, kisiasa au kijamii.

2. Kwamba kuanzia leo sitachangia thread au post yeyote ile yenye mmwelekeo wa kuchafua hali ya hewa.

3. Kuanzia leo nta-report immediately kwa mod's thread au post yeyote inayoenda kinyume na kanuni za JF

4. Kuanzia leo usishabikie wala kufurahia upuuzi simply kwa sababu unakuwa directed kwa mtu au kikundi usichokipenda.

5. Kuanzia leo utasuggest members to be banned ukipata ushahidi wa namna gani wanaleta karaha ndani ya JF.

Nawakilisha
 
Mkuu XP ulilosema ni point sana tatizo ni moja 2, ckatai kwamba hakuna ucdm na uccm hapa mjamvini ila wengi wanaoipinga au kuikosoa serikali wanaonekana ni wanacdm wala sijui ni kwanini!
And viceversa.....wana CCM kwa kweli wanadharauliwa sana humu jamvini,wanaonekana hawana ufahamu wa siasa na hawajui kinachoendelea au ni mafisadi au watoto wa mafisadi,usalama etc..
Hii si kweli
 
shikilia hapo hapo mkuu. Hata mimi nashangaa!!! Nafkiri ni vvema tukakomalia maisha halisi ya Mtanzania anaeishi chini ya dola mmoja. Naomba wachangiaji wote wasome katiba za vyama vyao. Kwenye malengo ya vyama vyote katiba zao zinasema " lengo kuu la Chama cha Siasa ni kushinda uchanguzi na kuchukua dola"
Ndio mambo mengine yatafuata. Ni vyema wachangiaji tukaelelekeza kelele zetu kukemea kila aina ya dhulma na unyanyasaji wanaofanyiwa waTz bila kuweka ushabiki wa vyama vyetu, kejeli, matusi nk

kuna serikali nyingi tu duniani zimeangushwa na mijadala. Hata serikali ya Kikwete pia imewahi kuanguka kwa mijadala yenye maslahi na ya sauti zilizopazwa na wachangiaji makini. Mmesahau Richmond!
 
Naunga mkono hoja yako X Paster. Kuna wakati mijadala huku inaboa sana yani hata kama mtu ni CCM au CDM anabisha ushabiki tu kama mtu wa kijiweni Manzese hata kama jambo linaonekana wazi kuwa si sahihi. Kashfa na matusi bila hoja. Yote hii inapunguza umaarufu wa jukwaa hili au labda ni mkakati wa kulimaliza. Kuna wakati unaamua kupita tu unaenda zako ukiona pumba na ubishi maana utapoteza precious time yako.
 
A breath of fresh air!!!


Nashukuru sana X plaster kwa kuliweka hili kwa namna ambayo imepata kuungwa mkono na wengi. Nasema hivi kwa sababu zimeanzishwa mada nyingi sana huko nyuma kulilalamikia hili, lakini naona kama hii ya leo imeweza kuvuka kile kiunzi cha kuonekana au kutikuonekana.

Nakubaliana na woooote wanaosema hali hii ibadilike
Jamani inakera!!!!
hv mtu mzima unawezaje kutoa maneno machafu hadharani, bila kujua unamuambia nani??? na ni nani na nani wanajua kuwa umefanya hivyo? Au huna unayemuheshimu usietaka ajue unavyotukana??

maoni/maswali/mapendekzo yangu
- siku hizi ukiona post ina page 5 ujue page 1 ni nje ya point kabisa, page moja itakuwa ya kutumiana salamu na page 2 zitakuwa za maneno ya kejeli na matusi na page moja ndio itakupa ufahamu kama unataka kufahamu. Utata unakuja kwako wewe msomaji jinsi ya kuzichambua na kupata point, bila kukereka.
- je inawezekana kuwa na mods wengi zaidi? manake kazi imeongezeka sana,
- Kuanzishwa kwa post kusiwe rahisi sana, post kabla haijaitwa post na watu kuruhusiwa kuiona, basi ipitie kwa mods, ili kam ani ya kuunganisha iunganishwe na za zamani ili kupata flow, na kama ikionekana hakuna tija irudishwe kwa mwenyewe, irekebishwe ili eweze kuendana ha hadhi ya jukwaa
- Wengi zaidi tujifunze na kujielimisha namna ya kuishi katika jamii, tusiwe kama wanyama
 
ILIFIKIA HATUA NILIKUWA ADDICTED NA JF......! NILIKUWA SIWEZI KOSA...HOJA MOTOMOTO, ZA UNDANI , ZENYE KUIBUA YALIYOJIFICHA KWA MASLAHI YA TAIFA.....!
LO! Baadaye ...mambo yakaanza kwenda mrama.....SIASA ZA CHUKI,UHAFIDHINA,UBAGUZI,KUCHAFUANA,MATUSI NDO IKAWA MAHALI YANAPOPATIKANA NI JF...PICHA ZA KUDHALILISHA, KEJELI ,KUTAMANI KUMWAGA DAMU,MAWAZO YASIYO ENDELEVU NA KILA OVU!
WE HAVE TO TURN BACK WHERE WE WERE

Kuna wakati nilikuwa nacheki new post za JF kwanza kabla sijacheki inbox yangu.
Those were golden times!!
Hoja inajibiwa na hoja!
kuna wale tuliitwa humu kutokea ile forum ya bussines times tulinogewa hadi tukasahau tulikotoka!!
Ila mie humu sitoki bado,
ninatafuta tu namna ya kubahatisha machache ntakayoypata kwa kichujio changu cha kero.
 
Well said boss,naamini sio wote wataisoma waimalize hii post

Ni kweli mimi ni mmojawapo siwezi kumaliza post nzima ambayo naona haina mashiko, labda aiondowe akasahihishe na aseme ni jukwaa la siasa ndani ya JF. kuna watu wa MMU humu ukiwaambia jukwaa la siasa wala hawakuelewi. kwahiyo usahihi wa point yake ni kwamba jukwaa la siasa limekuwa mbofumbofu, na wanaorialibu hawazidi 10.
 
Tatizo lililopo mimi nililibainisha kwa mada maalum ambayo niliita "MODS acheni ushabiki".

Ingawa ukweli unauma na MODS hao hao waliliondoa hilo bandiko lakini ukweli unabaki pale pale.

Tatizo MODS ni washabiki tena sana wa siasa za vyama hivyo. Hivyo wanashindwa kukemea sababu za ushabiki.

Nilishauri kuwa MODS wawe wanasheria na waandishi wa habari kitaaluma ambao wanajua ethics za taaluma zao na kulinganisha na za forum kama hizi ambazo siku zote zinakuwa na malengo makuu matatu yaani Kuelimisha, Kupashana habari na kuburudisha.
 
Status
Not open for further replies.
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom