X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,810
Nachukua nafasi hii nami nitoe yangu machache, kati ya mambo kadhaa yanayo kera ndani ya Jamiiforums. Siku za hivi karibuni limekuwa ni jambo la kawaida sana kukuta washabiki wa hivi vyama viwili wakirushiana vijembe na wakati mwingine hata kutukanana na kuitana majina yasio pendeza.
Hivi vyama viwili, kwa uoni wangu, vina wanachama wa aina mbali mbali, na haswa dini hizi mbili, Uislam na Ukikristo na pia wasio na imani za hizi dini mbili, vile vile wana wanachama wa kutoka makabila mbali mbali ya Tanzania.
Dini na Siasa ni sehemu ya maisha, mang'amuzi na maendeleo endelevu ya mwanadamu sanjari na haki zake zote msingi. Kashfa za kisiasa na kidini ni uvunjifu wa haki msingi za binadamu zinazohatarisha pia mafao ya wengi ndani ya jamii. JF tunao wajibu wa kulinda na kudumisha haki msingi za Kisiasa na Kidini, kwani hizi pia ni sehemu ya haki za kila mmoja wetu.
Mimi ambaye ni Muislam, na si mfuasi wa chama chochote kile cha kisiasa, nikisoma bandiko la mfuasi wa Chadema au CCM, na katika hoja zake akausema vibaya Uislam kwa ubaya bila ya ushahidi, kwa kuwa tu muhusika ni Muislam, atakuwa ajanitendea haki mimi ambaye ni mfuasi wa imani hiyo ya Kiislam. Alikadharika pia kwa wale wanao amini Ukristo. Inanishangaza sana watu wanaposhindwa kumjadili mtu kama yeye bila ya kumuhusisha na imani yake. Hii yote ni kutokana na kutojua misingi ya majadiriano, na kukimbilia kujibu hoja hata pale unapokuwa huna la maana katika kuchangia hizo hoja.
Watanzania tuliipokea Demokrasia ya vyama vingi kwa moyo mkunjufu miaka mingi iliyopita, baada ya kuamua kuachana na ukiritimba wa chama kimoja tukilenga kupata fursa zaidi ya kuchagua viongozi tunaowataka. Hiyo ilikuwa hatua muhimu katika kuhakikisha kila mwananchi anashiriki kikamilifu kutoa ridhaa juu ya nani anaefaa kuongoza nchi.
Demokrasia ni neno pana sana, linaweza kutafsiriwa kwenye kanuni ya wengi wape au ikimaanisha kuwa watu wawe huru kujieleza au kuelezea hisia zao lakini kwa kutumia maneno yalio na adabu na nidhamu, bila ya kuvuka mipaka ya kisheria.
JF ni mkusanyiko wa watu wa aina mbalimbali, wanasiasa, na wasio wanasiasa, wenye imani za dini na wasio na imani za dini. Mkusanyiko huu, unahashiria kuwa JF ni tovuti baraza linalo kusanya watu wa aina mbali mbali na wenye mitazamo tofauti tofauti.
Kipindi JF ilipokuwa inaitwa jamboforums, tulishuhudia wanachama wake wakitoa na wakishindana kwa kuchangia hoja zenye nguvu. Hoja ambazo zilweza kuamsha hari ya msomaji kuchangamsha akili yake na kufanya utafiti kabla ya kuja kujibu hoja husika. Na hii ndio ikapelekea kuwa na kauri mbiu ya Where we dare To Talk Openly. Kauli hii haimaanishi kuwa watu waseme tu kila kitu kinachopita kwenye akili zao, bila ya kuchunywa kwanza. Lakini hivi sasa tunashuhudia kila aina ya matusi na maneno yasio na maana kiasi ya kutia shaka akili ya wachangiaji wengi.
Ndani ya JF, kuna viongozi wa vyama hivyo viwili, nikimaanisha CHADEMA Na CCM, kama hakuna viongozi wa hivyo vyama basi kuna makada wake, ambao wanajulikana kwa majina yao, lakini cha ajabu sijawasikia wakikemea huu upuuzi unao endelea kila kukicha. Kwangu mimi inanipelekea kuamini kuwa wanayapenda haya yanayo endelea humu, kwa sababu ndio sera za vyama vyao. Na kama wanayakubali haya yaendelee humu ndani ya JF, yatashindikana vipi yasitokee huko nje kwenye utendaji!?
Tusifikie mahala ikaonekana kuwa JF inapendelea matakwa ya watu au kikundi fulani cha watu. Na hii ni hatari sana kwani itasababisha chuki kati ya wanaJF, wakati sote tu Watanzania na tunaitakia amani na utulivu nchi yetu. Mimi nilitegemea wenye kutete vyama vyao, wangekuwa wanatetea kwa kutumia sera za vyama vyao na si kwa kutumia matusi.
Teteeni sera zenu na kisha iachwe ridhaa ya wasomaji. Vitisho, ubabe, kashfa, matusi, upendeleo na kuitana majina yasio pendeza vitavuruga amani ndani ya JF...!
Najuwa kuwa kuna watu wanajiona wao wana haki ya kutukana, kukashifu na hata kuwaita wengine majina yasio pendeza, hii yote ni kuishiwa kwa hoja za msingi na kutokuwa na uvumilivu. Kwani kuna ulazima gani kama umeishiwa hoja, utukane ili uonekane kuwa umeshinda? Tuache huu ubalakala wa kujitia kujua sana.