CHADEMA mwendo mdundo

CHADEMA kiko salama, wanaCHADEMA tusonge mbele

TAARIFA KWA UMMA

  • Hakuna kiongozi aliyefukuzwa uanachama
  • Zitto Kabwe hakusudii kuhama CHADEMA
  • Mbowe, Dr Slaa wasichafuliwe wala kuchonganishwa na wanachama
  • Kuchafuliwa CHADEMA na viongozi wake ni proganda kuelekea 2010

UTANGULIZI

Katika siku za karibuni pamekuwepo na habari kwenye vyombo kadhaa vya habari zenye kupotosha hali ya mambo ndani ya chama baada ya uamuzi wa Katibu Mkuu wa chama - Dr Wilbroad Slaa kutengua uteuzi wa maafisa wawili wa chama tarehe 10 Novemba, 2009.

Natoa taarifa rasmi kwa umma kwamba CHADEMA kiko salama wanaCHADEMA tusonge mbele. Hakuna kiongozi aliyefukuzwa uanachama. Zitto Kabwe hakusudii kuhama CHADEMA kama alivyokwisha eleza katika mahojiano ya karibuni na wala chama hakiko mbioni kumfukuza. Mbowe, Dr Slaa wasichafuliwe wala kuchonganishwa. Kuchafuliwa CHADEMA na viongozi wake ni propaganda kuelekea uchaguzi wa 2010.

Nalazimika kutoa taarifa hii ya ufafanuzi kutokana na mfululizo wa habari zenye kujaribu kuhusisha maamuzi hayo na uchaguzi wa ndani ya chama wa mwezi Septemba, 2009. Aidha pamekuwepo na mfululizo wa habari zinazohusisha kutenguliwa maofisa hao na kile kinachoitwa msimamo wao hususani katika kuibua masuala mbalimbali yanayohusu matumizi ya fedha ndani ya chama. Mfululizo huo wa propaganda chafu katika siku za karibuni umechangiwa na tuhuma za uzushi zilizotolewa na David Kafulila katika Mkutano wake na waandishi wa habari wa tarehe 18 Novemba, 2009 na Danda Juju Martin wa tarehe 27 Novemba, 2009.

Napenda ieleweke kwa ujumla kwamba kutenguliwa kwao uteuzi wao hakukutokana na sababu zozote kati ya hizo bali ulifanywa na katibu mkuu wa chama kwa kuiuka kwao kanuni, maadili na itifaki ya chama katika utendaji wao wakiwa maofisa.

Vijana hao wawili hawajawahi kutoa madai wanayoyatoa sasa katika kikao chochote cha sekretariati ya chama; kwa mantiki hiyo hawajawahi pia kuhojiwa wakati wowote kutokana na matamshi yanayohusiana na masuala hayo waliyoyasema. Tuhuma hizo za uongo dhidi ya chama na viongozi wake wamezitoa baada ya kutenguliwa uteuzi wao.

Izingatiwe kuwa kikatiba, maofisa wa chama si wajumbe wa sekretariati ya chama wala kamati kuu ya chama. Wajumbe kutoka idara walizokuwa wao ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Erasto Tumbo na Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema ambao pamoja na watendaji wengine wanaendelea na utumishi wao katika makao makuu ya chama kama kawaida. Sekretariati ya chama ni Katibu Mkuu na wakurugenzi wa chama; hata hivyo wamekuwa wakialikwa katika baadhi ya vikao na hawajawi kuhoji kuhusu masuala hayo wanayoyasema sasa.

UFAFANUZI KUHUSU TUHUMA ZILIZOTOLEWA NA VIJANA WAWILI WALIOJITOA CHADEMA

Lakini kutokana na tuhuma hizi kutolewa hivi sasa na kurudiwa mara kwa mara, na zimetolewa tena kwenye magazeti mbalimbali leo 28 Novemba, 2009 natoa taarifa hii kwa umma kwa niaba ya Katibu Mkuu, kuzijibu tuhuma husika ili watanzania wasiendelee kupotoshwa na propaganda zenye kuichafua CHADEMA na viongozi wake tunapoelekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2010:

Danda Juju amedai kuwa amefukuzwa uanachama kwa siri, tuhuma ambayo ilitolewa pia na Kafulila jambo ambalo si la kweli; kwani hata barua zao walizozitoa zinaeleza wazi kuwa wametenguliwa nafasi zao za uafisa wa chama. Katibu Mkuu wa Chama aliwaeleza wazi kuwa wangeendelea kuwa wanachama, na kwamba akawahimiza waendelee kuwa wanachama waadilifu. Kwa sababu wanazozijua wao, wameamua kujitoa uanachama ambayo ni haki yao; lakini upotoshaji wao na kurudiwa rudiwa kwa hoja hii ya kwamba “CHADEMA wanafukuzana”, ni propaganda za kufanya watanzania waamini kwamba CHADEMA hakina demokrasia. Vijana hawa wawakuwahi kuvuliwa uanachama wala kuzuiwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi katika chama.

Danda Juju amedai kuwa imepangwa Zitto afukuzwe uanachama, na kwamba kutenguliwa uafisa wa chama kumetokana na alichokiita kuwa chuki dhidi ya kundi lake kulikotokana na uchaguzi wa ndani ya chama. Kauli ya namna hii ya kueneza propaganda kwamba kuna makundi yanayoendelea ndani ya chama kutokana na uchaguzi iliwahi pia kutolewa na David Kafulila. Ukweli ni kuwa CHADEMA haijawahi kujadili wala kufikiria kumfukuza Zitto uanachama; na viongozi wa chama wamesisitiza hivi karibuni kuwa hakuna mvutano wala makundi ndani ya chama hivi sasa kwa kile kinachodaiwa kuwa mpasuko kutokana na uchaguzi wa ndani ya chama. Kama ingekuwa ni masuala ya uchaguzi wa ndani ya chama, mbona hakutenguliwa uteuzi wake Kaimu Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi, Msafiri Mtemelwa ambaye inaeleweka wazi kuwa katika uchaguzi wa ndani ya chama alikuwa mstari wa mbele katika michakato iliyohusiana na kusudio la Zitto la kugombea uenyekiti wa chama? Mwenyekiti Mbowe, Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, mmoja wa waasisi chama Mzee Edwin Mtei na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mama Shida Salum wote kwa nyakati tofauti wametoa kauli za kupinga kuwepo kwa makundi katika chama baada ya uchaguzi wa ndani ya chama. Ni muhimu umma ukaelewa kwamba kauli kama hizi zina mwelekeo wa kujaribu kuwachonganisha viongozi wa chama na wanachama na kuzua mgogoro ama mpasuko ndani ya chama. Nichukue fursa hii kurudia mwito uliotolewa na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kuwa watulivu katika kipindi hiki.

Danda Juju amedai ametoa tuhuma za juu juu na za ujumla kuwa kuna ufisadi wa ruzuku ndani ya chama na kwamba kuna ukiritimba katika kutia saini na matumizi ya ndani ya chama. Madai kama haya yaliwahi kutolewa pia na David Kafulila aliyetuhumu kuwa kuna kuyeyuka kwa milioni 35 ndani ya chama mwezi Disemba 2008 na kwamba Mbowe na Komu wamehodhi mamlaka ya kutia saini benki. Na kwa ujumla kutaka hesabu za CHADEMA zikaguliwe na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG). Ni muhimu wakina Danda na yoyote anayetoa tuhuma juu ya CHADEMA ama viongozi wake, akaeleza wazi tuhuma hizo; kushindwa kutoa tuhuma zenye maelezo na vielelezo ni ishara ya kutoa tuhuma hizo kama sehemu ya propaganda za kuchafua chama na viongozi wake. Ieleweke kuwa hakuna milioni 35 za chama zilizoyeyuka mwezi Disemba 2008; matumizi ya CHADEMA yamekuwa yakipangwa na vikao vya chama, na taarifa za fedha zimekuwa zikitolewa kwa kamati kuu ya chama ikiwemo hiyo ya matumizi ya ruzuku ya mwezi Disemba 2008. Ieleweke kuwa makusanyo na matumizi ya fedha za CHADEMA yanafanywa na vikao halali vyama chama, na si uamuzi wa mtu mmoja yoyote iwe ni Mbowe ama mkurugenzi wa Fedha, Antoni Komu. Wanaotia saini, ambao ni pamoja na Mwenyekiti wa chama, Mwenyekiti wa baraza la wadhamini, Katibu mkuu na Mkurugenzi wa fedha wanafanya hivyo kwa nafasi zao kwa mujibu wa maazimio ya vikao vya juu vya chama na taratibu za fedha zilizowekwa; hawakujiteua wenyewe. Pia zipo akaunti maalum ambazo watia saini ni sisi viongozi wengine wa ngazi mbalimbali kutokana na aina ya akaunti na sababu ya kufunguliwa kwake kwa mujibu wa maazimio ya vikao vya chama. Mfumo umewekwa udhibiti (check and balance) wa namna mbalimbali, na CHADEMA kama taasisi inayokua kwa kasi ina utamaduni wa kuendelea kuboresha mifumo yake kwa kadiri ya wakati na maamuzi ya vikao. CHADEMA iko tayari kukaguliwa na mkaguzi mkuu wa serikali, Baraza kuu la Chama liliweka msimamo huu wa kuendeleza uwazi katika matumizi ya fedha za ruzuku ya kodi ya wananchi na hata michango ya wapenzi na wanachama toka mwaka 2006 tulipoweka wazi matumizi ya fedha zetu za uchaguzi za mwaka 2005. Kadhalika mchango huo ulitolewa na Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu wetu bungeni mwaka 2009 na kuingia katika sheria ya vyama vya siasa. Ikumbukwe kwamba hata kabla ya kuwepo kwa sheria husika kwa miaka mbalimbali mahesabu ya mwaka ya CHADEMA yamekuwa yakikaguliwa na wakaguzi na kupata hati safi. Aidha taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kwa serikali kupitia kwa Msajili wa vyama vya siasa. CHADEMA tunamkaribisha CAG kufanya ukaguzi wa mahesabu yetu kwa mujibu wa sheria na taratibu. Kati ya vyama vikuu vitatu vya siasa nchini, CHADEMA ndio yenye kupata ruzuku kiwango kidogo zaidi, CCM inapata zaidi ya milioni 2000 (bilioni mbili) kwa mwezi. CHADEMA imekuwa mstari wa mbele kuzungumzia hadharani mapato na matumizi yake, vyama vingine navyo vifanye hivyo.

Danda Juju na hata David Kafulila wameeleza Mbowe na Komu wamefungua akaunti kwa siri na kujiteua kuwa watia saini wa akaunti ya chama ya mfuko wa kuchangia chama kwa njia ya SMS. Ifahamike kuwa CHADEMA haijawahi kufungua akaunti maalum ya kupokea michango ya wachangiaji kwa njia ya SMS, bali akaunti zilizopo ni za kawaida za chama zilizofunguliwa kwa maazimio ya vikao vya kikatiba vya chama. Propaganda kama hizi zinalenga kupunguza imani ya wananchi ya kuichangia na kuingua mkono chini ya mpango huu ambao ni ubunifu wa pekee tofauti na vyama vyote Tanzania. Baada ya ufafanuzi huu nachukua fursa hii kuwaomba wote wenye kupenda demokrasia na maendeleo, waendelee kuchangia harakati za kupambana na ufisadi na kutetea rasilimali za taifa kwa kutuma neno CHADEMA kwenda namba 15710 kwa wateja wa Zain na Vodacom kwa sasa.

Danda Juju ametoa kauli kwamba mmiliki wa CHADEMA ni Freeman Mbowe na washirika wake, na kwamba mwanachama yoyote akitofautiana na mmiliki huyo anafukuzwa uanachama. Kauli hii ni dhihaka kwamba mamilioni ya watanzania wanachama na wapenzi wanaiunga mkono CHADEMA kwa hali na mali ndani na nje ya nchi yetu. Kauli inayokaribiana na hii ilitolewa na David Kafulila ya kuelezea kwamba CHADEMA inaendeshwa kidikteta na Mbowe na Dr Slaa. Kauli hizi ni matusi kwa wajumbe wa vikao vya juu vya chama kuanzia Kamati Kuu ya chama inayokutana kila baada ya miezi mitatu, Baraza Kuu la Chama ambalo limekuwa likikutana kila mwaka na Mkutano Mkuu wa chama ambao ndani ya kipindi cha miaka mitano pekee umefanyika mara tatu; mwaka 2005, 2006 na 2009 vikao vinavyohusisha wajumbe toka kona zote za Tanzania. Ni vikao hivi vya kikatiba ndivyo vimekuwa vikifanya maamuzi kuhusu mwelekeo wa chama; maamuzi ambayo leo vijana wawili waliojitoa na chama wanayabeza. Kauli kama hizi zinalenga kuwachafua viongozi wakuu wa chama waliochaguliwa na wanachama na kupunguza imani yao kwa umma; hata hivyo wajumbe wa chama wanaoshiriki vikao vya kimaamuzi wa chama wataendelea kuwa mashahidi wa namna viongozi hawa wakuu wa chama kwa kushirikiana na viongozi wenzao wameweza kuiongoza CHADEMA kidemokrasia kufikia kuwa chama mbadala na tumaini jipya la watanzania.

UFAFANUZI KUHUSU KUTENGULIWA UTEUZI WA MAOFISA WAWILI KATIKA KURUGENZI ZA CHAMA

Izingatiwe kuwa uamuzi wa kutengua uteuzi wa maafisa wao, uliofanywa na Katibu Mkuu akiwa ni mtendaji anayesimamia ajira za watumishi makao makuu ya chama ulitokana na kikao cha Sekretariati ya Kamati kuu ya chama cha tarehe 10 Novemba, 2009.

  • Izingatiwe kuwa sekretariati ya kamati kuu ya chama iliwaita kwa barua maofisa husika kujieleza kwenye kikao cha Kamati kuu ya chama kuhusu matamshi yao kwenye vyombo mbalimbali vya habari mwezi huu kuhusu vikao na viongozi wa chama.
  • Taarifa hizo kwenye vyombo vya habari zilipotosha si tu ajenda ya kikao hicho bali pia hata wajumbe walioshiriki kikao hicho. Umekuwa ni utaratibu wa CHADEMA kufanya vikao vya namna hiyo na kuandaa mipango mbalimbali inayopitishwa na vikao vya juu vya chama. Kikao hicho cha mashauriano (consultative retreat) kilitathmini utelekezaji wa mipango chama na kupanga mikakati ya kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010. Mathalani wabunge waliotajwa kushiriki kikao hicho kilichofanyika mwanzoni mwa mwezi huu ni Halima Mdee, Maulidah Anna Komu na Lucy Owenya ambao ukweli ambao hawakuwepo kabisa kwenye kikao husika kutokana na kuwa safarini kwa majukumu mengine. Wabunge ambao walishiriki kikao hicho ni Arfi Said, Dr Wilbroad Slaa, Suzan Lyimo, Grace Kiwelu na Charles Mwera ambao wana nyadhifa mbalimbali katika chama.
  • Mathalani gazeti la Majira Novemba 8 na Mwananchi Novemba 9 yaliwanukuu maafisa hawa wakituhumu viongozi wakuu, wabunge na wakurugenzi kuwa wamefanya kikao Dodoma kisicho rasmi kisichotambulika ambacho kiliazimia kuwafukuza wao uanachama; masuala ambayo hayana ukweli wowote.
  • Baada ya mahojiano ya kina kati ya maofisa hao wawili ya zaidi ya masaa manne, sekretariati ya chama iliridhika kuwa walikiuka kanuni, maadili na itifaki ya chama katika utendaji wao kama ilivyo kwenye kifungu cha 10.1(i), (viii), (ix), (xi), (xii) na 10(2)(iv), (ix), (ix).
  • Kutokana na hayo, katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa akachukua uamuzi na kuwaandikia barua za tarehe 11 Novemba 2009 kila mmoja wao za kutengua uteuzi wao wa kuwa maofisa katika kurugenzi za chama.

HITIMISHO

Natoa rai kwa watanzania kusoma alama za nyakati tunapoelekea uchaguzi wa mwaka 2010. Upo mkakati ambao ulianza toka miaka kadhaa ya nyuma wa kuwachafua viongozi wakuu wa CHADEMA, kwa lengo la kupunguza imani ya Watanzania juu ya chama. CHADEMA ni chama kinachojiendesha kitaasisi, ndio maana kimekuwa kikivuka salama katika propaganda za namna hiyo. Toka Mbowe na Dr Slaa wachaguliwe kwa awamu ya kwanza kukiongoza CHADEMA, propaganda kama hizi zimekuwa zijitokeza kwa vipindi mbalimbali. Baada ya uchaguzi wa ndani ya chama wa mwaka 2004 alijitoa aliyekuwa Mweka Hazina Taifa Paul Kyara na kuanzisha SAU lakini CHADEMA ikasonga mbele na kuongeza idadi ya wabunge na madiwani uchaguzi wa 2005. Mwaka 2006 baada ya kuandikwa kwa katiba mpya ya chama na kuzinduliwa kwa chama upya, Makamu Mwenyekiti Aman Kaborou alijitoa kwenda CCM, propaganda zikaandikwa lakini CHADEMA kikasonga mbele salama. Mwaka 2007 mwezi mmoja tu kabla hatujatoa Orodha ya Mafisadi(list of shame) Septemba 15, Naibu Katibu Mkuu Shaibu Akwilombe alijitoa kwenda CCM; lakini CHADEMA ikasonga mbele na kumchagua Zitto Kabwe kuziba nafasi yake; proganda zikaendelezwa zaidi alipoteuliwa kamati ya madini kuwa viongozi wanavutana na chama kikatabiriwa kufa; lakini vikao vikakaa; chama kikasonga mbele salama. Mwaka 2008 alisimamishwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Chacha Wangwe (Apumzike kwa Amani), propaganda zikasambazwa. Hata baada ya kifo chake, viongozi wa CCM na waliotuhumiwa kwa ufisadi wakajaribu kutumia msiba wake kuchafua CHADEMA na viongozi wake. CHADEMA kwa mara nyingine ikapita salama na kushinda pia uchaguzi wa marudio katika Jimbo la Tarime. Mwezi Machi 2009, chama kikamundoa mjumbe wa Kamati kuu Mecky Mziray, propaganda zikafanywa, na wakati wa uchaguzi wa chama Septemba propaganda zikafanywa kuwa chama kitavunjika wakati huo; chama kikapita salama na kuchagua viongozi wake. Sasa, CCM na serikali yake wakiwa kati kati ya malumbano ya kufilisika kimaadili na kushindwa kuchukua hatua dhidi ya mfumo wa ufisadi tuliutaja kwa maelezo na vielelezo, ambao umefanya Watanzania waiamini CHADEMA katika kutetea rasilimali kwa sera mbadala tunapoelekea mwaka wa mabadiliko 2010; propaganda zinaendelezwa kwa kasi. Hivyo, kama ambavyo kwa miaka yote CHADEMA chini ya uongozi wa Mbowe, Dr Slaa wakishirikiana na viongozi wenzao wameweza kukivusha chama katika majaribu makubwa zaidi, ndivyo itavyoendelea kuwa salama mpaka kieleweke. Viongozi wa chama, kupitia vikao vya chama na mamlaka yaliyopo kwa mujibu wa katiba, hawatasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni, maadili na itifaki kwa yoyote na kupanga mikakati makini kwa lengo la kuendesha CHADEMA ikiwa mbadala kwa maneno na vitendo wa mfumo wa utawala ambao umetaasisisha ufisadi; umeiteka dola (institutional corruption and state capture) na kuweka mashakani mustabali mwema wa Taifa letu.

Limetolewa tarehe 28 Novemba 2009 na:

John Mnyika

Kaimu Katibu Mkuu
na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje

.
 
Alisema ndani ya Chadema kuna makundi mawili, kundi la Mbowe lenye maisha mazuri na magari ya kifahari na lile la Zitto lenye wanachama wanaomuunga mkono mwanasiasa huyo.

Kama kweli chadema kuna makundi mawili, lazima hili kundi linaloitwa la Zitto liondoke tena haraka. Kundi hilo ndo hili la akina Kufulila na Danda? guess uwezo wao.

Hili linaonekana ni kundi la CCM lenye lengo la kuua upinzani na siyo kujenga. Kama kweli Kufulila na Danda wanasema kweli kwanini walivumilia kukaa ktk chama? kwanini hawakuchukua hatua wakiwa ndani ya chama? kwanini bossi wao (Zitto kama wanavyodai) hakuwasaidia kutatua hayo matatizo ya chama?

Kama Zitto hayupo nyuma ya hawa ni wakati wake kujitokeza na kuwakana. Mwanahalisi waliandika wakimnuu mama Zitto akisema mwane hahusika na wala hana kundi. Zitto akadai ***** kalishwa maneno. Sasa Zitto tumweleweje?

Natambua kwamba Zitto yupo masomoni, lakini hili ni kubwa. Je Zitto unakundi lako ndani ya chadema? lengo la hilo kundi ni nini?

Na hili kundi la Mbowe ndo lipi? eti ndo wanaopanda magari ya kifahari kwani Zitto hana magari ya kifahari? Kundi la Mbowe ni akina nani?
 
magezi uko right kinoma haya ni mapambano ya madaraka na chadema wamefanya vizuri kuondoa makapi
 
wanaompinga Mbowe wanachokosea ni wanasema baada ya kutoka, naomba atokeee mmoja atoke bila kusema kitu jamani, nyie mnaotoka funikeni uchi wa chadema kaeni kimya, kutaneni na hao akina Mbowe wapeni live face to face wabadilike endeleeni na maisha yenu,HII YA KUSEMEA MAELEZO inanipa wasiwasi sana hamjui maana ya upinzani, hamsomi alama za nyakati,

tuko vitani ala!

I am happy siko peke yangu kuna semenya, MTM waberoya, pasco na wengine wote wenye mrengo wa kweli [hakuna cha kulia wala kushoto hapa!!!]
 
ZITTO TWAMBIE WEWE UNA KUNDI(kama yale ya mtandao??)tueleze ili tujue masilahi ya kundi lako na malengo yake ktk chadema isije ikawa yale ya waridi bin kabburu
 
danda ni kafulila type, afadhali madai ya kafulila yanasubstance japo uamuzi wa kujivua uanachama was a wrong move, na kuamua kudandia nccr, is another wrong move, sasa huyu danda yeye ni empty kabisa hoja zake hazina mashiko.

Hii hoja eti mkaguzi akague hesabu za chadema wakipata hati safi, yuko tayari kuchukuliwa hatua za kisheria, yaani chadema wamchukulie hatua yeye nkwa lipi?.

Kwa mujibu wa danda, hati safi ndio kipimo cha matumizi mazuri!. Hana habari kuna hati safi za matumizi ya mabovu ajabu na kuna hati chafu za matumizi safi na halali kabisa.

Hebu tusubiri tuone huyu atadandia jahazi gani ila kwa maoni yangu, jamaa ni finito, kwisha, hakuna kitu hapa!.

Kwa chadema, hizi ni hatua muhimu, lazima pumba zitoke ili ubaki mchele safi, vinginevyo mtajikuta mnakwenda kwenye uchaguzi mkidhani mna watu, kumbe ni makapi matupu.
mkuu ngumu kukuamini kwani wewe tayari unajulikana uko upande gani chadema.
Pili ajira yako iko mikononi mwa watuhumiwa sasa tunashindwa kukuelewa kama unalinda mkate wako au laa.
 
Kwa vyovyote vile mlengo wa chadema ni conservative. wanachadema wao hawakubali updates zozote. Lazima hawa ni ma conservatives. Sawa uko servative sio tatizo ,tatizo ni nini wana conserve? . Hilo ndo tatizo kuu
 
Masatu, na mimi umenitumbukiza Chadema?. Kuna dhana potofu iliyojengeka kuwa kama sio CCM, basi ni mpinzani. Kwa hali hali Papana Nyangumi wote mbona ndio wanaendesha chama chenu.

Kwa watu safi wa kiukweli ukweli, papa na nyangumi wote ni samaki na akioza mmoja, wote wameoza ndivyo tunavyokiona chama chenu huku tukikubali ukweli kuwa upinzani upo upo tuu, ni mchanga na haujakomaa, but one thing for sure, "ipo siku"
mkuu kwa vile wewe ajira yako iko mkononi mwa kiongozi wa Chadema mmoja wapo.vigumu sisi tusiamini kuwa wewe si Chadema.
tusaidie.
 
Tunafurahi kupata ufafanuzi makini kama huu.
I think its just a storm in a glass, itapita.
Nidhamu ktk chama ni muhimu sana.
Nawaombea busara na hekima zaidi katika kutekeleza malengo na majukumu ya chama mliyokabidhiwa mpaka kieleweke.
 
ZITTO TWAMBIE WEWE UNA KUNDI(kama yale ya mtandao??)tueleze ili tujue masilahi ya kundi lako na malengo yake ktk chadema isije ikawa yale ya waridi bin kabburu

haya ni maswali yanayochekesha, katika kundi la watu 10 tu lazima kutakuwa na mgawanyiko! ni hulka za binadamu.

Kiongozi mzuri Ni yule anayewajua watu wake, makundi yake na jinsi gani ya kudeal nayo---positively siyo kwa visasi wala kufukuzana

Kiongozi mzuri anapokea ushauri na maonyo, anaweka wazi kila kitu

Kiongozi mzuri anakuwa clean yeye kabla ya wengine na anasimama akitoa hukumu hali akijua mikono yake haina damu!

Tuhuma za Chadema hazijaanza leo wala jana, zinatakiwa kufanyiwa kazi ili CCM wakose cha kusema huko kwenye kupata kura.

mcheZo wa kupata kura is far more than just being truth.Inawezekana tuhuma za Mbowe ni uongo mtupu, lakini he has to find a way kurudisha trust hii kwa watu.

Juzi trust ilianza kurudi, ishu ya uchaguzi na kukataa kutangaza matokeo yeye Mbowe na Slaa imewaweka kwenye wakati mgumu kwa kila anAyehubiri demokrasia na sensible person sidhani walikuwa sahihi, na walitakiwa basi kutofanya uchaguzi kabisa! inaonyesha ni vipofu

Ishu ya Mtei kuingilia Chadema ndiyo anaharibu kabisa.

Mtei bila aibu alisema CCM wamepenyeza pesa kuharibu uchaguzi alikua akimsema Zitto,ambaye baadae akampa uongozi! hii ni aibu, mbaya zaidi anasemea kwenye vyombo vya habari

Hawa akina Zitto pamoja na kudai kuwa Chadema iko shwari anasema kwa kujikaza na kutaka kuokoa jahazi, ila I do believe hakuna amani mle ndani

kila atakachosema Zitto basi lazima wakiangalie mara mbili...si mzee alimsema vibaya??

Please CHADEMA tunataka kiwe chama ambacho ni ndoto ya kila mtoto na kijana, kuna watoto wanaota watakuja kuwa marais nchi hii , tuataka watoto wakikua wakisema wanaenda CHADEMA wakiwa viongozi wazuri wachaguliwe na kushika uongozi mbali mbali ndani ya Chadema! sasa hivi kwa walichokifanya hivi majuzi sidhani kama kuna mtanzania mwenye ndoto ya kufanya kitu nchi hii atawaza kutimiza ndoto yake kupitia Chadema!

Makosa yanaweza kurekebishika, tunatamani kuona Chadema wakisimama, wakikaa chini na kutatua matatizo yao, Jamni NCCR ilikuwa kiboko nchi hii....

Chadema kiwe cha watu wote, kiwe na mfumo tofauti na wa CCM.....

Zitto ni mtu mdogo sana, kinachomfanya kuwa unique ni kusimamia anachokiamini na kuabudu hicho! ndiyo siri yake kubwa na hii ndiyo silaha ya kiongozi yeyote.

Zitto ana uwezo wa kusema vitu ambavyo hata JK hawezi, na mawaziri ndio hao tunawaona, Zitto anapropose vitu mpaka mtu akiwa nje huko anasema huyu mtu ndiye rais au! Kumbe ni mtu wa kwaida tu

Nilicheka issue ya Umeme Zitto akisema basi anaonekana kama rais kasema..ANAPINGWAAAAAAAAAAAA.whi is this guy, mawazo yake tu jamani mtoane macho. wabunge wengine 300 na mawaziri kimya!!

watu wa aina ya Zitto ni asset kwa chama, sadly, wengi wanachukulia ni uadui kwa sababu hawataki mawazo mapya na direction mpya.

wengi tunameza tunayoyaamini, watu hata JF kuchangia anaogopa! wakati hatujuani, kisa akiisema Chadema basi yeye msaliti!

Ona Obama anavyohangaika na health issues, ona anavyopingwa ,IFIKIE HAPO JAMANI KUONA ALIYE KINYUME CHETU SI ADUI YETU PENGINE ANATUPA MWANGA wa kuangalia upande mwingine!

Debate zimeisha siku hizi si mashuleni wala publi debate na hili dio tunalolikosa..

Chadema inatakiwa iwe zaidi ya mtu mmoja mmoja

Kuuliza uliza na kumsema Zito Zito ni ishara TOSHA KUWA HIKI SI CHAMA ILA KIMEKAA KI-INDIVIDUALLY-KWA HIYO ZITO TISHIO.. that is the visible sign ndugu!
Otherwise who is Zito? Ukiondoa heshima yake ya ubunge ni mtu aliye muwazi

Chadema deal na matatizo yenu jamani, kisiri na kiheshima, mkiwa na lengo moja, hii tabia yenu ya kusingiziana na kusemana hadharani haiwasaidii

Ikibadilika Chadema na kuwa chama cha wote, patakuwa mahali pa kusemea kwa kila mtu....na hii itawapa nguvu zaidi.
 
Vipi unamaanisha serikali hii hii ya CCM ambayo kwako haiswihi? nilidhani kuna mambo ya accounting na financial management regulations ambazo ni muhimu kufanya kazi zikilindwa na kanuni na sheria ya vyama vya siasa!!

Sasa serikali ya CCM tena inayopingwa na chadema ndio isaidie hapo?hii imekaaje?

Naomba kuelewa zaidi
ipo dhana moja ambayo MTM na wazawa wengine tunaconfuse kwamba serikalini kuna CCM tupu, maana kama ni hivyo hata Jaji mkuu , mwanasheria Mkuu, mkuu wa Majeshi, IGP, Mabalozi basi wote wawe CCM....HII DHANA NI MFU. hakuna sheria ya chama kushika hatamu.
na dhana hii inawatafuna watanzania wengi wakidhani kua Raisi anateua wasaidizi wake kwa kuangalia kama ni mwana CCM ama laah, zipo nafasi naamini , wanateuliwa watu kwa uwezo wao sio kwa kadi zao.
Sasa dhana hii ya uwajibikaji watendaji wengi wamekua waoga kusimama wakidhani katibu mkuu wa CCM anauwezo wakumfuta kazi, wengi tunafikiri kuwa bado chama kimeshika hatamu.
utendaji wa kila siku wa Serikali lazima utenganishwe na utendaji wa kila siku wa Chama, hivyo kuwekwa kanuni ya matumizi maridhawa ya pesa za vyama vya siasa inaweza kuunganishwa na sheria iliyoanzisha vyama vya siasa,.
naikumbukwe hapa kua, Serikali inahaki yakuandaa Bill , nakuipeleka bungeni kwa hatua zaidi.
 
Danda wa Kanda!
Hii kama koffiii!:D

When party state matters, mix with politics?

Utashambuliwa vibaya tu!

When state matters mix with parties?

Utashambuliwa vibaya tu Danda wa kanda ni mwongo na hafai katika ulimwengu wa uenezaji habari!
Kula Breki!!!
 
CHADEMA kiko salama, wanaCHADEMA tusonge mbele

TAARIFA KWA UMMA

  • Hakuna kiongozi aliyefukuzwa uanachama
  • Zitto Kabwe hakusudii kuhama CHADEMA
  • Mbowe, Dr Slaa wasichafuliwe wala kuchonganishwa na wanachama
  • Kuchafuliwa CHADEMA na viongozi wake ni proganda kuelekea 2010
UTANGULIZI

Katika siku za karibuni pamekuwepo na habari kwenye vyombo kadhaa vya habari zenye kupotosha hali ya mambo ndani ya chama baada ya uamuzi wa Katibu Mkuu wa chama - Dr Wilbroad Slaa kutengua uteuzi wa maafisa wawili wa chama tarehe 10 Novemba, 2009.

Natoa taarifa rasmi kwa umma kwamba CHADEMA kiko salama wanaCHADEMA tusonge mbele. Hakuna kiongozi aliyefukuzwa uanachama. Zitto Kabwe hakusudii kuhama CHADEMA kama alivyokwisha eleza katika mahojiano ya karibuni na wala chama hakiko mbioni kumfukuza. Mbowe, Dr Slaa wasichafuliwe wala kuchonganishwa. Kuchafuliwa CHADEMA na viongozi wake ni propaganda kuelekea uchaguzi wa 2010.

Nalazimika kutoa taarifa hii ya ufafanuzi kutokana na mfululizo wa habari zenye kujaribu kuhusisha maamuzi hayo na uchaguzi wa ndani ya chama wa mwezi Septemba, 2009. Aidha pamekuwepo na mfululizo wa habari zinazohusisha kutenguliwa maofisa hao na kile kinachoitwa msimamo wao hususani katika kuibua masuala mbalimbali yanayohusu matumizi ya fedha ndani ya chama. Mfululizo huo wa propaganda chafu katika siku za karibuni umechangiwa na tuhuma za uzushi zilizotolewa na David Kafulila katika Mkutano wake na waandishi wa habari wa tarehe 18 Novemba, 2009 na Danda Juju Martin wa tarehe 27 Novemba, 2009.

Napenda ieleweke kwa ujumla kwamba kutenguliwa kwao uteuzi wao hakukutokana na sababu zozote kati ya hizo bali ulifanywa na katibu mkuu wa chama kwa kuiuka kwao kanuni, maadili na itifaki ya chama katika utendaji wao wakiwa maofisa.

Vijana hao wawili hawajawahi kutoa madai wanayoyatoa sasa katika kikao chochote cha sekretariati ya chama; kwa mantiki hiyo hawajawahi pia kuhojiwa wakati wowote kutokana na matamshi yanayohusiana na masuala hayo waliyoyasema. Tuhuma hizo za uongo dhidi ya chama na viongozi wake wamezitoa baada ya kutenguliwa uteuzi wao.

Izingatiwe kuwa kikatiba, maofisa wa chama si wajumbe wa sekretariati ya chama wala kamati kuu ya chama. Wajumbe kutoka idara walizokuwa wao ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Erasto Tumbo na Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema ambao pamoja na watendaji wengine wanaendelea na utumishi wao katika makao makuu ya chama kama kawaida. Sekretariati ya chama ni Katibu Mkuu na wakurugenzi wa chama; hata hivyo wamekuwa wakialikwa katika baadhi ya vikao na hawajawi kuhoji kuhusu masuala hayo wanayoyasema sasa.

UFAFANUZI KUHUSU TUHUMA ZILIZOTOLEWA NA VIJANA WAWILI WALIOJITOA CHADEMA

Lakini kutokana na tuhuma hizi kutolewa hivi sasa na kurudiwa mara kwa mara, na zimetolewa tena kwenye magazeti mbalimbali leo 28 Novemba, 2009 natoa taarifa hii kwa umma kwa niaba ya Katibu Mkuu, kuzijibu tuhuma husika ili watanzania wasiendelee kupotoshwa na propaganda zenye kuichafua CHADEMA na viongozi wake tunapoelekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2010:

Danda Juju amedai kuwa amefukuzwa uanachama kwa siri, tuhuma ambayo ilitolewa pia na Kafulila jambo ambalo si la kweli; kwani hata barua zao walizozitoa zinaeleza wazi kuwa wametenguliwa nafasi zao za uafisa wa chama. Katibu Mkuu wa Chama aliwaeleza wazi kuwa wangeendelea kuwa wanachama, na kwamba akawahimiza waendelee kuwa wanachama waadilifu. Kwa sababu wanazozijua wao, wameamua kujitoa uanachama ambayo ni haki yao; lakini upotoshaji wao na kurudiwa rudiwa kwa hoja hii ya kwamba "CHADEMA wanafukuzana", ni propaganda za kufanya watanzania waamini kwamba CHADEMA hakina demokrasia. Vijana hawa wawakuwahi kuvuliwa uanachama wala kuzuiwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi katika chama.

Danda Juju amedai kuwa imepangwa Zitto afukuzwe uanachama, na kwamba kutenguliwa uafisa wa chama kumetokana na alichokiita kuwa chuki dhidi ya kundi lake kulikotokana na uchaguzi wa ndani ya chama. Kauli ya namna hii ya kueneza propaganda kwamba kuna makundi yanayoendelea ndani ya chama kutokana na uchaguzi iliwahi pia kutolewa na David Kafulila. Ukweli ni kuwa CHADEMA haijawahi kujadili wala kufikiria kumfukuza Zitto uanachama; na viongozi wa chama wamesisitiza hivi karibuni kuwa hakuna mvutano wala makundi ndani ya chama hivi sasa kwa kile kinachodaiwa kuwa mpasuko kutokana na uchaguzi wa ndani ya chama. Kama ingekuwa ni masuala ya uchaguzi wa ndani ya chama, mbona hakutenguliwa uteuzi wake Kaimu Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi, Msafiri Mtemelwa ambaye inaeleweka wazi kuwa katika uchaguzi wa ndani ya chama alikuwa mstari wa mbele katika michakato iliyohusiana na kusudio la Zitto la kugombea uenyekiti wa chama? Mwenyekiti Mbowe, Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, mmoja wa waasisi chama Mzee Edwin Mtei na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mama Shida Salum wote kwa nyakati tofauti wametoa kauli za kupinga kuwepo kwa makundi katika chama baada ya uchaguzi wa ndani ya chama. Ni muhimu umma ukaelewa kwamba kauli kama hizi zina mwelekeo wa kujaribu kuwachonganisha viongozi wa chama na wanachama na kuzua mgogoro ama mpasuko ndani ya chama. Nichukue fursa hii kurudia mwito uliotolewa na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kuwa watulivu katika kipindi hiki.

Danda Juju amedai ametoa tuhuma za juu juu na za ujumla kuwa kuna ufisadi wa ruzuku ndani ya chama na kwamba kuna ukiritimba katika kutia saini na matumizi ya ndani ya chama. Madai kama haya yaliwahi kutolewa pia na David Kafulila aliyetuhumu kuwa kuna kuyeyuka kwa milioni 35 ndani ya chama mwezi Disemba 2008 na kwamba Mbowe na Komu wamehodhi mamlaka ya kutia saini benki. Na kwa ujumla kutaka hesabu za CHADEMA zikaguliwe na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG). Ni muhimu wakina Danda na yoyote anayetoa tuhuma juu ya CHADEMA ama viongozi wake, akaeleza wazi tuhuma hizo; kushindwa kutoa tuhuma zenye maelezo na vielelezo ni ishara ya kutoa tuhuma hizo kama sehemu ya propaganda za kuchafua chama na viongozi wake. Ieleweke kuwa hakuna milioni 35 za chama zilizoyeyuka mwezi Disemba 2008; matumizi ya CHADEMA yamekuwa yakipangwa na vikao vya chama, na taarifa za fedha zimekuwa zikitolewa kwa kamati kuu ya chama ikiwemo hiyo ya matumizi ya ruzuku ya mwezi Disemba 2008. Ieleweke kuwa makusanyo na matumizi ya fedha za CHADEMA yanafanywa na vikao halali vyama chama, na si uamuzi wa mtu mmoja yoyote iwe ni Mbowe ama mkurugenzi wa Fedha, Antoni Komu. Wanaotia saini, ambao ni pamoja na Mwenyekiti wa chama, Mwenyekiti wa baraza la wadhamini, Katibu mkuu na Mkurugenzi wa fedha wanafanya hivyo kwa nafasi zao kwa mujibu wa maazimio ya vikao vya juu vya chama na taratibu za fedha zilizowekwa; hawakujiteua wenyewe. Pia zipo akaunti maalum ambazo watia saini ni sisi viongozi wengine wa ngazi mbalimbali kutokana na aina ya akaunti na sababu ya kufunguliwa kwake kwa mujibu wa maazimio ya vikao vya chama. Mfumo umewekwa udhibiti (check and balance) wa namna mbalimbali, na CHADEMA kama taasisi inayokua kwa kasi ina utamaduni wa kuendelea kuboresha mifumo yake kwa kadiri ya wakati na maamuzi ya vikao. CHADEMA iko tayari kukaguliwa na mkaguzi mkuu wa serikali, Baraza kuu la Chama liliweka msimamo huu wa kuendeleza uwazi katika matumizi ya fedha za ruzuku ya kodi ya wananchi na hata michango ya wapenzi na wanachama toka mwaka 2006 tulipoweka wazi matumizi ya fedha zetu za uchaguzi za mwaka 2005. Kadhalika mchango huo ulitolewa na Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu wetu bungeni mwaka 2009 na kuingia katika sheria ya vyama vya siasa. Ikumbukwe kwamba hata kabla ya kuwepo kwa sheria husika kwa miaka mbalimbali mahesabu ya mwaka ya CHADEMA yamekuwa yakikaguliwa na wakaguzi na kupata hati safi. Aidha taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kwa serikali kupitia kwa Msajili wa vyama vya siasa. CHADEMA tunamkaribisha CAG kufanya ukaguzi wa mahesabu yetu kwa mujibu wa sheria na taratibu. Kati ya vyama vikuu vitatu vya siasa nchini, CHADEMA ndio yenye kupata ruzuku kiwango kidogo zaidi, CCM inapata zaidi ya milioni 2000 (bilioni mbili) kwa mwezi. CHADEMA imekuwa mstari wa mbele kuzungumzia hadharani mapato na matumizi yake, vyama vingine navyo vifanye hivyo.

Limetolewa tarehe 28 Novemba 2009 na:

John Mnyika

Kaimu Katibu Mkuu
na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje

.
kama tuhuma za uongo wapelekeni mahakamani basi kwani wanawachafulia sana.kila siku hapa tunasema mafisadi wanaotajwa kama tuhuma ni za uongo waende mahakamani sasa leo swala liko kwenu chadema onyesheni mfano kwa kumpeleka huyu kijana mahakamani kwa kutoa tuhuma za uongo kuhusu ufujaji wa pesa ndani ya chama chenu,

tumechoka watukutupiana maneno kila siku kama swala uongo mnaweza kumshitaki na hapo mwenye nguvu ya ushaidi ndio atapona.lakini hayo mambo yakutupiana maandishi na maneno kila siku hayatupeleki popote.
 
Jahazi linazama hilo jamani nyie kaeni na ubishi wenu mficha ugonjwa mauti humfichua....
Masatu Tambua kua hakuna taasisi isiokua na migogoro, tatizo ni namna gani unayatatua matatizo yako, hii ndio inafanya CCM waiogope CHADEMA, maana nidhamu na utii kwa chama ni dira yao, cheo na umaarufu wako sio kinga wakati unapofanya madudu yakijinga, CCM wanaogopana, hakuna wakumfuta kazi mwenzie,, hakunawakutunza nidhamu ndani ya Chama, vurugu tupu,hawaaminiani wenyewe kwa wenyewe,,,.......CHADEMA inazuia chama kufika huko, wanaziba ufa kabla ya kujenga ukuta.
 
Jahazi linazama hilo jamani nyie kaeni na ubishi wenu mficha ugonjwa mauti humfichua....

Hakizami kitu, na hahami mtu!

We Masatu endelea kuchukua chako mapema huko uliko, lakini siku zenu zinahesabika!
 
kama tuhuma za uongo wapelekeni mahakamani basi kwani wanachafulia sana.kila siku hapa tunasema mafisadi wanaotajwa kama tuhuma ni za uongo waende mahakamani sasa leo swala liko kwenu chadema onyesheni mfano kwa kumpeleka huyu kijana mahakamani kwa kutoa tuhuma za uongo kuhusu ufujaji wa pesa ndani ya chama chenu,

tumechoka watukutupiana maneno kila siku kama swala uongo mnaweza kumshitaki na hapo mwenye nguvu ya ushaidi ndio atapona.lakini hayo mambo yakutupiana maandishi na maneno kila siku hayatupeleki popote.
tutapima ushauri wako,lakini siasa haiko kiivyo sana, yuko wapi mtikila na sera ya kukimbilia mahakamani, tutaangalia athari zake kwa chama, maana siasa hufanywa mbele za umma wa wapiga kura, wala si mbele ya hakimu mkazi.
 
kwahio na wale wanao toa tuhuma kwa mafisadi hawana haja ya kuwachukulia hatua kwa vile siasa haiko kiivyo sana? mie naona tuhuma za mbowe kufuja mil 35 ni nzito sana ukiangalia wananchi wengi wana moyo na chadema sasa kupatikana tuhuma kama hizi inatufanya tuone mambo ni yale yale kote kote.
 
Haya mambo hakuna mvutano, hakuna vurugu, hakuna... hata sura-ya-kwanza,hakuna!

take it or leave it!

Kuna umuhimu wa Serikali na Vyama vyote Tanzania vinavyohusika katika maamuzi ya "Wananchi" kuzingatia kuwa "Wananchi kwanza"!

Nitasema tena na nitarudia=Tanzania ni ya "Wananchi" na siyo matabaka yanayo taka kujiweka eti kwa sababu kuna "ruksa" kwa sababu ya "Uzalendo" kwa sababu ya "uhuru wa uchumi" kwa sababu... eti sababu kuna kasi mpya!

Mbowe mwache ashambuliwe...! Who is he?
naye ameshambulia vipi manung'uniko ya wananchi?
 
Nawaonea huruma vijana wenzangu. Kuanza Siasa bila tabia njema ni aibu kubwa. Sasa ikigundulika hakuna Ufisadi hao vijana waliko kimbilia wataaibika na hawataaminika hata kidogo. Hata huko walikokwenda watakutana na hayo hayo.
Pili kuwa signatory haina maana ya kuwa Mwizi. Basi tuombe wakurugenzi wote wasiwe masignatory. mbona maofisini masignatory ni hao watoa majukumu mbona hatuogopi kama ni wezi.
 
Back
Top Bottom