CHADEMA MUST now Reform and Restructure!

CCM , CUF na CHADEMA vyote ni vyama vya siasa na vyote vinafanya madudu na kwa maendeleo ya nchi vyote vinatakiwa viliform lakini mbona wewe uko busy na chadema tu, nini hasa lengo lako?

Anakitakia mema chadema, angependa aone kinaendelea mbele
 
CCM , CUF na CHADEMA vyote ni vyama vya siasa na vyote vinafanya madudu na kwa maendeleo ya nchi vyote vinatakiwa viliform lakini mbona wewe uko busy na chadema tu, nini hasa lengo lako?

Shalom my dear brother,

Nimeshawatukana CCM sana na kuwagangamalia kina Kikwete na wenzake. nanyi mlinishangilia na hata kuvua mashati kama zulia kufurahia nilivyowashambulia CCM.

Leo hii nawageukieni nyinyi kwa kufata nyayo za upuuzi za CCM mnaanza kudai lengo langu nini? Kama leo tunathubutu kudai Rostam ni Fisadi kwa kuwa alidokoa fedha za BOT, je Chadema wanajiita Chama mbadala wanapoanza kufuja kodi kwa kufanya madudu kama haya mnataka tukae kimya?

You should thank me I am still wasting time offering you alternatives and can devote time to think outside the box on how Chadema can counter CCM!

May be I should heed to that methali ya kiswahili "sikio la kufa, halisikii dawa" and that will be the title of my new thread!
 
Mkuu kereng'ende umenena nadhani umempatia saana mchungaji, ameshindwa kujua ana nafasi ya kutoa ushauri sio maamuzi, pia anashindwa kuelewa kwamba mbowe anamchango mkubwa chadema ilipofikia, na pia anashindwa kuelewa kuwa hii ni institution ina dira na sera zake ina katiba na kanuni zake. Yapo mambo kadhaa ambayo mchungaji ametoa ushauri na tunaamini yatafanyiwa kazi lakini sikubaliani kabisa na wazo la mchungaji chadema kuungana na cuf,tlp,nccr, hao ni matawi ya ccm na tunafahamu hilo na hututaki hilo, kwani hajui kama cuf imeshinda zanzibar sif akauza ushindi? Mbowe, slaa, baregu, mnyika, zitto ni viongozi wa sasa wa chadema ikifika wakati muafaka kuwabadili tutafanya hivyo ila siyo kukurupuka. Tuna taarifa pia kwamba ccm na mafisadi watawatumia saana watu wengi kama mcgungaji huyu kuleta ufa chadema labda nimwambie kwamba chadema inaongozwa kisayansi siyo kama anavyodhani.

Mchungaji ombi langu kwako nadhani tumia uchungaji wako kuelimisha umma kupeleka elimu ya uraia usisubiri dr slaa au mbowe au willy, tumia kalamu yako kuelimisha umma huko uliko chadema inatoa dira watanzania tunawaunga mkono.

Inaonekana ama hujasoma sera ya chadema au umepewa mafao na mafisadi kuandika uliyoandika sera kuu ya chadema ni nguvu ya umma, ambapo unapata nguvu ya umma kwa kutumikia umma si vinginevyo ndio maana dr slaa na chadema wamekuwa wakisema afya, elimu, uwajibikaji na matumizi bora ya resilimali ndiyo expected results (key results areas) sasa sijui umekurupuka wapi unasema wabadili wabadili nini wewe mchungaji? Kama umechakachuliwa tulia usilete sumu jamvini na chadema

mwisho asante wanajamii kwa uzalendo tunaouonesha na kuendeleza vita hii, mapambano haya si ya chadema ni mapambano kati ya udhalimu wa mafisadi, mfumo kandamizi wa ccm na unyonyaji dhidi ya uzalendo wa kweli
 
Chadema will never win presidency over 20 years due to lack of civil education to Tanzanians. We cannot blame these oppostion parties, the blame should go straight to the ruling party and our Univerity students. We had higher anticipation that these so called students will challenge status quo, but we have seen how they discourage step taken by opposition to boost democracy. They criticize Chadema and equate it with "Osama". I want the president to tell people that opposition is healthy for our democracy and it is not source of chaos. Peace no hate.
 
Nikiwa nimekaa chini kutafakari ni kwa nini katika nafasi 23 za Chadema za wabunge wa kuteuliwa hawakuteua wawakilishi kule Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pemba, Tanga, Dodoma, Pwani, Tabora na kuongeza kule Iringa, Mbeya, Arusha, Rukwa na Mara, leo tunasikia kauli za chapati maji, kudai walinukuliwa isivyo kuhusu kutomtambua Kikwete kama Rais.

Hivyo swali langu kwenu wana Chadema, bado mnapingana nami kuwa hamuhitaji uongozi mpya ikiwa tayari kuna pande tatu zinavutana; Zitto, Freeman Mbowe na Dr. Slaa kwenye hili jambo moja la kuyakubali matokeo ya urais?

So take a minute again and think of what I was trying to relate to indirectly and assess the last 120 hours of life of Chadema!

chama kina grow in stages, wakati kinaenda sehemu nyingine kinatakiwa kihakikishe ile strong base yake ina remain intact na pia wakati wana grow lazima wawe realistic, ni kama biashara tu inavyokuwa.

kabla ya kufikiria jinsi gani utatoboa mikoa kama ya pemba na dodoma, lazima uangalie mikoa ambayo ni rahisi kupokea mabadiliko. hii mikoa ikipokea mabadiliko kwa kishindo ndio waje kuanagalia mikoa kama dodoma
 
CHADEMA kimekubalika ZAIDI kwa wananchi kwa sababu ya kutetea maslahi ya taifa kupitia wabunge wake katika bunge lililopita.
Wananchi wanavutiwa na kiongozi anayetetea maslahi yao na wala siyo jina la chama.
Ili chama kipendwe lazima viongozi wao wajitoe mhanga kutetea maslahi ya walio wengi.
Mifano ni mingi ( Nyerere, Sokoine, Mrema, Slaa na wengine wengi).
Ubunifu wa viongozi wakiongozwa na Mbowe, ukisaidiwa na hoja za wabunge wake katika bunge lililopita ndivyo vimefanya CHADEMA ifike hapo ilipo leo. ( Ukiona Vyaelea ujue Vimeundwa).
Ni muhimu kusonga mbele kwa kutumia mbinu hiyo hiyo ya kutetea maslahi ya taifa badala ya maslahi ya kundi dogo huku tahadhari ikichukuliwa dhidi ya wachumia tumbo waliojiunga na watakaojiunga baada ya kuona dalili za mafanikio.
Chama siyo kuwa na wabunge na propaganda tu, idara ya usalama na ujasusi ni muhimu kwa wakati huu kuliko wakati mwingine wote kwa CHADEMA!
 
ccm na mafisadi watawatumia saana watu wengi kama mcgungaji huyu kuleta ufa chadema
Mchungaji ombi langu kwako nadhani tumia uchungaji wako kuelimisha umma kupeleka elimu ya uraia usisubiri dr slaa au mbowe au willy, tumia kalamu yako kuelimisha umma huko uliko chadema inatoa dira watanzania tunawaunga mkono.

Tafadhali huyu sio mchungaji anatumia tu neno Rev na hajui maudhui yake . nawajua wachungaji, wamenilea na kunikuza, nawajua pia kauli zao na mienendo yao, kishoka sio mchungaji
 
Shalom my dear brother,

Nimeshawatukana CCM sana na kuwagangamalia kina Kikwete na wenzake. nanyi mlinishangilia na hata kuvua mashati kama zulia kufurahia nilivyowashambulia CCM.

LAW 3: CONCEAL YOUR INTENTIONS
Keep people of balance and in the dark by never revealing the purpose behind your actions. If they have no clue what you are up to they can not prepare for a defence. Guide them far enough down the wrong path, envelop them enough smoke, and by the time they realise your intentionns, it will be too late.

Leo hii nawageukieni nyinyi kwa kufata nyayo za upuuzi za CCM mnaanza kudai lengo langu nini? Kama leo tunathubutu kudai Rostam ni Fisadi kwa kuwa alidokoa fedha za BOT, je Chadema wanajiita Chama mbadala wanapoanza kufuja kodi kwa kufanya madudu kama haya mnataka tukae kimya?

LAW 4
Always say less than necessary

You should thank me I am still wasting time offering you alternatives and can devote time to think outside the box on how Chadema can counter CCM!
LAW 8. make other people coame to you -use bait if necessary

May be I should heed to that methali ya kiswahili "sikio la kufa, halisikii dawa" and that will be the title of my new thread!

Pose as friend and work as spy

Tumechoka na wajenzi huru!
 
Tafadhali huyu sio mchungaji anatumia tu neno Rev na hajui maudhui yake . nawajua wachungaji, wamenilea na kunikuza, nawajua pia kauli zao na mienendo yao, kishoka sio mchungaji

Unaacha kujibu hoja unaanza kunijadili..ndiyo malezi ya Wachungaji hayo!
 
Tukubaliane moja, Chadema can never be a radical party period, ndio maana kuna hii wishy washy tendency. Upande mmoja wanachukua millitant stance, wengine wanainua white flag. Then wapenzi na wanachama wanapotea njia, hawajui mweleko wa Chama, guess what is wrong with this picture? It is leadership.

Huwezi ukawa opposition wa CCM halafu ukafanana nao kila kitu!
 
Chadema will never win presidency over 20 years due to lack of civil education to Tanzanians. We cannot blame these oppostion parties, the blame should go straight to the ruling party and our Univerity students. We had higher anticipation that these so called students will challenge status quo, but we have seen how they discourage step taken by opposition to boost democracy. They criticize Chadema and equate it with "Osama". I want the president to tell people that opposition is healthy for our democracy and it is not source of chaos. Peace no hate.

Yale yule ya kudai tumeshindwa kuendelea sababu Nyerere alituletea ujamaa. When are we going to take ownership of our shortcomings?
 
Katika chama mtendaji mkuu ni katibu na si mwenyekiti. CHADEMA ilionekana kuwa ni chama cha upande wa kaskazini hususani Uchaggani na ndo maana unaona Mbowe hana mvuto maana fikra zetu hatujazifungua kuwaamini wachaga. Lakini unapoongelea People's power, Mavazi, ukunjaji ngumi na kurusha hewani, uwamasishaji unaogusa vijana, msimamo wa kukiweka chama sawa na kusimamia mipaka ya demokrasia, kutumia misingi ya utafiti kama kigezo cha maamuzi, matumizi ya helkopter hakika Mbowe amefanikiwa kwa hayo na anastahili haki yake. Tambua kuwa ametuhumiwa na baadhi ya viongozi wenzake kulazimisha Dr. Slaa kugombea Urais aliheshimu utafiti kuliko matakwa ya kidemokrasia ambayo kwa sasa inaweza kutumiwa vibaya kukivuruga chama kwa manufaa ya CCM. Ndugu yangu Rwakatare anafaa kuwa Katibu mwenezi. Lakini pia ujiulize kama si Mbowe kutuaminisha kuwa Dr. Slaa atashinda uchaguzi si tungebaki na mazoea yale kuwa Rais aliyepo anashinda kwa ulaini. Kwa upande wa vijana ambao ni wapiga kura wa 2015 wanapaswa kulelewa tu maana wapo ndani ya chama. Kama ukuwaone ndiyo waliyoshiriki kulinda na kusherekea ushindi. CCM ndo inakazi kubwa kwenye hili. Chama kipo ktk mpito na kinajipanga vyema kutumia ruzuku kujijenga upya. Chadema si copy maana nyuma ya pazia kuna kundi kubwa la maprofesa na wasomi wanaoratibu na kuweka mipango mizuri. Walituaidi kuwa na mikakati mizuri na tumeiona. Walipanga kuwa na idadi ya wabunge 70 tumeona kweli walidhamiria na sasa natambua wana mikakati bora hakika watatimiza na ndo maana sherehe yao haikuwa ya kujipongeza bali kutambua jukumu zito walilotwishwa wabunge na wananchi. Ni chama ambacho mbunge ni mbunge hakuna viti maalum. Mchango wa mbunge ktk kukijenga chama kwa kukidhi mahitaji ya jamii ndiyo nguzo ya ubunge
 
Ndugu Kichore,

Naomba unipe maoni yako ya ukweli bila ushabiki kuhusu uongozi wa Freeman katika suala hili la kujitoa wakati wa hotuba ya Kikwete Bungeni na kilichofuatia.
 
.

Mchungaji ombi langu kwako nadhani tumia uchungaji wako kuelimisha umma kupeleka elimu ya uraia usisubiri dr slaa au mbowe au willy, tumia kalamu yako kuelimisha umma huko uliko chadema inatoa dira watanzania tunawaunga mkono.

Denyo,

Nawahubirieni nyinyi Chadema, mnahitaji uongozi mpya na damu mpya kuwapeleka Kaanani. Mmembadilisha Musa tangu Mzee Mtei, Makani na sasa Freeman, mnamhitaji Joshua awafikishe mlikoahidiwa.
 
Big up Rev.
Kwa hakika wanatakiwa kutokuchelewa kufanya mabadiliko ambayo yata hakikisha 2014 kuna kuwa na madiwani by 75% Nchi nzima.Huu utakuwa mthihani wa Mock kwao.
Ila na tofautiana na wewe Dr.Slaa kuwa mwenyeketi,wamtafute mtu mwingine,Dr amefanya kazi nzuri akiwa kama Katibu na afaa miaka mitano ijayo aendelee kuwa katibu hadi 2015 baada ya hapo aweza pisha mtu mwingine.
 
Si Mbowe, Si Slaa, Chadema kimetegemea mtandao wao makanisa na hakitaenda zaidi ya maeneo ya ushawishi wa makanisa hayo, period!

Walio maofisini wanafanya kazi ya uwakala wa kanisa na chadema no wonder sasa hivi ofisi za serikali na mashirika zimegeuka vijiwe vya siasa! But its known na hakuna siri. Kuna vyuo vya makanisa sasa hivi ni kama matawi ya Chadema. Uchaguzi unakwisha anaetoa kauli ya kukubali matokeo ni Pengo!

Hakuna strategist awe Kitila au Baregu anayeweza kuwavua Chadema hiyo ngozi ya Ukrsito waliyojivika. Kamwe chadema hakitakuwa chama cha Kitaifa. Kinaweza kuwa kama chama-mwenza wake wa Ujerumani ambacho mnajua ni wakala wa kanisa.

This is a poison that have been coated with a chocolate materials to hide the contents, its small like a point of syringe but then its slowly grow and become bigger than a Baobab tree.

Watanzania wenzangu, lazima ifike sehemu tutathimini athari zilizo mbele kabla ya kutenda jambo lolote. Fikra hizi za udini na ukabila hazijengi, wala haziwaharibii CHADEMA peke yao, bali zinaathiri mifumo ya umoja wa nchi, na mihimili ya amani, utu wema na umoja wa kitaifa. Katu hakuna atakaye irudisha tena misingi hii hata kama Nyerere atafufuka leo hawezi tena. Aliweza once and once its broken it will never stand firm any more.

I hate you Nungux2, I hate JK for been waumini katika hili, for there I know its end will be bitter than anything under the sun.

Stop spreading these poison.
 
I am glad that I paid so little attention to good advice; had I abided by it I might have been saved from some of my most valuable mistakes.
- Edna St. Vincent Millay
Don't follow any advice, no matter how good, until you feel as deeply in your spirit as you think in your mind that the counsel is wise.
- Joan Rivers

Take it easy -- but take it.
- Woody Guthrie​
 
Wabz,

We unataka wengine tutafutiwe fatwa zaidi baada ya kudaiwa tumenunuliwa. Sasa angalia yaliyotokea Bagamoyo or wherever walipokuwa wamejificha.

Sasa ukiangalia ule mvutano unaosadikika uko kati wa rafiki yetu Zitto na mwenyekiti na uongozi wa Chadema, uamuzi wa Bagamoyo unampa Zitto point za bure!
 
Back
Top Bottom