CHADEMA MUST now Reform and Restructure!

Muundo wa CCM ni matokeo ya legacy ya utawala wa chama kimoja na mfumo wa kikomunisti wa chama kushika hatamu, ambapo chama kinakuwa juu ya serikali. Kwa hiyo chama, ili kudhibiti mwenendo wa serikali yake, kinajitanua na kuwa virtual state ambayo inafika kila mahali serikali inapofikia. Katika mazingira ya sasa hakuna chama chochote kitakachoweza kuiga hali hiyo. Hata CCM huo mnaouita mtandao uta-collapse siku watakapoondoka madarakani. Mtandao uta-collapse immediately. Hilo ndo limetokea kwa nchi zote za kiafrika zilizokuwa na mfumo wa chama kimoja.

Kuishauri Chadema kujenga mtandao wa kiCCM hadi vijijini, ni kuishauri Chadema ijiue kabla ya kufika popote. Mfumo huo wa mtandao mpana hauigiki na hautekelezeki. Mojawapo ya nightmare kubwa ya CCM leo, ni huo mtandao. Kusema ukweli huo mtandao ndo unaoiua CCM kwani kutokana na ugumu wa kuuunganisha na kuratibu shughuli zake, mapambano ya ndani kwa ndani ya mtandao ndo chanzo kikubwa cha kufa kwa vyama vya aina ya CCM. Vyama ndani ya chama vinakuwa vingi mno. Unahitaji viongozi wa aina ya Mwalimu kuiweka CCM hai kwa muda mrefu. In absence of that, Nikuhakikishie, CCM haiwezi kuendelea na muundo huo katika next 15 years na ikaendelea kutwaa madaraka.

Back to Chadema. Huwezi kutenganisha mafanikio ya Chadema ya sasa na uongozi uliopo madarakani. Halafu haya mawazo kuwa kiongozi akishaonekana star basi apewe uenyekiti siamini kama ni mawazo ya kimageuzi badala ya mawazo ya kimgando mgando, au ki CCM CCM. Jamani, Chama kinahitaji viongozi mahiri at all levels. Kila kiongozi ana karama na vipaji tofauti tofauti. Kiongozi kung'ara mahali au kwenye post fulani, ina maana kiongozi huyo anaimudu nafasi yake na yuko mahali sahihi. Sasa kumuona kiongozi kang'ara kwenye urais, unataka umpe uenyekiti wa chama. Hii ni harufu ya Chama kushika hatamu, kwamba kiongozi akishakuwa kwenye position ya kuchukua madaraka ya nchi, basi huyo huyo akabidhiwe na uenyekiti wa chama. Sikubaliani na hili. Slaa amekuwa mzuri sana kama katibu mkuu na naamini anafanya kazi nzuri sana kama katibu mkuu. Katibu mkuu ndo mtendaji, kwa hiyo ni nafasi inayohitaji mtu ambaye ni technocrat. Slaa ame-prove kuwa anaimudu hiyo nafasi, tena akipewa urais, atakuwa rais bora, rais mtendaji si rais wa kuagiza na kuomba mambo yafanyike!

Huwa najitahidi sana kukwepa kujadili majina ya watu, but katika mada hii mchungaji kanikoroga zaidi kwa kujadili watu. Chadema under Mbowe imekuwa fluid na very focused vile vile kimekuwa more strategic kiasi cha kushinda majimbo ambayo tunaweza kuyaita uti wa mgongo. Kwa nini tunarudha lawama zisizokuwa na msingi kwa Mbowe? 2005 Mbowe alisimama kama mgombea urais, kwa mara ya kwanza Chadema kilionekana katika stage ile na kupata kura kama alizopata Lipumba mwaka huu. Alichofanya mbowe ilikuwa ni u-pioneer, alisafisha njia. Tuliona creativity ya helkopta ilivyo-shake-up siasa za Tanzania. Pamoja na nguvu ya matumaini makubwa waliyokuwa nayo watanzania juu ya Kikwete kutokana na utawala uliopita wa Mkapa kuanza kuboa, bado Mbowe alifanya monumental task. Ni kazi hiyo iliyoanzisha hiki tunachokishuhudia leo kuwa wote tunakubali kuwa Slaa aliibiwa kura (ingawa bado hatujapata ushahidi kamili kutoka Chadema). Hatuwezi kuyatenganisha mafanikio hayo na Mbowe kama mwenyekiti wa Chama na Kama mgombea wa urais wa mwaka 2005. Momentum yake ndo tunayoiona leo.

Kwa ujumla, kuishauri timu inayoonesha mafanikio makubwa, ingawa ni gradual, eti ifanye major overhaul ni kutoelewa. Chadema ifanye major overhaul ili ipate nini? Tunataka waendelee kuwa focused. Leadership iliyopo ni competent engough. Mawakala wa mabadiliko wayapeleke mawazo yao kwa CCM. Mawakala wa mageuzi, tunataka Chadema hii hii iendelee na mbinu na mikakati hiyo hiyo. Wabunge 23, mwaka 2015, wakifika zaidi ya mia, CCM imekwisha!
 
Kipima Pembe,
Mkuu shukran sana yaani umefunga kazi isipokuwa tu pale pa kusema Chadema ikifika viti 100.. hilo sijui labda CCM hii iwe imekufa kabla ya uchaguzi huo..
UCHAKACHUAJI - ni adui mkubwa wa demokrasia Tanzania.
 
this week kila kona kuna thread za kumshambulia mbowe
for the past 5 years hamna mtu aliyeshambuliwa chadema kama mbowe, ccm imeshambulia sana lakini amesimama strong.
ndiyo mbowe hana vyeti kama vya dr slaa au zitto na hichi ndio watu wengi mnachokisema lakini ufanisi wake wa kazi kama mwenyekiti ni first class.
mbowe alikubali kuacha ubunge kwa ajili akuze chama, amejitahidi kwa hali na mali.
hata leo hii mbowe na dr slaa, zitto na wengine wanafanya kazi pamoja as a team na kila mtu anapata air time chadema. mnyika anapata airtime, zito anapata airtime, slaa anapata airtime, lissu anapata airtime na wengine pia watapata wakati wao itakapofika.

mr mbowe keep up the good work, mwendo mdundo
 
Jasusi,

..binafsi ningependa Chadema wawe na viongozi wengi zaidi wa juu wanaoshughulika na siasa FULL TIME.

..wakati wengine wanakwazwa na Uchaga wa Mbowe, mimi nakwazwa na the fact kwamba huenda atakuwa na majukumu mengi mengine kama biashara zake na ubunge.

..kitu kingine ningependa Chadema wawe na kitengo cha RESEARCH kuwasaidia wabunge wao ktk kujenga hoja bungeni. hoja wanazojenga zisitegemee uchacharikaji wa mbunge husika bila kuongezewa uzito with research uliyofanywa na staffers.

..suala lingine ni VISIBILITY kama alivyolielekeza Zakumi. kama serikali inapitisha bajeti inayopunja fedha ktk miradi ya maendeleo ya mkoa kama Rukwa, basi Chadema wanapaswa kwenda kuzungumza na wananchi wa mkoa huo kuwaelezea kilichojiri bungeni.

..kuna wakati CCM ilituma mawaziri kwenda "kuwaeleza" wananchi kuhusu bajeti. ingependeza na Chadema nao wawe na utaratibu wa kwenda kuwaeleza wananchi mapungufu ya bajeti kila baada ya kipindi cha bunge.

..Chadema pia wawe efficient zaidi ktk kutoa habari zao. wakati wa uchaguzi CCM wali-dominate mno magazeti, radio stations, blogs, and tv. kunatakiwa kuwepo na mkakati wa ku-challenge CCM dominance ktk vyombo vya habari.

Kwenye post moja week hii nimechambua yakinifu kabisa suala la Kuwa na Startegy Department ( ambayo wewe umeita Research depertment). Nikasema ni wazi kabisa kutokana na ruzuku Chadema sasa inaweza kuajiri watu kadhaa kuwa full time employees, na nikaandika umuhimu wa KITILA kuwa kiongozi wa kitengo hichi na kuacha kazi ya uadhiri pale chuo. Nikaeleza kwa mapana kabisa kwamba
Chadema sasa haiwezi kukua tena kwa kupitia mabomu kama EPA, Richmond and n.k kwani zile zama zinakwenda ukingoni. Bali chadema sasa itakuwa kwa ajili ya sera zake ambazo zinatakiwa ziwe mbadala wa sera mbovu za CCM.

Mfano halisi ni swala la Dr. Slaa kuletea hot debate kuhusu kufanya elimu iwe bure mpaka form 6. Hii ilikuwa sera nzuri, lakini ni wazi kabisa palitakiwa kuwepo na department ambayo inge research jinsi ya kulipia hii expenses, not for three years but for the next dacades. Au CCM wanaposema hatuwezi kujiendesha wenyewe, basi Chadema ni lazima wakae nchi watengeneze budget forecast ambayo itaonyesha mpaka kufikia 2020 tutaomba 0 kutoka IMF, DBA, WB or Paris Club.

Jingine, Mwenyeketi wa chama ni kama CEO, yeye ndie anayesimamia maono na mikakati ya chama. Katibu ni mtendaji, sasa kama lengo ni kuongeza wanachama katika mikoa ya kusini kwa asilimia 25% kati ya 2010-1013 maana ya kwamba time kubwa inabidi iwekezwe kwenye maeneo haya, na mambo mengine. Mboe hana huo muda, atafanya mangapi? Aendeshe chama, ahakikishe watu wajimboni kwake wanatimiziwa mambo yao, awepo bungeni ahakikishe kambi ya upinzani itandewa haki, haya ni majukumu mengi.

Ni imani yangu hata Zitto Kabwe ataachia unaibu katibu, na John Mnyika ataachia nafasi yake ili wengine ambao wana muda wawekeze kwenye haya.Ikumbukwe kwamba hii sio one person politics, huwezi kuwashinda CCM kama unatumia centralized system. Lazima nguvu itawanywe na CCM wabanwe full court.
 
Just a thought, kama Dr. Slaa asingegombea Urais, success ya Chadema ingekuwa kama ilivyo? If Chadema wangeng'ang'ania kuwa wao ni Bunge na kutoweka mtu mwenye wasifu kama Dr. Slaa, je matokeo yake yangekuwa sawa na ya leo?

Hata kama ni Ngeli na Ngali, lakini lazima tujiulize, ni vipi Dr. Slaa amekisaidia Chadema hususan wakati wa Uchaguzi au hata mchango wake tangu aingie Chadema kwa Chadema kupata mvuto na msukumo ulioko sasa hivi.

Simvunjii Freeman Mbowe heshima wala kudharau mchango wake binafsi katika kuongoza. Naomba nifafanue suala la mvuto. Freeman ameshafanya kazi kwa muda na ameifikisha Chadema hapo ilipo na kwa kushirikiana na viongozi wengine. Sasa gari liabidi liingie kwenye overdrive na ndio maana natamka kuwa ni bora kwa kuongeza kasi na nguvu, Mbowe ambaye ni more of a technocrat, aachie ngazi kama Mwenyekiti na awekeze nguvu zake bungeni na kwenye utungaji wa sheria na kumwachia Dr. Slaa ambaye si technocrat pekee bali ni pure politician mwenye uwezo wa kufanya yote mawili awe msimamizi wa kukiongoza chama kisiasa na kukijenga.
 
Rev. Kishoka,
Unachosema ni sahihi, lakini kuna historia watu wanaogopa isije jirudia kwao. Ni ile iliyomkuta Mapalala.
Kwa sababu Freeman amewezesha chama kuendelea kuwa stable katika mawimbi mazito, sio mbaya akindele kuongoza kikatiba ingawa kiutendaji anaweza kudelegate kazi nyingi kwa Slaa na wengine.
 
Rev. Kishoka:

Matokeo ya uchaguzi huu ni accummulation ya matukio mbalimbali na jinsi CHADEMA walivyoweza ku-capitalize matukio hayo. Katika capitalization ya matukio hayo, mwenyekiti wa CHADEMA alikuwa na input ndogo. Hii sio disrespect ya mwenyekiti wa CHADEMA bali ni pure fact.

Kwa kuwa Dr. Slaa hatakuwa na ubunge ambao utampa visibility kwa umma, basi ni muhimu kwa CHADEMA ku-elevate position yake na kuiipa bajeti nzuri ambayo itamfanya Dr. Slaa azungumze na kufanya mambo relevant ambayo yata-keep momentum.

Sisi tusio na vyama vya siasa we don't give a d@mn. Hatukawii kusahau.
 
Rev. Kishoka,
Unachosema ni sahihi, lakini kuna historia watu wanaogopa isije jirudia kwao. Ni ile iliyomkuta Mapalala.
Kwa sababu Freeman amewezesha chama kuendelea kuwa stable katika mawimbi mazito, sio mbaya akindele kuongoza kikatiba ingawa kiutendaji anaweza kudelegate kazi nyingi kwa Slaa na wengine.

Katika politics za kiAfrika hakuna vyama vinavyoendeshwa ki-stable. Ni personality za watu ndio zinazokipa chama u-stable. Kama Freeman anaweza kuongoza chama, mpeni uenyekiti wa chama kisicho na personality na tuone matokeo yake. Mpeni TLP na awaleteeni viti 20 vya ubunge.
 
Kiongozi,
Kama hizo personalities ziko in-line with Mbowe, huoni kuwa tutakuwa tunaziweka kwenye test tukupresume kuwa zitakuwa in-line na Slaa. ninachoamini ni kwamba stability, hata kama basis yake siyo deep rooted, ikisimama kwa muda mrefu inakuwa tradition na ikisimama kwa muda mrefu zaidi inakuwa order. Hivyo basi, ni vyema Mbowe akaendelea kuwa mwenyekiti mpaka stability iliyopo ikawa ni tradition ya chama.
 
ZeMar:

Mbowe hana personality. Alishindwa kuhamasisha watu kupigia kura CHADEMA kwa kutumia helikopta. Lakini mwenzake aliweza kwa Bajaji.
 
Just a thought, kama Dr. Slaa asingegombea Urais, success ya Chadema ingekuwa kama ilivyo? If Chadema wangeng'ang'ania kuwa wao ni Bunge na kutoweka mtu mwenye wasifu kama Dr. Slaa, je matokeo yake yangekuwa sawa na ya leo?

Hata kama ni Ngeli na Ngali, lakini lazima tujiulize, ni vipi Dr. Slaa amekisaidia Chadema hususan wakati wa Uchaguzi au hata mchango wake tangu aingie Chadema kwa Chadema kupata mvuto na msukumo ulioko sasa hivi.
.
kama freeman asingekubali kuwa mwenyekiti wa chadema na angeendelea kuwa mbunge wa hai, nae angepata kuwalipua watu bungeni je umaharufu wake kisiasa ungekuwaje? je freeman angeendelea kuwa mbunge wa hai 2005 chadema kingefika hapa kilipo? hamna mtu ambaye anajua haya majibu.....

je slaa angegombea urais 2005 na freeman angeendelea kuwa mbunge wa hai, je chadema kingekuwa wapi na wao wawili wangekuwaje? no body knows

je malecela angeshinda urais, chama cha ccm kingekuwa better than sasa hivi? no body knows

je ronaldo asingecheza mechi ya juzi madrid wangeshinda? no body knows

kabla ya slaa kuchaguliwa kugombea urais watu wengi walikuwa wanasema slaa aendelee kuwa mbunge maana yake bado wanamuhitaji bungeni, walikuwa wanataka wabunge wachadema waongezeke na chama kijikite katika kuchukua nchi 2015.

chadema is a team na wote wanafanya kazi kama team chadema, na chadema ina katiba yake na jinsi ya kuteuwa viongozi. Na huwa wanateua mwenyekiti one year before the general election, na hii ni ample time kwa mtu atayechaguliwa kuweza kukipanga chama vizuri. Uenyekiti wa freeman sio wa milele una kikomo chake, Time ikifika wataangalia position zote na kuona nani afae kuwa mwenyekiti, katibu mkuu na position nyingine zote ndani ya chama.

lakini unavyotaka wewe watu watolewe kwenye uongozi sasa hivi bila kufata mpangilio ni sawa sawa na kuwatupia lawama baadhi ya watu wakati wapiga kura wenyewe bado mentality zao hazijabadilika.
chadema is a team, they win together they lose together.
Divisive politics must end, they do more to undermine chadema than the intended individuals
enoguh said
 
Semilong,

Upende usipende popularity ya Dr. Slaa ni moto chini. Tangu alipokuwa Bungeni na akiongea na hata kwenda MwembeYanga na kwingineko, anavutia watu na kama nzi kufuata harufu watu wanakwenda left and right.

Free, kakiokoa sana chama kwa kwanza kutumia fedha zake mwenyewe na huo ni utegemezi ambao inabidi uachwe. Narudia tena, kama Musa alivyowavusha Wakaguru kuvuka Sinai, sasa Dr. Slaa ni Joshua wa Wakaguru kuwafikisha watu Kaanani.

Chadema kina hitaji kiwe na safu kuu ya viongozi ambao ni full time viongozi na si part time. CCM wanaweza kufanya mambo part time kwa kuwa tayari wameshajijenga na wana mfumo mbovu wa mabavu na ndio maana hata maoni ya watu wanayapuuza na kukaa kama kamati maalumu kuvunjilia mbali mawoni ya wanachama na hata wananchi.

Moja ya mapendekezo yangu ya siku nyingi ni kwa Chadema kuondokana na mfumop wa kiuendeshaji na kiuongozi kama wa CCM, haya ya Halmashauri kuu, kamati kuu na upuuzi mwingine na kama ulimsikia Kikwete wakati wa kampeni, alidai kuwa wapinzani ni nakala na wao CCM ni irijino.

Chadema wakiweza kujiimarisha kwa kuwafikia wananchi kwa wingi kupitia full time Wanasiasa na kuboresha mfumo wao na kuondokana na ile structure ya ki-CCM, watafungua wigo mkubwa sana wa watu hata ndani ya CCM kuondoka na kwenda kweny chama chenye Demokrasia ya kweli.

Labda nitoe mfano wa Howard Dean ambaye aliwahi kugombea tiketi ya Democrats kugombea Urais wa Marekani. Alipopigwa ngwala, na John Kerry, akahamia na kuwa mwenyekiti wa Chama na kazi yake ikawa ni kuhamasisha Democrats na kuwavuta independents wakipigie kura na kukubali sera na itikadi za Democrats.

Hii ndio role ya sasa inayomfaa Dr. Slaa na Mbowe Zitto, Mnyika, Lissu na wengine ambao ni wabunge, focus yao iwe kuisambaratisha CCM Bungeni na huku nje kisiasa, Dr. Slaa awapeleke mputa mputa kina Msekwa na Makamba.

Lakini tukimtaka Mbowe afanye vyote, Mbunge, kiongozi wa upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chama on top of that bado ni Mfanyabiashara, there is no way he will be able to mutlitask efficiently and achieve sound results kila kona. Kuna sehemu atashindwa na kuzidiwa na demand ya kila upande itasababisha ashindwe kufanya vizuri. Si mnasema kiswahili mpenda vyote au mtaka vyote humponyoka?

So ninaposema mvuto, ni kuangali ani namna gani Dr. Slaa (ambaye kadhulumiwa kura milioni 3) ambavyo ameweza kuhamasisha Watanzania bila kujali Chama na watu kuanza kuona kuna tumaini jipya.

Same approach should be used to expand and reinforce the network and strength of Chadema na hilo lianze mapema na si late stage. Slaa apigane na Kikwete, Mbowe amkomalie Makinda na Pinda.

Slaa aende kwa Wazee wa Mikasi (Shein na Hamad) akakiuze Chadema kwa ngovu zote na kuhamasisha mvuto mpya kule wa kuonyesha chama cha umoja na si utengano kama CUF au kutenganisha watu kama CCM.

Kazi hii Freeman hawezi kuifanya bila kutolea kafara kimoja cha majukumu yake.

Aidha kuwa na mwenyekiti mpya na mwingine, kutaondoa zile desturi na tamaduni za migongano ambazo tumeziona zikiviandama vyama vingi vya kisiasa Tanzania na hata Afrika ambapo Nyerere alifanya kosa alipoamua kuunganisha Kofia mbili na kuzivisha kwenye kichwa kimoja katika ule mfumo wa kikomunisti au kijamaa ambapo Chama ni nguvu na si Serikali.
 
Semilog,

No one here is wish evil for Chadema, lakini baadhi yetu tunacho chambua ni kuhusu swala zima la kuongeza kasi na kutumia mwanya ambao unaonekana. Ikumbukwe ya kwamba CCM hawajalala, na wanajua ya kwamba wajeruiwa na wanona mwanya wakujibu mashambulizi.

Chadema wana uamuzi, either kuendelea na mwendo na muundo uliopo ambao ni obvious kwamba CCM wanaweza kuukoroga over night. Au kudecentrelized na kuwapa ugumu CCM kwani ngome zitakuwa kila kona ya nchi.

Ikumbukwe kwamba ushindi wa viti 20+ kati 200+ ni hatua na hakuna ane pinga, lakini ni atua fupi sana ukilinganisha na kiu ya maendeleo tuliyo nayo. Ni wazi kabisa kwamba 2010-2015 hatutapata katiba mpya ambayo ni kiu kuu ya Watanzania, hatutapata serikali ndogo, hatutaanza safari ya kukomesha umasikini ndani ya asilimia 70 ya Watanzania. Lakini tumeanza safari ya kuelekea kwenye mageuzi ambayo tukifika hapa tutaanza ili safari ambayo Mwalimu Nyerere aliwaza tangu 1950s.
 
Semilong,

Upende usipende popularity ya Dr. Slaa ni moto chini. Tangu alipokuwa Bungeni na akiongea na hata kwenda MwembeYanga na kwingineko, anavutia watu na kama nzi kufuata harufu watu wanakwenda left and right.

Free, kakiokoa sana chama kwa kwanza kutumia fedha zake mwenyewe na huo ni utegemezi ambao inabidi uachwe. Narudia tena, kama Musa alivyowavusha Wakaguru kuvuka Sinai, sasa Dr. Slaa ni Joshua wa Wakaguru kuwafikisha watu Kaanani.

Chadema kina hitaji kiwe na safu kuu ya viongozi ambao ni full time viongozi na si part time. CCM wanaweza kufanya mambo part time kwa kuwa tayari wameshajijenga na wana mfumo mbovu wa mabavu na ndio maana hata maoni ya watu wanayapuuza na kukaa kama kamati maalumu kuvunjilia mbali mawoni ya wanachama na hata wananchi.

Moja ya mapendekezo yangu ya siku nyingi ni kwa Chadema kuondokana na mfumop wa kiuendeshaji na kiuongozi kama wa CCM, haya ya Halmashauri kuu, kamati kuu na upuuzi mwingine na kama ulimsikia Kikwete wakati wa kampeni, alidai kuwa wapinzani ni nakala na wao CCM ni irijino.

Chadema wakiweza kujiimarisha kwa kuwafikia wananchi kwa wingi kupitia full time Wanasiasa na kuboresha mfumo wao na kuondokana na ile structure ya ki-CCM, watafungua wigo mkubwa sana wa watu hata ndani ya CCM kuondoka na kwenda kweny chama chenye Demokrasia ya kweli.

Labda nitoe mfano wa Howard Dean ambaye aliwahi kugombea tiketi ya Democrats kugombea Urais wa Marekani. Alipopigwa ngwala, na John Kerry, akahamia na kuwa mwenyekiti wa Chama na kazi yake ikawa ni kuhamasisha Democrats na kuwavuta independents wakipigie kura na kukubali sera na itikadi za Democrats.

Hii ndio role ya sasa inayomfaa Dr. Slaa na Mbowe Zitto, Mnyika, Lissu na wengine ambao ni wabunge, focus yao iwe kuisambaratisha CCM Bungeni na huku nje kisiasa, Dr. Slaa awapeleke mputa mputa kina Msekwa na Makamba.

Lakini tukimtaka Mbowe afanye vyote, Mbunge, kiongozi wa upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chama on top of that bado ni Mfanyabiashara, there is no way he will be able to mutlitask efficiently and achieve sound results kila kona. Kuna sehemu atashindwa na kuzidiwa na demand ya kila upande itasababisha ashindwe kufanya vizuri. Si mnasema kiswahili mpenda vyote au mtaka vyote humponyoka?

So ninaposema mvuto, ni kuangali ani namna gani Dr. Slaa (ambaye kadhulumiwa kura milioni 3) ambavyo ameweza kuhamasisha Watanzania bila kujali Chama na watu kuanza kuona kuna tumaini jipya.

Same approach should be used to expand and reinforce the network and strength of Chadema na hilo lianze mapema na si late stage. Slaa apigane na Kikwete, Mbowe amkomalie Makinda na Pinda.

Slaa aende kwa Wazee wa Mikasi (Shein na Hamad) akakiuze Chadema kwa ngovu zote na kuhamasisha mvuto mpya kule wa kuonyesha chama cha umoja na si utengano kama CUF au kutenganisha watu kama CCM.

Kazi hii Freeman hawezi kuifanya bila kutolea kafara kimoja cha majukumu yake.

Aidha kuwa na mwenyekiti mpya na mwingine, kutaondoa zile desturi na tamaduni za migongano ambazo tumeziona zikiviandama vyama vingi vya kisiasa Tanzania na hata Afrika ambapo Nyerere alifanya kosa alipoamua kuunganisha Kofia mbili na kuzivisha kwenye kichwa kimoja katika ule mfumo wa kikomunisti au kijamaa ambapo Chama ni nguvu na si Serikali.

Mchugaji Amen.

Case close, yaani umezungumza yote ambayo tumekuwa tukiyazungumza kuanzia mwanzoni mwa Forum. Narudia tena Amen.
 
Naomba kuuliza, katika viti maalum walivyopewa Chadema, ni wateuliwa wangapi wametoka Zanzibar na mikoa ambayo Chadema hawakuweka wagombea wa kutosha?
 
Naunga mkono 50% 50%

Slaa awe mwenyekiti ila mpaka wakati wa uchaguzi
Mbowe apambane bungeni sawa; watu kama akina mwita waitara ndio wanafaa kupewa propaganda au lwakatare yes; naona anayetakiwa kupunguziwa nguvu ni Zitto amekuwa anacahnganya sana watu na inaonekana haoni umhimu wa chama kukua ndio maana misimamo ya chama mingi yeye ndio mpipnzani wake; lazima k uwe na ethics na huyu anatakiwa kuwekwa ktk tanuru. otherwise mengi umeongea vema kabisa wayafanyie kazi
 
Rev. Hivi Kazi unazotaka Dk. Slaa afanye hawezi kuzifanya sasa hivi kwa kofia yake? Kuna kitu gani cha kumzuia kujenga chama kama tayari ndiye mtendaji mkuu. Wapo viongozi wengi wanaoweza kuendelea kumsaidia na hawapo bungeni. Dk anaendesha sekretariati nzima ya chama. Hivi hiyo kweli haitoshi kumjengea mazingira ya kujenga chama?

Sioni ulazima wa Dk. kuwa mwenyekiti na kama ilivokwishasemwa muda wa uchaguzi bado. Naamini muda utakapokuja CHADEMA watajireposition kulingana na demands za muda huo. Nina imani mfumo uliopo si wa matatizo kiasi cha kushindwa kutimiza malengo hayo mazuri. Cha msingi ni wanachama kuendelea kumpa moyo Dk. Watu kujitolea zaidi kukijenga zaidi chama maeneo inakohitajika. La muhimu kabisa ni kucement nguvu ya chama maeneo yote yaliochukliwa yasije kutokea tena ya tarime.
 
Nikiwa nimekaa chini kutafakari ni kwa nini katika nafasi 23 za Chadema za wabunge wa kuteuliwa hawakuteua wawakilishi kule Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pemba, Tanga, Dodoma, Pwani, Tabora na kuongeza kule Iringa, Mbeya, Arusha, Rukwa na Mara, leo tunasikia kauli za chapati maji, kudai walinukuliwa isivyo kuhusu kutomtambua Kikwete kama Rais.

Hivyo swali langu kwenu wana Chadema, bado mnapingana nami kuwa hamuhitaji uongozi mpya ikiwa tayari kuna pande tatu zinavutana; Zitto, Freeman Mbowe na Dr. Slaa kwenye hili jambo moja la kuyakubali matokeo ya urais?

So take a minute again and think of what I was trying to relate to indirectly and assess the last 120 hours of life of Chadema!
 
CCM , CUF na CHADEMA vyote ni vyama vya siasa na vyote vinafanya madudu na kwa maendeleo ya nchi vyote vinatakiwa viliform lakini mbona wewe uko busy na chadema tu, nini hasa lengo lako?
 
Nikiwa nimekaa chini kutafakari ni kwa nini katika nafasi 23 za Chadema za wabunge wa kuteuliwa hawakuteua wawakilishi kule Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pemba, Tanga, Dodoma, Pwani, Tabora na kuongeza kule Iringa, Mbeya, Arusha, Rukwa na Mara, leo tunasikia kauli za chapati maji, kudai walinukuliwa isivyo kuhusu kutomtambua Kikwete kama Rais.

Hivyo swali langu kwenu wana Chadema, bado mnapingana nami kuwa hamuhitaji uongozi mpya ikiwa tayari kuna pande tatu zinavutana; Zitto, Freeman Mbowe na Dr. Slaa kwenye hili jambo moja la kuyakubali matokeo ya urais?

So take a minute again and think of what I was trying to relate to indirectly and assess the last 120 hours of life of Chadema!

Mchakato wa kupata wawakilishi wa ubunge viti maalum ulikuwa wazi kabisa, kwa nini basi chadema isipate wawakilishi toka mikoa hiyo uliyotaja? hivi mnajua kwamba CHADEMA haijulikani hasa katika mikoa hiyo aliyotajwa?, Kwa mfano mimi natoka Sikonge vijijini, nikapiga simu siku 3 kabla ya uchaguzi kuongea na Mandungu zangu cha ajabu wanasema DR. Slaa tunamsikia tu kwenye ITV, sasa hao wawakilishi utawapata kwa namna gani? Huwezi kumchagua mtu tu then anaingia CHADEMA hao ndiyo wanaleta mifarakano isiyo na tija ndani ya CHAMA.

Ungefanya utafiti kwenye hiyo list ya wanawake waliojitokeza kuomba viti maalum uone kama hata kuna wanawake walau 10 tu wenye sifa toka mikoa hiyo uliyotaja?

Mimi naona huu ndiyo wakati wa CHADEMA kujitanua zaidi katika mikoa hiyo, uongozi ulioifikisha CHADEMA hapo ilipo uendelee sioni tatizo la haraka zaidi la kufanya restructring kubwa kabisa ndani ya CHAMA mapema hivi, ni sawa na mtoto anaanza kutambaa then unambadilisha mfumo wake wote wa ukuaji kwa ghafla hapo lazima atadumaa.
 
Back
Top Bottom