Elections 2010 CHADEMA muda wa kuwaandaa makada ni huu

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,464
Chama cha Maendeleo na Demokrasia kinakua kwa kasi nzuri sana. sera zake na viongozi wake na wabunge wengi wanakubalika kwa Jamii ya tanzania ya leo.

Kuna angalizo muhimu sana linahitajika kufanyiwa kazi kubwa sana na kulichukulia kwa uzito wake. Chama kinapokuwa na kuleta upinzani mkubwa kwa chama tawala tayari kinatengeneza mwanya wa kubomolewa kwa siasa za kiafrika na hasa east afrika. Makada na wagombea wa nafasi mbali mbali lazima wawe ni watu wanaokijua chama kwa undani na kuelewa sera za chama, itikadi na mfumo. Viongozi wote lazima wajua misingi na imani za chama na nini wanasimamia, huo ndio msingi wa kujenga chama imara na serikali imara. Chama legelege kinazaa serikali legelege.

Napendekeza utaratibu ambao tumekuwa tukiutumia wa kuwapata wagombea kuubadilisha haraka iwezekanavyo. Najua Viongozi waliopo wamepitia kwenye vipindi vigumu sana, wanahitaji pongezi ya namna ya pekee na sifa kubwa na kuenziwa ndani ya chama. Wamefanya kazi katika mazingira magumu na kwa wakati mgumu sana. Viongozi wote wa CDM kuanzia 1992 hadi leo poleni sana na hongereni sana. Utaratibu ambao umetumika wa kuwapata wagombea wa nafasi mbali mbali za kitaifa, wilaya, mkoa, ubunge, udiwani nk lazima ubadilike. mabadiliko haya lazima yafanyiwe mabadilko kwenye katiba ili kutoa mwanya wa malalamiko na uonevu.

Moja mwanachama ambaye anataka kugombea nafasi yeyote ile ya uongozi, ndani ya chama au ile ya udiwani, ubunge lazima awe na muda utakaokubalika ndani ya chama, awe mwanachama hai, anayeshiriki shughuli za chama pale alipo, napendekeza walau awe mwanachama kwa miaka miwili kabla ya kuomba au kupewa nafasi yeyote ya uongozi. Hii itasaidia kuwapata viongozi imara na wenye kuelewa chama na sera zake.

Mchakato huu utasaidia kuwa na viongozi wanajua misingi na uimara wa chama badala ya sasa kuvizia wanaotemwa au wanaovizia vyeo au wanaopima upepo kwa faida za matumbo au kusaidia vyama vingine kwa kuingiza mamluki. Najua kunagharama zake ila hii itasaidia kuwa na chama imara chenye watu madhubuti.

Chama kinakua kinahitaji misingi imara, wimbi la wasaliti linakuwa kwani chama tawala kinaangamia, kinatumia hila, fedha, na ushushu kuua upinzani kwa kununua wapinzani. Njaa za viongozi wasio na mwelekeo wa kuwakomboa wananchi, wasioelewa nini CDM wanafanya wananunulika kirahisi na kutengeneza makundi, fujo, tamaa nk.

Ni mimi
Chief Mkwawa wa Karenga
 
Mkuu naunga mkono hoja mia kwa mia. Sasahivi magamba wanahaha kuimaliza nguvu chadema,na mbinu mojawapo ni kupandikiza mamluki ndani ya chadema. Hawa mamluki wengine wanatoka ccm moja kwa moja na wengine wanawachukua toka vyama vingine na kuwapandikiza. Ni vizuri chadema waandae mkakati maalum kuwajengea uwezo wanachama wake waliopo sasahivi na hususan viongozi kuanzia ngazi ya matawi hadi mikoani ili kunaookuwa na uchaguzi chama kisifikirie tena kuzoa walioasi magambani,ingawa wapo wachache wanahamia chadema kwa nia thabiti ya kujenga chama na kutumikia wananchi lakini wengi ni vimeo. Ni muda muafaka sasa chadema kutayarisha wanachama wake kwa ajili ya kuongoza kwani tunakoelekea magamba wanakwenda kuzikwa na chadema inakwenda kukabidhiwa uongozi wa nchi.
 
Mageuzi ni SASA,kama si sasa ni SASA hivi hakuna lisilowezekana chini ya jua hili.
 
Chief Mkwawa

Umekiongea kitu muhimu sana kwa ustawi wa chama chochote lakini sidhani kwa jinsi ninavyowaelewa watanzania kama kuna mtu atakuelewa kwa sasa hata viongozi wenyewe wa Chadema maana wengi wetu tunaendeshwa na matukio(events) na sio mipango (Strategies). Angalia hata humu JF watu tunaongelea zaidi diwani au mbunge fulani katoka chama hiki kwenda kile bila kujiuliza sababu na kiini hasa ni nini. Kina Kitila Mkumbo wapo wanasubiri baada ya uchaguzi ndipo waje na fomular za zima moto kupata wabunge wa viti maalum badala ya kuanza leo kuangalia jinsi ya kuwaandaa hao wagombea.

Hii mada yako inaihusu moja kwa moja kurugenzi ya Oganizesheni na Mafunzo na ile ya Kampeni na Uchaguzi za Chadema zinazoongozwa na Dady Igogo, Suzan Kiwanga na Msafiri Mtemelwa, akiwemo Kitila Mkumbo, wao ndio hasa wanaotakiwa kuja na long plan na kuushauri uongozi wa Chadema nini kifanyike ili kupata viongozi na wagombea bora si bora wagombea kama kina Shibuda wasiojua misingi na itikadi za chama.

Kama mtoto akuavyo nguo za mwaka juzi zinaweza zisimtoshe mwaka huu Chadema nayo hivyo hivyo inakua wajaribu kupanua wigo wa kupata viongozi na wagombea ikibidi wabadilishe, tumejionea uchaguzi uliopita walivyozoa zoa na kujikuta wanazoa hata mizoga sijui kama hilo wameliona na kujifunza. Au tuseme mafanikio wanayoyapata hawakutegemea kama yatakuja kwa kasi namna hii kifupi yamewazidi kimo, wajue kadri wanavyokua ndivyo wanavyoongeza matatizo na kuongeza maadui bila kujiimarisha kwa kila kitengo ni rahisi kwa wabaya wao kujipenyeza.

Chadema wanatakiwa wasiende na matukio kuwa hadi tatizo litokee ndipo watafute namna ya kulisolve, je wana kitengo cha inteligensia at least kwa kila mkoa au wilaya wameweka mtu wa kuwaletea ukweli wa mambo mbali na viongozi wa wilaya, mfano tukio la madiwani wa Arusha kama wangekuwa na kitengo hicho cha siri wangepata habari mapema na kuzuia kabla mambo hayajaharibika kuliko kutegemea habari kutoka kwa mwenyekiti au viongozi wa wilaya ambao wanaweza kuwa chanzo cha tatizo. So Chadema wanatakiwa kukua na kubadilika ikibidi kubadilisha mfumo wao wakupata viongozi ili waendane na wimbi la ukuaji wa chama chao.
 
leo ndio mnaliona hilo, tuliwaambia chadema hamna chama na chama ni matawi ndipo unapoweza kuwajua makada na wanachama wako
 
Chief mkwawa,

Mawazo yako ni mazuri sana,hongera!

Kuna kipindi tulishawahi kujadili kuhusu ideologies na kitu kinachosababisha cross carpeting kwa vyama vya siasa.Hii ni setback kubwa kwa vyama vya upinzani

Vyama kama Communist Party of China vina succession plan nzuri sana,vyama vya NPP na NDC vya Ghana,NDP na Action Congress ya Nigeria hali kadhalika.Hatuwezi kuwa na mfumo kama wa Orange democratic Movement(ODM) katika mfumo wa kukuza na kulea makamanda/comrades wake,mfumo wa kisiasa wa Kenya w uliothiriwa na ukabila na na ubepari unawafaa sana ndiyo maana wanafanikiwa.Tufuate pia mfumo kama wa chama cha rais Carlos wa Mexico kilichowaondoa madarakani chama kilichooongoza/tawala kwa zaidi ya miaka 70.Tuweke strong ideological and structural pillars ili hata ikitokea mtu akahamia ndani ya chama na anakubalika na wananchi basi tuwe tunalindana kwa kutumia hizo values.Akipandikizwa mamluki akafanya kazi za umamluki wake automatically anaenguliwa na hizo principles na wananchi wake wataelewa na hata tukiingia kwenye uchaguzi mdogo ni lazima chama na mgombea atakayewekwa atashinda.Chadema bado step by step kinafanya radical change within the sysytem.

Ila kidogo tu nitofautiane na hilo jina la ukada,ukada unazaa umateka wa fikra...ni bora tuwe na jina tutakaloitana kwa viongozi na wafuasi wa chama kuliko neno KADA ambalo lina traits za Ki-CCM,limekaa kishabiki zaidi,limekaa katika mkao wa kujiandaa kuwa mateka wa fikra.Mapambano ambayo chadema inafanya ni mapambano ya kifikra!

Otherwise,Comrade Chief Mkwawa bravo and have great weekend ! ! !

 
ni kweli kabisa kamanda, ila mwanzo chama kilikuwa kinachukua mgombea hata kama kadi yake ni ya muda siku moja ni kwa vile chama kilikuwa na uhaba wa rasimali wagombea na ndio maana uchaguzi ulikwisha uanakuta majimbo mengi haapkuwa na wagombea na hata wengine walidiliki kuuza majimbo, lakini kwa sasa haiwezi tokea hivyo naamini unapozungumzia chadema unazungumzia tanzania. na natumaini viongozi watabadili mfumo huu na umri wa mgombea katika chama.
 
Naunga mkono hoja....muhimu kuwa macho na mamluki ambao wanaweza kuwa ni kutoka vyama vingine, kupandikizwa au kutumia waliopo na kuwabadilisha!!
Mfano wa Madiwa ni wa Arusha ambao wanataka kuuonesha wao ni zaidi ya chama..ni dalili nzuri kuanza kuifanyia kazi..! Kama chadema wanataka kujenga chama imara lazima wakubali kufanya maamuzi magumu. Hawawezi kuwa na wanachm ambao ni jeuri kuliko chama chenyewe ahalfu tukawaamini watatutetea bila kudubuniwa!
 
Naunga mkono hoja niwakati mwafaka kwa vyama vyote kuonyesha uwezo wao kisiasa kwa kunadi sera zinazolenga kutuletea tanzania mpya na ziwe zinatekelezeka na wananchi tuwe tayari kuchagua viongozi bora na sio bora viongozi wananchi tuwe tayari kuondoa tofauti za vyama kisha tupime sera kwa kuangalia tumetoka wapi tuko wapi tunataka kwenda wapi na nani atatufikisha huko tunakotaka kwenda
 
Chief, nakubaliana na mapendekezo yako..... Ni wajibu wa viongozi wachadema kufanyi kazi ushauri huu uliyowapatia
 
kwa kuongezea, CDM NI LAZIMA KIJENGE MIZIZ KUANZIA CHINI KABISA YAANI KATA NA HASAHASA UDIWANI AMBAO NDIO WADAU WAKUBWA KATIKA MAENDELEO YA JIMBO, NASHAURI UCHAGUZI UJAO, WANACHAMA NA WAPIGA KAMPENI WAJIKITE KWA KASI ILE YA UBUNGE KWENYE UDIWA, UKICHUNGUZA KWA MAKINI UTAONA MAENEO MENGI AMBAYO CHADEMA WANGEWEZA KUCHUKUA UDIWANI WALIPOTEZA. MFANO IRINGA MJINI, NILIPOWAULIZA WANACHAMA KWANINI WAMEPOTEZA SANA UDIWANI? WENGI WALIKILI KUWA WALIJIKITA SANA KATIKA UBUNGE
 
Back
Top Bottom