Elections 2010 Chadema msipumbazwe na CCM vijijini hawahitaji kujua sera

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Kama ni kuelezea sera mbona CCM wao 80% ya muda wa kampeni wanapiga miziki
Kama ni kuelezea sera mbona CCM wanatumia muda mwingi kukejeri wapinzani(tutawachana)
Kama ni kuelezea sera mbona CCM wanatoa ahadi za meli kwani meli ndio sera yao
Kama ni kuelezea sera mbona CCM wanatumia press conference kutukana(mbumbumbu)
Kama ni kuelezea sera mbona CCM wanaingilia mambo binafsi ya ndoa za watu
Kama ni kuelezea sera mbona CCM wanadharau wagombea kwa elimu zao
Kama ni kuelezea sera mbona CCM wanataka kuwagawa watu kwa imani zao
Kama ni kuelezea sera mbona CCM wanawatenga watu kwa matabaka na makabila yao
Kama ni kuelezea sera mbona CCM....................

Kama wao CCM wanayafanya hayo kwa nini walazimishe Chadema kuelezea sera zao ilhali wao hawafanyi hivyo. Chadema be careful CCM inachotaka ni kuwapotezea muda wakati kwenye kampeni kinachotakiwa ili ujumbe ufike kwa mlengwani ni hamasa ya wasikilizaji kama wanavyofanya wao.

Kwanini CCM inagharamia wanamziki karibu wote wa Bongo flava na karibu kwaya zote za dini, wanajua kuwa bila vitu hivyo ni vigumu sana kukusanya watu na kufikisha ujumbe.

Nashauri CHADEMA wafanye yafuatayo: Sambamba na sera mlizonazo...

Hamasa ya wasikilizaji ni pamoja na miziki piga miziki mikutanoni kwanini wawalazimishe kuongelea sera na wakati wao hawaongelei, hizo ni mbinu za kilaghai na kuwapotezea malengo.

Kama sera zipo zipo tu na hata ukizizungumza kwa kutoa machozi haisaidii utasema leo kesho wote wameshasahau watakumbuka vile mdundo wa bongo flava ulivyokuwa unadunda.

-wakikejeri na nyie mtindo huo huo wakejeri msiogope kuambiwa sio wastaarabu
-wakileta personal issues hakuna kuwalazia damu tit for tat
-piga bongo flava na nyimbo za dini na mapambio ikiwezekana mbona wao wanafanya

-Kama mnaona mabomu yanasaidia yalipueni ila angalia yasiwapasukie, hata Mrema yalimsaidia. CCM wanayaogopa sana ndio maana kila siku wanaomba eti kampeni za kistaarabu ili wapate pumzi wakati wao wakiendelea kuwaumiza kwa vyombo vyao vya habari.

Chadema mkifanya hivyo mta win wapenzi wengi ambao ni vijana na mtazishinda mbinu za wapinzani wenu wanaotaka kampeni zilizodumaa. Lakini kama mkitaka kufuata yale CCM wanayotaka mtaumia.

Ni utafiti mdogo nilioufanya kulingana na mahitaji ya siasa za Tanzania. Naomba kutoa hoja.

Luteni.
 
Endeleeni ku- copy and past ya CCM, kwani inaeleweka viongozi wenu wa Chadema ni Darasa la 7, mwenye digrii ni ya bibilia, lol
 
Endeleeni ku- copy and past ya CCM, kwani inaeleweka viongozi wenu wa Chadema ni Darasa la 7, mwenye digrii ni ya bibilia, lol

Hata wewe Bull, sikutegemea kusoma hii kutoka kwako! Unawezaje kwenda that low! Maana ya kusoma sio madarasa au vidato au digrii jamani! Hii ni kubweteka, jaribu tu kulinganisha elimu unayoizungumzia na utendaji wa wanasiasa, ujidhihirishie mwenyewe kama kweli kuna uhusiano huo! Utashangaa. Hii kwangu ni dhahiri mno, kiasi sipendi nipoteze muda wa kukusaidia kufanya utafiti ambayo majibu yake tunayajua
 
Njilembera hayo anayoyasema Bull ana represent tabia ya kejeri ya viongozi wa CCM ninayoiongelea ambayo inatakiwa ijibiwe na viongozi wa Chadema kama tunavyowajibu humu.
 
Endeleeni ku- copy and past ya CCM, kwani inaeleweka viongozi wenu wa Chadema ni Darasa la 7, mwenye digrii ni ya bibilia, lol

mbona wewe hata hiyo degree ya madrasa huna...
 
Endeleeni ku- copy and past ya CCM, kwani inaeleweka viongozi wenu wa Chadema ni Darasa la 7, mwenye digrii ni ya bibilia, lol

na huo usomi wa viongozi na wagombea wenu mbona wanaogopa kwenda kwenye debate!!! jibu ni simple VILAZA
 
Vijijini wamechoka na CCM; Jana Dr slaa kawahutubia maelfu ya wanakijiji wa Haydom Mbulu, Zama ilikuwa ngome ya CCM, wengi niliwapigia wakaniambia hata CCM wakiiba watakipigia kura CHADEMA maana wamejua maana yamabadiliko, Filip Marmo anahali mbaya mwaka huu,

Ni kweli vijiji vingi, sera haieleweki sana, kukosoa kunaeleweka zaidi.

Ushauri wako ni muhimu sana
 
Vijijini wamechoka na CCM; Jana Dr slaa kawahutubia maelfu ya wanakijiji wa Haydom Mbulu, Zama ilikuwa ngome ya CCM

Kuna wakati huwa tunakuwa na machizi kibao baada ya uchaguzi, nadhani ni hizi false hope tunazojipa, kwanini ninyi mnaopenda mabadiliko msi face reality na muweke juhudi vijijini ili mabadiliko ya ukweli yatokee.
 
Hata wewe Bull, sikutegemea kusoma hii kutoka kwako! Unawezaje kwenda that low! Maana ya kusoma sio madarasa au vidato au digrii jamani! Hii ni kubweteka, jaribu tu kulinganisha elimu unayoizungumzia na utendaji wa wanasiasa, ujidhihirishie mwenyewe kama kweli kuna uhusiano huo! Utashangaa. Hii kwangu ni dhahiri mno, kiasi sipendi nipoteze muda wa kukusaidia kufanya utafiti ambayo majibu yake tunayajua

Hakuna utendajo bila shule wewe. Darasa la saba aje atende nini humu nchini?! Acheni ujuha nyie Chadema
 
Kuna wakati huwa tunakuwa na machizi kibao baada ya uchaguzi, nadhani ni hizi false hope tunazojipa, kwanini ninyi mnaopenda mabadiliko msi face reality na muweke juhudi vijijini ili mabadiliko ya ukweli yatokee.
Mwenzetu umeridhika na maisha hutaki tena mabadiliko.
 
" BRIA; phd ya heshima kaka dah....DR K....... "
Naungana nawe. Lakini itakuwa vyema sana iwapo CHADEMA watakuwa na waratibu wa kuchukua maoni ya maana na kuyafanyia kazi fasta!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom