maghambo619
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 1,537
- 1,360
Ondoa shaka ndugu,... Alama ya CHADEMA ni ''V'' na vazi lake ni 'GWANDA'
kwenye karatasi za kura hakuna gwanda
Ondoa shaka ndugu,... Alama ya CHADEMA ni ''V'' na vazi lake ni 'GWANDA'
Chadema wanatakiwa kulalamika, lakini watalalamikia wapi wakati wametangaza mgogoro na msajili?
Wanabodi,
Mpangilio wa rangi za chama kipya kilichopata usajili wa kudumu cha ADC unafanana kwa kiasi kikubwa sana na ule wa bendera za chadema.
Hata wakati anakipatia usajili wa muda, msajili wa vyama vya siasa alilitanabaisha hilo ila akasema anasubiri chadema walalamike ili kuangalia uwezekano wa kuwaambia ADC wabadilishe rangi hizo. Hadi sasa chadema ipo kimya kuhusu suala hilo.
Nionavyo mimi, kuna uwezekano mkubwa sana bendera ya ADC imekuwa designated hivyo ilivyo kwa makusudi mazima na wala si bahati mbaya.
Baadhi ya sababu zaweza kuwa hizi:
1. Kupata umaarufu kupitia mgongo wa chadema ambayo kwa sasa ipo juu katika medani za siasa nchi. Kwamba utakaposema bendera ya ADC imefanana na ya chadema, automatically utakuwa umeitaja na hivyo kuifanya isifutike kirahisi kwenye midomo na vichwa vya watu.
2. Kuleta mkanganyiko wa makusudi.
Kwa first impression ni vigumu kuitofautisha bendera ya ADC na ile ya chadema hasa kwa watu ambao ni "colour blind". Impact yake itakuwa kwenye chaguzi. Mtu anaweza akadhani ameipigia kura chadema kumbe kaipigia ADC. Kama chadema itaendelea kukaa kimya basi itarajie madhara makubwa sana katika eneo hili.
Kwa kuwa inawezekana kabisa uanzishwaji wa ADC ni "mkakati maalum", basi chadema isikae kimya hata kidogo. Ni lazima chadema ipeleke malalamiko yake kwa msajili ili ADC ibadilishe rangi zake. Kama chadema wataendelea kukaa kimya basi wasishangae kuona nguvu kubwa wanayotumia kujenga chama kumbe wanawafanyia watu wa chama kingine bila kujijua.
bendera ya chadema
bendera ya ADC
Mkuu suala la kufanana rangi za bendera ni suala kubwa wala halihitaji kufanyiwa dharau.Kwa hakika ukitamka tu CDM bila hata bendera watu wanaamka!!! Kuna mahali nilitembelea rafiki yangu na nyumba yake na watoto from grade one to 6 wa kwake na wa ndugu about 6 na wote ni CDM. Nikawauliza kwa nini wakasema nanukuu "SSM gani wakati kila siku wao wanashiba tu na wengine hata kule shuleni wanatembea peku hawana viatu na waalim juzi waliacha kufundisha halafu eti mgambo wa Temeke wakaja kuwapiga na mwingine wakaba hela yake kwenye bag...." Yaan hayo ni maneno ya watoto under 12 years. Nlishika mdomo. Yaani wanajua eti hata waalim wao kuwalazimisha kununua mihongo, karanga, kashata, na uji ni ili waalim wapate hela maana hawana mshahara wa kutosha. Watoto walitetea waalim kuliko ambavyo naweza kuwatetea. Kwa mantiki hii hata kikitokea chama kingine with the copy of CDM flag, bado hakiwezi kufika CDM ilikofikia, it is a nightmare!!
Think wide!Mchele mmoja mapishi mengi. Hizo rangi tu mpangilio tofauti.
Wakiweza kulamba kura 1000 ambazo zilikuwa zienda chadema, hiyo ni hasara kubwa kwa chadema.nawahakikishia chama hiki hakitavuka mipaka ya dsm na zenji na kwenye uchaguzi wa 2015 hakitafikisha asilimia moja ya kura zote na hakitapata diwani wala mbunge hata mmoja.take it from me!
Mimi nilidhani chadema wangeifanyia kazi hii kitu toka kipindi kile, kimsingi hizi rangi zitaleta sana confusion hasa kny upigaji wa kura,ufahamu na uelewa wa watu unatofautiana kuna watu watashindwa kutofautisha hizi bendera mfano wazee.
CHADEMA waliacha rangi zao za asili na kuchukua zile za CUF, viwavi nyinyi hamkusema lolote!
Naona mnaogopa sana, kule kuna nyota huku kuna vidole viwili wapi na wapi! We ukila wali mweupe wa maji wengine watakula wali wa nazi mchele ni uleule viungo na radha tofauti sasa utasema hujashiba kwa sababu wewe umekula wali mweupe wa maji na yule kala wali mweupe wa nazi wakati nyote mmepewa vipimo sawa?Think wide!