CHADEMA mnataka mteremshiwe gunia la chawa?

Wewe ambaye unafikiri vizuri anzisha maandamano Dr Slaa yeye atakuwa hoteli kapumzika nyie ndio mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kupambana na polisi kuwakomboa watanzania au nyie maandamano yenu mnayafanyia JF.

Sometimes i really wonder,this Person does he really have morals and think on his own?
 
  • Thanks
Reactions: ral
Ningetaka kuandika kwa kirefu sana kuelezea jambo ambalo labda kwa kifupi lingetosha kuelezewa. Sijaelewa kwanini hadi leo hii masaa zaidi ya 24 tangu Jaji Manento atoe muhtasari wa ripoti yake ya Tume ya Kudumu ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyonyoshea kidole serikali (Polisi na Msajili wa Vyama vya Siasa) kuwa ndio walioingilia kati uhuru wa CDM kufanya mikutano yake na kusababisha uvunjwaji wa amani, kupigwa kwa wananchi na kuuawa kwa mwandishi wa habari Daud Mwangosi.

Inashangaza kuwa CDM ambao siku mbili nyuma walilaumiwa na Kamati ya Nchimbi kuwa ndio chanzo hasa cha vurugu wamejikuta wakisafishwa na chombo cha juu zaidi na chenye nguvu zaidi za kisheria na badala ya wao kutumia nafasi hiyo wameamua kukaa kimya kana kwamba lililosemwa ni dogo. Ikumbukwe kuwa tangu tukio lile la Iringa litokee ni CDM ambao walikuwa wanafanywa mashetani wa tukio hilo huku viongozi mbalimbali wakikituhumu kuwa ndiyo kilichosababisha tukio hilo baya kwa kutotii amri 'halali' ya serikali.

Tume imeweka wazi kuwa amri iliyotolewa haikutolewa kihalali na hivyo CDM hawakutakiwa kutii isipokuwa kwa busara tu lakini hakukuwa na legal basis ya wao kutii amri isiyo halali. Kumbe tukio zima linawaangukia Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa na Kamishna Kamuhanda pamoja na viongozi wa juu wa jeshi la Polisi waliohalalisha uvunjivu wa haki za binadamu na matumizi mabaya ya madaraka.

Yale maandamano ambayo wamekuwa wakiyanfay kwa M4C hadi hivi sasa hayajabadilisha mfumo wowote, hayajamuondoa mtu yeyote madarakani na kwa hakika yamekuwa ni maandamano ya kuhubiria waumini tayari! Sielewi kwanini Kamuhanda bado yupo, Kagonja bado yupo na Tendwa bado yupo?

I mean najua sehemu ya jibu - wanasubiri kukaa kama kikao cha kamati kuu ili waamue kwa pamoja bla bla bla bla bala... well.. ukivumilia ujinga utatendewa kijinga! CDM needs to seize this opportunity to force the resignations of those who were implicated! Vinginevyo kama nilivyowahi kuwaambia huko nyuma.. wasubiri kuendelea kubeba majeneza na kutoa hutuba za uchungu hadi qiyama.
Vicent nyerere kashatoa tamko kitambo mkuu.


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
mimi mwenyewe nna vibrate kila dk watanzania tumelala jamani kwa nini tusiingie mtaani tukamtimue yule mpangaji fedhuli pale magogoni? aaaaaaaaargh

Sometimes what they are doing is right kila mtu hasira itakapo jaa sawasawa kifuani mwake itakuwa kazi rahisi kwao kuwaambia the time has come and now is.....
 
Wametoa tamko kupitia waziri kivuli wa mambo ya ndani vincent nyerere kwamba wanamtaka waziri nchimbi ajiuzulu na akikataa rais kikwete amuwajibishe

REally? mbona hili lilisemwa kabla na wote tena wamerudi kutaka Kikwete amuwajibishe...
 
Pengine Mkuu Mwanakijiji unaharaka sana!!! nadhani strategy hapa ilikuwa ni kusubiri Tendwa akane, police plus mchimvi wajibu mapigo kwakusaidiana na yule jaji wa kwenye list ya Lisu IHEMA...

eti wauaji wa M/Kiti wa CDM marehemu MBWAMBO wametoroka baada ya kumpora askari silaha!!! hivi wale waliomua yule kada wa CDM kule igunga walipatikana?...waziri anangoja nini kujiuzulu?...CDM tumieni siku ya tarehe 14/10 kuwaaambia wananchi na mataifa kuwa ile amani, haki na usawa iliyo asisiwa na JK Nyerere imeshatoweka...

"TANZANIA TANZANIA...NCHI YENYE MALI NYINGI, WATU WENGI WA ULAYA WANAILILIA SANAA" nimeona majizi wauaji, CCM inatia fora...
 
Mtajipanga hadi lini jamani?
Angalia Ulimboka baada ya mateso yote aliyoyapata lakini hadi leo hii anasema anajipanga kuwataja wahusika
na nini na nini,au mshalogwa??

Chelian ya ulimboka na hili kesi tofauti: ww ulitaka ulimboka aongee ni nini tena?
Kila kitu alishaweka wazi pindi alipookotwa mabwe na kama hiyo haitoshi kubenea wa mwanahalisi alimwaga kila kitu hadi gazeti likafungiwa.. Tatizo watu hapa harakati zenu mnaendeshea nyuma ya keyboard..
 
Last edited by a moderator:
Ni kichaa au mwendawazimu tu anayeweza kuyaamini yale yanayosemwa na serikali au yeyote kuwa CDM ndiyo sababu ya mauwaji ya Mwangosi.
Mimi nimesema na ninarudia kuwa Tanzania haina kiongozi kabisa ndiyo maana washikaji wanaowamba ngozi badala yake wanapeleka kule inakoelekea. Ukweli uko wazi sana wala hauhitaji tume, tendwa, sijui na vijinyama gani kutueleza kilichotokea Nyololo. Tunakijua na sababu za mauwaji tunazijua tena sana. Mhusika alikuwepo kwenye eneo la tukio, alitoa mari ya kumwua Mwangosi, na alisimamia hadi akalipuliwa. Alitakiwa kwa kuliangalia kwa aibu kubwa kaburi lake mwenyewe ajiuzulu bila kuambiwa na aombe kunyongwa na wala sii CDM wamwambie cha kufanya. Kamuhanda ni mfu anayetembea na aliyesahau "Mwosha huoshwa"
 
Baada ya ripoti ya tume ya jaji Manento ambayo ndio tume halali yenye mamlaka ya kisheria yanatakiwa yafanyike maandamano ya yasiyo kuwa na kikomo mkoani Iringa kuhakikisha kuwa Kamanda Kamuhanda,Mwema, chagonja na Nchimbi wanang'oka kwenye nafasi zao. Kuna mambo viongozi wetu wa chama wanatakiwa kuongozwa na busara lakini sio hili ambalo mara baada ya tukio chama kikapakwa matope kupitia vipindi vya kupika kwenye runinga.

1. Dr slaa.
2. Mbowe
3. Lissu
4. Zitto
Popote mlipo, amkeni mhamasishe umma wa wana Iringa ili kumtendea haki marehemu Daudi Mwangosi,ally zona na wengine wengi walio uwawa mikononi mwa Polisi, ile kauli ya hakuna kulala mpaka kieleweke ndio inatakiwa kutumika hapa kuwaondoa mabaradhuri walio sababisha vifo vya watanzania wenzetu! Chama kitatuangusha kama kitanyamaza baada ya kutolewa ripoti yenye nguvu za kisheria.

Tusisubiri kesho, tuanze sasa maana ukimya wetu ni mauti kwa wengine, 'hakuna kulala mpaka haki ipatikane, na ikipatikana wahusika wawe wameshapoteza nafasi zao'

Mkuu hapo no. 4 nadhani umepitiwa kidogo. Huyo kwa sasa anapambana na Prof. Muhongo kwenye gesi na mafuta. Haya mambo ya harakati za CHADEMA kwa sasa ameachana nazo maana anasema amejenga chama vya kutosha na sasa ni zamu ya wengine kuendeleza libeneke
 
Chelian ya ulimboka na hili kesi tofauti: ww ulitaka ulimboka aongee ni nini tena?
Kila kitu alishaweka wazi pindi alipookotwa mabwe na kama hiyo haitoshi kubenea wa mwanahalisi alimwaga kila kitu hadi gazeti likafungiwa.. Tatizo watu hapa harakati zenu mnaendeshea nyuma ya keyboard..

nyinyi mnazofanya mbele ya keyboard si mfanye tuzione basi...! Harakati za wengine waliokuwa kwenye keyboard zimekuuwa na nguvu kuliko wale wanaojifunika mablanketi na watawala mbele ya keyboard.
 
NI LAZIMA CDM IFANYE MAANDAMANO MAKUBWA MWEZI HUU KUSHINIKIZA IGP-mwema, chagonja, shilogile, RC, DC, RCO, DCO, RPC-kamuhanda na OCD wajiuzulu!..
 
Nilishawahi kusema hapa jamvini, Kurugenzi ya Habari ya CDM either haiko huru kutoa matamko au inachelewa kureact.
 
Wametoa tamko kupitia
waziri kivuli wa mambo ya ndani vincent nyerere kwamba wanamtaka waziri
nchimbi ajiuzulu na akikataa rais kikwete amuwajibishe

Hizi kauli zimeshazoeleka sana, kinachotakiwa sasa sio matamko tena ni wakati wa kuingia barabarani kumng'oa kikwete aliyeshindwa kuwawajibisha watendaji wake wa chini.
 
Mwanakijiji, tunakuhitaji makao makuu Chadema usaidie kwenye mambo ya communication.
images
 
Kama kweli wewe una uchungu anzisha maandamano yasiyo na kikomo ingia barabarani wewe familia yako makamanda watakufuata anza kesho.

yakhe fitna tu maandamano taka waume haswa waliokamili; mtoi; babukijiji kelele nyingi hawana lolote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom