Elections 2010 CHADEMA mnangoja ni ni kuishitaki TBC?

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
216
kuna habari kuwa TBC wameweka hadharani makubaliano waliyoingia na vyama vya siasa ya kuzingatiwa kila wanaporusha matangazo ya mikutano ya hewani. binafsi sijafanikiwa kuyaona,kama kuna mwenye hayo makubaliano itakuwa vyema akitubandikia apa.

hoja yangu ni kuwa; kama kweli hakukuwa na matusi kwenye uzinduzi wa kamapeni za chadema pale jangwani, basi kwa kukatisha matangazo ya ule mkutano TBC walikiuka mkataba na hivyo wanapaswa kushtaiwa na kilipa fidia kwa hasara yoyoyte iliyotokea.

mimi si mwanasheria lakini wanasheria naomba mtusidie kwa kufafanua hili. na kama chadema wasiposhitaki, tuwaeleweje hata kwa case obvious namna hii ya breach of contract?
 
Chadema watakuwa wanajichimbia kaburi, maana mpaka sasa habari zao hazitosomwa mpaka watakapojua JK ni nani

Nawashauri Chadema wakubali yaishe, wakiendelea kulalama hatoonekana mpaka uchaguzi unaisha

Kwani na hapa JF kusoma habari mbadala mpaka tumjue JK ni nani? Mwambie JK aje pia hapa JF ili tusiwasiliane mpaka uchaguzi uishe. Acha kutishia nyau wewe, hizi sio zama za Zinjanthropus
 
Thithiemu :fencing: CHADEMA Sasa hapa ni nani Rais twende kwa mzeee :cheer2: CHADEMA :becky: ameshida Dr. Slaa.:A S 100:
 
Chadema watakuwa wanajichimbia kaburi, maana mpaka sasa habari zao hazitosomwa mpaka watakapojua JK ni nani

Nawashauri Chadema wakubali yaishe, wakiendelea kulalama hatoonekana mpaka uchaguzi unaisha

Pamoja na ukilaza wako, hapa naona umesema kitu ambacho kimetokea leo. Kwenye taarifa yao habari saa mbili usiku na saa nne, TBC hawakutoa kabisa habari za mikutano ya kampeni ya Chadema. Walionyesha sana mambo ya CCM, ikifuatiwa na CUF; na kidogo TLP. Mh! Mwaka huu tutaona vioja vingi.
 
Aibu tupu, na pia ni uvunjaji wa haki. Sasa huu ni ukoloni ngozi nyeusi za thithiem!!!:eyeroll2:
 
Haina maana.wanaongeza hasira za wananchi.kila mtu mwenye kuumizwa na hilo,atume msg kwenye cm za mkoni kwa watu kumi kuelezea hujuma hiyo.
 
Habari yenyewe hii hapa:
TBC yaweka bayana makubaliano kati yake na vyama vya siasa

TBC.JPG
Shirika la Utangazaji TANZANIA, TBC limeweka bayana makubaliano kati yake na vyama vya siasa, juu ya masharti, mwenendo na utekelezaji wa utangazaji wa matangazo ya moja kwa moja kuhusu mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010.

Hatua hii inafuatia sintofahamu iliyojitokeza katika jamii juu ya hatua ya TBC ya kukatisha kwa muda matangazo ya moja kwa moja ya uzinduzi wa kampeni za CHADEMA katika viwanja vya JANGWANI tarehe 28 mwezi Agosti mwaka huu hatua ambayo ilielezwa na uongozi wa TBC kuwa ilitokana na CHADEMA kukiuka makubaliano kati ya pande mbili hizo.
Makubaliano hayo yaliyo katika kurasa mbili, yalitiwa saini na pande mbili husika yaani TBC na vyama vya siasa, ambapo kwa upande wa CHADEMA yalitiwa saini na Kaimu Katibu mkuu wa Chama hicho JOHN MNYIKA tarehe 26 mwezi Agosti mwaka huu.
Kipengele cha Tano cha makubaliano hayo kinaeleza wajibu wa mtangazaji, yaani TBC wa kukatisha matangazo iwapo chama kitadhihirika kuvunja sheria yoyote ya uchaguzi au sheria yoyote ile nyingine huku kipengele cha Nane kifungu cha “C” kikisema kuwa chama kitawajibika kuepuka lugha zenye kuashiria kashfa na kuashiria uvunjifu wa amani.
Halikadhalika kipengele cha Kumi na Mbili cha mkataba huo kinaeleza kuwa makubaliano hayo yatasomwa pamoja na Mwongozo wa Uandishi na Utangazaji wa Habari za uchaguzi 2010 kama zilivyoandaliwa na TBC.


source: TBC yaweka bayana makubaliano kati yake na vyama vya siasa
 
Chadema watakuwa wanajichimbia kaburi, maana mpaka sasa habari zao hazitosomwa mpaka watakapojua JK ni nani

Nawashauri Chadema wakubali yaishe, wakiendelea kulalama hatoonekana mpaka uchaguzi unaisha

Hizi ni dalili za UDIKTETA namba moja. Asubiri kusulubiwa atakapomaliza uongozi kama anavyosulubiwa Mkapa hivi sasa maana hata majukwaani kujitokeza ni nadra. What goes around comes around.
 
ningependa kama wanasheria wangekuja kutufafanulia...

lakini kama chadema hawatakuja na kesi ya madai dhidi ya TBC basi kwa kiasi fulani watakuwa maweridhika kuwa uamuzi wa TBC wa kukata matangazo ulikuwa sahihi kwa mujibu wa mkataba na sisi tunatakiwa kuwahoji kuwa kama watu wastaarabu, ina maana hawawezi kupiga kampeni bila kutumia maneno yanayoitwa na TBC "matusi"?..

watujibu tafadhari...
 
Back
Top Bottom