rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 15,190
- 20,153
chadema mnafahamu mnachokidai
Nnimekuwa nikifatilia kwa makini siasa za tanzania na hasa vyama viwili chadema na ccm.nimekuwa nikikifatilia ccm kama tawala na chadema kama chama mbadala wengi tumezungumzia mapungufu ya chama tawala ambayo yanaonekana waziwazi na mpaka sasa wamekuwa na kigugumizi kuyarekebisha lakini hatuwezi kuwazungumzia chama tawala bila kuangalia na chama ambacho kinaweza kuwa mbadala wake. moja ya mambo yanayowakera wananchi wengi na hasa walipa kodi ni ukubwa wa serikali kiasi cha kufikiri nafasi nyingine zimewekwa ili kulipa fadhila.
ukubwa huo umezidi kuwapa mzigo wananchi wa kawaida yaani walipa kodi.bahati nzuri chadema wameliona na wamelipigia sana kelele iwe kwenye majukwa ya siasa na hata bungeni kwenye hotuba zao na hata kwenye ilani yao ya uchaguzi wamezungumzia haja ya kupunguzwa ukubwa wa serikali.
jambo jingine ambalo limezua mjadala na hasa kuwa kero ni suala la muungano.wapo wanaopendekeza muundo wa muungano uwe serikali moja,wengine tatu wengine tubaki na muundo tulionao na wengine wameenda mbali zaidi kufikiria kwa sasa hivi hakuna haja ya muungano bora uvunjike.kwa bahati nzuri chadema nao wameweka msimamo wao ni kutaka tuwe na serikali tatu yaani serikali ya tanganyika ,zanzibar na serikali ya muungano.
bahati nzuri haya maswala yalisha jadiliwa kipindi cha nyuma juu ya muundo wa muungano.wakati tunaungana zanzibar iliachiwa kwa makusudi iwe na serikali yake ili isipoteze uasili wake na pia ilionekana itakuwa ni mzigo mzito kwa wananchi wa tanganyika kuhudumia serikali ya tanganyika na muungano tofauti na zanzibar ambayo ukubwa wake ni sawa na mkoa au baadhi ya wilaya za bara watanganyika watakamuliwa zaidi kugharamia serikali yao na serikali ya muungano.
swali langu kwa chadema wakati wanapigia kelele juu ya ukubwa wa serikali hawaoni kuwa na serikali tatu ni kuwabebesha mzigo wananchi wa tanganyika kwani watabeba gharama zaidi kuwahudumia{serikali ya tanganyika} rais wa tanganyika mawaziri wake pia kuwahudumia {serikali ya muungano}rais wa muungano na mawazir wake na bado wastaafu kwani juzijuzi tu tumejulishwa viongozi wastaafu wametengewa bilioni 9 kwa ajili ya matibabu.