CHADEMA mmemuona Regia Mtema na Morogoro yake? Hii ya kilombero mpaka ifakara je? Wabunge mmeona?

jamani huyu jamaa alikuwa anaandika huku analia ndo maana kaandika kwa fujo..

hilo ninakiri bila haya, ukiacha edward moringe sokoine 1984 nikiwa na miaka 11 darasa la nne, the great jk.nyerere ktk siasa za tanzania ndio wameniliza, ujumbe wangu wa maombolezo ya regia ni tamaa na kuamini kuwa wana ccm wenzangu, wasio wana ccm na umma wetu wa tanzania tunahitaji politicians ambao wanaingia mioyoni mwetu kwa udhati wao.

Ninatoka bonde hilo la asili la regia, mteketa,mponda,kombani, ngasongwa, mwesiumo,itatiro,kasapila,kyulule na kiongozi wao mzee kapilima- bonde la mto kilombero, zao la mito ya ruhuji, mpanga, furua; sisi tunauita mto mnyela ila tanzania inauita mto kilombero.

Regia, pumzika kwa amani dada yangu.

Tuliobaki tunakuombea ila kwakweli tunakuomba utuombee sisi sote.
Shukrani kwa cdm, bunge, serikali na kwa dhati kabisa mh. Jakaya kikwete kwa kumpa heshima stahiki kijana wako regia.
Mungu ibariki tanzania
 
hebu tudokezee japo kidogo kilichompata mteketa.

abdi yupo jimboni na tangu huu msiba umetokea amekuwa akirandaranda na hummer yake mjini ifakara na vitongoji vyake, hili limewakera sana wananchi wakirejea mchakato wa uchaguzi 2010. Yale majeraha ya uchaguzi mkuu hayajapona wilaya nzima na hii inatokana na uhai wa kisiasa wa vyama husika......,

Watu hawakutaka Abdi aonekane msibani wala kujihusisha na msiba .... Si haki kumfanyia hayo hata kama msuguano wa kisiasa ungalipo lazima utu na heshima vitangulie yote.

Naamini chini ya familia na usaidizi wa mzee canute mtema+wazazi wake Regia hilo la kumtimua mteketa halina nafasi, cdm ni wakomavu na hawataruhusu hilo kama walivyoidhibiti hali ya baadhi ya wananchama wao kilombero kulumbana juu ya Suzy na marehemu Regia ambao ndio walioshindana jimboni ktk kura ya maoni.

Mwacheni mungu aitwe mungu; jina lake lihimidiwe
 
Mteketa alichowakosea wana ifakara ni kuonyesha fahari za maisha ktk kipindi cha msiba!! Pengine angelijitahidi tu kuisha maisha rahisi especially ktk kipindi cha msiba wa mwenzake. Aache mambo ya lumumba, ifakara ni tofoauti sana na lumumba, misiba ya town magari meusi, suti na miwani myeusi na pamba za kisharo sawia tu ila ifakara chivembu ni chivembu tu, watu wanalia wake kwa waume tena kwa kuruka makambi na kwing'onyola in respect of marehemu.

Msijeshangaa kuwaona wamama/wababa wakiomboleza kwa style hii. Umma huu ungependelea kumuona mh. Abdi akiwa yuko low na siyo high kama anavyoonekana sasa. Angalizo la hatari " ukiwa unahisiwa vibaya ktk misiba na ukaamua kuwa low nayo ni hatari utang'ongwa eti unaona haya kwa unyama wako"

All in all abdi anapaswa kushiriki kwa hali na mali lakini anapaswa kuishi maisha rahisi kulingana na mazingira
 
hakika huyu alikuwa mwana wa Mungu"haya maneno yalisemwa na wale jamaa waliomsulubu Yesu baada ya kuona hali ya nchi ilivyobadilika baada ya jamaa kukata roho, na mimi nayasema leo baada ya kuona haya yaliyotokea dar na ifakara kwenye msiba wa mpendwa wetu Regia.
 
Maneno haya ni makali saana, hakika msiba huu wa Regia umemgusa kila mtu, MUNG ilaze mahali pepa peponi ROHO ya Regia, Amen
 
Mteketa ni nani?? tupe CV yake!!

naskia tu jina lake kwa ngwasumaaaAaa

1698.jpg



School Name/LocationCourse/Degree/AwardStart DateEnd DateLevel
Lipangalala Primary SchoolPrimary Education19581961PRIMARY
Nawenge Middle School, MahengePrimary Education19621962PRIMARY
Iwemba Middle School , KidodiPrimary Education19631965PRIMARY
Lutengo United College, UgandaSecondary Education19671970SECONDARY
R.T.C Nairobi, KenyaAccounts, Store & Management19711971CERTIFICATE


EMPLOYMENT HISTORY
Company NamePositionFrom DateTo Date
The Parliament of TanzaniaMember - Kilombero Constituency20102015
East African HarboursClerical Officer19711988
 
waombolezaji ni wengi saana hakika marehemu dada yetu Regia atazikwa na umati mkubwa saana, hii inaonyesha jinsi watu walivyo mpenda wakati wa uhai wake, ni mtu wa watu, ni mtu wa MUNGU, watu wameloa jasho, wengine wamevua mashati lakini hawajali kitu
 
lol! imebidi nicheke japokuwa sitakiwi kucheka!

naona Camaraderie umaamua kuleta C.V ya huyo Mteketa kabisa.
 
1698.jpg



School Name/LocationCourse/Degree/AwardStart DateEnd DateLevel
Lipangalala Primary SchoolPrimary Education19581961PRIMARY
Nawenge Middle School, MahengePrimary Education19621962PRIMARY
Iwemba Middle School , KidodiPrimary Education19631965PRIMARY
Lutengo United College, UgandaSecondary Education19671970SECONDARY
R.T.C Nairobi, KenyaAccounts, Store & Management19711971CERTIFICATE


EMPLOYMENT HISTORY
Company NamePositionFrom DateTo Date
The Parliament of TanzaniaMember - Kilombero Constituency20102015
East African HarboursClerical Officer19711988
Vi CV vya wabunge wetu vinachekesha hao ndio watunga sheria wetu. RIP Regia
 
CDM MMEMUONA REGIA E. MTEMA NA MOROGORO YAKE? HII YA KILOMBERO MPAKA IFAKARA JE? WABUNGE MMEONA?

KWA MARA YA MWISHO KUWASILIANA NA REGIA ILIKUWA KTK SALAMU ZAKE ZA MWAKA MPYA, NILIMPONGEZA NA KUMKOSOA NA NINAMSHUKURU ALINIELEWA NA KUNIPA TUMAINI KUWA NILICHOMKOSOA KIMO KTK KALENDA YAKE YA 2012......,

NILIFARIJIKA SANA HASA PALE ALIPOSISITIZA NA ALIPONIBAINISHA KWA LUGHA YA NYUMBANI, ALIAHIDI PIA ATANI PM .........; NAUGUA KWA KIFO CHAKO NA LICHA YA U CCM WANGU NILITAMANI NIWE HAPO VIWANJA SITINI-BENKI MUDA HUU ILA MUNGU AMENIPA FARAJA KWA YALIYOTOKEA LEO PALE DADA YANGU ULIPOUGUSA MKOA WA MOROGORO-MIKUMI-RUAHA-KILOMBERO-MANG'ULA-KIBEREGE-SAGAMAGANGA-KAPORO-KIBAONI NA DAKIKA 40 ZILIZOPITA UMEINGIA IFAKARA VIWANJA SITINI -BENKI KTK UWANJA WA FAMILIA YA MTEMANYENJA aka MTEMA.

MLONGU WANGU UMEIANDIKA HISTORIA NA UMEACHA FUNDISHO KWA WOTE WALIOKUSINDIKIZA LEO KUINGIA HUKO NYUMBANI. WAN JF. NAWATAKA WABUNGE WOTE WALIOENDA LEO IFAKARA NA KESHO WAKISHAMLAZA NYUMBANI REGIA WAJIULIZE KAMA WATAIPATA HESHIMA HII ALIYOIPATA REGIA TANGU AMEFARIKI NA SASA MKO IFAKARA NYUMBANI KWAO?

BINT WA 1980 AMEUNYAMAZISHA MKOA WETU, AMEZILIZA WILAYA NA NINAWAPOANDIKIA HII TAARIFA MUULIZENI PEDESHEE MTEKETA AMEKUMBWA NA NINI IFAKARA, CCM, CDM, CUF NA WENGINEO TUJIFUNZE KUINGIA MIOYONI MWA WANANCHI WETU KWA NAMNA NJEMA NA YENYE MASHIKO.

IMEANDIKWA "JILILIENI.........." NENO HILI HUTIMIA KWA UTU WEMA WETU NA SIYO VINGINEVYO. RUDINI BUNGENI MPIGANIE ALICHOAMINI REGIA WABUNGE ULANGA -KILOMBERO POKEENI KIJITI CHAKE, ACHENI ZECOMEDY ILIYOFANYWA MALINYI SIKU AMBAYO REGIA ALIPOPATA AJALI JUU YA MASHAMBA YA MPUNGA, DKT MPONDA, MAIGE NA DKT HOVISA KUPINGANA MBELE YA WAHANGA WA SAKATA HILO.

MMEIDHALILISHA SERIKALI. SUZAN KIWANGA CHAPA KAZI MSAIDIE MTEKETA TUPATE MAGEUZI KILIMO NA MIUNDO MBINU.

LALA KWA AMANI DADA YANGU REGIA MTEMA.
Summarize please!!!!
 
cdm mmemuona regia e. Mtema na morogoro yake? Hii ya kilombero mpaka ifakara je? Wabunge mmeona?

Kwa mara ya mwisho kuwasiliana na regia ilikuwa ktk salamu zake za mwaka mpya, nilimpongeza na kumkosoa na ninamshukuru alinielewa na kunipa tumaini kuwa nilichomkosoa kimo ktk kalenda yake ya 2012......,

nilifarijika sana hasa pale aliposisitiza na aliponibainisha kwa lugha ya nyumbani, aliahidi pia atani pm .........; naugua kwa kifo chako na licha ya u ccm wangu nilitamani niwe hapo viwanja sitini-benki muda huu ila mungu amenipa faraja kwa yaliyotokea leo pale dada yangu ulipougusa mkoa wa morogoro-mikumi-ruaha-kilombero-mang'ula-kiberege-sagamaganga-kaporo-kibaoni na dakika 40 zilizopita umeingia ifakara viwanja sitini -benki ktk uwanja wa familia ya mtemanyenja aka mtema.

Mlongu wangu umeiandika historia na umeacha fundisho kwa wote waliokusindikiza leo kuingia huko nyumbani. Wan jf. Nawataka wabunge wote walioenda leo ifakara na kesho wakishamlaza nyumbani regia wajiulize kama wataipata heshima hii aliyoipata regia tangu amefariki na sasa mko ifakara nyumbani kwao?

Bint wa 1980 ameunyamazisha mkoa wetu, ameziliza wilaya na ninawapoandikia hii taarifa muulizeni pedeshee mteketa amekumbwa na nini ifakara, ccm, cdm, cuf na wengineo tujifunze kuingia mioyoni mwa wananchi wetu kwa namna njema na yenye mashiko.

Imeandikwa "jililieni.........." neno hili hutimia kwa utu wema wetu na siyo vinginevyo. Rudini bungeni mpiganie alichoamini regia wabunge ulanga -kilombero pokeeni kijiti chake, acheni zecomedy iliyofanywa malinyi siku ambayo regia alipopata ajali juu ya mashamba ya mpunga, dkt mponda, maige na dkt hovisa kupingana mbele ya wahanga wa sakata hilo.

Mmeidhalilisha serikali. Suzan kiwanga chapa kazi msaidie mteketa tupate mageuzi kilimo na miundo mbinu.

Lala kwa amani dada yangu regia mtema.


hakika nimekusoma ndugu yangu kweli da regia alikuwa mtu wa watu!
 
hili la utapeli wa Mteketa sina ushahidi wake hata chembe ila kule kwetu 2010 tulikumbwa na watu wa aina ya Gulamali kwa kuanzia na Mteketa mwenyewe Kilombero na upande wa pili wa mto kilombero Ulanga Magharibi ni Yassin Njayagha, Simon Ngonyani wote hawa waliamini ktk nguvu ya pesa kupata ubunge. Mteketa alipita njia ileile aliyoiasisi marehemu gulamali na akafanikiwa kwa hawa ndg zangu wawili wao walivamia chaka ama walivamia maji pasipo kutumia kijiti kuyapima hawakuvuka mto wa CCM na kutoka patupu Ulanga Magharib. Ila siasa ya 2010 CCM itaitesa Ulanga-Kilombero 2015 kama hukutafanyika mageuzi ya kweli ndani ya chama chetu.
 
Back
Top Bottom