CHADEMA mlifunika kombe WAZANZIBARI WAMELIFUNUA. Kazi kwelikweli.

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
"TABIA YA KUFUNIKA KOMBE MWANAHA APITE ITAKUJA ITUcost" ni kauli aliyotoa mbowe bungeni wakati wa kupitisha mswaada wa katiba wenye mapungufu kibao. Ambao zenji walichana na hawakufuatwa kuuliza tena.

Baada kuupigia kelele. Zitto akawaelekeza pa kuwazibia mdomo. Mkaenda ikulu mlichojadilia na kukubaliana siri yenu mpaka leo.

Mkakubali tusijadili kuwepo au kuwepo kwa muungano. Siwalaumu kwani mlipofikia iliitajika busara zaidi.

Biblia inasema mkinyamaza ata milima itasema.

WAZANZIBAR TENA BILA YA MUONGOZO WA CHAMA CHOCHOTE WANASEMA MUUNGANO HAWAUTAKI. Moto ndio unakolea. Na wanahaki ya kufanya hivyo kwani wasiwasi wao ni halali.

Mafuta kuwa ya muungano wakati dhahabu, tanzanaiti na almasi mikataba inatuachia mashimo na milahaba ya 4% na tunajisifu imepanda!

Wezi wa bajeti ya muungano wanavyotanua mtaani.

Hawajadanganyika na nusu ya wajumbe wa kamati. Chadema mlifunika kombe zenji wamelifunua akuna mwanaharamu

Nb. Wachangiaji wengi hawataki kukosolewa nategemea kutukanwa humu. Ila ukilazimisha tuwe na mtazamo moja hakuna haja ya kujadili. Na naamini mtu hujifunza zaidi kwa kukosolewa kuliko kusifiwa. Sifa zinalevya. Mf watz wakarimu madini yanaenda.
 
kutokuutaka muungano karne hii ni kama wewe ukiamua kujipa haki ya kuingia mitaani bila nguo, ama ukijipa haki ya kutokula vyakula vya kulinda mwili wako na maamuzi mengine ya aina hiyo ambayo yataheshimiwa lakini hayataachwa kuhojiwa.

.Agenda ya wazanzibari wenye akili ingekuwa siyo kuutaka muungano au la. Agenda ya wenye akili ni AINA ya MUUNGANO,SHIRIKISHO NA SERIKALI TATU, SERIKALI MOJA,AMA SERIKALI ZA MAJIMBO NA MOJA YA SHIRIKISHO ama huu wa Serikail ya Muungano na ya Zanzibar
 
Hongera kwa mada hii Mkuu,

Tutafute serikali moja tu ya Tanzania, tupunguze kelele zizizo na mpango, Muungano sasa haupo tena kama wananavyoujadili, Muungano washaufanya Mkombozi wa nchi zote mbili Nyerere na Karume aliyereuliwa na Nyerere kuchukua jina la kiongozi wa mapinduzi (japo kwa kipigo alimtumia John Okello wa Uganda), sasa ipo Tanzania na haiguswi mipaka yake, asiyependa kuwa ndani ya mipaka ya Tanzania ahamie kwengine.

Je leo Wamarekani leo watawauliza Wa Texas kuwa wanataka kuendelea kuwa ndanu ya Marekani au wanataka kujitenga? ikumbukwe ilikombolewa toka Mexico.

Katiba ianze kwa kusomeka JAMHURI YA TANZANIA (SIO TENA JAMHURIYA MUUNGANO) UKISHATAJA TANZANIA USHATAJA MUUNGANO.
 
Hi kwanini mafisadi yapo bara tu,sisikii kama kuna mafusadi zenji
 
..CDM wangejitokeza kupinga muungano, au muundo wake, wangesingiziwa wanafanya hivyo kutokana na chuki dhidi ya Waislamu.

..pia wa-Tanganyika tukisema jambo lolote lile kuhusu kutoridhishwa kwetu na muungano, wa-Zanzibar wanachukulia kama ni matusi na dharau kwao. Matokeo yake wanaachana na hoja, wanaanza kushambulia mtoa hoja, au chama chake. Rejea hoja za Tundu Lissu na matusi aliyovurumishiwa.

..mimi naona CDM wametumia busara kuwaachia wa-Zanzibari washughulikie masuala ya muungano. hakuna haja ya kugombea fito na wa-Zanzibar wakati hata CDM nao wanataka serikali 3 au muungano wa mkataba.
 
Huo ni upepo mwanana toka marashi ya zenji utapita tu! Muúngano utadumu mpaka kizazi hadi kizazi.
 
familia ya Karume na baadhi ya mawaziri huko nako wana kashfa pia mfano mauzo ya majengo ya makumbusho bila kufuata kanuni za uuzaji wa mali za serikali ya mapinduzi.ukifuatilia utaambiwa.usisahau kuwa ufisadi ni sera isiyoandikwa ya ccm
 
Hi kwanini mafisadi yapo bara tu,sisikii kama kuna mafusadi zenji

Excellent,

..hujasikia kashfa ya Amani Karume kupora ardhi mpaka makaburi ya Waanglikani kule Zanzibar??

..biashara na matumizi ya madawa ya kulevya ambavyo vimekithiri Zanzibar unadhani siyo ufisadi??

..kujaza abiria kwenye meli na kusababisha izame na mamia ya wa-Zanzibar kupoteza maisha siyo matokeo ya ufisadi??

..tatizo la wa-Zanzibar ni kulundika kila uchafu ktk maisha yao, ikiwemo ufisadi[ujambazi, ushoga, umalaya, madawa ya kulevya] kwenye muungano.
 
..CDM wangejitokeza kupinga muungano, au muundo wake, wangesingiziwa wanafanya hivyo kutokana na chuki dhidi ya Waislamu.

..pia wa-Tanganyika tukisema jambo lolote lile kuhusu kutoridhishwa kwetu na muungano, wa-Zanzibar wanachukulia kama ni matusi na dharau kwao. Matokeo yake wanaachana na hoja, wanaanza kushambulia mtoa hoja, au chama chake. Rejea hoja za Tundu Lissu na matusi aliyovurumishiwa.

..mimi naona CDM wametumia busara kuwaachia wa-Zanzibari washughulikie masuala ya muungano. hakuna haja ya kugombea fito na wa-Zanzibar wakati hata CDM nao wanataka serikali 3 au muungano wa mkataba.

Wao wenyewe ni wabaguzi wa hatari na roho mbaya angalia wakristo wa zanzibar walioanza kujenga miaka 600 iliyopita mpaka akawakuta sultani,leo wananyimwa haki zao.
 
Madawa ya kulevya yanashushwa mbele ya kijiji cha Paje, kuna vikampuni vya wahindi na wazanzibari weusi wanajifanya ni ma divers na wana boti za kassi kweli, sasa meli kubwa toka arabuni inapita mbele ya kisiwa ikiendelea na safari, kwakuwa kuna mawasiliano, maboti yanakurupuka na kwenda pembeni ya meli kwenye maji makubwa, mzigo unashushwa hapo.wakubwa wote wanajua ni zanzibar hata siku moja hawaumbuani
 
Wao wenyewe ni wabaguzi wa hatari na roho mbaya angalia wakristo wa zanzibar walioanza kujenga miaka 600 iliyopita mpaka akawakuta sultani,leo wananyimwa haki zao.

Pharaoh,

..CCM wamepata ganzi baada ya Mashekhe kuikamata hoja ya muungano kule Zanzibar.

..CCM walishatumia udini dhidi ya CDM huku Tanganyika, wakajiweka karibu na Waislamu. Sasa wakigeuka na kuwashambulia wale Mashekhe wataonekana vituko na wendawazimu.

.
 
kutokuutaka muungano karne hii ni kama wewe ukiamua kujipa haki ya kuingia mitaani bila nguo, ama ukijipa haki ya kutokula vyakula vya kulinda mwili wako na maamuzi mengine ya aina hiyo ambayo yataheshimiwa lakini hayataachwa kuhojiwa.

.Agenda ya wazanzibari wenye akili ingekuwa siyo kuutaka muungano au la. Agenda ya wenye akili ni AINA ya MUUNGANO,SHIRIKISHO NA SERIKALI TATU, SERIKALI MOJA,AMA SERIKALI ZA MAJIMBO NA MOJA YA SHIRIKISHO ama huu wa Serikail ya Muungano na ya Zanzibar

Na pia agenda ya Watanganyika wenye taswira ya akili timamu isingekuwa kunga'nga'nia Zanzibar kubaki ndani ya muungano huu wa kihunihuni.
 
..CDM wangejitokeza kupinga muungano, au muundo wake, wangesingiziwa wanafanya hivyo kutokana na chuki dhidi ya Waislamu.

..pia wa-Tanganyika tukisema jambo lolote lile kuhusu kutoridhishwa kwetu na muungano, wa-Zanzibar wanachukulia kama ni matusi na dharau kwao. Matokeo yake wanaachana na hoja, wanaanza kushambulia mtoa hoja, au chama chake. Rejea hoja za Tundu Lissu na matusi aliyovurumishiwa.

..mimi naona CDM wametumia busara kuwaachia wa-Zanzibari washughulikie masuala ya muungano. hakuna haja ya kugombea fito na wa-Zanzibar wakati hata CDM nao wanataka serikali 3 au muungano wa mkataba.

kaka una hekima sana, una vision ya juu.
 
Pharaoh,

..CCM wamepata ganzi baada ya Mashekhe kuikamata hoja ya muungano kule Zanzibar.

..CCM walishatumia udini dhidi ya CDM huku Tanganyika, wakajiweka karibu na Waislamu. Sasa wakigeuka na kuwashambulia wale Mashekhe wataonekana vituko na wendawazimu.

.

Asante Mkuu Jokakuu, sasa nimefahamu.
 
Back
Top Bottom