AruMeru sio Pemba ambako CUF haina na haitakuwa na mpinzani. Sioi, mkwe wetu akiteuliwa, Nape na Lowasa wataongea lugha moja!Kwa taarifa yako yeyote atakaye simama kwa chadema ana nafasi ya kulinyakua jimbo.Sizungumzii ushabiki
bali ni hali halisi.CCM wameishaichoka kabisa.
basi bwana msiungane mtashinda...chama chenu kina nguvu na ushawishi mkubwa tanzania...But mimi naamini katika umoja ni nguvu utengano ni udhaifu wewe unaamini vinginevyo,ndio demokrasia hiyo tusonge mbele..
ni ujinga wa watanzania wanaoneshwa njia ya uzima hawataki kupita sasa itakuaje?
Mrema hakutaka kumsikiliza Mwalimu. Mwalimu alimwambia mapema tu kuwa amejiunga na wahuni ambao wanataka kutumia umaarufu wake wa kisiasa wakati huo kwa malengo yao. Mrema akamdharau Mwalimu hasa baada ya kupata support kubwa sana toka kabila lake ili awe Rais wa JMT. Uchaguzi wa 1995 ukafanyika yaliyofuata baada ya hapo ni historia tamu mno kusimulia. Mrema atuuzie mikanda ya video alizorekodi tangu anahama CCM, anagombea Urais kwa tiketi ya NCCR hadi anatimkia TLP. Asiisahau ile episode ya Tanga!
CHADEMA inaonekana kujijenga kitaasisi zaidi ukiondoa mapungufu ya hapa na pale. Bado safari ya kujenga taasisi hii ni ndefu na yenye vikwazo vingi. Kinachotakiwa nchi hii ni TAASISI na ASASI zenye nguvu sio watu. Si unaona CCM waliwaachia watu flani wakawa na nguvu wanavyohangaika nao? Kumvua mtu uongozi kwa kukosa sifa imekuwa shughuli pevu!
Ni kweli umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Lakini ni vyema kumfahamu vizuri unayeungana naye. Mnaweza kuwa na muungano wa hamasa kama wa ODM ambao hauna tija yoyote. Tusiwe na muungano kama wa gunia la viazi ambalo likichanika viazi vyote vinatawanyika. Mpaka sasa CDM ina potential kubwa msikurupuke jengeni nguvu kubwa kwa vijana na kupanga safu ili mtakapoingia madarakani muwe na mipango endelevu kama ya Kagame.Msitengeneze mtandao wa kiushikaji na baadaye mnaiacha nchi kwenye umasikini.
Nikishajua post ni ya Kimkardash sisomi kabisa napita mazima
Nyie CCM Mmeungana na nani?
Correction. Chadema haishindani na Lowassa Arumeru. Kwa hiyo ufananisho wako na Razza wa Uzini hauna mshiko.Uzini ilikuwa 5% magwanda 95% CCM, Arumeru na Lowassa ni kama Uzini na Razza.
Hayo mapande ya CCM unayoyafikiria yatakupigia wewe kura, ujuwe unajipa moyo tu lakini matokeo umesha yajuwa. Huna chako.
Aah, yaani wazee wa chama kumshauri Zitto Kabwe asigombee wenyekiti 2010 ndiyo kubakwa kwa demokrasia, eeh?umesema vizuri sana,lakini nina mashaka pia na chadema kuridhika mapema na vitendo vinavyoshiria ubakaji mkubwa wa demokrasia ndani ya chama hicho kinachojitambulisha kutokana jina lake kama cha kidemokrasia,ipo mifano mingi sina haja ya kuitaja kusapoti tuhuma hizi za ubakaji ndani ya chadema,natamani kuanzisha mada kuhoji hii lakini nachelea cuz najua haitasurvive itafungwa haraka sana,lakini jambo hili lipo na mifano ipo,hii itakipasua chama siku moja kama hiyo hadithi ya tanga na mrema na marando pamoja na magenge yao.
Aah, yaani wazee wa chama kumshauri Zitto Kabwe asigombee wenyekiti 2010 ndiyo kubakwa kwa demokrasia, eeh?