CHADEMA: Mbowe atafuta wa kumrithi uenyekiti

Kwa muda kumekuwepo na tetesi kwamba Mbowe angependa sana kuwania nafasi ya urais 2015. Kama hili ni kweli CHADEMA watakuwa na wakati mgumu kwa sababu pamoja na kwamba ametoa mchango mzuri kwenye chama chake lakini kukubalika kwa Mbowe ni tofauti sana na Dr. Slaa. Hapa Mbowe na uongozi mzima wa CHADEMA wanatakiwa wawe very realistic na wajue ni kwanini watanzania wengi wamekikubali hiki chama kwa kasi ya ajabu mara pale tu Dr Slaa alipotangazwa kuwa mgombea wa nafasi ya urais.
 
Amesoma ishara za nyakati na kuona hawezi mziki wa Nape. Tunamtakia maisha marefu ya kustaafu ila najua lazima atamuweka mchaga mwenzake.
Acha pumba wewe, Nape angekuwa na mziki si angeuonyesha kwa Lowasa na Chenge? Usituletee habari za huyo vuvuzela wako hapa.
 
Ha ha haaa, Heche ndiye kiboko yako unafyata mkia kama mbwa koko aliyekurupushwa. Magamba bila kuwafokea hawaelewi kabisa.
Vipi bado anakaa kwa kaka yake pale Sinza Mori? Mtafutieni nyumba hata pale Tandale kwa Mtogole
 
Tunamtaka LEMA awe mwenyekiti baada ya mbowe kustaafu.Wengine wachumba tu hawawezi kuthubutu na hawajisimamii.

Mimi na wewe tuko upande mmoja. lakini kwenye hili la Lema kuwa mwenyekiti wetu wa Taifa niwie radhi, sikubali hata kwa kulambishwa Jamvia.
 
Huo ni makati wa kujiandaa kugombea urais kwa mwaka 2015 kwa kuwa sasa chama kimeanza kuwa maarufu na Dr. Slaa ni boya tu, atarudi Karatu kugombea ubunge. Kwani Natse(Mb) wa Karatu anapwaya. Anaumiza kichwa ya nini wakati kijana Zitto yupo ndio alitaka kumg'oa katika uchaguzi uliopita.
 
Kwani jamaa ni mwizi wa magari.
Mkuu, unauliza kikoi Yemeni? Ngoja niku-PM namba ya simu ya Zombe umpigie mwambie tu mimi ni Mwananchi mpenda amani naomba unipe habari za Lema, utalia ndugu yangu kwa jinsi alivyoshiriki ujambazi sehemu nyingi za Tanzania mpaka Kenya
 
Cdm ni chama cha vijana.hivyo MWK lazima awe kijana dkt slaa amezeeka sasa basi tu magwanda ndio yanamfanya awe kijana.Zito ni kijana tatizo hatokei kwetu na ni kinyume cha goals zetu za underkapeti.Lema anazo sifa zote na anakubalika kwa vijana.
 
Cdm ni chama cha vijana.hivyo MWK lazima awe kijana dkt slaa amezeeka sasa basi tu magwanda ndio yanamfanya awe kijana.Zito ni kijana tatizo hatokei kwetu na ni kinyume cha goals zetu za underkapeti.Lema anazo sifa zote na anakubalika kwa vijana.
Unamaana sio mchaga sio?
 
Mbowe amesahau kuwa Zito aligombea uenyekiti wakamchakachua? Leo unadai unamtafuta mbadala wako kama si unafiki ni nini?
 
Mwenyekiti machahari wa chama machachari na makini cha upinzani nchini kamanda wa anga bw. Freeman mbowe amesema hana tena mpango wa kuendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini na badala yake anaumiza kichwa nani awe mrithi wake huku akifurahia mafanikio aliyokifikishia chama hicho..

Kamanda mbowe ameyasema hayo jana baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mkubwa wa kumnadi mgombea udiwani..

Nikimnukuu Mbowe alisema ''nawashukuru sana makamanda kwa moyo mnaotuonyesha, hakika nafarijika sana na ndio maana nimeamua kutoendelea tena kuwa mwenyekiti ili tuwanyamazishe wabaya wetu wanosema sisi ni chama cha wachaga na wakaskazini wakati ukweli ni kwamba watu wa kaskazini ni mimi na slaa tu"..

Naomba tumtakie kila la heri kamanda wetu huyu..

Nawasilisha.
Wapi huko?
 
Uzuri ni kwamba mambo yanaenda vizuri Igunga,Ukombozi kwa mara ya pili

Kauli ya Mbowe ni nzuri,ni katika harakati za kuachiana uongozi
 
Mtei alishasema hawez mpa mtu chama CHAKE m2 acyemjua hapo ni wakat zito alpogombea uwenyekiti akimaansha m/kiti lazma awe wa kaskazn(mchaga)...alaf mbowe nd anaongea upuuz huo khaaa atawadanganya nyie mazuzu tu...mtakuja kuniambia m/kit atakaemwachia lazma awe mchaga....over kidumu
 
Mkuu, unauliza kikoi Yemeni? Ngoja niku-PM namba ya simu ya Zombe umpigie mwambie tu mimi ni Mwananchi mpenda amani naomba unipe habari za Lema, utalia ndugu yangu kwa jinsi alivyoshiriki ujambazi sehemu nyingi za Tanzania mpaka Kenya
Mbona hajakamatwa na kushitakiwa, polisi wanamuogopa? au kwakuwa Zombe alikuwa mahabusu kwa muda mrefu alishindwa kumshughulikia? au alikuwa sehemu ya madili ya mheshimiwa akawa anayafumbia macho?
 
Back
Top Bottom